Kumbe ukiona haya mamtu yenye sura mbaya yamekimbilia upolisi yameenda kutimiza azma yao ya ubaya na ujambazi bwana eeh!!. Muwe makini ndugu zangu kila kitu kimeshaharibika, ukikutana na haya majambazi pasipo na mtu porini kimbia kama una usafiri. Nimeshashuhudia uporaji unaofanywa usiku wakiwa wenyewe au wakiazima silaha majambazi.Last I checked, Kamuhanda kasema anakaribia kustaafu na pia amepokea maagizo toka ngazi fulani za juu kuwathibiti CHADEMA (read at all costs).
Elimu sifuri, maadili sifuri hao ndio polisi wa Tanzania. Hasara wanazosababisha tunaziona na kupata machungu sana. Kikwete akitaka kujua anavyodharaulika si tu na wananchi abali hata na watendaji wake athubutu kuangalia mtiririko wa matukio ya hivi karibuni. Tokea mwezi wa sita lile tukio la Dk Ulimboka hadi jana hili la Mwangosi, ni unyama, uhuni na kutotii sheria. Nchi ilishamshinda ila kwa vile hakuwa na exit plan basi ana hang-around!
wamlete mbeya apate joto ya jiweJina la Michael Kamuhanda nilipolisikia tu nilihisi kama nimewahi kulisikia tena siku si nyingi. Nina uhakika na wengine wamelikumbuka pia k Natamani wamlete Dar-es-Salaam pia ili watu waelewe tatizo tulilonalo. Nikimuita ni mhalifu sijui kama nitakuwa nimetia chumvi sana... haiwezekani ndani ya mwaka mmoja kamanda unasimamia mauaji ya raia kisa wanataka kuandamana tu! Hivi hana mbinu nyingine zozote kichwani mwake zaidi ya kuwa trigger
happy!
Poleni watanzania wenzangu. Huku USA hali ya Democrasia imekuwa kwa kiasi kikubwa na hivi hayo ni yakawaida pindi yanapotokea. Lakini huko nyumbani ni matatizo matupu. Ila ndio tupo katika kipindi cha mpito. Yote hayo yatapita na tutakomaaa tu. Ila kwa hili Kamhanga yupo sahihi katika kutekeleza majukumu yao. Kumbuka Dola wana kwenda kwa amri tena amri ya mwisho ndio mara zote hufuatwa. Tatizo la baadhi ya Watanzania hawataki kukubali ukweli kwamba kuna wakati ukifika yapasa kutii dola. Mimi sijaona sana sababu ya M4C KUSHINDANA NA DOLA. Serikali ikisema yatupasa kusikiliza. Tukileta ubishi madhara yake ndo kama haya. Wenyewe wanasema "UTII WA SHERIA BILA KUSHURUTISHWA" Kwa kuwa hatutii sheria na sasa tunashurutishwa na kwenye kusurutishwa kunakuwa na matokeo mabaya ndo hayo sasa. Tujifunze kutii dola na si kulazimisha mambo. Poleni!
Jina la Michael Kamuhanda nilipolisikia tu nilihisi kama nimewahi kulisikia tena siku si nyingi. Nina uhakika na wengine wamelikumbuka pia kuwa ndiye aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Ruvuma ambapo mapema mwaka huu (Februari) wananchi 4 waliuawa napolisi walipokuwa wakijaribu kuandamana kwenda ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Natamani wamlete Dar-es-Salaam pia ili watu waelewe tatizo tulilonalo. Nikimuita ni mhalifu sijui kama nitakuwa nimetia chumvi sana... haiwezekani ndani ya mwaka mmoja kamanda unasimamia mauaji ya raia kisa wanataka kuandamana tu! Hivi hana mbinu nyingine zozote kichwani mwake zaidi ya kuwa trigger happy!
Tatizo wanavuta sana bangi hawa....
Sitoshangaa kwani hata wakati wa Mkapa wale waioua Zanzibar walisifiwa kwa "kazi nzuri" na wengine kupandishwa vyeo.Mkuu Mwanakijiji Polisi ya sasa,hii ya kutenda kazi kwa kutotumia weledi bali kwa lengo la kujipendekeza kwa chama tawala haitashangaza kuona Kamuhanda safari hii akapandishwa cheo c kuhamishwa mkoa tena
Hayati Daud Mwangosi siku ya tukio akiwa kazini mwenye suruari nyeupe na ameshika camera mkono, hakujua kama mauti yatamfika tena kwa unyama kama ule.
INGEKUWA zamani Nyerere angekemea uovu huu wa polisi na kuamru watafute njia mbadala za kukabiliana na waandamanaji wasio na silaha yoyote.unajua wakati wanakabilianana waandamanaji hawachukui tahadhari ya kulinda mabomu yao yasifyatuke.
Polisi wanafanya wanachokijua kwa kuwa hakuna mahali wanapowajibika...
Hiyo ndiyo kazi waliyoelekezwa kuifanya na wanaifanya kwa juhudi zote...
Hakika wamesahau jukumu namba moja la Jeshi la Polisi...
Nalo ni kulinda na kutetea haki za raia dhidi ya waovu na maovu...