Kama wewe mtoto wa kiume, dada zako wakiolewa furahi sana, shukuru Mungu

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,647
9,574
Kwenye familia yetu tumezaliwa wavulana 6 wasichana 2, dada yetu mkubwa aliolewa mapema sana. Huyu mwingine wakati anaolewa mama alilia sana maana alimzoea sana na ndo alikua msaidizi wake mkubwa sana, "ajabu baba alifurahi sana" sikumwelewa baba alimaanisha nini mpaka baada ya miaka 6 alikuja kuniamba "KUOLEWA KWA DADA ZENU NDO SALAMA YA NDOA ZENU"

Leo baba amefariki nakuja kuyaona haya kwenye nyumba ya baba yangu mkubwa. Baada ya watoto wake wawili kuoa nyumba imejawa na vurugu dada(mawifi) wameanzisha vita ya hatari.

Maneno kila kukicha japo ya kila mtu kuishi kwake bado hawajaridhika. Bado wanaona wana haki na kaka zao wanaona mawifi wanafaidi nafasi yao yaani vurumai tupu.

Wangekua wameolewa haya mambo yangeoungua au yasiwepo kabisa

Kijana kama dada zako wanataka kuolewa furahi sana kama unaweza suport fanya. Usije ukaweka kikwazo as long wamekubliana waache waoane. Hata ukiweka kikwazo kamwe huwezi kumtafutia mwanaume wa kumuoa.

Kuolewa wao ndo salama ya ndoa yako.
 
Ajabu baba alifurahi sana" sikumwelewa baba alimaanisha nini mpaka baada ya miaka 6 alikuja kuniamba " KUOLEWA KWA DADA ZENU NDO SALAMA YA NDOA ZENU"

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Nadhani umeelewa barabara
 
Kwa iyo hao ndugu zako wameoa huku wanakaa wote hapo nyumbani?

Ama wana maisha ya kihindi ya kukaa nyumba moja babu, baba, watoto, wajukuu, vitukuu.
 
Kwa iyo hao ndugu zako wameoa huku wanakaa wote hapo nyumbani?

Ama wana maisha ya kihindi ya kukaa nyumba moja babu, baba, watoto, wajukuu, vitukuu.
Kila mtu ana kwake. Kwenye nyumba yetu hakuna shida ila kwa baba mkubwa ndo kuna shida japo waliooa wanakaa kwao ila dada(mawifi) bado wapo nyumbani na wanaamini kua wana haki na kaka zao.
 
Back
Top Bottom