Korogwe: Bodaboda wadaiwa kuchoma basi la Saibaba baada ya mwenzao kugongwa

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Basi la Kampuni ya Sai Baba linalofanya Safari kutoka Dar es Salaam kuelekea Mkoani Arusha limeteketezwa kwa Moto mara baada ya kusababisha Ajali kwa kumgonga Dereva wa Bodaboda na kudaiwa kusababisha kifo kwa dereva huyo wa Bodaboda katika eneo la Msambiazi wilayani Korogwe mkoani Tanga leo Februari 27, 2024.

Waendesha Pikipiki (Bodaboda) katika eneo hilo wamejichukulia sheria mkononi mara baada ya kushuhudia ajali hiyo ikitokea kwa kulichoma basi hilo moto kwa kutumia mafuta ya Petroli.

Habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa kundi la waendesha bodaboda, leo Februari 27, 2024 wamelichoma moto na kuliteketeza basi linalodaiwa kuwa ni mali ya Kampuni ya Saibaba, lililokuwa linatoka jijini Dar es Salaam kuelekea Arusha, baada ya kudaiwa kumgonga bodaboda mmoja na kusababisha kifo chake.

Habari zilizotufikia hivi punde, zimeeleza kuwa tukio hilo limetokea katika eneo la Kona ya Semkiwa, Korogwe mkoani Tanga na kusababisha kukatika kwa mawasiliano kati ya pande mbili za barabara hiyo, jambo lililosababisha foleni iliyodumu kwa takribani saa mbili.

Kwa mujibu wa mashuhuda, baada ya ajali iliyosababisha kifo cha mwendesha bodaboda, wenzake walijikusanya na kulizingira basi hilo, wakawaamuru abiria wote kushuka na kushusha mizigo yao kabla ya kuliteketeza kwa moto.

s3.jpg
s2.jpg
 
Hao wapuuzi sana. Juzi kuna mmoja kaja kunigonga mi nikiwa na gari. Jamaa nimemuona toka mbali akikimbiza pikipiki pamoja na kumpungia mkono kuashiria apunguze mwendo bado kaja nivaa.

Siku wakinigonga na kujifanya kutaka choma gari au nipiga mawe, mtasikia jamaa kaua Bodaboda 20 kwa kuwagonga na gari. Mapuuzi sana, hayajui sheria yenyewe ni kukimbia na kujichomeka kila sehemu.
 
Navyofahamu mimi waendesha pikipiki huwa na adabu sana kwa mabus ila madereva wa haya mabus hujiona wao ndio wenye haki ya barabara. Pia huwa na viburi sana barabarani.

Imeshawahi kunitokea, nilikuwa natoka kisesa Mwanza naelekea mjini na kipikipiki changu. Mbele yangu kulikuwa na Lori linatokea mjini na nyuma yake ilikwepo bus ya Zakaria. Ghafla bus likaovertake likajaa upande wangu na sikua na nafasi ya kupita. Ilibidi niingize pikipiki mtaroni ili kuepuka kusababishiwa ajali.

Mara nyingi hakuna haki yoyote anapata bodaboda akigongwa na bus, hii imesababisha hasira kwa hawa watu, wanaona nibora mmalizane upate hasara kuliko kwenda kuzungushwa kisha aambulie patupu.
 
Nawalaani kwa nguvu zote waliohalalisha pikipiki kubeba abiria, nawalaani askari wa usalama barabarani kwa kutofuatilia na kuangalia mwenendo wa bodaboda hapa nchni, nawalaani wanasiasa wote hasa wa ccm kuwatumia bodaboda kisiasa. Majanga wanaosababisha bodaboda na hayaripotiwi Au kuupuuziwa na mamlaka ni makubwa mno
 
Juzi tu hapo tuliwapa cheo as maafisa usafirishaji na wengi vichwa vilijaa maji kwa sababu ya aliyewapa jina.

Haya hao maafisa usafirishaji a.k.a vibaka na wauaji wamefanya yao na bahati mbaya hapo kijijini kwa wiki au mwezi hawataonekana kwa uharibifu wa mali.

Watetezi wao waibuke tuone.
 
Navyofahamu mimi waendesha pikipiki huwa na adabu sana kwa mabus. Pia watu wa mabus huwa na viburi sana barabarani.

Imeshawahi kunitokea, nilikuwa natoka kisesa Mwanza naelekea mjini na kipikipiki changu. Mbele yangu kulikuwa na Lori linatokea mjini na nyuma yake ilikwepo bus ya Zakaria. Ghafla bus likaovertake likajaa upande wangu na sikua na nafasi ya kupita. Ilibidi niingize pikipiki mtaroni ili kuepuka kusababishiwa ajali.
Kisesa ipi labda hii inayoanzia Kanyama hadi kufikia isangijo kona ya kayenze au kisesa b ile inayotokea bugomba hadi kahangala? Hakuna sehemu yenye bodaboda wapuuzi kama hizi! Li mtu unakuta limetoka kayenye lina mshikaki wa abiria 4 kinapita mbele ya polisi hadi jiwe la mkapa!
 
Habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa kundi la waendesha bodaboda, leo Februari 27, 2024 wamelichoma moto na kuliteketeza basi linalodaiwa kuwa ni mali ya Kampuni ya Saibaba, lililokuwa linatoka jijini Dar es Salaam kuelekea Arusha, baada ya kudaiwa kumgonga bodaboda mmoja na kusababisha kifo chake.

Habari zilizotufikia hivi punde, zimeeleza kuwa tukio hilo limetokea katika eneo la Kona ya Semkiwa, Korogwe mkoani Tanga na kusababisha kukatika kwa mawasiliano kati ya pande mbili za barabara hiyo, jambo lililosababisha foleni iliyodumu kwa takribani saa mbili.

Kwa mujibu wa mashuhuda, baada ya ajali iliyosababisha kifo cha mwendesha bodaboda, wenzake walijikusanya na kulizingira basi hilo, wakawaamuru abiria wote kushuka na kushusha mizigo yao kabla ya kuliteketeza kwa moto.

1709048622041.png

1709048638706.png
 
Back
Top Bottom