Kamati ya maadili hatari kuliko zote Tanzania ogopa sana

Ashampoo burning

JF-Expert Member
May 12, 2023
420
1,582
images - 2024-03-07T010800.089.jpeg

Basi tulivyokuwa wadogo enzi mwaka 1996 nikiwa zangu mgeni kabisa iringa mafinga ndo mara kwanza niliwaona hawa wana kamati ya nidhamu(nyigu)...

Hawa wanakamati ya nidhamu(nyigu) mara nyingi walipenda sana kujenga nyumba zao vibarazani hasa karibu na meter za umeme sasa tukiwa wadogo tulipenda sana kupiga nyumba zao mawe zinabomoka wakitoka tunakimbia ..

Hawachoki wanajenga tena kama kawaida yetu watoto wa mtaa ule tulikuwa tunapenda kuchezea sana nyumba zao kwa kuzibomoa sasa kumbe wanakamati wanatusoma tu jinsi gani ya kututia adabu

Sasa siku moja tukiwa kuna mtoto mmoja mtaani alirusha jiwe kwenye nyumba ya wanakamati haikubomoka ...asee walitoka kama 30...kwa hasira walimfanyia operation ya kichwa aasee alivimbaaa kichwa macho akawa kama mchina mimi nilipona siku hiyo maana tulikimbia mno ....yule mtoto aliyefanyie operation ya kichwa alikuwa jiran yetu alipelekwa hospital mafinga na kulazwa... nyigu ni mdudu balaaa wana hasira sana yaani kukufanyia open surgery dakika mbili

Baaada ya wiki kupita tukawa tuna cheza cheza tuko na kakangu mmoja sasa hivi anafanya kazi njombe huko.... sasa tukamuona mwanakamati ya maadili katua kwenye maua tukamua kwa hasira kulipa kisasi ....sasa mwanakamati aka nyigu hata ukimua ule mkia wake bado unakuwa unafanya kazi

Kiutani yule kaka angu akachukua ule mkia akijua amekufa si akaniweke ndani ya sweater maeneo ya kifuani asee nilifanyiwa operation ya kifua fasta nilipiga yowe sito sahau kifua kilivimba balaaa ......aseee nililiia balaaaa nilitoka naruka ruka nimeshika kifua hadi nyumbani kwa maza mungu amrehemu akaninipooza akanishauri nikiiona nyigu nikae pembeni hadi leo nikiwaona sina hamu nao

Walinipa nidhamu hadi leo sina hamu nao

Andika kisa chako ni hii kamati ya nidhamu aKA nyigu
 
Udogoni nilikuwa bingwa wa kukwea miti, msimu wa maembe umefika nikapanda juu ya mti wa embe, ile miti mirefu.
Kule juu kumbe jeshi la NATO aka nyuki wametulia wananisoma, ghafla wakaanza kutoa dozi.

Nilikua nashuka kwenye mti kwa utaratibu nipo kimya huku nikivumilia maumivu nisije anguka, nilipoweka miguu chini tu nilikimbia napiga kelele nadhani katika maisha yangu sitokuja vunja ile rekodi ya ile kasi ya mbio.
 
Hivi kati ya hawa
wakubwa


Masai_Mara_National_Reserve_01_-_African_paper_wasp_%28Belonogaster_juncea%29.jpg

Na wadogo,
Oriental_wasp_%28Vespa_orientalis%29.jpg


Yupi ana maumivu zaidi??
Hao wakubwa ndo walinifanyia operation mimi wanapatikana maeneo ya baridi

Hao wachini hawana sana maumivu wanapatikana maeneo ya hapa dar kipindi cha miti ikianza kutoa maua..... hao wa juu ni nyigu original maumivu yake ni unasikiliza katikati ya ubungo ngoja leo nichek sumu yao ni aina gani
 
Udogoni nilikuwa bingwa wa kukwea miti, msimu wa maembe umefika nikapanda juu ya mti wa embe, ile miti mirefu.
Kule juu kumbe jeshi la NATO aka nyuki wametulia wananisoma, ghafla wakaanza kutoa dozi.

Nilikua nashuka kwenye mti kwa utaratibu nipo kimya huku nikivumilia maumivu nisije anguka, nilipoweka miguu chini tu nilikimbia napiga kelele nadhani katika maisha yangu sitokuja vunja ile rekodi ya ile kasi ya mbio.
Bora ulikutana nyuki anapiga stingy moja anakufa hawa wahuni wavuta bangi nyingi anaweza kukupinga hata sting 100 mmoja

Inshort hawa wakiwa 50 wanakutoa uhai kabia
 
Early 2000s nikiwa kitoto niliambulia kichapo toka kwa hawa. Since then nawaheshimu kila niwaonapo.
 
hivi ng’e na tandu ni sawa?
Hapana. Ni wadudu wawili tofauti kabisa (Scorpion na Centipede). Ila zingatia usicheze nao, usiwadhihaki na wala usijenge mazoea nao. Watakutia adabu chap.
 
Kwangu mimi nyuki ndio balaa zaidi. Nilishuhudia jeshi la nyuki likimsululubisha mtu pale Shelui 2008. Hatimaye alipumnzika kwa amani.
 
Back
Top Bottom