Kama Wazazi wa leo ni kama huyu je, tuendelee Kuwekeza katika Elimu za Watoto wetu ili waje kuwa na Maendeleo yao na Faida kwa Taifa?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,571
108,922
Leo nimedokezwa kuwa Wanafunzi wa Darasa la Nne wanafanya Mtihani wa Moko sijajua kama ni kwa Taifa zima au labda ni kwa baadhi ya Shule tu.

Nikiwa katika zunguka zunguka yangu nimekutana na Mzazi Mmoja wa Kike akifanya Tukio moja ambalo kutokana na kwamba namjua vyema lakini limenishtua pia nikasema si vibaya nikilileta hapa Kwenu ili liwe la Kimjadala zaidi tuweze kuona alikuwa sahihi au amekengeuka.

Huyu Mama siku zote huwa hana muda wa Kusimamia Taaluma ya Mwanae ( na hata akisimamia huwa ni kwa Kuzuga kama si kutimiza Wajibu tu ili asionekane hapendi au hajali Elimu ) na anachokijua ni Umbea, Udangaji, Majungu na mara kwa mara akimpa Simu yake Mwanae huyo awe anachezea Game na hata kuangalia Matukio yasiyokuwa na Maadili kutokana na Umri wake.

Leo Asubuhi akijua kuwa Mwanae hakumuandaa vyema kuelekea Kufanya vyema huo Mtihani wa Moko wakati anamuaga alimuita na kuanza Kumpaka na hata Kummwagia Mafuta ya Upako ya Tapeli Mmoja Maarufu wa Kiroho anayepatikana Kawe akiamini kuwa yatageuza Ubongo Mzito wa Mwanae ghafla na kuwa Mwepesi na safari hii awe wa Kwanza Kimatokeo badala ya nafasi yake aliyoizoea ya mwisho.

Sina shida sana na Yeye kupakwa hayo Mafuta ya Tapeli huyo wa Kiroho wa Kawe na Mama yake huyo Mzazi, ila Kilichonishtua kama siyo Kunisikitisha pia ni pale tu baada ya Kumpaka hayo Mafuta ya Kiroho aliyoyaamini yatamuongezea Akili Mwanae huyo ili afaulu baadae akamtaka akae Jirani na Wanafunzi wenye Akili na awe anaibia ( anawaibia ) pale akiona Maji ni Mazito Kwake kwa Maswali magumu atakayokumbana nayo.

Je, ni Wazazi wangapi wa sasa wapo kama huyu? Je, kwa Aina hii ya Mzazi huyu tutegemee kuwa na Kizazi cha Watoto Werevu kama chetu akina GENTAMYCINE kilichoishia rasmi mwaka 2000 kutokana na Utafiti wangu Binafsi nilioufanya na Kujiridhisha nao?

Je, kwa Kizazi hiki cha sasa na ambacho Kinaandaliwa na Wazazi ( Mzazi ) kama huyu Mama tutegemee kuwa na Kizazi cha Wabunifu na wenye IQ's Kubwa ambazo zitakuwa ni Chachu kwa Maendeleo ya Tanzania na Ustawi wa Watanzania ili kiweze Kushindana na Vizazi vingine kama vya Kiisraeli, Kirusi, Kiingereza, Kimarekani, Kikanada, Kiswideni na hata cha Kinyarwanda?

Naionea tu Huruma Elimu ya Tanzania.
 
Mashuleni wanafundisha uwizi na ubinafai ulafi uvaaji vr wa suti na kujihakikishia shria hazikubani haaaa mashimba yuko sahihi kosa ni hyo msirikina wa kikristu wa mitaa ya weka
 
Back
Top Bottom