Misingi 21 Ya Biashara Itakayo fikisha Buashara Yako Hadi Kwa Wajukuu Zako [ MBA YA MCHONGO]

Sharo empress

Member
Jul 29, 2022
13
45
Hello!

Habari za muda huu....

Wazaramo wanasema

"Kidire Mwali"

Kama hujui kizaramo basi fahamu maana yake ni Mwali yuko uwanjani...

Leo ndo ile siku yetu maalumu ya kuanza darasa letu lile la

MBA ya MCHONGO

Misingi 21 ya Biashara itakayofikisha Biashara yako kwa wajukuu zako....

Ukifahamu hii misingi itakusaida sana kwenye safari yako ya Biashara...

Twende sote!

👇🏾👇🏾👇🏾

Leo tutaanza na msingi wa kwanza

1. MALENGO (goals)

Nikupe angalizo moja!

Hapa tunazungumza lugha nyepesi ya kuelewana na kuweza kufanyia kazi...

Tunaposema malengo kwa lugha nyepesi ni hitimisho la safari yako ya Mafanikio...

Malengo ya binadamu yapo kwenye sehemu kuu saba.

1. Uchumi
2. Afya
3. Imani na dini
4. Elimu
5. Mahusiano
6. Uongozi
7. Uhuru wa muda.

Malengo yote ya mwanadamu huzingatia mambo hayo 7.

Hata wewe ukipanga malengo yako ni lazima yatadondokea hapo katika moja ya sehemu 7...

Sisi leo tunazungumza kwenye kipengele cha uchumi hasa hasa kwenye upande wa Biashara...

Malengo makubwa ya Biashara ni kuongeza mauzo kutoka chini kwenda juu.

Ili Kuongeza Mauzo Kwenye Biashara Kuna Njia Kuu 3...

1. Kuongeza bei ya mauzo.

Mfano kama ulikuwa unauzia wateja 50 kwa bei ya buku.

Hapa mauzo yatakuwa 50,000.

Sasa hapa kwa wateja hao hao 50 unaweza kuongeza mauzo hadi 2,000

Hapa mauzo yanakuwa 100,000.

Hii njia ni nzuri lakini inaweza kuua Biashara.

2. Kuongeza idadi ya manunuzi ya mteja.

Mfano kama mteja alikuwa ananunua bidhaa moja kwa buku basi unatafuta bidhaa nyingine ambayo anaweza kununua bila shida.

Mfano unauza mkate unaweza kuongeza blueband.

Au unauza viatu basi unaweza kuongeza soksi.

Hapa unaangalia ni bidhaa gani ambayo inaendana na bidhaa unayouza.

Kaa chini utafakari ni bidhaa gani za kuongeza kwenye Biashara yako.

3. Kuongeza idadi ya wateja unaohudumia.

Mfano kama ulikuwa unahudumia wateja 50 basi unajitahidi kuongeza wateja hadi 100.

Ili kuongeza idadi ya wateja unaweza fanya hivi.

👇🏾👇🏾👇🏾

Hapa ni kufanya matangazo na kuboresha huduma kwa wateja...

Pia kuomba wateja wakutaje kwa ndugu jamaa na rafiki zao.

Pia waambie waje wanunue bidhaa kwako.

Hizo ndo njia kuu tatu za kuongeza mauzo kwenye Biashara yako..

Tukirudi kwenye upande wa malengo!

Malengo Wamegawanyika Kwenye Makundi Makubwa Matatu.

1. Malengo ya muda mfupi

2. Malengo ya muda wa kati

3. Malengo ya muda mrefu.

Je Ni Vitu Gani Vya Kuzingatia Kwenye Kupanga Malengo Yako..

Chukulia malengo ni sawa na safari ya kutoka dar kwenda Moro.

Yaaani Magufuli to Msamvu...

Hivi ndo vitu vya kuzingatia kwenye kupanga malengo yako.

1. Hali yako ya mauzo ya sasa.

Mfano unauza 100,00 kwa mwezi.

2. Ujuzi ulionao kwa sasa kwenye mauzo.

Kama elimu yako ya mauzo ni ndogo basi inatakiwa kuongeza elimu.

3. Watu ulio nao sasa hivi..

Hawa ni watu watakao kusaidia kuongeza mauzo kwenye Biashara yako.

4. Muda gani unataka kukamilisha malengo ya mauzo yako.

Mfano mwaka au miaka 10.

5. Vikwazo gani vya kuepuka ili kufikia malengo yako.

Hakuna safari isiyo na vikwazo.

6. Tambua vitu vyenye thamani ambavyo ukifanya vinaweza kuongeza mauzo ndani ya muda mfupi.

7. Unataka kufikia mauzo ya kiasi gani kwa huo muda.

8. Tumia muda wako vizuri usipoteze muda sehemu zisizoweza kuongeza mauzo.

9. Ifahamu Biashara yako na bidhaa zako nje ndani.

Hii itakusaida kwenye kushawishi wateja.

10. Tumia muda wako mwingi kuongea na wateja kuliko watu ambao sio wateja wako.

11. Jitahidi kuwa na maono makubwa muda wote.

12. Ongeza huduma kwa wateja kwenye Biashara yako.

13. Shirikisha malengo yako kwa watu wako ofisini.

Malengo yasibaki kwenye kichwa chako peke yako.

Hivyo ni vitu muhimu kuzingatia...

SIFA ZA MALENGO!

1. Yawe wazi yaani yaweze kueleweka kwa wepesi.

2. Malengo yanatakiwa kuandikwa.

Usiweke malengo kichwani peke yake.

Fanya kuandika malengo yako...

3. Yawe na uhalisia.
Usiweke malango nje ya uhalisia.

Usiweke malengo ya mauzo ya 100M kwa mtaji wa 10,000.

4. Yaweze kupimika.
Usiweke malengo ambayo hayawezi kupimika kwa muda husika.

5. Malengo yategemee hali ya sasa..

Usiweke malengo nje ya uhalisia wako wa sasa.

6. Yawe na muda maalumu...

Usiweke malengo yasiyo na muda maalumu.
Inaweza kuwa mwaka au mwezi.

7. Weka malengo ambayo yanaweza kutekelezeka..

Usiweke malengo magumu sana mpaka unaogopa kutekeleza.

8. Malengo hayatakiwi kuwa mengi mpaka yakakuvuruga...

Unakuta mtu ana malengo mengi mpaka yanamvuruga..

9. Jitahidi malengo yako yakite sehemu nyeti kwenye Biashara yako..

Hizo ni sifa za malengo bora kwenye jambo lolote...

Tumalizie na mfano hapa chini...

👇🏾👇🏾👇🏾

Mfano.

Sasa tufanye unataka ufike mauzo ya 3,000,000 kwa mwezi( milioni 3) je utafanyaje???

Tumia mbinu hii.

Lakini zingatia kanuni ya 80/20 Rule.

1. Gawanya mauzo ya 3M kwa siku 30.

Kwa siku ni mauzo ya 100,000(laki moja)

2. Gawanya laki 1 kwa masaa ya kazi kwenye Biashara yako.

Mfano masaa ya kazi yakiwa 12 basi utahitajika kuuza 8,500 kwa saa..

3. Tambua idadi ya wateja wako ambao wanaweza kufikia hayo mauzo kwa siku.

4. Usifunge Biashara mpaka ufikie mauzo yao kwa siku.

Fanya hivyo kila siku bila kuchoka.

Kanuni ya 80/20 Rule inasema hivi.

80% ya mauzo ya laki moja yanatakiwa yatoke kwenye 20% ya wateja.

Mfano ikiwa wateja 10 wanaweza kukupa mauzo ya laki kwa siku basi kanuni ya 80/20 itakuwa hivi...

Wateja 2 waweze kukupa 80,000/=

Kwenye Biashara unatakiwa kuzingatia wateja wenye hela nyingi kwa wingi...

Usisahau kuweka malengo yako sawa sawa...

Hapa ili kuongeza maarifa unaweza kusoma vitabu vyenye kuzungumzia kuhusu Malengo.

Kesho tutaendelea na msingi wa pili..

Usikose!

Imeandaliwa na

Pay Less.....
 
Back
Top Bottom