Kamati Teule ya Richmond ilitumia sh 400 milioni?!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati Teule ya Richmond ilitumia sh 400 milioni?!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wazalendo halis, Oct 31, 2009.

 1. W

  Wazalendo halis Member

  #1
  Oct 31, 2009
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania ni Nchi na sio NGO

  Kamati ya bunge ya kuchunguza kampuni ya kufua umeme, Richmond, ilitumia kiasi cha shillingi za Tanzania zisizopungua millioni 400.

  Vyanzo vya uhakika kutoka hazina vimethibitisha kuwa, kiasi hicho kikubwa cha pesa za wakipa kodi zilitumika kwa kusudi la kuwezesha uchunguzi makini na kamilifu ili haki iweze kutendeka.

  Baadhi ya maofisa wa serikali wamesema wanashangazwa sana na habari kuwa, baada ya kutumia pesa hizo zote, kamati hiyo ilishindwa kukabidhi vithibitisho kamili kwa wakati mmoja na badala yake, wanasema leo kuwa walificha vielelezo ambavyo wameanza kutoa katika vyombo vya habari.

  Wataalamu wanasema, hatua hii ni kinyume cha sheria kwa sababu vithibitisho vyote ni mali ya bunge iliyoagiza uchunguzi huo, na kwa wanakamati kutokabidhi nyaraka zote ni ishara kuwa walishindwa kukamilisha kazi waliopewa.

  Pia, hatua hizi zinaonyesha kuwa, wanakamati walikuwa na agenda binafsi kwa kuchagua kipi cha kuorodhesha na kipi cha kuficha.

  "Duniani sehemu zote, ukikabidhiwa kazi ya uchunguzi wowote na kilipwa kwa kazi hiyo, unatakiwa kukabidhi yote uliyoyathibitisha. Kushikilia vielelezo kadhaa ili uje kuyatoa kwa sababu zako binafsi ni kosa kubwa na kamwe haiwezi kuhalalishwa kwa kigezo cha maslahi ya umma," alieleza mtaalamu na kuongeza kuwa, kama maslahi ya umma yangezingatiwa, basi ripoti kamili ingetolewa wakati huwo wa kuwasilisha ili maamuzi kamili yachukuliwe.

  Malumbano ambayo hayana tija kuhusu suala la Richmond na ambayo yanaendelea kupoteza wakati na akili za watanzania leo yamekithiri katika vyombo vya habari. Wakati nchi inaelekea uchaguzi, badala ya kuweka kipaumbele kuzungumzia habari zinazowasumbua wananchi kama huduma za elimu, afya n.k, vyombo vya habari vinaendeleza poroja za wanakamati wa Richmond.

  Wanakamati hao wanatakiwa kushtakiwa kwa kushindwa kukabidhi vielelezo vyote vya uchunguzi walioufanya kwa pesa za wananchi. Kwanza, hawakuwatendea haki wananchi kwa kutumia hela hizo zote na kutokamilisha ripoti yao. Pia, eti walishikilia vielelezo hivyo ili waje watoe baadae. Je sababu ni nini? Ili kuwasaidia kisiasa? Hapo hawajawatendea haki wananchi.

  Pia, kuzitoa habari walizopata kwa kutumia pesa za umma kwa vyombo binanfsi vya habari ni kosa la jinai.

  Wasomi wanasema milioni hizo 400 zingeweza kununua genereta na wananchi wasingeendelea kuwa gizani leo. Kwa uzembe wa kamati hiyo, wananchi wako gizani kwa kutokuwa na umeme leo, na pia wako gizani kwa kutojua ukweli kamili wa waliyojia katika ufatiliaje kamili wa Richmond.
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Oct 31, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  So what?...
  Ama kweli Mafisadi huja na mbinu za kila aina...
   
 3. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #3
  Oct 31, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Mkuu,

  You cannot convince me niamini ulichoandika... Milioni 400 (tena za kitanzania) haziwezi kuliokoa taifa katika mgawo unaoendelea sasa!

  Jaribu kuja kivingine, katika hili nadhani siafikiani nawe. Kajue tunalipa kiasi gani kwa siku kwa IPTL ili ujue kuwa milioni 400 ni pesa kidogo sana, na kwakuwa ilikuwa ni kwa ajili ya kamati (si Mwakyembe binafsi) basi pesa hiyo ni muafaka kabisa kwa kazi iliyofanywa kwani wali-print vitabu ambavyo walivisambaza bungeni na wote tuliweza kuona nakala hizo na pia waliweza kuja na viambatanisho kadha wa kadha.

  Kama sijakusoma vema kumradhi lakini sijashawishika!
   
 4. O

  Ogah JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  umewashtukia eeh..........wanatumia every possible opportunity ku-blanket mabaya yao.....duhh
   
 5. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tena waambie siyo viambatanisho tu wengine walisafiri hadi marekani. Watanzania tunakubali kazi ya mwakyembe na wenzake. Fisadi anza upya au achana na ufisadi wadanganyika tunawafahamu sasa hatudanganyiki tena
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hahahaha

  wewe Wazalendo halisi, umefulia na hadithi yako hatuitaki.
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Oct 31, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  ..sasa ndiyo maana "wajasiramali" wanapigana vikumbo kuingia bungeni.

  ..hizi Tume za Uchunguzi za serikali na bunge ni mzigo mkubwa kwa walipakodi wa nchi hii.

  ..halafu unakuta Tume nyingine zinafanya kazi kwa kujirudia-rudia. tumekuwa na Tume karibu nne za kuchunguza mikataba ya Madini ukianza na ile ya Dr.Kipokola, Gen.Mboma sijui Brig.Mangenya, then ya Laurian Masha, na mwisho ya Jaji Bomani.

  ..kwenye nchi za wenzetu siasa na ubunge ni kazi za wito na kujitolea. hapa kwetu Tanzania Ubunge ni nafasi ya kutajirika kwa malipo yasiyoendana na ubora wa kazi, na hali halisi ya uchumi wa nchi yetu.

  ..ukichanganya haya madubwana yote ya ununuzi wa mashangingi, gharama za ajabu-ajabu za Tume za uchunguzi, malipo ya kustaajabisha ya kuwahudumia viongozi wakuu, safari za Raisi zisizokuwa na maana yoyote kama kwenda "kujitambulisha" Marekani, malipo mara mbili-mbili ya wabunge na maofisa wa serikali, etc etc unaweza ukakuta tuna ma-IPTL, ma-Richmond, au ma-Dowans kibao.
   
 8. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #8
  Oct 31, 2009
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Lakini mkuu milioni 400 ni lundo la hela, kwa kazi gani hasa walioifanya? Wakati mwingine hawa vinara wetu wa vita dhidi ya ufisadi wanajipiga bao mwenyewe. Milioni 400, posho mbilmbili, ebo!

  Alishatuasa Katibu Mkuu wetu Dk Slaa kuwa hii vita dhidi ya ufisadi inahitaji sifa moja kubwa, nayo ni: unyoofu. Sasa hawa wenzetu kila siku wanapoteza sifa za kuwa majemadari wa vita hii. Tutayajua mengi huko tuendako!
   
 9. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sisi tuliwahi kusema kuwa mambo kama haya Tanzania ni lazima tutajua mkweli ni yupi
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Sadly, majority ya hao makamanda wa vita ya ufisadi hawako kwenye unyoofu!!!

  Kinachouma posho zenyewe ni shilingi ngapi jamani? si warudishe tu na kusema hawakujua yaishe... waweza kuta ni sh 90,000 kwa siku zinawachafua milele

  naumia roho!!!!!
   
 11. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #11
  Oct 31, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Mkuu,

  Nakiri ni kubwa kwa kulinganisha na hali ya maisha ya mtanzania. Lakini mkuu unajua JK anatumia kiasi gani kwa mavazi tu kila mwezi? Uliza uambiwe, unaweza kuibamiza pc yako hivihivi!

  Unakumbuka ofisi ya Waziri Mkuu ilikuwa imetengewa kiasi gani kwa ajili ya fenicha tu? Bajeti hiyo ni ya kila mwaka kumbuka...

  Hii ya kina Mwakyembe as long as ilionesha outcome kwenye public bado naweza kusema ni afadhali. Tena, mwanzisha hoja anasema walipewa Mil 400, ana uthibitisho kuwa hakuna masalia ya kiasi chochote? Manake tusiangalie upande mmoja wa kupewa bila kuangalia marejesho.

  Natambua kuwepo kwa mpango wa kuhakikisha 'kina Mwakyembe' wanashindwa kwa gharama zozote, udhaifu wao kupokea posho ambazo hawakujua zingewageukia ndo unawagharimu kwa sasa!

  Am not 'pro Mwakyembe' and at the same time am not 'pro Lowassa'!
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu,

  wote ni hao hao, si ndio wanapitisha bajeti jamani ??????????
   
 13. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #13
  Oct 31, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Mi nadhani hata Zitto hapa anapata ujumbe kwa namna moja ama nyingine... Kila senti ambayo mbunge aliipokea kama bakshishi (kama yeye ni mwiba kwao) basi ajue ataulizwa ilitumikaje!

  Sina imani na gia wanayoitumia 'wapiganaji ndani ya CCM' lakini siamini kama namna hii ya kuwashughulikia kabla ya kushughulikia kile kilichopendekezwa ni njia sahihi.

  Hivi hizi posho huwa wanazisaini? Manake hapo traces zitakuwepo tu, hajikwamui mtu
   
 14. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Interesting how u trying to protect hosea with reference to the 1971 act...enhe endelea kutudanganya kama hatujui resources and powers of takukuru if used properly ........kweli mwakyembe akae chonjo kwa mwendo huu hivi iyo kamati alikuwa pekeyake na aliiunda mwenyewe??...naona mambo si mchezo...the more you guys bring up these silly arguements mara alichukua 400mil ,mara hana influence or power in kyela, mara conflict of interest, mnamwongezea umaaarufu tuu.....richmond created mwakyembe, he is a victim of circumstance..deal with richmond na umaarufu wa mwakyembe utaisha..zaida ya ile kamati nothing else separates him from other ccm wabunge..no way 1 man can shake such a big group of individuals..its a shame...all this while the country is in darkness..let me guess lets blame mwakyembe for our power issues in the country??
   
 15. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #15
  Oct 31, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160

  Mkumbo, usiingie mkumbo please. Ni kweli kamati ilitumia 438m tshs kwa kazi ile. Lakini sio kweli kuwa kazi ile haikuwa na tija. Kuna makosa fulani fulani ikiwemo kutomhoji Lowasa ambayo itatugharimu sana siku si chache zijazo, lakini ukipima mapungufu hayo na faida unaona kamati ile ilifanya kazi. 438m tshs hazimalizi mgawo na haina maana walipewa kina Mwakyembe mfukoni - kuna nauli za safari humo nk.
  Tutafanya dhambi kubwa sana iwapo tutaingia mtego wa kuona kazi yote ile haina thamani. Kazi iliyoangusha serikali nzima? Jamani!

  Hata hivyo, ni vema Kamati itwambie bila kumung'unya maneno na kwa vielelezo RICHMOND ni nani? Nilishtuka juzi Dkt. Mwakyembe alilitaka gazeti la Mtanzania litwambie Richmond ni nani. Hapana. Kamati ndiyo ilipaswa itwambie maana tuliwalipa watwambie hivyo na sio magazeti. Mnakumbuka Lowasa alisema alipokuwa anajiuzulu 'put it on the table, who is Richmond'

  Pili, kuna suala la gharama za Richmond ambapo tunaamini kuwa gharama za mradi ule ni 172m usd. Hii imerudiwa kweli kweli. Serikali ilisema Richmond hawakuchukua hata senti tano. Sisi kwenye Kamati ya Mashirika ya Umma tulipopitia hesabu za TANESCO zinazoishia Disemba 2008 tulikuta kuwa RICHMOND/DOWANS walilipwa advance ya 30m usd kwa makubaliano ya kuzilipa kutokana na makati ya umeme watakaouza. Walipoanza kuuza umeme wakaanza kukatwa na mpaka tulipovunja mkataba ule na DOWANS zilibaki 8m usd hazijalipwa.

  Wiki ijayo ni lazima tuelezwe tunapataje pesa hizi maana dowans tumeshavunja mkataba kabla ya kumaliza deni letu (pamoja na deni la 4m usd kama faini ya kuchelewa kuzalisha umeme). Hizi 12m usd tunazipataje. Haya ndio mambo ya msingi sana kwangu katika mjadala huu wa wiki ijayo.

  Gharama zilizotumika na kamati kufanya uchunguzi zina value for money. Zoezi lile pamoja na mapungufu hayo madogo ya juu limeleta nidhamu serikalini sana. Tusibeze kazi ile jamani.
   
 16. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #16
  Oct 31, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  You nailed it Zitto!

  Kamata tano...
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Oct 31, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Nashukuru sana mkuu

  kwasababu waswahili wanasema chovyachovya humaliza buyu la asali!!! hii ndio haswa maumivu yangu!!!

  Hii tabia ya posho mbili ipo kila mahala, tuimalize halafu tupambane kiume towards clean house
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nafikiri tuendako tunahitaji Zero tolerance. Kuna mafisadi na vifisadi.

  Ukimchunguza saana Mwakyembe utagundua kuwa kama angelipata nafasi nzuri, mhhhh.........

  Kwa habari ambazo mie nimeshazisikia tayari ambazo mwakani zitaanikwa hadharani wakati wa uchaguzi, jamaa si mzuri kiasi hicho.

  Hivi kwa nini asingelikuwa ni MFANO WA KUIGWA kama alivyo Dr. Slaa? Kwani anashindwa nini kuwa msafi na hasa ukichukulia alisoma sheria? Kuna vitu anajiingiza kichwa kichwa hadi unamhurumia. Wengi wanamkubali Mwakyembe kwa uwezo wake mkubwa na kama asingelikuwa na papara na akawa ametulia, sasa hivi angelikuwa kashamziba hata Dr. Slaa na nafikiri ndani ya CCM angelikuwa tishio kubwa sana na siyo sasa kila siku yuko busy kujibu mapigo. Mara huku umeme wa upepo, mara kateka watu, mara kagombanisha watu mara kagombana na mkuu wa Mkoa, mara kagombana na madiwani mara kaficha data za bunge..... Mara moja, mbili sawa ila sasa inakuwa too much hadi mtu unaanza kuamini kuwa huyu na yeye mhhhhhhh......

  Ila nashindwa kufahamu kuwa hawa watu wa tume, walichaguliwa wale ambao pia wana makosa? Maana wao inakuwa rahisi sana kuwatisha (tishia ya Hosea) kuwa "mkinitenda, ntakutendeni...." Alipomparamia RA, alipigwa kishock cha umeme kidogo tu, akawa akilalamika kila sehemu. Ukweli ukabaki wazi kuwa alitumia data alizozipata kwenye utafiti na yeye akataka kuanzisha kampuni ya kuzaa umeme wa upepo ili na yeye afyonze. Mtu mwenye mapenzi ya nchi yake, lazima angelifahamu kuwa swala la energy, inabidi libaki mikononi mwa nchi milele na hasa kwa nchi masikini.
   
 19. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #19
  Oct 31, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Nimepata ujumbe wako kaka.
  Nimejiweka kwenye uchunguzi na niko tayari kuwajibika katika hili. Chama changu CHADEMA kimeamua kuweka hili kama ajenda ya kikao kijacho cha kamati kuu ambapo wabunge wote wa CHADEMA wameagizwa kuhojiwa na TAKUKURU na yeyote atakayekutwa amejichotea posho hizi zisizohalali kwanza arejeshe na pili awajibike.
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Oct 31, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160

  Zitto,

  YOu just dont know how much relief you give to ordinary peasants like me!!!! we are dreaming of a fair life!! you just dont know!!

  Kama machozi yetu yangeweza kuweka nchi yetu sawa basi na mimi ningesema nimejenga chi hii!!!

  tuwajibike wherever we are, tusaidie nchi yetu

  Big up to you and all who are for this country [kikweli]

  .....poleni yanga pia!!!!!!!!
   
Loading...