Rais Samia kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa visiwani Zanzibar leo

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,334
9,755
Ndugu zangu Watanzania,

Fanya shughuli mapema na kwa haraka sana huku macho na masikio yako yakitegwa na kuelekezwa visiwani Zanzibar ambako Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu ambaye ndiye mwenyekiti wa CCM Taifa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nuru ya wanyonge, nyota ya matumaini ataongoza kikao cha kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM Taifa leo Jumatatu januari 15 visiwani Zanzibar.

Ikumbukwe ya kuwa vikao vya CCM ndio hutoa muelekeo wa nchi na mustakabali wa mambo mbalimbali hapa nchini. Ndio vikao ambavyo hufuatiliwa na vyombo vyote vikubwa Duniani kwote kutokana na umuhimu wake. Ni vikao vilivyosheheni vigogo na watu wazito hapa nchini. Ni vikao ambavyo hata sisiminzi hutulia na kuacha kukatisha eneo husika.

Tutarajie mambo makubwa na mazito na yenye maslahi kwa Taifa letu kutoka katika kikao hicho. Tutarajie mtetemeko na mtikisiko mkubwa kwa watu, kwa kuwa ndio vikao pekee vya CCM ambavyo matamko na maazimio yake huchukuliwa na kuheshimiwa na watanzania tofauti na matamko ya vile vyama vinavyopigania maslahi yake binafsi na matumbo yao kama ilivyo kwa genge la CHADEMA.

Kaeni kwa kutulia maana CCM Ndio wenye kutoa njia na mstakabali wa Taifa letu. Ndio wenye kutoa muelekeo sahihi wa kila jambo, ndio wenye kuongoza mambo nyeti na muhimu kwa njia iliyo sahihi, ndio wenye uchungu na maisha ya Watanzania, ndio wanaojuwa wapi Taifa hili linapaswa kuelekea na kupita, ndio wanaojuwa vyema watanzania wanahitaji nini na kwa wakati gani na kiasi gani. Ndio maana wakati wote huzungumzia lugha za Watanzania na kueleweka kwa urahisi na wepesi.

Mpaka sasa vyombo vya kimataifa na waandishi wake mahili na wenye uzoefu wanaendelea kumiminika na kufurika kwa wingi visiwani Zanzibar ili kuijulisha Dunia kitakachojili kutoka katika kikao hicho. Usalama ni wa kutosha ambapo hata sisiminzi wanalindwa wasikanywagwe.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Naona unatafuta Connection za wakubwa wa CCM. Na namba umetuwekea ili wakuone unaupiga mwingi kama Mama. Siasa za njaa ndizo zinatuponza mnasifia hadi mnaboa, uchawa hadi sio vizuri yote kujali maslah ya matumbo yenu binafsi ndio maana taifa halisongi mbele.

Ebu tuishi kwenye uhalisia, inasikitisha kizazi cha vijana kama wewe bado tunaishi kwenye mifumo hiyo... Nchi itazidi kuhangamia 0787 56 24 66.
 
Bila shaka yawezekana katibu mkuu mpya kutangazwa hivi leo🔥,

Subira yavuta kheri, twawatakia kikao chema cha kamati kuu ya halmashauri kuu Taifa.
 
....Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
hakika amewajaza wanyonge mahela mifukoni na sasa wanamudu kununua sukari Tshs 5000 kwa kilo.

Wanyonge sasa wanatibiwa bila kuhofia gharama kubwa za matibabu kwa sababu mama amewafikia na kuwajazia fanaka kwenye akaunti zao.

Wanawake wajawazito wanatetemeka nchi nzima kwa furaha kwani wanapata huduma bure za uzazi salama.

Hakika tunatetemeka nchi nzima kwa uhakika wa Umeme na maji.
 
Aliletwa Barbacar Sarr nchi haikutetemeka ije kuwa kikao cha mzanzibar. Acha masihara, unashitua watu bana
 
bilashaka,
yawezekana katibu mkuu mpya kutangazwa hivi leo🔥,

subira yavuta kheri,
Twawatakia kikao chema cha kamati kuu ya halmashauri kuu Taifa.
Kwa hakika Ngoja tuendelee kuwa wenye subira maana CCM Ndio Tumaini la watanzania na ndio chama chenye kutoa muelekeo na Dira kwa Taifa letu.
 
Aisee ukiwa chawa huna tofauti na wale wafungwa wa kizanzibari waliokuwa wanafanyiana mambo ya kisengerema mbele ya wafungwa wenzao bila aibu
 
Aliletwa Barbacar Sarr nchi haikutetemeka ije kuwa kikao cha mzanzibar. Acha masihara, unashitua watu bana
Watanzania mpaka sasa baada ya kupata taarifa ya kufanyika kwa kikao hicho wameshaanza kupeana taarifa mitaani kwa kasi ya mwanga ,maana kila mtu anajuwa ukubwa na unyeti wa vikao vya aina hiyo na mambo mazito ambayo hujadiliwa .
 
hakika amewajaza wanyonge mahela mifukoni na sasa wanamudu kununua sukari Tshs 5000 kwa kilo.

Wanyonge sasa wanatibiwa bila kuhofia gharama kubwa za matibabu kwa sababu mama amewafikia na kuwajazia fanaka kwenye akaunti zao.

Wanawake wajawazito wanatetemeka nchi nzima kwa furaha kwani wanapata huduma bure za uzazi salama.

Hakika tunatetemeka nchi nzima kwa uhakika wa Umeme na maji.
Serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais Samia imefanya mengi makubwa na ya kugusa maisha ya watanzania ambao kwa sasa wamejaa matumaini ya kutimiza ndoto zao katika vifua vyao.hasa baada ya serikali yao kuweka mazingira wezeshi kwa kila mtu mwenye kufanya kazi kwa kujituma na kwa bidii kuweza kufikia malengo yake.
 
Ila mwanangu we ni chawa njaa kinyama alafu una tabia za kike
Acha ujinga wewe.nakuletea taarifa inayogusa hisia za watanzania halafu wewe unasema nina njaa. Nani kasema hapa jukwaani ndio jikoni au mezani kwa kila mwenye njaa kupata chakula.
 
Back
Top Bottom