Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,339
- 51,883
Kwema Wakuu!
Namna Bora ya ku-deal na vijana wa sasa ambao Asilimia 90% ni Vijana wa hovyo ni kuwa na roho ngumu tuu. Kama unahitaji mahusiano mazuri yenye furaha na vijana hawa na hautaki kuumia basi nakushauri kuwa na roho ngumu.
Kama sio mtoto wako uliyemzaa basi usimpe connection ya kazi, au usimpe mchongo wa pesa. Ni akheri umuuzie hiyo connection.
Kwa wale wasiojua ni kuwa siku hizi kupata kazi ni mpaka uwe na pesa, hiyo ni biashara inayoendelea mjini. Na haijaanza Leo wala jana. Hilo watoto wa mjini wanalifahamu vizuri tuu.
Kuuza connection ya kazi ni Sawa na kuuza ramani ya nyumba. Hakuna kitu cha Bure. Mwambie mtu Kama unataka kazi nipe kiasi kadhaa nikupe kazi.
Mfano; kazi hii Mshahara wake Kwa mwezi ni Tsh Milioni moja hivyo ili nikupe hii kazi nipe 1M nikupe connection, hataki muache apite kushoto.
Au kijana anahangaika anatafuta kibarua chochote anakulilia shida, wewe usimuonee huruma machozi yake au anavyolalama. Mwambie kuna kazi ya laki tano, nipe laki tano nikupe connection ukafanye kazi. Masuala ya burebure mwambie huna.
Unajua KAZI Kama haujaitolea jasho kuitafuta huwezi kuithamini.
Uza kazi
Uza michongo
Uza ramani ya maadili
Hakuna kutoa burebure. Utanishukuru na hata unayempa hiyo connection atakushukuru.
Kijana ukimpa kazi anadhani uliipata kirahisi. Hiyo ndio mindset ya Vijana wengi ilivyo.
Kwanza kijana akikuambia umtafutie kazi ukamkubalia Kwa akili yake ameshachora Aina ya kazi na Mshahara ambao anautaka. Hivyo kitendo cha kumuambia umepata kazi roho yake itafurahi lakini utakapomuambia kazi gani na Mshahara wake wengi hunyong'onyea.
Na wengi wanaweza kukubali kishingo upande.
Elewa kuwa wakati huyo kijana unayemtafutia kazi hiyo akinyong'onyea Kwa kutoridhishwa na kazi na Mshahara huo, kuna kijana mwingine ambaye hamna mahusiano ya karibu anayekuambia umpe kazi hiyo na yupo tayari kukupa hata PESA Kwa ajili ya kazi hiyo.
Wewe Kwa vile unampenda nduguyo unaacha pesa unampa kazi alafu baada ya mwezi Kuisha anakuambia au unasikia ameacha kazi.
Hiyo inaitwa Shukrani ya Punda
Hajui anapoacha kazi anavunja uaminifu wako na boss wa hiyo Ofisi au Kampuni.
Yeye hajui na hataki kujua na anahaki ya kufanya hivyo Kwa sababu kila binadamu yupo Kwa ajili yake mwenyewe. Wewe ndio ulikosea kumpa kazi na connection mtu ambaye hanamsaada wowote na wewe. Ni Bora ungemuuzia hiyo kazi ili hata akiacha kazi basi uwe umepata chochote.
Haya unakuta mtu hajasoma lakini anchagua kazi, anataka kazi ya ofisini au Hotelini. Unamuambia hizo kazi zinahitaji vyeti yaani waliosomea, anajisikia vibaya.
Sasa unahitaji kazi nzuri na haujasoma unaakili Kweli?
KAZI nzuri zinahitaji walau elimu ya Diploma au Shahada.
Haya imetokea KAZI ya ofisini au hotelini umeunganishiwa lakini unaambiwa Kwa vile wewe haujasomea hayo mambo na hauna taaluma hiyo utalipwa nusu ya Mshahara wa waliosomea. Ati unajisikia vibaya.
Elimu inaongeza value ya mtu mahali pa kazi.
Hata kama utafanya majukumu yaleyale kama afanyavyo mwenye elimu lakini kamwe hamuwezi kulingana.
Kwa hasira unaacha kazi, unamgharimu aliyekutafutia na kuonekana anaakili za kipuuzi kama zako.
Taikon huwaga nashauri, hakikisha mtu anagharamia Kwa jasho na damu kupata nafasi unayoenda kumpa. Hiyo inajenga nidhamu na heshima ya kazi.
Lakini ukimpa kirahisi rahisi naye atafanya na kuacha kirahisi rahisi.
Hata Mungu ndivyo afanyavyo, hawezi kukupa kitu kirahisi rahisi ili ukidharau na kukiona hakina thamani.
Kijana akikuambia umtafutie kazi labda Kwa vile anakuona upo katika nafasi Fulani au Kampuni Fulani mwambie hakuna nafasi na huna huo muda wa kutafutia watu kazi.
Ila Kama itatokea utamuambia. Ikitokea mwambie akupe pesa kiasi Fulani umuunganishe, kama Hana mwambie huna msaada wowote kwake.
Uza kwingine.
Hivyo ndivyo Dunia ya sasa ilipofikia, na hivyo ndivyo tunapaswa kuishi.
Elewa mambo haya,
Wewe sio mungu wao, na wewe sio Baba Yao uliyewazaa hivyo hakuna popote utakapolaumiwa.
Watu tujifunze kujipigania, tujifunze kupambana wenyewe bila kumtegemea yeyote.
Ogopa watu wanaolialia wakiomba msaada. Ni hatari Sana.
Ogopa watu wenye lawama. Hao ndio hatari zaidi.
Mfano mzuri ni kijana Jackson majaliwa, alijitoa mhanga kuokoa Maisha ya watu wengine kwenye Ndege, sio Taaluma yake kuokoa watu lakini alifanya tuu bila kutegemea chochote, lakini hiyo ndio gharama aliyolipia na anachokipata ni sehemu ya malipo.
Unamtafutia mtu kazi mtu anayelala nyumbani anaangalia Series za kikorea au anayecheza PS unategemea nini?
Ni Bora umpe Bodaboda au anayeuza machungwa ambaye amekuomba.
Hawa vijana wanaochagua kazi ni wakuwakimbia au kuwafanyia biashara tuu
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam