Mwenyekiti anajipa maelekezo mwenyewe kwanini asifanye maamuzi juu kwa juu!?
Sambamba na hilo mabadiliko yaende sambamba na kung'oka kwa waziri wa fedha

Niliwahi kuuliza uwezo wa huyu mwenyekiti kupambanua mambo nikaambiwa nawachukia wanawake.
Mwigulu ana makusudi yake dhidi ya huyu mama asiyeelewa kinachoendelea.
Nilifungua Uzi kumkumbusha ujanja wa Mwigulu kutaka yeye achukiwe wapambe wakaja juu. Mwigulu ni jipu changa likiiva litapasuka na Mtu.
 
CCM inayoongozwa na Samia imeitaka Serikali ya Samia kusikiliza kero la tozo linalolalamikiwa na wanachi ili iweze kulitatua.

Kwenu studio.
Drama kubwa.

Ina maana moja kubwa kwamba wanatengeneza tatizo ili walitatue kwa minajili ya kuongezea kwenye CV.

Kwa nini CCM isiamue kumtaka rais avunje baraza lake la mawaziri na kumtaka kuubda Baraza jipa litakalokuja na majibu ya kero za wananchi?

CCM hii imekosa kitu kinaitwa Damage Control mechanism
 
Ripoti ya voda imewashtua

Walikua hawaamini kuwa tozo haikuwa sahihi.

Sasa tusikilizie mabenki.

Maamuzi yenye kuligharimu Taifa.

Kama ingekua ni pengine wanaita Professional negligence.

Unatoa ushauri ambao unaleta hasara.

Mambo kama haya yakifanyika wananchi wa kada zote washirikishwe.

Na sio mtu anakaa ofisini kwake na kompyuta anaandika jambo lake anakusanya marafiki wachache anadai wananchi wameshirikishwa.
 
Kuna jamaa aliwahi kumpiga kibao Rais wa awamu ya pili itakuwa alijiuliza mambo mengi sana juu ya nchi yake hadi kufikia maamzi hayo sasa ndo hawa jamaa wanatuona watanzania kama mazombie flani hivi.

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
CCM inayoongozwa na Samia imeitaka Serikali ya Samia kusikiliza kero la tozo linalolalamikiwa na wanachi ili iweze kulitatua.

Kwenu studio.
Hizo tozo zimekuwa shubiri pamoja na ukweli kwamba mama anahusika kuzibariki lakini tunajua pia waziri Mwitozo anahusika sana pale wizara ya fedha kuwawekea watanzania wenzake tozo kama vile hajui ugumu uliopo tukiwa na tozo nyingi kiasi hiki.
 
CCM inayoongozwa na Samia imeitaka Serikali ya Samia kusikiliza kero la tozo linalolalamikiwa na wanachi ili iweze kulitatua.

Kwenu studio.
Serikali ya Rais Samia Suluhu ni sikivu sana kama alivyowasiliza wananchi kuusu bei ya mafuta
 
Hizo tozo zimekuwa shubiri pamoja na ukweli kwamba mama anahusika kuzibariki lakini tunajua pia waziri Mwitozo anahusika sana pale wizara ya fedha kuwawekea watanzania wenzake tozo kama vile hajui ugumu uliopo tukiwa na tozo nyingi kiasi hiki.
Tozo kwa maendelo ya jamii me sitamani itolewe ibaki tu
 
Back
Top Bottom