Kampuni ya basi la Shabiby, hii ni hatari sana kwa abiria wenu

Nimekuwa mpenzi wa kutumia usafiri wa basi la Shabiby mimi na familia yangu kwa miaka zaidi ya mitano

Dar, Dodoma, Dodoma Arusha.

Ila leo kwa yaliyo nikuta kupitia dereva huyu, imeniuma sana

Tulikata tiketi siti namba 4 kwa ajili ya mke wangu kusafiri toka Arusha kuelekea Dodoma ni katika basi linalo wasili Arusha saa nne asubuhi ili kuelekea Dodoma.

Katika pilikapilika za safari nikajikuta nimesahau kadi yangu ya benki ambayo nilidhamiria kuitumia kutoa pesa ili kumpa mke wangu pesa ya matumizi njiani na hii ndio ikawa sababu kwa mimi kukutana na maumivu niliyoyapata kwa dereva nisiye mfahamu jina lake ila ndiye dereva wa basi tulilo kata tiketi hii,yaani basi la Shabiby.

Kutokana na kusahau kadi ya benki nililazimika kumuacha ndani ya gari mke wangu ambaye nilikuwa nikimsindikiza kutafuta namna nyingine ya kupata pesa ili nimpe ya kula njiani,

Baada ya kufanikiwa nikarejea ndani ya gari, kwa lengo la kumpa hiyo pesa mke wangu,ndipo dereva huyu wa shabiby baada ya kuona kuwa mkononi mwangu nimeshika speaker ndogo ambayo huwa naitumia kwa ujasiliamali ,yeye akahisi labda naingia kuuza bidhaa fulani

Hata hivyo kwa upole nilimweleza kuwa, mimi siingi kuuza ila lengo langu ni kumpa mke wangu pesa ya matumizi njiani.

Kilicho niumiza, bado aliendelea kuni zuia kibabe

Hakuishia hapo tu alinikunja huku kondakta wake akinivuta mguu kwa nje,mbele za mke wangu,abiria na watu wengine,kiukweli nimedhslilishwa,naamini kosa langu ni kuutumia usafiri wa shabiby kumsafirisha mke wangu,halafu kuamua kumletea pesa ya matumizi mke wangu.

Kweli nimejaribu kumwelezea mtu niliye fahamishwa kuwa ni kiongozi wake hata sijaridhishwa na namna alivyoshughulikia kudhalilishwa kwangu,kiukweli nimeamua,maana mimi huwa hakuna aina ya biashara mbayo huwa naifanya ndani ya mabasi,zaidi ya leo kumsindikiza mke wangu.

Kweli,kama kampuni ya mabasi ya shabiby haita muwajibisha huyu,aliye nikunja hata kunitishia kunipiga,kisa,nimemweleza kuwa nampa mke wangu pesa ya matumizi njiani, basi kwa mimi binafsi na familia yangu nitafikiria kuto penda kuutukimia usafiri huu kwa mara nyingine,maana nimeaibishwa sana.

Nimejaribu kutafuta mawasiliano ya kampuni ya basi la shabiby makao makuu ili kutoa taarifa ya kero hii, ila sijatambua namna ya kuwapata,ndio maana nimeandika hapa ili wahusika wapatapo ujumbe angalau walishughulikie hili kama wana upendo na wateja wao,tafadhali wasilifumbie macho

Muda huu basi hilo bado lipo njiani kuelekea dodoma, mke wangu niliye msafirisha anaitwa Silvero Mwacha ,yupo sit namba 4, tafadhali wahusika popote mlipo nimekereka, naomba msilifumbie macho hili.

Ni mimi Emmamuel.

Pole sana mkuu
 
Pole Sana.

Ila wewe bado mshamba wa safari, ukidekezwa ipo siku utaharibu zaidi. Kusindikiza kwako kunaishia nje ya Basi , ndani ni Abiria na Wahudumu wa Basi.

Ulikuwa na uhuru wa kumwagiza hata konda akampe mkeo kisha mkeo akakujulisha iwapo amepata ama lah.

Punguza deko mtoto wa kiume.
 
Nikupe pole, ila kwa maelezo yko nahisi kunakitu unakificha. Kwanini.

1. Kama wangekuona kabla ukimsindikiza mkeo sidhani kama wangekukatalia kuingia.

2. Baada yakukataliwa kuingia bado ulikuwa na nafasi yakumuita dirishani na mambo yakaenda bara bara.

3. Wakati wavurugu bado mkeo alikuwa na nafasi ya kutoka nakuja kuchukua hiyo posho kuepuka dhahama hiyo.

Kifupi kosa ni lakwako.
Kwani kuna mahali ameandika mkewe hakupata ile posho? Anacholalamikia yeye ni kuvutwa vutwa na kukunjwa kunjwa bila kusikilizwa tena mbele ya kadamnasi na mkewe akishuhudia.
 
Hii dongo liende kwa shabiby bus na mabus yote yanayojiita n luxury kwa uhuni wanaofanyia abiria wao siku hizi.

Haya MABUS tunajua n LUXURY hvyo Kuna huduma nzuri pamoja na KIYOYOZI cha ajabu n wajinga wanafungua zile VENT za juu na kuacha abiria wanapigwa na UPEPO Kama wapo kwenye FUSO Yan hata usikivu ndan ya bus inakuwa hakuna mnaohusika mjirekebishe.

Mkiona tunapanda chuma zetu za alinunua Babu mpaka kitukuu wa kitukuu anatumia msituone sie wajinga kwanza tunasave karibu nusu ya pesa ambayo tungewapa hvyo n faida Kwetu pili tunakuwa huru na safari sababu kule wanajua kuwa kabisa wao wanatuhitaji sisi kuliko wao.
 
Kwani hiyo spika ilikuwa kubwa kiasi gani? Kama ilikuwa kubwa sana lazima ingewafanya huyo dereva kufikiri vinginevyo.
Pole hata hivyo! Nikuombe tu samehe hayo yamepita.
Harafu ungemrushia mkeo hiyo pesa kwa njia ya mtandao wa simu harafu angeitolea mbele ya safari,after theni kutoka Arusha mpaka Dom ni masaaa machache angeweza kuvumilia.
Ni vidogo hivi ,kama horn,ni
Pole sana mkuu!
Asante sana mkuu
 
Pole sana . Na pole kwa kuendekea kubezwa tena humu ndani.
1. Shabbiby inaweza isiathirike kwa kutopanea familia yako leo lkn ipo siku itaathirika tu, maana kisasi ni chake Mungu atalipa.
2. Ni mazoea ya wengi huwa tunaingia kusindikiza ndugu hii ya kumpiga mtu ni dharau na kuangaliana watu kwa hadhi. Yaani kuwa na speaker kuwaliwaonesha wewe ni hohehahe. Kudharau watu kwa hadhi jambo la kijinga kabisa.

3. Hata kama ulikosea njia ya kukuelimisha haikuwa hiyo, ndio maana tunalaumu polisi kutumia nguvu kubwa kwa raia wenzao. Kumbe na sisi ni washiriki wa unyama na kukosa utu.
4. Ipo siku wamfanyia mwingine namna hiyo halafu atajitoa mhanga maana wengine hata haya maieha hawaoni raha yake bora wafe na mtesi wao, ndipo uzi mwingine utakuja DEREVA AKATWA KOROMEO AKIMZUIA ABIRIA KUSINDIKIZA MKEWE. Tutaanza ku comment kila mtu maoni yake
 
Tatizo sio ofisi ya Shabiby,Nina mlenga dereva

Mimi nine eleza kilicho nikera

Wengine wamenifariji pia wengine wamenidharirisha mtandaoni japo hawanijui mimi ni nani

Dunia ni mzunguko

Usimdharau usiye mjua

Wala usiongee KWA hisia

Kitajulikana
Hatujui wewe ni nani! Wewe si yule uliyejitambulisha unatembea na Ndugai (spika), wewe ni mtu mkubwa sana na mmewekewa kinga ya kushitakiwa.
 
Huyo Kitimoto mawazo yanamsumbua naomba apatiwe matibabu watalaamu wa saikolojia njooni mumsaidie kwabure kabisa vinginevyo mambo yataendelea kuwa sio mambo.

Tafadhali ndugu Kitimoto chukulia hili kama Tiba
 
Jamaa kaongea ili apate watetezi watetezi nao wanamkimbia na kesi wanamrudishia yy dah! Kweli usitarajie majibu uyatakayo ww
emoji1787.png
Huu ni mtandao wa kijamii,wamiliki wa mabasi ya shabibu wawachunguze wafanya Kazi wakorofi
Ni vidogo hivi ,kama horn,ni

Asante sana mkuu

IMG_20210906_011333.jpg
 
Nimekuwa mpenzi wa kutumia usafiri wa basi la Shabiby mimi na familia yangu kwa miaka zaidi ya mitano

Dar, Dodoma, Dodoma Arusha.

Ila leo kwa yaliyo nikuta kupitia dereva huyu, imeniuma sana

Tulikata tiketi siti namba 4 kwa ajili ya mke wangu kusafiri toka Arusha kuelekea Dodoma ni katika basi linalo wasili Arusha saa nne asubuhi ili kuelekea Dodoma.

Katika pilikapilika za safari nikajikuta nimesahau kadi yangu ya benki ambayo nilidhamiria kuitumia kutoa pesa ili kumpa mke wangu pesa ya matumizi njiani na hii ndio ikawa sababu kwa mimi kukutana na maumivu niliyoyapata kwa dereva nisiye mfahamu jina lake ila ndiye dereva wa basi tulilo kata tiketi hii,yaani basi la Shabiby.

Kutokana na kusahau kadi ya benki nililazimika kumuacha ndani ya gari mke wangu ambaye nilikuwa nikimsindikiza kutafuta namna nyingine ya kupata pesa ili nimpe ya kula njiani,

Baada ya kufanikiwa nikarejea ndani ya gari, kwa lengo la kumpa hiyo pesa mke wangu,ndipo dereva huyu wa shabiby baada ya kuona kuwa mkononi mwangu nimeshika speaker ndogo ambayo huwa naitumia kwa ujasiliamali ,yeye akahisi labda naingia kuuza bidhaa fulani

Hata hivyo kwa upole nilimweleza kuwa, mimi siingi kuuza ila lengo langu ni kumpa mke wangu pesa ya matumizi njiani.

Kilicho niumiza, bado aliendelea kuni zuia kibabe

Hakuishia hapo tu alinikunja huku kondakta wake akinivuta mguu kwa nje,mbele za mke wangu,abiria na watu wengine,kiukweli nimedhslilishwa,naamini kosa langu ni kuutumia usafiri wa shabiby kumsafirisha mke wangu,halafu kuamua kumletea pesa ya matumizi mke wangu.

Kweli nimejaribu kumwelezea mtu niliye fahamishwa kuwa ni kiongozi wake hata sijaridhishwa na namna alivyoshughulikia kudhalilishwa kwangu,kiukweli nimeamua,maana mimi huwa hakuna aina ya biashara mbayo huwa naifanya ndani ya mabasi,zaidi ya leo kumsindikiza mke wangu.

Kweli,kama kampuni ya mabasi ya shabiby haita muwajibisha huyu,aliye nikunja hata kunitishia kunipiga,kisa,nimemweleza kuwa nampa mke wangu pesa ya matumizi njiani, basi kwa mimi binafsi na familia yangu nitafikiria kuto penda kuutukimia usafiri huu kwa mara nyingine,maana nimeaibishwa sana.

Nimejaribu kutafuta mawasiliano ya kampuni ya basi la shabiby makao makuu ili kutoa taarifa ya kero hii, ila sijatambua namna ya kuwapata,ndio maana nimeandika hapa ili wahusika wapatapo ujumbe angalau walishughulikie hili kama wana upendo na wateja wao,tafadhali wasilifumbie macho

Muda huu basi hilo bado lipo njiani kuelekea dodoma, mke wangu niliye msafirisha anaitwa Silvero Mwacha ,yupo sit namba 4, tafadhali wahusika popote mlipo nimekereka, naomba msilifumbie macho hili.

Ni mimi Emmamuel.
Wasambaa mtaacha lini kuzunguka na redio?
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom