Kampeni ya kuikataa Vodacom

Kampeni ya kuikataa Vodacom

Bwana Ali Mufuruki

Nadhani sasa ni wakati muafaka ukaonesha imani yako kwenye misingi bora ya uendeshaji mashirika ya kibiashara (Corporate Governance).

Wewe ni mmoja wa waasisi wa CEO Round Table, na ni kinara wa kuhimiza mambo ya Corporate Citizenship na Corporate Governance,

Responsibility and Accountability, ni moja ya misingi ya mambo hayo.

Sasa hii VODACOM ambayo wewe ni mwenyekiti wa Board ya Wakurugenzi wake, chini ya uongozi wako tumeshuhudia kitu ambacho naweza kukiita one of the biggest Corporare Governance scandle baada ya executives wake kushutumiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi. Ni bahati nzuri kwako kwamba wakati scandle hii inatokea mpaka mnaizima kimya kimya kwa kukubali kulipa mabilioni ya pesa ambayo mimi nayatambua kama Rushwa hakuna aliyekunyooshea kidole kwa sababu ya negative sentiment ya wananchi dhidi ya serikali ya awamu ya Tano, Hasa wananchi walio kwenye social networks au la kwa sababu ya utamadurni wa watanzania ambao unautambua vizuri tu.

Kabla hilo halijapoa, Chini ya Uongozi wako, inaonekana tena VODACOM inatumika na vyombo vya serikali kuingilia faragha za wateja wake. Misingi ya mafanikio ya kampuni yoyote katika sekta ya mawasiliano ni umadhubuti wake katika kutunza siri za mawasiliano ya wateja.

Leo uchumi wa dunia unatetemeka kwa sababu tu Wamerakani wana wasiwasi kampuni ya Kichina ya UHAWEI inaweza ikatumiwa na serikali ya CHINA kufanya upuuzi ambao leo VODACOM inaruhusu vyombo vya serikali kuwafanyia wananchi wake.

Haya ni mapungufu makubwa ya kiuongozi, naona watu wengi wanakimbilia kulalamikia uwezo mdogo wa technologia ya ulinzi ya VODOCOM, hii sio kweli. Makampuni yote ya simu yanatumia equipment vendors wale wale, na wala hakuna kampuni hapa inaweza kudai inajivunia kuwa na uwezo mkubwa wa kiulinzi kwenye mitambo yake, hakuna.

Hili ni tatizo la kiongozi, kuna ethical conduct breakdown hapo Vodacom, na ni wajibu wa Board chini ya Mwenyekiti wao kuhakikisha kwamba wanaweka Appropriate ethical tone juu ya mambo kama haya, yote mawili, yale yalipelekea wakurugenzi wenu wakafikishwa mahakamani kutokana na makosa ya uhujumu uchumi pamoja na huu ushenzi, huu ni ushenzi wala siwezi kuuelezea na ndio maana wala sishiriki mijadala yake hapa JF.

Sasa Bwana Ali, mbele yako umepata fursa hadhimu, kuuthibitishia ulimwengu wote kwamba wewe ni Board Room Guru, you have alot of justifications, unaweza ukachagua mawili.

Ama ukasema, haukubaliani na muenendo wa vyombo vya serikali kuingilia mitandao yenu ya mawasiliano ambayo wana access nayo kutokana na nafasi yao ya usimamizi wa makampuni ya mawasiliano, useme hauko Tayari kuwa sehemu ya uhuni huu. U RESIGN.

Au useme tu kwamba, kumekuwa na Governance Failure, na umeamuwa kutake responsibility, U RESIGN.

Na sio lazima useme maneno yote yao, unaweza ukatumia maneno very general lakini ukaresign, tutakuelewa.

Ama sivyo unachafua jina lako na washirika wako.

Nakuangalia.
 
Ulichofanya ni sawa na kuibomoa screen ya Tv yako kwa nyundo baada ya kusikia mtangazaji akisoma taarifa amvayo haikukupendeza wewe, na tv yako itazimika na wewe kuzani umemkomoa Mmiliki wa Tv na kwamba woote hawataona taarifa. Kumbe umejikomoa mwenyewe na sisi wengine ndiyo kwanzaa tunasajiri laini tatu tatu. Pole kwa ujinga uliokukumba, chukua tahadhali karibu utakuwa Nyumbu
Kwa kuwa vodacom wameamua kutumia tabaka dhalimu la watawala badala ya kufanya biashara...

Na kwa kuwa vodacom wameamua kuwa sehemu ya mhimili huo wa uovu...

Na kwa kuwa sasa ni dhahiri wanashiriki kusaidia raia wema kufuatiliwa mawasiliano yao na kufanyiwa uhalifu na vyombo dhalimu vya dola...

Nimeamua kuungana na watanzania wazalendo walioamua kususia bidhaa za vodacom na hivi natangaza rasmi kuivunja vipande na kuichoma moto line yangu ya Vodacom ambayo nimekuwa nikiitumia tangu mwaka 2002.

Nimewaachia salio la Shilingi 0.56 kwenye akaunti yangu ya m'pesa...wale wafaidi.

May the unscrupulous and evil dogs of Vodacom go to hell and burn among the rocks!

Shubaaamit!
 
Mimi nimeivunja Jana kwa kweli ni hatari
Nadhani ipigwe kampeni wateja wa voda wazime simu zao kwa siku mbili tuu. Iwe fundisho kwa huu mtandao.
Kwanza huduma zao ni ghali ukilinganisha na mitandao mingine halafu bado wana fanya ushenzi.
 
halafu mpaka wasomi kabisa na akili zao, eti....wanaacha kutumia VODA!!! wakati ni mitambo ya TCRA na makampuni yote wanafanya hivyo
Hayo makampuni mengine unayajua wewe kwa sababu unachofanya ni speculation! Sisi tunazungumzia kampuni ambazo tayari imeshathibitika! And FYI, issue sio kutolewa hizo taarifa za wateja bali kutolewa na kuwa public! Kila nchi udukuzi upo lakini unafanyika kwa ajili ya kufanyia kazi udukuzi husika na sio ili hatimae uweke public! Taarifa hizo kuwa public inaonesha wanaofanya huo udukuzi ni wahuni, na kama kampuni ya simu inahusika, ina maana inafanya kazi na wahuni! Tukichukulia issue ya akina Membe kwa mfano! HAKUNA taasisi yoyote ya kiserikali inayoweza kufanya ule upumbavu kisheria! Kama ilikuwa lazima wafanye eavesdropping basi wangefanya hivyo kimya kimya!!!!!
 
Mitandao yote ipo chini ya TCRA na sheria ya mawasiliano ,sasa mtahamia mtandao gani ambao TCRA na sheria hazifanyi kazi!?
Ni kifungu gani kinawalazimisha kutoa maongezi ya wateja kiholela? Kama wangekuwa makini walitakiwa wamshitaki huyo aliyerusha mazungumzo ya wateja wao hadharani.

Vv
 
Hayo makampuni mengine unayajua wewe kwa sababu unachofanya ni speculation! Sisi tunazungumzia kampuni ambazo tayari imeshathibitika! And FYI, issue sio kutolewa hizo taarifa za wateja bali kutolewa na kuwa public! Kila nchi udukuzi upo lakini unafanyika kwa ajili ya kufanyia kazi udukuzi husika na sio ili hatimae uweke public! Taarifa hizo kuwa public inaonesha wanaofanya huo udukuzi ni wahuni, na kama kampuni ya simu inahusika, ina maana inafanya kazi na wahuni! Tukichukulia issue ya akina Membe kwa mfano! HAKUNA taasisi yoyote ya kiserikali inayoweza kufanya ule upumbavu kisheria! Kama ilikuwa lazima wafanye eavesdropping basi wangefanya hivyo kimya kimya!!!!!

aisee, unazungumza kwa confidence ya ajabu!...kama una akili vile

Vodacom wasingejikaanga na kusema kitu kupoteza wateja

wame respond na kueleza kuwa taarifa zinaombwa na, serikali na TCRA

ambao kwa akili zako za Ulaya unasema hawawezi kufanya vile

kwa akili zako za ulaya unadhani ni wahun
ila kwa akili zako za Tandale chooni, haujawahi kuwaza mbona mawasiliano mengine mengi huwa hayavuji?

Membe kasema anajua yametokea wapi,jasusi mbobezi angesema tu ni voda

hao wahuni wangetoa sana taarifa mpaka za mapenzi ya siri za watu, hao wahuni

msijifanye wajuaji sana
 
Mambo ya kudukuliwa yanafanyika kwenye system za serikali makini kama Marekani, sembuse company kama vodacom. Achana vodacom ifanye kazi kwa mujibu wa sheria.
 
Kuandika tu Voda -Com Tanzania inamaana kubwa na ni jibu kwanini wametoa taarifa za wateja wao kuliko hata maelezo mengi uliyotoa.

Kifupi % kubwa ya wananyakazi ni watanzania sawa na katibu wetu mwenezi wa chama na mkuu wetu wa mkoa pendwa! Nahii ndiyo maana pana zaidi ya mfumo! Mimi na wewe inawezekana tunapiga kelele cz tuko nje lakini tungekuwa kwenye nafasi hizo tungetoa tu taarifa upende au usipenda otherwise kaapembeni na wasiojulikana wakufuata hata kama umeacha kz! Hii ndiyo Tz ya sasa, Mungu ibariki Tz, Mungu ibariki Africa.
 
Pumbavu! Hii nayo mtaishia patupu kama kipindi kile.

Sikia, watu hawatumii Voda sababu Lema au Msigwa au Mbowe kasema tumieni, Bali wa natumia voda sababu ya huduma zao,

Huduma zao ndio zitakazoamua uitmuie au laa!

Wakati mwingine tumieni akili.

Mtoa mada kasema kuhusu Msigwa au Lema? Nyie ndiyo mnafanya wanawake waonekane wana upeo mdoga kwa sababu ya watu kama wewe
 
Kwa kuwa vodacom wameamua kutumia tabaka dhalimu la watawala badala ya kufanya biashara...

Na kwa kuwa vodacom wameamua kuwa sehemu ya mhimili huo wa uovu...

Na kwa kuwa sasa ni dhahiri wanashiriki kusaidia raia wema kufuatiliwa mawasiliano yao na kufanyiwa uhalifu na vyombo dhalimu vya dola...

Nimeamua kuungana na watanzania wazalendo walioamua kususia bidhaa za vodacom na hivi natangaza rasmi kuivunja vipande na kuichoma moto line yangu ya Vodacom ambayo nimekuwa nikiitumia tangu mwaka 2002.

Nimewaachia salio la Shilingi 0.56 kwenye akaunti yangu ya m'pesa...wale wafaidi.

May the unscrupulous and evil dogs of Vodacom go to hell and burn among the rocks!

Shubaaamit!
Tuachie voda yetu, we don't care. Usalama kwanza.
 
Back
Top Bottom