Ushauri wangu kwa kampuni ya mabasi ya Shabiby

soulesh

New Member
Nov 3, 2013
2
3
Nina maoni/ushauri kwa kampuni ya Shabiby Line

1. Wasikubali kushusha/kuharibu brand yao waliyoitengeneza kwa muda mrefu kwa sababu ya watendaji wachache wasiokua na weledi/utendaji mzuri ikiwemo lugha nzuri kwa wateja hususani watu wa customer care unaweza piga simu kwa ajili ya kupata msaada mtu anapokea simu kama vile amelazimishwa,ushirikiano unakua hafifu.

2. Kuwepo na mfumo rafiki pindi mteja anapohitaji kusogeza(reschedule)muda wa safari. Leo Jumamosi tarehe 25/11/2023 nilikata tiketi ya shs 40,000 (Dar-Dodoma)kwa ajili ya gari inayoondoka 11:30am lakini masaa mawili kabla ya safari nilipiga ili kuomba nisogeze muda mbele kwa kuangaliziwa gari nyengine bila ya kujali kiwango nilicholipa(hata ningepata gari yenye nauli ya chini kulinganisha na kiwango nilicholipa)nisingedai nikaambiwa haiwezekani naomba hili suala lifanyiwe review ili mteja aweze ku-reschedule safari pindi anapopata changamoto. Na nimeshangazwa kuambiwa haiwezekani hali ya kuwa nilishawahi ku-reschedule safari Dom-Dar na nikakubaliwa.

Kwa heshima na taadhima naomba hayo machache yafikishwe kwa wahusika ili changamoto hizo zitatuliwe kwa hekima na busara.

Naomba radhi mahali ambapo nitakua nimekwaza kwa namna yoyote.

Natanguliza Shukran
 
Back
Top Bottom