Mtoto Wa Mbale
JF-Expert Member
- May 15, 2011
- 457
- 300
Ndugu wana JF:
Katika taarifa ya habari ya leo usiku kupitia TBC1 nimeona habari ya JK kuzindua kamati maalum ya kitaifa ya Okoa maisha somalia. Sina tatizo na kampeni hiyo, kwa misingi ya utu!
Hata hivyo nina shaka na dhamira yake hasa nikizingatia ukweli kwamba maeneo mbalimbali ya nchi yetu yanakabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa chakula. Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma, Manyara, Mara, Mwanza nk inakabiliwa na njaa hata kusababisha mahindi kuzuiwa kuuzwa nje ya nchi.
Kinachokera zaidi ni pale ambapo serikali haijachukua hatua yeyote kuwafidia wakulima kutokana na hasara walizopata kutokana na ukame, achilia mbali mkakati mahsusi wa kukabiliana na njaa!
Tunaelekea wapi??