Kampuni ya SuperFeo Ruti ya Songea-Arusha-Moshi mbona mmeanza nyodo na maringo? Au kwa vile mko wenyewe?

saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
4,173
6,156
Hii kampuni ya SuperFeo ilianza safari zake za kutoka Songea-Dodoma-Arusha mwanzoni mwa mwaka jana 2002. Tulifurahi sana maana ilikuwa ni ukombozi wa safari ya moja kwa moja kutoka kusini mwa nchi yetu mpaka kaskazini.

Kwa wiki huwa na safari 2, walianza vizuri sana, ulikuwa unakata tiketi yako muda wowote, hata zaidi ya mwezi moja kabla ya safari.

Badala ya kwamba tungetegemea wangeongeza mabasi kwa maana ya kuwa na basi kila siku badala yake sahivi mpaka leo hii huwezi kupata tiketi ya kusafiri tarehe 1 mwezi wa 12. Kinachotufanya tukate tiketi kabla ni uhakika wa kupata nafasi maana huwa linajaa mapema.

Kwa uzi huu napenda kuwauliza shida ni nini mpaka kuja kutunyanyasa na kututesa? Ni nyodo na maringo kwa kuwa wako wenyewe? Kumbukeni SuperFeo yamekufa makampuni makubwa kuliko ya kwenu, unyanyasaji huu hautawaacha salama.

Mwisho ningeomba makampuni mengine yajitokeze, mfano Shabiby, Abood na wengine kuwe na ushindani. Shabiby najua una basi lako kutokea Songe-Dodoma kila siku, kwanini usiunganishe angalau mpaka Arusha?
 
Back
Top Bottom