Tunapomnyanyua mtoto wa kike tunamsahau mtoto wa kiume

reymage

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
11,900
27,922
Salaam sana jf

Imekua kawaida kwa hali ilivyo kwa sasa,kila tunakozunguka ktk maisha ya kawaida tunakutana na mijadala na hotuba mbali mbali za kumnyanyua mtoto wa kike ktk masuala kadhaa wa.

Dunia nzima sasa hivi inazungumza lugha moja tu ya usawa wa kijinsia kati ya ke na me na imekua ikipigiwa debe sana jinsia ke ambayo inaaminika ndo ilikua nyuma ktk nyanj mbalimbali huko mwanzoni,nchi ambacho hazifanyi hiki kitu ni chache mnoo tena za bara Asia na zinaonekana zinakandamiza haki za wanadamu.

Ila tujiulize hiki kinachofanyika kumbeba sana mtoto wa kike mbeleni kitaleta athari kubwa sana,kwa vizazi vyetu vya mbele!Mwanamke anapewa kipaumbele kikubwa mnoo kiasi tunasahau kama kuna jinsia nyingine ya kuinuliwa ya kiume ambyo yenyewe ndo inapaswa kubeba jukumu la kulea na kujenga familia bora na msingi wa ukoo...!!!

Feminist wamejaa kila kona kuhutubia kua mwanamke na mwanaume ni sawa ktk kila hali,hvyo vyoote anavyofanya jinsie me na ke aweza fanya pia.Ila tujiulize ni sahihi juu hili?miye naweza kutia mimba?mwanaume anaweza kushika mimba ile bila ushirkishwaji wa sayansi na teknolojia ktk hiloo?

Usawa wa hizi jinsia mbili upo ila sio kwenye kila kitu,zote zina haki ya kupata elimu,haki ya kumiliki Mali nakadhilika lakini kila kitu kina mipaka yake,kwa siye tuliyo na dini zetu tumeambiwa ktk vitabu vitukufu kua Mwanaume ni kiongozi wa mwanamke,Mungu hakosei na hajawahi kosea.Ila hao viongozi dunia ya sasa inawatambua kama hawa ndo viongozi badili yake tumewaacha sasa tunaanza kuwakuza wengine kabisa.

Sisemi wanawake hawafai kua viongozi tunafaa sana tena mnoo ila mwanaume anapaswa awe pembeni yetu.

Wazazi wa sasa hata kwenye malezi tunajisahau sana tena mnoo hawa wenye watoto wa kiume ndo kichefuchefu haswaa wakina'junia',enzi hizo watoto wa kiume walikua na michezo yao,wanakaa na baba zao wanafundishwa mambo ya kiume ,kama kuwinda ,kupigana ,kuchunga na namna ya kulea familia zao vizuri,na wa kike walikua wanafundishwa na mama zao namna ya kuwa walezi bora kwa watoto na kazi za nyumbani na kuwa wake watiifu..

Leo sasa tunasema mtoto wa kike anampenda baba ,wa kiume anampenda mama!!wa kike anafanya ya kiume na wa kiume anafanya ya kike!Mbaba anaacha kushindwa kuongozana na mwanawe maeneo yake ya kazi amfundishe uwajibikaji,amfundishe kumwagia bustani,kuosha gari au ht kusimamia vimiradi vidogo vya nyumbani badili yake anabaki nyumbani na mama au Dada zake wanapiga story na bimkubwa wake then baadae baba analaumu kijana kua anamkumbatia mama mda wote.

Mwishowe wake tunapata vijana ambao marioo wanapendwa kulelewa mda wote maana wanaona hali za kawaida tu kupewa kwa kua hawajawahi kufundishwa kuvuja jasho,tunapata wanaume wasiojua majukumu yao ya kifamilia wanaona kila kitu sawa tu!vijana wanaingiwa na tamaa na kujiona hata wakiwa machoko sawa tu maana hakuna wanachopoteza.

Kingine ndoani mwanaume anataka 50/50 kwa mkewe yaani ile ile yaani ye Annue chumvi we ununue kiberiti kisa nyote mwafanya kazi.

Watoto wa kike tunakua na ujasiri wa hali ya juu na kujiona sisi tunaweza kuishi bila me,tunaweza kulea familia ,tunaoa wanaume tunaotaka simply uwezo upo!!

Mwanaume ukiona anakuchosh tu umemtema kwanza akapumzike maana uwezo wa kutafuta upo.
Sio kua kizazi cha zamani kilikua bora sana ,hapana ila waliishi ktk misingi inayotakiwa wazazi wachache sana ndo walikua wakwepa majukumu ktk familia zao,ila kwa sasa wanaume wengi wanakwepa majukumu ya kulea familia zao hali yatisha sana!!!

Wazazi wetu yaweza kua walinyanyasika kwa vipigo n.k hvyo vitu vilikuwepo na vipo mpk leo.
Wazazi wetu zamani walikua wanahudumiwa na waume zao100% isipokua familia chache sana wababa walikua pombe mtu!!wamama ndo wanahaha kusomesha n.k

Sasa hivi wanaume wambea kuliko wanawake maana wameiga tabia zetu wanawake za vijora pambe

NB.Tunapomuinua mtoto wa kike tusimuache wa kiume nyuma ,tuwabebe wote kwa usawa na Ili kutengeneza kizazi bora chenye maadili na uwajibikaji ktk sekta zote ,maisha yote katika ndoa zao na malezi bora ya watoto pia.Wanaume wafundishwa kubeba majukumu yao na wanawake wafundishwe kubeba majukumu yao pia.
 
Super Women hawezi kuinuka kwa makongamano.

Super Women anainuka mwenyewe tu bila mbwembwe za matamasha,
Hajaj!!siku ya wanawake makongamano ka yote kumkuza mwanamke daahhh
 
Umesema kweli kabisa.

Yaani hii dunia ya leo inashangza sana, mwanamke anapigiwa debe aache majukumu yake na awe kama mwanaume.
Na mtoto wa kiume wanataka awe kama mwanamke(ushoga).

Ushoga ni haki ya binadamu, na mwanamke yupo sawa na mwanaume.

Hapa ninachoona ni kama zinapotezwa jinsia na kuunda vitu vya ajabu.

Maana mwanaume hawezi kuwa mwanamke na wale mwanamke hawezi kuwa mwanaume.
 
Dhana ya 50/50 huwa naiona sana ikitumika kwenye maslahi

Mrusi kacharuka kaingia ukraine tunasikia tamko "wanaume waliozidi umri 18+ hawatakiwi kuondoka lazima mpambane vita"

Na wanawake je?

Mafeminist mko wapi na mnaruhusuje haki ya mwanamke ya kupambana kwenye vita ikipokwa kirahisi hivi na nyinyi mmekaa kimya?
 
Dhana ya 50/50 huwa naiona sana ikitumika kwenye maslahi

Mrusi kacharuka kaingia ukraine tunasikia tamko "wanaume waliozidi umri 18+ hawatakiwi kuondoka lazima mpambane vita"

Na wanawake je?

Mafeminist mko wapi na mnaruhusuje haki ya mwanamke ya kupambana kwenye vita ikipokwa kirahisi hivi na nyinyi mmekaa kimya?
Hizi 50/50 sio kwenye vitu hatarishi mkuu. Hiyo iko applied kwenye vitu vitamu vitamu, kama pesa na kadhalika.
 
Mbinu za kishetani tu ili kuweza kuipotosha jamii kusahau majukumu yao
 
Wakija kishtuka watakuja kukuta hii 50/50 inawaumiza wenyewe. Hamna kitu kina niuma kama haya maswala ya 50/50 ,kuingizwa kwenye mitaala ya shule kwani ni hatari sana mtoto wa kiume akuzwe na kuaminishwa katika 50/50.

Wazazi wa kiume kaeni na watoto then wajue na kujitambua wao ni akina nani na mfundishe kuwa mwanaume jasiri, mashuleni huko hizo NGO zisha haribu mitaala kwa kuingiza vitu vyao vya kipuuzi.
 
Tunarekebisha kosa kwa kutengeneza kosa kosa, twende hivyo maana maisha yenyewe ni mchezo wa makosa...
 
Back
Top Bottom