Kampuni ya basi la Shabiby, hii ni hatari sana kwa abiria wenu

EMMANUEL JASIRI

Senior Member
Feb 2, 2015
108
225
Nimekuwa mpenzi wa kutumia usafiri wa basi la Shabiby mimi na familia yangu kwa miaka zaidi ya mitano

Dar, Dodoma, Dodoma Arusha.

Ila leo kwa yaliyo nikuta kupitia dereva huyu, imeniuma sana

Tulikata tiketi siti namba 4 kwa ajili ya mke wangu kusafiri toka Arusha kuelekea Dodoma ni katika basi linalo wasili Arusha saa nne asubuhi ili kuelekea Dodoma.

Katika pilikapilika za safari nikajikuta nimesahau kadi yangu ya benki ambayo nilidhamiria kuitumia kutoa pesa ili kumpa mke wangu pesa ya matumizi njiani na hii ndio ikawa sababu kwa mimi kukutana na maumivu niliyoyapata kwa dereva nisiye mfahamu jina lake ila ndiye dereva wa basi tulilo kata tiketi hii,yaani basi la Shabiby.

Kutokana na kusahau kadi ya benki nililazimika kumuacha ndani ya gari mke wangu ambaye nilikuwa nikimsindikiza kutafuta namna nyingine ya kupata pesa ili nimpe ya kula njiani,

Baada ya kufanikiwa nikarejea ndani ya gari, kwa lengo la kumpa hiyo pesa mke wangu,ndipo dereva huyu wa shabiby baada ya kuona kuwa mkononi mwangu nimeshika speaker ndogo ambayo huwa naitumia kwa ujasiliamali ,yeye akahisi labda naingia kuuza bidhaa fulani

Hata hivyo kwa upole nilimweleza kuwa, mimi siingi kuuza ila lengo langu ni kumpa mke wangu pesa ya matumizi njiani.

Kilicho niumiza, bado aliendelea kuni zuia kibabe

Hakuishia hapo tu alinikunja huku kondakta wake akinivuta mguu kwa nje,mbele za mke wangu,abiria na watu wengine,kiukweli nimedhslilishwa,naamini kosa langu ni kuutumia usafiri wa shabiby kumsafirisha mke wangu,halafu kuamua kumletea pesa ya matumizi mke wangu.

Kweli nimejaribu kumwelezea mtu niliye fahamishwa kuwa ni kiongozi wake hata sijaridhishwa na namna alivyoshughulikia kudhalilishwa kwangu,kiukweli nimeamua,maana mimi huwa hakuna aina ya biashara mbayo huwa naifanya ndani ya mabasi,zaidi ya leo kumsindikiza mke wangu.

Kweli,kama kampuni ya mabasi ya shabiby haita muwajibisha huyu,aliye nikunja hata kunitishia kunipiga,kisa,nimemweleza kuwa nampa mke wangu pesa ya matumizi njiani, basi kwa mimi binafsi na familia yangu nitafikiria kuto penda kuutukimia usafiri huu kwa mara nyingine,maana nimeaibishwa sana.

Nimejaribu kutafuta mawasiliano ya kampuni ya basi la shabiby makao makuu ili kutoa taarifa ya kero hii, ila sijatambua namna ya kuwapata,ndio maana nimeandika hapa ili wahusika wapatapo ujumbe angalau walishughulikie hili kama wana upendo na wateja wao,tafadhali wasilifumbie macho

Muda huu basi hilo bado lipo njiani kuelekea dodoma, mke wangu niliye msafirisha anaitwa Silvero Mwacha ,yupo sit namba 4, tafadhali wahusika popote mlipo nimekereka, naomba msilifumbie macho hili.

Ni mimi Emmamuel.
 

Mkakombinga

Member
Jul 5, 2021
21
75
Nikupe pole, ila kwa maelezo yko nahisi kunakitu unakificha. Kwanini.

1. Kama wangekuona kabla ukimsindikiza mkeo sidhani kama wangekukatalia kuingia.

2. Baada yakukataliwa kuingia bado ulikuwa na nafasi yakumuita dirishani na mambo yakaenda bara bara.

3. Wakati wavurugu bado mkeo alikuwa na nafasi ya kutoka nakuja kuchukua hiyo posho kuepuka dhahama hiyo.

Kifupi kosa ni lakwako.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,555
2,000
Ndani ya basi wanatakiwa kuingia abiria tu waliokata tiketi na wafanyakazi wa basi tu sio mtu mwingine

Waliokukunja na kukuvuta miguu wamekuhurumia walitakiwa wakutandike mangumi na makofi juu

Ungempigia simu mkeo ashuke achukue hivyo vipesa vyako koko chini sio wewe upande basi

Ukome kabisa tabia hiyo ya kupanda ndani ya basi wakati wewe sio abiria
 

Me too

JF-Expert Member
Feb 9, 2015
5,300
2,000
ndani ya basi wanatakiwa kuingia abiria tu waliokata tiketi na wafanyakazi wa basi tu sio mtu mwingine waliokukumja na kuvuta miguu wamekuhurumia walitakiwa wakutandike na makofi juu

ungempigia simu mkeo ashuke achukue hivyo vipesa vyako koko chini sio wewe upande basi

ukome kabisa tabia hito ya kupanda ndani ya basi wakati wewe sio abiria
Dereva punguza makali
 

Golden C

JF-Expert Member
Jul 31, 2019
3,220
2,000
ndani ya basi wanatakiwa kuingia abiria tu waliokata tiketi na wafanyakazi wa basi tu sio mtu mwingine waliokukumja na kuvuta miguu wamekuhurumia walitakiwa wakutandike na makofi juu

ungempigia simu mkeo ashuke achukue hivyo vipesa vyako koko chini sio wewe upande basi

ukome kabisa tabia hito ya kupanda ndani ya basi wakati wewe sio abiria
Akili yako inafanana mgogo flani anayeongoza taasisi/mhimili flani.
Haijalishi alikosea utu wa mtu uheshimiwe
 

Sodium

JF-Expert Member
Feb 14, 2014
742
500
Wewe ndo mwemye makosa , kwanza unaingia kwenye gari na vifaa vyako vya kazi , pili ulipaswa kumsikiliza dreva anasema nini ili ufate maagizo kabla ujavutwa mguu na hyo kondakita .

Fata utaratibu maana inawezeka mda wa kuondoka ulikuwa umewadia kwaiyo walikuwa wanaanza safari kwaiyo wasingeruhusu uingie.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,555
2,000
Akili yako inafanana mgogo flani anayeongoza taasisi/mhimili flani.
Haijalishi alikosea utu wa mtu uheshimiwe
Lazima kuzingatia sheria za usafirishaji

Wewe kama sio abiria huruhusiwi kuingia ndani ya basi .Hata choo cha manispaa huwa wanaingia waliopia tu sembuse basi.Huna tiketi unaingia kufanya nini?

Hongera wafanyakazi wa SHABIBY ila hiyo tabia yenu ya kutowatandika makofi watu kama huyu mleta mada ambaye hakuwa abiria akitaka kuingia ndani ya basi sijaipenda mlitakiwa mhakikishe anaondoka na ngeu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom