Uchaguzi 2020 Jimbo la Kawe naamini Askofu Gwajima ataleta Mapinduzi makubwa ya maendeleo kuliko Mdee

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
680
1,338
Jimbo la Kawe limekuwa likiongozwa na CHADEMA kwa zaidi ya miaka kumi sasa chini ya Mbunge Halima Mdee.

Ki ukweli pasi na shaka yoyote sijaona juhudi zozote za Mbunge kupeleka hoja yoyote Bungeni kuhusu maendeleo ya Jimbo la Kawe zaidi ya kujikita na migogoro isiyo na tija.

Kitendo cha CCM kipindi hiki kumuweka Askofu Josepaht Gwajima kupeperusha Bendera ya CCM Jimbo la Kawe nawapa kongole kwa kutumia jicho la Tai.

Naamini Askofu Josepaht Gwajima atapata ushindi wa kishindo dhidi ya Mdee na vyama vingine na zaidi sie watu wa Jimbo la Kawe tutegemee maendeleo ambapo kwa zaidi miaka kumi Jimbo lilikuwa kama halina Mbunge.

Shime wa Kawe wote tuweke pembeni Uvyama na ushabiki ambao hauna afya bali sasa kura zetu zote tumpe Askofu Josepaht Gwajima kama kweli tunadhamira ya dhati ya kupata maendeleo.

Alex Fredrick
 
Wanakawe tunaenda kiivi.
Screenshot_20200921-191930_1600758337061.jpg
 
Nilijua ni jemba kumbe kiazi hana sera!
Roho wa Bwana kawafuta Bashite na Gwajiboy kwenye ulimwengu wa siasa...

Huyu ni mweupeee kwenye sera, mie naamini kadoneti samsing kwenye chama, wakamuachia jimbo akufe kivyake, aisee!

Mdee anashinda saa 2 asubuhi! Gwaji kapelekwa kumsaidia Mdee achukue ushindi!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Mbunge haleti maendeleo ila serikali pekee,
Mbunge ni mwakilishi wa wananchi bungeni katika kuwasemea shida zao tuu ila serikali ikiamua kuzifanyia kazi itazifanyia pia isipotaka itafanya ka tuonavyo
 
Kama kashindwa hata kujenga kanisa lake tu huko kwingine atawezaje?
Hilo swali halijibiki...gumu sana
Kawe wananchi wote kuhamishiwa jimbo la BIRMINGHAM, U.S. wakati Gwajiboy akiwajengea Kawe upya...
Anatia huruma, anapiga siasa za 1995..

Everyday is Saturday............................ :cool:
 
Hatutaki mapinduzi wala maendeleo tukio linalotarajiwa ni kuiondoa CCM,basi msituletee uvundo na kutaka kuondosha watu kwenye reli,CCM kwa ujumla wenu mnaondoka.
 
Yes mapinduzi makubwa yanakuja...

Just imagine... Wakazi kadhaa wa Kawe wanakwende Jimbo la Birmingham, Marekani (sijui ya wapi but na mimi natamani niende) na wa huko wanakuja Kawe.

Wana Kawe wapewe nn?!
 
Mbunge haleti maendeleo ila serikali pekee,
Mbunge ni mwakilishi wa wananchi bungeni katika kuwasemea shida zao tuu ila serikali ikiamua kuzifanyia kazi itazifanyia pia isipotaka itafanya ka tuonavyo
Magufuli anawaambia wawachague watu wenye connection
 
Back
Top Bottom