Biashara sita (6) unazoweza kuanza na mtaji wa laki moja tu na ukapata faida kubwa

Ally Nassor Px

JF-Expert Member
May 6, 2022
2,040
2,610
Juzi niliwauliza wanaJF. una mshauri nini kijana ambae yupo mtaani tu hana ajira mawazo yalikuwa ni mengi na ni mazuri pia.

Ila na mimi leo nimeamua kuja na uzi ambao utakuwa na biashara kadhaa ambazo unaweza kuanza nazo kwa mtaji wa laki moja lakini cha kwanza kabisa lazima tujue kuwa biashara yoyote ina changamoto ujiandae kupambana na changamoto itakapo tokea mda wowote ule.

Hapa nitaelezea changamoto za biashara zenyewe na suluhu na jinsi ya kuepeuka changamoto.

Kwanza napenda kutoa maarifa machache sana katika mchakato wa kuanzisha biashara.

Tujifunze katika kutengeneza au kuchambua wazo zuri la biashara swala la mtaji linakuja mwisho kabisa katika hitimisho. Tupende kufanya biashara tunazozipenda kwani katika kufanya biashara unayoipenda kuna ubunifu lakini pia kuna bidii. Mie naamini hata kama biashara yako ni ndogo sana kama punje ya mchele ukiipenda na kuwa na bidii nayo basi biashara ile itafana. Tusikimbilie mitaji hali ya kuwa mawazo mazuri ya biashara hatuna hii ni changamoto kubwa sana, matokeo yake unaweza kupewa wazo bimaana katika biashara hiyo ni ya uhakika katika kupata wateja na wewe utajibweta lengo ni kupata wateja mwisho wa siku unakosa ubunifu na bidii matokeo yake biashara inafeli

Karibu mwana JF forum's.

______________________________
1. BIASHARA YA GENGE

Biashara ya genge ni biashara yenye uhitaji mkubwa sana kwa sababu watu kila siku wanakula.pia biashara unayoweza kuanza kwa mtaji kidogo.

Ni biashara ambayo huhitaji kuwa na eneo la gharama kubwa kuifanyia.Na ni biashara ambayo haina vitu vingi, hivyo unaweza kuisimamia vizuri tu.Hii ni biashara ambayo mtu ambaye hana shughuli nyingine ya kufanya anaweza kuianzisha, akaiendesha vizuri na ikawa sehemu ya yeye kupiga hatua na kuelekea kwenye biashara kubwa zaidi.

• Biashara yako inapaswa kuwa eneo ambalo ni rahisi kuwafikia wateja wako na hata wateja kuifikia pia kwahiyo kwakuwa uachouza ni mahitaji muhimu ya maisha kila siku, biashara itafanya vizuri inapokuwa na mzunguko mkubwa sana wa watu lakini pia hata makazi ya watu yawe kwa wingi maana wanunuzi wa bidhaa hizi ni kina mama wa majumbani kwani wao ndiyo wameshika usukani mkubwa sana wa jiko hata mama lishe pia.

Lakini pia mazingira ya eneo lako la biashara yanapaswa kuwa safi na mazuri.

yamfanye mteja aiamini na kuithamini biashara yako.Wengi wanaofanya biashara ya genge hawaweki maeneo yao ya biashara kwenye mwonekano mzuri, ukifanyia kazi hilo unajitofautisha kabisa na wengine.

Nikirudi katika namna ya uanzishaji kwanza unatakiwa ujue machimbo ya kupata mzigo wa kutosha. Na chimbo kubwa ni masokoni na masokoni utapata bidhaa zote za gengeni.

Andaa na pesa ya usafiri na ubebaji 5000+ au 5000- .

Vifaa vya biashara ikiwemo meza, stuli, kipande cha turubai ikilazimu ama mwamvuli(mabati ndo mazuri zaidi), visu, ndoo, nakadhalika vinapaswa kutoka katika mtaji huo huo. Lakini pia unatakiwa kujua vitu vya msingi na vyenye uhitaji mkubwa katika genge lako mfano Mboga za majani, Vingia mchuzi kama nyanya, carrots, hoho, vitunguu, etc, Viungo vya ziada kama hiliki, mdalasini, swaumu, etc, Matunda kama tikiti, tango, chungwa, papai, parachichi, embe, nanasi, etc, Viazi, nazi, ndizi mbivu etc

•• Njia ya kujua faida ni kuorodhesha hivi vitu katika karatasi ya shopping na uweke idadi. utapita magenge kadhaa na ukifika uliza bei ya vitu hivyo na nakili.

Ukishamaliza hesabu za hapo juu linganisha jumla ya pesa utakayotumia kununulia vitu hivyo kwa bei ulizoona sokoni na jumla ya mapato utayoyapata ukiuza bidhaa hizo.

Tofauti yake huwa ni faida .

Kwa mfano; kawaida sado moja ya viazi linauzwa kati ya 3,000 hadi 4,500 kulingana na sehemu. Lakini katika kupangilia mafungu hauwezi kosa mafungu 9 kwa wastani. Kuna baadhi ya sehemu mafungu hayo wanauza kwa 500 na sehemu nyengine wanauza kwa 1000. Ukinunua sado moja kwa 3,000 ukauza fungu kwa 500 na ukapanga fungu 9 utapata 4,500. Hapa faida ghafi ni 1,500. Nikinunua kwa 4,500 ukipanga fungu 7 na kila fungu ukauza kwa 1,000 utapata 7,000. Hapa faida ghafi ni 2,500. Kwa ufupi katika biashara ya genge katika kila 10,000 utakayoingiza faida chache sana utayoipata ni 2,500. Sasa kazi ni kwako kuangalia sehemu yenye mzunguuko mzuri. Ukiuza bidhaa za 60,000 kwa siku utapata zaidi ya 15,000 faida kwa siku.

CHANGAMOTO

Changamoto kubwa katika biashara ya genge ni mabadiliko ya bei kutokana na kwamba bidhaa nyingi ni za msimu na kwamba zinategemea sana hali ya hewa, lakini jambo jingine ni kodi maana unaweza kupanga sehemu ikawa mlikubaliana kuwa malipo ni elfu 30 kwa mwezi, kwakuwa anaona unauza sana basi figisu zinaanza Mara kodi inapandishwa mpaka elfu 50 kama huwezi beba vyako, lakini pia utunzaji wa bidhaa maana bidhaa nyingi huwa hazikawii kuharibika, pia usafirishaji katika kutoa bidhaa soko kuu kuja katika eneo lako la kazi na mwisho nimalizie katika mikopo hususani kama ni mikopo yenye riba kubwa na muda wa marejesho ni mdogo haswa

SULUHISHO

Katika kutatua changamoto hizi maana kama patakuelemea lakini kuzitatua kwa uzuri ni kule kuwa na mtaji vifaa yaani kwa mfano ukawa na eneo lako nyumbani ambapo linatosha kuweka genge lako, uwe na mtaji wako labda hata elfu 20(lengo kuepusha mikopo), usafiri wako (mkokoteni) na sehemu nzuri ya kuhifadhi bidhaa zako. Lakini yapendeza ukawa mkulima wewe mwenyewe yaani uwe na shamba lako mahususi kwa biashara ya genge

••Kuwa na maono makubwa. Japo unafanya biashara ya genge, kwenye fikra zako usione genge, bali ona biashara kubwa kabisa. ona ukiwa na maduka mengi ya kuuza mahitaji hayo ya msingi na ona ukifanya kwa kiwango kikubwa zaidi.

maono makubwa utakayo kuwa nayo ndiyo yatakusukuma kupiga hatua kubwa.
Pia nipendelee kuwa na bidhaa bora wateja wanaangalia vitu vikuu viwili, •bidhaa bora na

•kwa bei nafuu.

ukiwa na vitu hivyo viwili utajenga imani ya wateja kwenye biashara yako.

Pia uwe na huduma nzuri kwa wateja. hudumia vizuri wateja wako ili waweze kurudi tena na tena.

••Pia uweke mafungu. kutokana na mahitaji ya wateja wako, unaweza kutengeneza mafungu ya vitu vinavyonunuliwa kwa pamoja na kisha kumshawishi mteja anunue kama fungu badala ya kununua kimoja kimoja. Kumsukuma kuchukua hatua, hakikisha bei ya fungu inakuwa na unafuu kuliko mteja akinunua kimoja kimoja. Njia hii itaniwezesha kuuza zaidi kwa wateja ambao tayari unao, ambao ni wateja wazuri tayari.

••Pia uwafikie wateja. usisubiri tu wateja waje, badala yake wafuate kule walipo. Watu sasa wametingwa na mambo mengi wanaweza kusahau kabisa hata uwepo wako. Hivyo tembelea wateja wako maeneo walipo na kuwashawishi kuja kununua.

Pia Kutokana na utandawazi, unaweuza bidhaa zangu kidigitali pia.

_________________________________
1. BIASHARA YA DAGAA WA MWANZA WALE WANAOKAANGWA WABICHI

• Mboga ni kitu cha muhimu na lazima kwa maisha ya kila siku ya kila mwanadamu.

🤔 Utaitumia vipi mtaji wako.

Sado kwa Mwanza utanunua elfu 13000, nauli Mwanza Dar elfu 10000 kwa box. pesa ya nauli kutoka mbezi hadi labda mbande weka 3000+ au 3000- kwa waliopo dar .

Kwa hiyo kwa laki utaagiza sado 6 sawa na elfu 78,000 nauli Mwanza Hadi Dar elfu 10000. Nauli ya kwenda kuchukua chukua box la dagaa elfu 3000 jumla kuu 91,000. Kwa laki nabaki na 7000 hii utanunua bando la buku mbili na vifungashio vya buku 2 inaleta jumla Kuu 95,000. Elfu tano naitunza Kama dharula.

2. Biashara hii utaifanya kwa kutumia status za Whatsapp kutangaza biashara na kwa kufunga za buku buku kutembeza mtaani.

Wateja wako lenga hasa wa uwezo wa kununua nusu sado kwa elfu 10000 na sado nzima kwa 20000. Kwa hiyo hata ukifunga za buku buku hakikisha unapata pack 20+.

Mteja utamuweka wazi kuwa lazima achangie usafiri kwa hiyo Ile dharula ya buku 5 utatumia kwenye delivery ya dagaa door to door in case kunahitajika kupanda daladala. Ambapo ukimfikishia mteja atalipia na usafiri kabisa kwa hiyo narudisha kwenye Ile Baki yangu ya elfu 5.

FAIDA

Faida katika biashara hii itatakiwa kila sado upate faida ya elfu 5000 na kuuza hizo sado sita target ndani ya siku 2 Hadi tatu. Kwahiyo sado 6*20000= 120,000 ukitoa mtaji ambao ni elfu 95000 Babaki na elfu 25000 kujumlisha na ile tano ya dharula utakuwa na mtaji wa 100000 na faida 25000 jumla utakuwa na 125000. Ukiweka muda wa kuagiza kusafirisha na kuuza angalau kwa wiki uagize Mara mbili na kila upoagiza utakuwa unaongeza sado moja kutokana na faida utayopata.

Kwa hiyo Kama wiki ya kwanza utapata 25000*2 =50000 faida wiki moja. Mwezi una wiki nne kwa hiyo Kama utapata faida elfu 50000 kwa wiki kwa mwezi ntakuwa na 200,000 faida maximum (. 50000*4=200000).

CHANGAMOTO YA BIASHARA YA DAGAA.

Changamoto utakayokumbana nayo ni kutoka kwa wateja wakopaji. Hawa wanaweza kufanya biashara ife lakini ili hakikisha biashara yako isife unatakiwa kuwa na kauli nzuri lakini usikopeshe. Hii itapunguza hadara na chuki baina yangu na wateja wangu.

Changamoto ya pili nidagaa kuvunda.

Ukiwapaki wakiwa wa Moto kwenye vifungashio like joto baadae linatengeneza unyevu ambao uanza kutoa fangasi.

-Dagaa kunywea, dagaa waliokaangwa wakiwa wabichi Wana tabia kadili wanavyozidi kukaa hunywea hivyo kama.mzigo hautoki haraka inaweza kusababisha mchuuzi kupata hasara.

SULUHISHO

Njia ya kutatua changamoto ya kucheleweshwa au kutokulipwa kabisa na ili kuepuka ugomvi na wateja wako kuwa muwazi haukopeshi .

•• Ili kutatua changamoto ya dagaa kuoza au kuvunda muandaaji hakikisha dagaa inakaangwa inakauka vizuri, inachujwa mafuta vizuri na kuacha ipoe kabisa ndo upark .mzigo kwenye box.

•• Kuondokana na hadha ya kupata hasara kutokana na kunywea kwa dagaa hakikisha unatafuta wateja wapya kila mara ili angalau.target yako ya kuuza mzigo ndani ya siku 2-3 itimie hivyo utakuwa umepuka hasara.

••Jifunze kuwa na elimu ya customer care.

hakikisha na deal na supplier mmoja kwa kusikiliza mapungufu ya bidhaa yako kutoka kwa wateja na kuongea na supplier kuboresha hivyo kufanya wale wale wateja kuwa mawakala wa wengine hivyo kuongeza idadi ya wahitaji ambayo itaniongezea idadi ya sado unazoziagiza hivyo faida kuongezeka.

- Kutanua wigo wa biashara kwa kuanza kuuza kwa wasambazaji wengine ( kwa jumla jumla) hasa wale wa magengeni na Min Super Market hivyo kuwezesha kuitangaza biashara yako zaidi.

Pia Kutokana na utandawazi, unaweuza bidhaa zako kidigitali pia.
_____________________________________

BIASHARA YA MATUNDA / FRUITS

Biashara ya matunda inafaa zaidi hasa maeneo ya chuo au shule au stand kutokana na muingiliano wa watu mda wote soko uhakika
Mfano matunda ukipata kideli ambacho hakizidi elfu 5 tikiti kama tikiti au nanasi inatosha sana

•Vitu utakavyo takiwa kuwa navyo ni vifuatavyo
Kideli -10000
Kisu- 2000
Magazeti Kama vifungashio -5000
Kijiko-2000
Matikiti-matanox3000
Deli la taka- 15000

Uuzaji wa matunda. utaangalia bei ya wastani ya hayo matunda. Kama unakata na kupanga nami nitafanya hivyo. Mfano; tikiti la elfu 5 sokoni linaweza kukatwa vipande 8 vya 200, vipande 6 vya 500 na vipande 4 vya 1,000. Hii ina maana kila tikiti litatoka vipande 17 vya saizi tofauti tofauti na bei tofauti tofauti na jumla utapata faida ghafi 3,600. ukiweza kuuza vipande 50 kwa siku ni sawa na wastani wa matikiti matatu. Faida itakuwa 10,800 kutoka kwenye matikiti matatu pekee.Bado una maparachichi, mapapai na machungwa. Kiufupi hauwezi kosa 20,000 ya faida kwa siku. Kwa mwezi nitakuwa na angalau 500,000 kwenda juu ya faida.

CHANGAMOTO

••Changamoto ni nyingi ukiangalia hasa upatikanaji wa matunda
Kuoza kwa matunda

••Matunda kutoisha kwa wakati
Usumbufu wa Askari na tozo za ushuru

SULUHISHO

••Kutokana na changamoto hizi hakikisha unakua msafi mda wote ili kuondoa usumbufu wa Askari na bwana afya
Kulipa ushuru kwa wakati kuondoa usumbufu

••Njia ya kupambana na changamoto
Usafi na kauli nzuri kwa wateja pia kuongeza kipato lazima ujenge tabia ya kuwahi kazini ili kuondoa changamoto ya kutomaliza matunda kwa wakati.

•• Kutotegemea wapita njia tu pia kujenga mazoea na wanafunzi na wakufunzi,au makondakta au madereva wa eneo husika ni njia bora zaidi ya kuongeza kipato

Pia Kutokana na utandawazi, unaweuza bidhaa zako kidigitali pia.

_________________________________
BIASHARA YA KUUZA KWENYE MADUMU

Hii biashara inaitaji maeneo yenye mchanganyiko wa watu wengi kama maeneo ya uswahili na maeneo ya pwani wanapoanika dagaa.

Utanunua madumu 10 kila dumu mmoja elfu 2 itakugharimu elfu 20 kwa matumizi upatikanaji wa madumu.

unaweza ukatengenezesha kokoteni kwa elfu 70 hivyo utabakiwa na elfu 10 ambayo hiyo elfu 10.

Elfu 5 utaweka kama akiba ya kukulinda.

lakini elfu 5 utanunua nyingine utanunua sabuni ya elfu 2 kusafishia ayo madumu yako mara nyingi madumu ya mafuta yanakuwaga na mafuta mabaki ya mafuta yaliyoganda.

utabakiwa na elfu 3 elfu 1 unaweza kuitumia kununulia maji ya kwenye bomba ya elfu 1 kwa makisio ya kila dumu mmoja 100 hivyo madumu 10 itakuwa buku.

elfu mbili utaitumia katika kula yako.

NB: hakikisha unatafuta wateja kabla ya kuanza hizo harakati pia tazamia zaidi sehemu ambayo kuna shida na mahitaji ya maji.

FAIDA.

Dumu moja la maji linauzwa mia 5 hivyo basi kama una madumu 10 kwa round moja unaweza ukapata faida ya elfu 5 . kila round toa elfu 1 ya ununuzi kwahiyo faida elfu 4.

kama utaweza kwenda round 3 na maji yakatoka basi kwa siku unaweza ukawa na uhakika wa kukamata elfu 12.

CHANGAMOTO.

•• Midomo michafu ya wateja ujiandae a kauli za ovyo kutoka kwa wateja kwa sababu wateja wakubwa wa biashara hizi ni wamama wa majumbani.

•• Jiepushe na tamaa za kimwili kama nilivyoanza kusema hapo hawali biashara hii utadeal sana na wamama basi jiandae kukutana na majaribu ya pita ndani nisaidie kumimina maji ndani.

•• Maji kuwa na mabaki ya mafuta. hakikisha unayaosha vizuri madumu yako yasiwe na mafuta ili usipate lawama kwa wateja wako.

SULUHISHO.

••Kuwa mstaamilifu na kuwa na lugha nzuri

•• Epuka vishawishi kwani vinaweza kukusababishia matatizo au magonjwa usiyotarajia.

•• Kuwa msafi wewe mwenyewe na vitendea kazi vyako itakusaidia kujitofautisha na wengine pia utawavutia wateja wako wengi.___________________________________

BIASHARA YA SAMAKI PEREGE

1. SAMAKI WA MAJI BARIDI (PEREGE NA KITOGA) ni biashara utaanza kwa kufata mzigo wa samaki Rufiji na sehemu nyingine. na kuja kuuza majumbani/ofisini kwa kutembeza na kuchukua oda. Sababu za majumbani ni kwamba wengi wetu tunapenda vitu vinavyo tufikia hadi mlangoni hii ni rahisi kwangu muuzaji kukutana na mteja ana kwa ana lakini pia maofisini kuna kuwa na urahisi kwa mteja kununua mboga mapema na kufika nyumbani kuingia jikoni kuna mpunguzia mizunguko ya kwenda sokoni.

Faida inayo kadiliwa kuwa ni 40000 na mchakato wa kupatikana faida iyo. upo hivi - Ikiwa Mzigo wa samaki ni 30000/= na makaango ni 20000/= bila kusahau na leseni ya samaki ambayo ni ( 20000=/ kwa mwaka) hapo nitachukua nauli ambayo ni 12000/= ya kwenda rufiji na kurudi Dar es salaam .

Pia utaitaji kuwa na magezeti pamoja na mbanio wa samaki ambayo jumla yake ni 3500/= bila kusahau na ndoo itakayo gharimu 2000/= hapo utaongeza na 2500/= ya chakula kwahiyo siku utakayo fata mzigo. jumla ya mtaji ni 90000/=

ambapo ukitoa mtaji yani 130000 - 90000 = (40000/=) faida.

N:B Ukisha kata leseni ya biashara ya samaki kwa Awamu ya kwanza. Utakuwa unachukua mzigo wa 50000 ivyo faida itaongezeka kutokana na ukubwa wa mzigo.

CHANGAMOTO

••Kwanza changamoto kubwa itakayo kuwa ina inakusumbua ni kuto kukaangwa vizuri kwa hao samaki wataoza.

••changamoto ya pili utafutaji wa soko. pamoja na kukutana na wale wateja wanao chagua chagu kisha hawanunui hii wanapelekea samaki kukatika na kumeguka😣.

SULUHISHO

••Kutokana na changamoto hizo hivyo hakikisha unasimamia vizuri kipengele cha kuangwa vizuri.

wakiangwa vizuri kwa makadilio wanafika hadi siku 6 bila kuoza ama kuvunda. jitahidi kutembea umbali mrefu na ofisi tofauti tofauti ili kutafuta soko.

Pia Kutokana na utandawazi, unaweuza bidhaa zako kidigitali
_______

BIASHARA YA SABUNI

Biashara ya sabuni sababu ni muhimu na ni hitaji la lazima kwa binadamu wandunia yetu ya sasa

utaanza kwa kununua sabuni yako kwa jumla na utawauzia na kuwakopesha watu wa nyumbani na kutembeza mtaani kwenye manyumba ya watu na ofisi mbalimbali kwa sababu biashara hii unawateja wengi uswahilini wengi.

watakopa ndio wanavyopenda na ndio watumizi wazuri wa hizo sabuni kwa kufulia na kuoshea hata kudekia pia.

FAIDA

Upatikanaji wa faida katika biashara yako unapatikana kwa sabuni utakavyopata sokoni kutokana na mabadiliko ya bidhaa hiyo unaweza nunua kiroba Cha sabuni yenye pakti 24 kwa sh.30000.

utauza parket moja kwa 1500 na kukopesha 2000 muda wa siku5 sababu ya wateja wengi watakuwa mtaani na majumbani hivyo.

utakopesha zaidi badala ya kuuza na ukikopesha parket 5 ndani ya siku utapata 10000 ndani ya siku5 na faida 5000

CHANGAMOTO

••Soko la kibiashara au ushindani kwenye biashara sababu unapoanza kitu lazima atatokea mwengine nae atafanya.

••wateja kukopa bila kulipa au kukosa wateja wenyewe kabisa,na kudharauliwa

SULUHISHO

•• Katika suala la kudharauliwa hautaki kujali sana hiyo changamoto sababu jua unatafuta na suala la wateja.

•• Wateja wasiolipa usiwakopeshe tena ili kujiondolea usumbufu katika biashara na suala la kukosa wateja jitahidi kuwa nadhifu na heshima katika biashara ili kupata wateja zaidi na kuepukana na changamoto hizo.

••Tafuta elimu juu ya bidhaa yako ili upate kuielezea na kuipenda zaidi,kuwa na ulimi wenye maneno ya busara na ustaarabu kuwa mchangamfu mda wa kazi na sio ukali hata pasipo na sababu jitahidi kutoa na offer pia hata kila weekend ili kuwavutia zaidi.
____________________________________________________________________________

NB: °°MWISHO jifunze kuweka akiba. Kwa lengo la kufika kwenye mafanikio makubwa kibiashara.

utapaswa kuweka akiba kwenye kila faida unayoingiza kwenye biashara yako.Wakati biashara inafanya vizuri, nisijibweteke na kuona mambo yataenda hivyo wakati wote

.ukiweka akiba ambayo itakusaidia wakati biashara haiendi vizuri. Akiba hiyo ndiyo itanisaidia kwenye ukuaji wa biashara yako.

Pia jifunze kila siku kwani ni hitaji muhimu la ukuaji wa biashara yangu. Kila siku hakikisha unajifunza kitu kwenye kuikuza biashara yako. Biashara inahitaji ubobezi maeneo mbalimbali kama masoko, mauzo, fedha, ushawishi na uongozi.•••• Shukrani Sana nawasilisha hii
Kama una wazo jingine la biashara lenye ambalo unaweza kuanza na mtaji wa laki 1 hadi 150000+.

liandike ili watu tujikwamue kiuchumi namba ya watu wasiokuwa na ajira ni kubwa sana na swala la kupata ajira ni ngumu.

CHANGIA WAZO LAKO HATA KAMA UTONUFAIKA NA HILO WAZO AMBALO LITAMTUFAISHA MTU LAKINI MUNGU ATAKULIPA TU.
 
Lello199

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
825
2,049
Biashara ya kuuza miwa. Muwa unanunua 500 sokoni unakata vipande 4 vya jerojero. Hapo faida yako inekuwa 1500. Kama utachonga na kukatakata ukaweka kwenye vimifuko utapata faida kubwa zaidi
 
sophy27

JF-Expert Member
Mar 20, 2022
6,685
15,961
Biashara ya juis fresh nayo inafaida Sana ila kama una friji ni nzuri zaidi kama hauna unaweza nunua hata mabarafu makubwa wanauzaga elfumoja
Ila inategemea unauza sehemu zenye mikusanyiko sokoni hata kutembeza mtaani
Vya kuzingatia ni usafi na ubora.
 
Vanree

JF-Expert Member
Jan 3, 2017
216
161
Juzi niliwauliza wanaJF. una mshauri nini kijana ambae yupo mtaani tu hana ajira mawazo yalikuwa ni mengi na ni mazuri pia.

Ila na mimi leo nimeamua kuja na uzi ambao utakuwa na biashara kadhaa ambazo unaweza kuanza nazo kwa mtaji wa laki moja lakini cha kwanza kabisa lazima tujue kuwa biashara yoyote ina changamoto ujiandae kupambana na changamoto itakapo tokea mda wowote ule.

Hapa nitaelezea changamoto za biashara zenyewe na suluhu na jinsi ya kuepeuka changamoto.

Kwanza napenda kutoa maarifa machache sana katika mchakato wa kuanzisha biashara.

Tujifunze katika kutengeneza au kuchambua wazo zuri la biashara swala la mtaji linakuja mwisho kabisa katika hitimisho. Tupende kufanya biashara tunazozipenda kwani katika kufanya biashara unayoipenda kuna ubunifu lakini pia kuna bidii. Mie naamini hata kama biashara yako ni ndogo sana kama punje ya mchele ukiipenda na kuwa na bidii nayo basi biashara ile itafana. Tusikimbilie mitaji hali ya kuwa mawazo mazuri ya biashara hatuna hii ni changamoto kubwa sana, matokeo yake unaweza kupewa wazo bimaana katika biashara hiyo ni ya uhakika katika kupata wateja na wewe utajibweta lengo ni kupata wateja mwisho wa siku unakosa ubunifu na bidii matokeo yake biashara inafeli

Karibu mwana JF forum's.

______________________________
1. BIASHARA YA GENGE

Biashara ya genge ni biashara yenye uhitaji mkubwa sana kwa sababu watu kila siku wanakula.pia biashara unayoweza kuanza kwa mtaji kidogo.

Ni biashara ambayo huhitaji kuwa na eneo la gharama kubwa kuifanyia.Na ni biashara ambayo haina vitu vingi, hivyo unaweza kuisimamia vizuri tu.Hii ni biashara ambayo mtu ambaye hana shughuli nyingine ya kufanya anaweza kuianzisha, akaiendesha vizuri na ikawa sehemu ya yeye kupiga hatua na kuelekea kwenye biashara kubwa zaidi.

• Biashara yako inapaswa kuwa eneo ambalo ni rahisi kuwafikia wateja wako na hata wateja kuifikia pia kwahiyo kwakuwa uachouza ni mahitaji muhimu ya maisha kila siku, biashara itafanya vizuri inapokuwa na mzunguko mkubwa sana wa watu lakini pia hata makazi ya watu yawe kwa wingi maana wanunuzi wa bidhaa hizi ni kina mama wa majumbani kwani wao ndiyo wameshika usukani mkubwa sana wa jiko hata mama lishe pia.

Lakini pia mazingira ya eneo lako la biashara yanapaswa kuwa safi na mazuri.

yamfanye mteja aiamini na kuithamini biashara yako.Wengi wanaofanya biashara ya genge hawaweki maeneo yao ya biashara kwenye mwonekano mzuri, ukifanyia kazi hilo unajitofautisha kabisa na wengine.

Nikirudi katika namna ya uanzishaji kwanza unatakiwa ujue machimbo ya kupata mzigo wa kutosha. Na chimbo kubwa ni masokoni na masokoni utapata bidhaa zote za gengeni.

Andaa na pesa ya usafiri na ubebaji 5000+ au 5000- .

Vifaa vya biashara ikiwemo meza, stuli, kipande cha turubai ikilazimu ama mwamvuli(mabati ndo mazuri zaidi), visu, ndoo, nakadhalika vinapaswa kutoka katika mtaji huo huo. Lakini pia unatakiwa kujua vitu vya msingi na vyenye uhitaji mkubwa katika genge lako mfano Mboga za majani, Vingia mchuzi kama nyanya, carrots, hoho, vitunguu, etc, Viungo vya ziada kama hiliki, mdalasini, swaumu, etc, Matunda kama tikiti, tango, chungwa, papai, parachichi, embe, nanasi, etc, Viazi, nazi, ndizi mbivu etc

•• Njia ya kujua faida ni kuorodhesha hivi vitu katika karatasi ya shopping na uweke idadi. utapita magenge kadhaa na ukifika uliza bei ya vitu hivyo na nakili.

Ukishamaliza hesabu za hapo juu linganisha jumla ya pesa utakayotumia kununulia vitu hivyo kwa bei ulizoona sokoni na jumla ya mapato utayoyapata ukiuza bidhaa hizo.

Tofauti yake huwa ni faida .

Kwa mfano; kawaida sado moja ya viazi linauzwa kati ya 3,000 hadi 4,500 kulingana na sehemu. Lakini katika kupangilia mafungu hauwezi kosa mafungu 9 kwa wastani. Kuna baadhi ya sehemu mafungu hayo wanauza kwa 500 na sehemu nyengine wanauza kwa 1000. Ukinunua sado moja kwa 3,000 ukauza fungu kwa 500 na ukapanga fungu 9 utapata 4,500. Hapa faida ghafi ni 1,500. Nikinunua kwa 4,500 ukipanga fungu 7 na kila fungu ukauza kwa 1,000 utapata 7,000. Hapa faida ghafi ni 2,500. Kwa ufupi katika biashara ya genge katika kila 10,000 utakayoingiza faida chache sana utayoipata ni 2,500. Sasa kazi ni kwako kuangalia sehemu yenye mzunguuko mzuri. Ukiuza bidhaa za 60,000 kwa siku utapata zaidi ya 15,000 faida kwa siku.

CHANGAMOTO

Changamoto kubwa katika biashara ya genge ni mabadiliko ya bei kutokana na kwamba bidhaa nyingi ni za msimu na kwamba zinategemea sana hali ya hewa, lakini jambo jingine ni kodi maana unaweza kupanga sehemu ikawa mlikubaliana kuwa malipo ni elfu 30 kwa mwezi, kwakuwa anaona unauza sana basi figisu zinaanza Mara kodi inapandishwa mpaka elfu 50 kama huwezi beba vyako, lakini pia utunzaji wa bidhaa maana bidhaa nyingi huwa hazikawii kuharibika, pia usafirishaji katika kutoa bidhaa soko kuu kuja katika eneo lako la kazi na mwisho nimalizie katika mikopo hususani kama ni mikopo yenye riba kubwa na muda wa marejesho ni mdogo haswa

SULUHISHO

Katika kutatua changamoto hizi maana kama patakuelemea lakini kuzitatua kwa uzuri ni kule kuwa na mtaji vifaa yaani kwa mfano ukawa na eneo lako nyumbani ambapo linatosha kuweka genge lako, uwe na mtaji wako labda hata elfu 20(lengo kuepusha mikopo), usafiri wako (mkokoteni) na sehemu nzuri ya kuhifadhi bidhaa zako. Lakini yapendeza ukawa mkulima wewe mwenyewe yaani uwe na shamba lako mahususi kwa biashara ya genge

••Kuwa na maono makubwa. Japo unafanya biashara ya genge, kwenye fikra zako usione genge, bali ona biashara kubwa kabisa. ona ukiwa na maduka mengi ya kuuza mahitaji hayo ya msingi na ona ukifanya kwa kiwango kikubwa zaidi.

maono makubwa utakayo kuwa nayo ndiyo yatakusukuma kupiga hatua kubwa.
Pia nipendelee kuwa na bidhaa bora wateja wanaangalia vitu vikuu viwili, •bidhaa bora na

•kwa bei nafuu.

ukiwa na vitu hivyo viwili utajenga imani ya wateja kwenye biashara yako.

Pia uwe na huduma nzuri kwa wateja. hudumia vizuri wateja wako ili waweze kurudi tena na tena.

••Pia uweke mafungu. kutokana na mahitaji ya wateja wako, unaweza kutengeneza mafungu ya vitu vinavyonunuliwa kwa pamoja na kisha kumshawishi mteja anunue kama fungu badala ya kununua kimoja kimoja. Kumsukuma kuchukua hatua, hakikisha bei ya fungu inakuwa na unafuu kuliko mteja akinunua kimoja kimoja. Njia hii itaniwezesha kuuza zaidi kwa wateja ambao tayari unao, ambao ni wateja wazuri tayari.

••Pia uwafikie wateja. usisubiri tu wateja waje, badala yake wafuate kule walipo. Watu sasa wametingwa na mambo mengi wanaweza kusahau kabisa hata uwepo wako. Hivyo tembelea wateja wako maeneo walipo na kuwashawishi kuja kununua.

Pia Kutokana na utandawazi, unaweuza bidhaa zangu kidigitali pia.

_________________________________
1. BIASHARA YA DAGAA WA MWANZA WALE WANAOKAANGWA WABICHI

• Mboga ni kitu cha muhimu na lazima kwa maisha ya kila siku ya kila mwanadamu.

Utaitumia vipi mtaji wako.

Sado kwa Mwanza utanunua elfu 13000, nauli Mwanza Dar elfu 10000 kwa box. pesa ya nauli kutoka mbezi hadi labda mbande weka 3000+ au 3000- kwa waliopo dar .

Kwa hiyo kwa laki utaagiza sado 6 sawa na elfu 78,000 nauli Mwanza Hadi Dar elfu 10000. Nauli ya kwenda kuchukua chukua box la dagaa elfu 3000 jumla kuu 91,000. Kwa laki nabaki na 7000 hii utanunua bando la buku mbili na vifungashio vya buku 2 inaleta jumla Kuu 95,000. Elfu tano naitunza Kama dharula.

2. Biashara hii utaifanya kwa kutumia status za Whatsapp kutangaza biashara na kwa kufunga za buku buku kutembeza mtaani.

Wateja wako lenga hasa wa uwezo wa kununua nusu sado kwa elfu 10000 na sado nzima kwa 20000. Kwa hiyo hata ukifunga za buku buku hakikisha unapata pack 20+.

Mteja utamuweka wazi kuwa lazima achangie usafiri kwa hiyo Ile dharula ya buku 5 utatumia kwenye delivery ya dagaa door to door in case kunahitajika kupanda daladala. Ambapo ukimfikishia mteja atalipia na usafiri kabisa kwa hiyo narudisha kwenye Ile Baki yangu ya elfu 5.

FAIDA

Faida katika biashara hii itatakiwa kila sado upate faida ya elfu 5000 na kuuza hizo sado sita target ndani ya siku 2 Hadi tatu. Kwahiyo sado 6*20000= 120,000 ukitoa mtaji ambao ni elfu 95000 Babaki na elfu 25000 kujumlisha na ile tano ya dharula utakuwa na mtaji wa 100000 na faida 25000 jumla utakuwa na 125000. Ukiweka muda wa kuagiza kusafirisha na kuuza angalau kwa wiki uagize Mara mbili na kila upoagiza utakuwa unaongeza sado moja kutokana na faida utayopata.

Kwa hiyo Kama wiki ya kwanza utapata 25000*2 =50000 faida wiki moja. Mwezi una wiki nne kwa hiyo Kama utapata faida elfu 50000 kwa wiki kwa mwezi ntakuwa na 200,000 faida maximum (. 50000*4=200000).

CHANGAMOTO YA BIASHARA YA DAGAA.

Changamoto utakayokumbana nayo ni kutoka kwa wateja wakopaji. Hawa wanaweza kufanya biashara ife lakini ili hakikisha biashara yako isife unatakiwa kuwa na kauli nzuri lakini usikopeshe. Hii itapunguza hadara na chuki baina yangu na wateja wangu.

Changamoto ya pili nidagaa kuvunda.

Ukiwapaki wakiwa wa Moto kwenye vifungashio like joto baadae linatengeneza unyevu ambao uanza kutoa fangasi.

-Dagaa kunywea, dagaa waliokaangwa wakiwa wabichi Wana tabia kadili wanavyozidi kukaa hunywea hivyo kama.mzigo hautoki haraka inaweza kusababisha mchuuzi kupata hasara.

SULUHISHO

Njia ya kutatua changamoto ya kucheleweshwa au kutokulipwa kabisa na ili kuepuka ugomvi na wateja wako kuwa muwazi haukopeshi .

•• Ili kutatua changamoto ya dagaa kuoza au kuvunda muandaaji hakikisha dagaa inakaangwa inakauka vizuri, inachujwa mafuta vizuri na kuacha ipoe kabisa ndo upark .mzigo kwenye box.

•• Kuondokana na hadha ya kupata hasara kutokana na kunywea kwa dagaa hakikisha unatafuta wateja wapya kila mara ili angalau.target yako ya kuuza mzigo ndani ya siku 2-3 itimie hivyo utakuwa umepuka hasara.

••Jifunze kuwa na elimu ya customer care.

hakikisha na deal na supplier mmoja kwa kusikiliza mapungufu ya bidhaa yako kutoka kwa wateja na kuongea na supplier kuboresha hivyo kufanya wale wale wateja kuwa mawakala wa wengine hivyo kuongeza idadi ya wahitaji ambayo itaniongezea idadi ya sado unazoziagiza hivyo faida kuongezeka.

- Kutanua wigo wa biashara kwa kuanza kuuza kwa wasambazaji wengine ( kwa jumla jumla) hasa wale wa magengeni na Min Super Market hivyo kuwezesha kuitangaza biashara yako zaidi.

Pia Kutokana na utandawazi, unaweuza bidhaa zako kidigitali pia.
_____________________________________

BIASHARA YA MATUNDA / FRUITS

Biashara ya matunda inafaa zaidi hasa maeneo ya chuo au shule au stand kutokana na muingiliano wa watu mda wote soko uhakika
Mfano matunda ukipata kideli ambacho hakizidi elfu 5 tikiti kama tikiti au nanasi inatosha sana

•Vitu utakavyo takiwa kuwa navyo ni vifuatavyo
Kideli -10000
Kisu- 2000
Magazeti Kama vifungashio -5000
Kijiko-2000
Matikiti-matanox3000
Deli la taka- 15000

Uuzaji wa matunda. utaangalia bei ya wastani ya hayo matunda. Kama unakata na kupanga nami nitafanya hivyo. Mfano; tikiti la elfu 5 sokoni linaweza kukatwa vipande 8 vya 200, vipande 6 vya 500 na vipande 4 vya 1,000. Hii ina maana kila tikiti litatoka vipande 17 vya saizi tofauti tofauti na bei tofauti tofauti na jumla utapata faida ghafi 3,600. ukiweza kuuza vipande 50 kwa siku ni sawa na wastani wa matikiti matatu. Faida itakuwa 10,800 kutoka kwenye matikiti matatu pekee.Bado una maparachichi, mapapai na machungwa. Kiufupi hauwezi kosa 20,000 ya faida kwa siku. Kwa mwezi nitakuwa na angalau 500,000 kwenda juu ya faida.

CHANGAMOTO

••Changamoto ni nyingi ukiangalia hasa upatikanaji wa matunda
Kuoza kwa matunda

••Matunda kutoisha kwa wakati
Usumbufu wa Askari na tozo za ushuru

SULUHISHO

••Kutokana na changamoto hizi hakikisha unakua msafi mda wote ili kuondoa usumbufu wa Askari na bwana afya
Kulipa ushuru kwa wakati kuondoa usumbufu

••Njia ya kupambana na changamoto
Usafi na kauli nzuri kwa wateja pia kuongeza kipato lazima ujenge tabia ya kuwahi kazini ili kuondoa changamoto ya kutomaliza matunda kwa wakati.

•• Kutotegemea wapita njia tu pia kujenga mazoea na wanafunzi na wakufunzi,au makondakta au madereva wa eneo husika ni njia bora zaidi ya kuongeza kipato

Pia Kutokana na utandawazi, unaweuza bidhaa zako kidigitali pia.

_________________________________
BIASHARA YA KUUZA KWENYE MADUMU

Hii biashara inaitaji maeneo yenye mchanganyiko wa watu wengi kama maeneo ya uswahili na maeneo ya pwani wanapoanika dagaa.

Utanunua madumu 10 kila dumu mmoja elfu 2 itakugharimu elfu 20 kwa matumizi upatikanaji wa madumu.

unaweza ukatengenezesha kokoteni kwa elfu 70 hivyo utabakiwa na elfu 10 ambayo hiyo elfu 10.

Elfu 5 utaweka kama akiba ya kukulinda.

lakini elfu 5 utanunua nyingine utanunua sabuni ya elfu 2 kusafishia ayo madumu yako mara nyingi madumu ya mafuta yanakuwaga na mafuta mabaki ya mafuta yaliyoganda.

utabakiwa na elfu 3 elfu 1 unaweza kuitumia kununulia maji ya kwenye bomba ya elfu 1 kwa makisio ya kila dumu mmoja 100 hivyo madumu 10 itakuwa buku.

elfu mbili utaitumia katika kula yako.

NB: hakikisha unatafuta wateja kabla ya kuanza hizo harakati pia tazamia zaidi sehemu ambayo kuna shida na mahitaji ya maji.

FAIDA.

Dumu moja la maji linauzwa mia 5 hivyo basi kama una madumu 10 kwa round moja unaweza ukapata faida ya elfu 5 . kila round toa elfu 1 ya ununuzi kwahiyo faida elfu 4.

kama utaweza kwenda round 3 na maji yakatoka basi kwa siku unaweza ukawa na uhakika wa kukamata elfu 12.

CHANGAMOTO.

•• Midomo michafu ya wateja ujiandae a kauli za ovyo kutoka kwa wateja kwa sababu wateja wakubwa wa biashara hizi ni wamama wa majumbani.

•• Jiepushe na tamaa za kimwili kama nilivyoanza kusema hapo hawali biashara hii utadeal sana na wamama basi jiandae kukutana na majaribu ya pita ndani nisaidie kumimina maji ndani.

•• Maji kuwa na mabaki ya mafuta. hakikisha unayaosha vizuri madumu yako yasiwe na mafuta ili usipate lawama kwa wateja wako.

SULUHISHO.

••Kuwa mstaamilifu na kuwa na lugha nzuri

•• Epuka vishawishi kwani vinaweza kukusababishia matatizo au magonjwa usiyotarajia.

•• Kuwa msafi wewe mwenyewe na vitendea kazi vyako itakusaidia kujitofautisha na wengine pia utawavutia wateja wako wengi.___________________________________

BIASHARA YA SAMAKI PEREGE

1. SAMAKI WA MAJI BARIDI (PEREGE NA KITOGA) ni biashara utaanza kwa kufata mzigo wa samaki Rufiji na sehemu nyingine. na kuja kuuza majumbani/ofisini kwa kutembeza na kuchukua oda. Sababu za majumbani ni kwamba wengi wetu tunapenda vitu vinavyo tufikia hadi mlangoni hii ni rahisi kwangu muuzaji kukutana na mteja ana kwa ana lakini pia maofisini kuna kuwa na urahisi kwa mteja kununua mboga mapema na kufika nyumbani kuingia jikoni kuna mpunguzia mizunguko ya kwenda sokoni.

Faida inayo kadiliwa kuwa ni 40000 na mchakato wa kupatikana faida iyo. upo hivi - Ikiwa Mzigo wa samaki ni 30000/= na makaango ni 20000/= bila kusahau na leseni ya samaki ambayo ni ( 20000=/ kwa mwaka) hapo nitachukua nauli ambayo ni 12000/= ya kwenda rufiji na kurudi Dar es salaam .

Pia utaitaji kuwa na magezeti pamoja na mbanio wa samaki ambayo jumla yake ni 3500/= bila kusahau na ndoo itakayo gharimu 2000/= hapo utaongeza na 2500/= ya chakula kwahiyo siku utakayo fata mzigo. jumla ya mtaji ni 90000/=

ambapo ukitoa mtaji yani 130000 - 90000 = (40000/=) faida.

N:B Ukisha kata leseni ya biashara ya samaki kwa Awamu ya kwanza. Utakuwa unachukua mzigo wa 50000 ivyo faida itaongezeka kutokana na ukubwa wa mzigo.

CHANGAMOTO

••Kwanza changamoto kubwa itakayo kuwa ina inakusumbua ni kuto kukaangwa vizuri kwa hao samaki wataoza.

••changamoto ya pili utafutaji wa soko. pamoja na kukutana na wale wateja wanao chagua chagu kisha hawanunui hii wanapelekea samaki kukatika na kumeguka.

SULUHISHO

••Kutokana na changamoto hizo hivyo hakikisha unasimamia vizuri kipengele cha kuangwa vizuri.

wakiangwa vizuri kwa makadilio wanafika hadi siku 6 bila kuoza ama kuvunda. jitahidi kutembea umbali mrefu na ofisi tofauti tofauti ili kutafuta soko.

Pia Kutokana na utandawazi, unaweuza bidhaa zako kidigitali
_______

BIASHARA YA SABUNI

Biashara ya sabuni sababu ni muhimu na ni hitaji la lazima kwa binadamu wandunia yetu ya sasa

utaanza kwa kununua sabuni yako kwa jumla na utawauzia na kuwakopesha watu wa nyumbani na kutembeza mtaani kwenye manyumba ya watu na ofisi mbalimbali kwa sababu biashara hii unawateja wengi uswahilini wengi.

watakopa ndio wanavyopenda na ndio watumizi wazuri wa hizo sabuni kwa kufulia na kuoshea hata kudekia pia.

FAIDA

Upatikanaji wa faida katika biashara yako unapatikana kwa sabuni utakavyopata sokoni kutokana na mabadiliko ya bidhaa hiyo unaweza nunua kiroba Cha sabuni yenye pakti 24 kwa sh.30000.

utauza parket moja kwa 1500 na kukopesha 2000 muda wa siku5 sababu ya wateja wengi watakuwa mtaani na majumbani hivyo.

utakopesha zaidi badala ya kuuza na ukikopesha parket 5 ndani ya siku utapata 10000 ndani ya siku5 na faida 5000

CHANGAMOTO

••Soko la kibiashara au ushindani kwenye biashara sababu unapoanza kitu lazima atatokea mwengine nae atafanya.

••wateja kukopa bila kulipa au kukosa wateja wenyewe kabisa,na kudharauliwa

SULUHISHO

•• Katika suala la kudharauliwa hautaki kujali sana hiyo changamoto sababu jua unatafuta na suala la wateja.

•• Wateja wasiolipa usiwakopeshe tena ili kujiondolea usumbufu katika biashara na suala la kukosa wateja jitahidi kuwa nadhifu na heshima katika biashara ili kupata wateja zaidi na kuepukana na changamoto hizo.

••Tafuta elimu juu ya bidhaa yako ili upate kuielezea na kuipenda zaidi,kuwa na ulimi wenye maneno ya busara na ustaarabu kuwa mchangamfu mda wa kazi na sio ukali hata pasipo na sababu jitahidi kutoa na offer pia hata kila weekend ili kuwavutia zaidi.
____________________________________________________________________________

NB: °°MWISHO jifunze kuweka akiba. Kwa lengo la kufika kwenye mafanikio makubwa kibiashara.

utapaswa kuweka akiba kwenye kila faida unayoingiza kwenye biashara yako.Wakati biashara inafanya vizuri, nisijibweteke na kuona mambo yataenda hivyo wakati wote

.ukiweka akiba ambayo itakusaidia wakati biashara haiendi vizuri. Akiba hiyo ndiyo itanisaidia kwenye ukuaji wa biashara yako.

Pia jifunze kila siku kwani ni hitaji muhimu la ukuaji wa biashara yangu. Kila siku hakikisha unajifunza kitu kwenye kuikuza biashara yako. Biashara inahitaji ubobezi maeneo mbalimbali kama masoko, mauzo, fedha, ushawishi na uongozi.•••• Shukrani Sana nawasilisha hii
Kama una wazo jingine la biashara lenye ambalo unaweza kuanza na mtaji wa laki 1 hadi 150000+.

liandike ili watu tujikwamue kiuchumi namba ya watu wasiokuwa na ajira ni kubwa sana na swala la kupata ajira ni ngumu.

CHANGIA WAZO LAKO HATA KAMA UTONUFAIKA NA HILO WAZO AMBALO LITAMTUFAISHA MTU LAKINI MUNGU ATAKULIPA TU.
Mawazo mazuri haya
 
20 Reactions
Reply
Top Bottom