Kama wewe unajua kuuza. Biashara ya U MC wa Harusi ndie biashara nyepesi kukupa faida ya milioni 20 kwa mwezi. Kwa mtaji wa mdomo wako tu na suti

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,527
Habari wadau.

Kwenye jukwaa la biashara leo tuongelee kuhusu biashara ya ku sherehesha sherehe.

Ni biashara ambayo watu wengi hawaiwazi. Ila inaingiza hela nyingi sana kama faida.


Unapaswa kuwa mjanja kuelewa biashara yao wanavyoifanya na cost wanazotumia.

Hiyo biashara imejigawa pande mbili yaani upande mmoja Mc na upande wa pili muziki na Dj.

Muziki na Dj huwa unalipiwa pesa around laki 2 mpaka laki 3 kulingana na idadi ya spika.

Ma mc huwa hawana muziki.. hivyo huwa wanakodi muziki na dj.

Ukiona mc umemlipa milioni moja na nusu.. tambua yeye mc kapata faida zaidi ya milioni 1 day tu ,yaani kakodi muziki na dj kwa laki mbili ama tatu kisha kachukua iliyobaki milioni moja na laki 2 peke yake kisa kuongea maneno masaa matatu tu pale mbele.. kuelezea matukio.

Mfano Mc Gara B. Anachaji milioni 3 kwa sherehe.. na kajiongeza mpaka video anafanya yeye.

Unakuta harusi moja anaichaji milioni 3 ya U MC. Na wakijichanganya anawaongeza na milioni 2 kwa ajili ya video. . Yaani siku moja tu anatengeneza milioni 5.

Na hapo unakuta kwa wiki anahudumia sherehe 3 mpaka 4. Mwa mwezi hapo ni sherehe zaidi ya 20.
 
Back
Top Bottom