Kama wana CHADEMA 'wanaozunguka' kuomba 'Kura' za Halima Mdee 'Kawe' wana 'Udhaifu' huu, basi 'namtabiria' Askofu Gwajima Ushindi asubuhi tu!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,545
108,861
Jana nilibahatika Kukutana na wana CHADEMA baadhi ambao nadhani ( nahisi ) walipewa 'Jukumu' la Kupitapita Kawe hasa katika 'Nyumba' za Watu na Kumuombea 'Kura' Mgombea Ubunge CHADEMA Halima Mdee. Sina tatizo na 'Mbinu' yao hii ila GENTAMYCINE nina tatizo Kubwa sana na 'Competence' ya hawa wana CHADEMA wanaozunguka.

Huku nikiwa katika 'harakati' zangu za hapa na pale na jana nikiwa Jimbo la Kawe nilibahatika Kukutana na hawa wana CHADEMA kwa 'nyakati' tofauti ambapo wote kila walipokuwa wakikutana na Watu na Kuwaelezea 'Sera' zao ( CHADEMA ) na 'Kumnadi' Mgombea wao Halima Mdee walikuwa wanaonyesha 'Udhaifu' wa wazi wazi katika 'Kuchambua' na 'Kufafanua' Mambo ( Masuala )

Nilipishana na mwana CHADEMA 'mzungukaji' wa Kwanza ambapo alimsimamisha Mama Mmoja hivi na kuanza 'Kujinadi' na 'Kumnadi' Halima Mdee ambapo aliulizwa na huyo Mama kuwa ampe tu 'Tathmini' fupi ya 'Mema' yanayoonekana yaliyofanywa na Mdee ambapo kwa 'Masikitiko' yangu makubwa Yule Kijana aliishia 'Kujiumauma' tu na 'Kujilamba' mdomo kama Chatu wa Gamboshi.

Wakati naikatiza Mitaa ya Kawe mbele tena nikakutana na wana CHADEMA 'wanaozungukazunguka' na kuna Mmoja nikamuona 'kambananisha' Mzee wa Watu huku 'akimnadi' Halima Mdee amnbapo nilimsikia Yule Mzee akimuuliza Je, anadhani Siasa anazozifanya Mdee zinaendana na 'nyakati' tuliopo Kimaadili na Kimaendelea Jamaa akabadili 'Mada' na Kuanza Kuzungumzia Mechi ya Leo ya Yanga SC na Kagera Sugar.

CHADEMA Kawe nilikuwa nawaamini na kuwa na 'Imani' nanyi ila kwa 'Udhaifu' huu tu mchache niliouona Askofu Gwajima ni Mbunge rasmi Kawe.
 
Yawezekana tunatofautiana itikadi kisiasa, ila uliloligundua ndilo nimekuwa nikijiuliza:
Je, viongozi, wanachama na wanachama wa CHADEMA wanaifahamu na wanaweza kuilezea kwa ufasaha Ilani ya Chama, 2020?

Je, viongozi, wanachamana wafuasi wa CHADEMA, kwa kuponda, kubeza, kukejeli, na kudharau yaliyofanywa na CCM, kupitia Serikali inayongozwa na Magufuli, wanayo ya mazuri ya mfano waliyoyafanya katika utawala wa Mgufuli?

Sasa twende nyumba kwa nyumba, wanao omba kura wajibu hayo maswali na kueleza kitakachofanyika CHADEMA ikiingia mdarakani.
 
Halima hafai
Gwajima hafai zaidi...
Halima hafai kuwa mbunge.
Gwajima hafai kuwa hata mgombea tu..

Kawe mwaka huu I wish wawakatae wote
Halafu sijui hii hulka ya kumwambia mbunge hakuleta maendeleo watu wanaitoa wapi ?

Yaani karne ya 21 watu bado hawaelewi na kutofautisha majukumu na hisani.

Mwingine anakusanya kodi yako halafu maendeleo anabembelezws kuleta ila asiyepokea hata mia ndio anatakiwa kuleta maendeleo.

Hili ni tatizo la wananchi kukaa kusaidiwa saidiwa badala kudai haki ya kodi yao ndio maana wanaona maendeleo ni hisani au msaada kutoka kwa yeyote.
 
Yawezekana tunatofauriana itikadi kisiasa, ila uliloligundua ndilo nimekuwa nikijiuliza:
Je, viongozi, wanachama na wanachama wa CHADEMA wanaifahamu na wanaweza kuilezea kwa ufasaha Ilani ya Chama, 2020?

Je, viongozi, wanachamana wafuasi wa CHADEMA, kwa kuponda, kubeza, kukejeli, na kudharau yaliyofanywa na CCM, kupitia Serikali inayongozwa na Magufuli, wanayo ya mazuri ya mfano waliyoyafanya katika utawala wa Mgufuli?

Sasa twende nyumba kwa nyumba, wanao omba kura wajibu hayo maswali na kueleza kitakachofanyika CHADEMA ikiingia mdarakani.

Kwa hawa wana CHADEMA ambao naona 'wanazungukazunguka' hasa huku Jimboni Kawe nisifiche kiukweli hawako 'Competent' kwa Kuchambua.
 
Halafu sijui hii hulka ya kumwambia mbunge hakuleta maendeleo watu wanaitoa wapi ?

Yaani karne ya 21 watu bado hawaelewi na kutofautisha majukumu na hisani.

Mwingine anakusanya kodi yako halafu maendeleo anabembelezws kuleta ila asiyepokea hata mia ndio anatakiwa kuleta maendeleo.

Hili ni tatizo la wananchi kukaa kusaidiwa saidiwa badala kudai haki ya kodi yao ndio maana wanaona maendeleo ni hisani au msaada kutoka kwa yeyote.

Kwamba hulka ya kumwambia mbunge hakuleta maendeleo watu wanaitoa wapi? ni swali la msingi kwa asiyejua wajibu na nafasi ya mbunge kwa maendeleo ya jimbo analowakilisha bungeni.

Ni swali la msingi kwa mpiga kura anayeacha shughuli zake kwenda kwenye kampeni, lakini hajui kinachompleka huko!

Ni swali la msingi kwa mgombea anayetumia muda na rasmali zake kufanya kampeni, asijue atakapochaguliwa atapaswa kufanya nini, ili asiulizwe!
 
Kwamba hulka ya kumwambia mbunge hakuleta maendeleo watu wanaitoa wapi? ni swali la msingi kwa asiyejua wajibu na nafasi ya mbunge kwa maendeleo ya jimbo analowakulishabungeni.

Ni swali la msingi kwa mpiga kura anayeacha shughuli zake kwenda kwenye kampeni, lakini hajui kinachompleka huko!

Ni swali la msingi kwa mgombea anayetumia muda na rasmali zake kufanya kampeni, asijue atakapochaguliwa atapaswa kufanya nini, ili asiulizwe!
Mfano Zitto alisema amesaidia kupatikana kwa maendeleo kigoma,akataja mpaka kuinua zao la mchikichi kigoma maana ni zao la biashara lilikuwa limesahaulika!

JPM akasimama akasema Zitto anatafuta umaarufu kwani ni serikali kwa kupitia Dr Mpango ndio wamefanikisha suala hilo!!

Sasa hapa ninachojiuliza,mbunge anapaswa hayo maendeleo ayalete kutokea wapi?Akatafute pesa mwenyewe kwa wadau na azitumie kuleta maendeleo?Au atumie za kwake za mfukoni?Au atumie vijisenti kidogo vya mfuko wa mbunge ambazo haziwezi kufanya miradi mikubwa?Afanye lipi hasa ukizingatia kuwa akitimiza wajibu wake bungeni wa kuelezea matatizo ya wananchi bungeni na serikali ikaona haja ya kufanya hivyo na ikatatua basi mbunge anaambiwa hana mchango wowote kwani serikali imefanya!!!

Nilichoona ni kuwa wabunge wa CCM ndio wana haki ya kutumia miradi iliyotekelezwa na serikali kujinadi!Ila mbunge wa upinzani akitumia miradi iliyotekelezwa na serikalj yeye akiwa mbunge basi anaambiwa hapaswi kujinadi nayo kwani ni serikali imetekeleza!!!

Daaah mpaka kichwa kinauma,kazi ya mbunge hasa ni nini?????
 
Back
Top Bottom