Kama wana CHADEMA 'wanaozunguka' kuomba 'Kura' za Halima Mdee 'Kawe' wana 'Udhaifu' huu, basi 'namtabiria' Askofu Gwajima Ushindi asubuhi tu!

Wewe na mimi, rejea maswali yangu ya awali, tujiulize wajibu wa Mbunge ni nini.

Nahisi, vitendo vya wabunge wa upinzani kutokuwakilisha waliowachagua ipasavyo (kususia baadhi ya vikao, kupinga bajeti, nk) ndio msingi wa wao kuwaulizwa kipindi chao wamefanya nini.

Yawezekana, kuhusu zao la mchikichi, ni wazo la Serikali kuinua zao hilo, na ndiyo maana Waziri Mkuu amekuwa akienda huko mara kwa mara kuhimiza, wakati Zitto, Mbunge anakula BATA, dsm.
 
Wewe NDIYO huelewi na ukae kimya Kwa kuwa hujui, ni kweli Mbunge Hana pesa za moja Kwa moja, lakini Mbunge mjanja, hawezi kuisubiri serikali ifanye kila Changamoto iliyoko kwenye Jimbo,

Ukiwa Mbunge, unauwezo wa kuingia kila ofsi zilizopo ktk nchi hii

Kwa hiyo, kama unauhuru wa kuingia kila ofsi,maana yake kinachokosekana Kwa wabunge wetu ni ushawishi wao kupitia ofsi zao kutumia vema ofsi na taasisi zilizopo ktk nchi hii, ofsi za mabalozi nchini na taasisi mbalimbali
wanazitumiajee hawa wabunge wetu?

Ni wakati gani wabunge wetu wamewatumia vema Kwa kutumia ushawishi wao kwa wadau wa maendeleo, Mr Makonda, ni mtu aliyedharauliwa na kila mtu, lakini ni kijana aliyeweza kuitumia vema nafasi yake Kwa kuwashawishi wadau wa maendeleo na kujikuta akifanya Miradi mingi na ingawa mingine hsikufika mwisho

Licha ya wadau wa maendeleo, kuna mfuko wa Bunge, ukisimamiwa vizuri, kuna mahali utafanya
 
Weka picture
 
Kwanini unaamini kupinga bajeti sio kuwatumikia wananchi?Huo ni wajibu wao kikatiba lasivyo isingekuwepo kura ya ndio au hapana kwa bajeti!
Waziri mkuu huenda amekwenda baada ya kusikia mbunge anatoa hoja kuhusu jambo hilo!Na ndio nguvu ya mbunge inapoishia,kutoa hoja ili serikali ipime na ione kuna umuhimu wa kutekeleza jambo fulani!
 
Kwanini unaamini kupinga bajeti sio kuwatumikia wananchi?Huo ni wajibu wao kikatiba lasivyo isingekuwepo kura ya ndio au hapana kwa bajeti!
Waziri mkuu huenda amekwenda baada ya kusikia mbunge anatoa hoja kuhusu jambo hilo!Na ndio nguvu ya mbunge inapoishia,kutoa hoja ili serikali ipime na ione kuna umuhimu wa kutekeleza jambo fulani!
 

Issue ya Kawe ipo kihivi:
1: KIKATIO cha mtu mmoja ... hao jamaa flani ... kitapiga kura, kitatumika zaidi ya vituo vitano at least
2: Focus iko kulee ... bonde la mpunga, kata za MSASANI na vijimambo vya huko.... wamefocus huko. Wasichojua ... soma 3

3: Wasiojulikana ... miaka mitano mingine ya GRANITE? HAIPANDI upstairs
 
Omba omba mentality
 
Halima hafai
Gwajima hafai zaidi...
Halima hafai kuwa mbunge.
Gwajima hafai kuwa hata mgombea tu..

Kawe mwaka huu I wish wawakatae wote
Ulichosema kina uwekli fulani kuwa wote hawafai, lakini ukikutana na uchaguzi kati ya kuliwa na fisi au kuliwa na chui utachagua nini. Ni afadhali uliwe na Chui kwa sababu atakuua kwanza ndipo anakupandisha mtininda kukulia huko ukiwa husikii maumizvu tena kuliko kuliwa na fisia anyeanza kukula ungali hai ukiwa unasikia maumivu sana.

Swali ni kuwa kati ya gwajima na mdee ni nani fisi na ni nani chui.
 
Bunge la Tanzania usipokuwa na Halima Mdee, Esther Bulaya, Esther Matiko Godbless Lema, Patrick Msigwa, Heche, Sugu wa Mbeya, Mnyika, Mbowe, Zitto Kabwe, na wengine kutokana upinzani bunge litakuwa la ndiyooooooo!!!! Tu. Ndiyo tunachotaka???
 
Halima anatetea sana Mashaka ya wanawake, ya JamiiForums kama kupatiwa barabara, maji, fedha kwa ajili ya dawa, matibabu ya wajawazito, kuongeza Bajeti ya kilimo na kadhalika!
 
Mbunge siyo serikali kwani wao hawana fedha ila wanatetea huduma ziwafikie watu wao na Halima Mara nyingi ametetetea Mashaka ya taifa pamoja na ya kawe!
 
..Halima Mdee alikuwa akipigwa vita na mkuu wa mkoa.

..kama alishindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo ni kwasababu ya mkuu wa mkoa aliyekuwepo.

..wapiga kura wajiulize kwanini Mdee alikuwa effective 2010 -- 2015, lakini akashindwa kuwa effective 2015 -- 2020.

..kwa waliokuwa wakimfuatilia Mdee akiwa bungeni hawatapata shida ku-conclude kwamba Gwajima hawezi kuchangia mle bungeni kwa kiwango na umahiri kama Halima Mdee.

..Katika bunge lililopita wako wabunge ambao kutokana uzito wa michango na hoja zao waliitwa Maseneta. Halima Mdee ni mmoja wa wabunge hao.

..msikilizeni Halima Mdee hapa chini.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…