Uchaguzi 2020 Mechi kali nne za Uchaguzi Mkuu wa Wabunge ni majimbo ya Arusha Mjini, Kawe, Mbeya Mjini na Tarime Vijijini

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
8,256
9,085
1: Mwita Waitara Vs John Heche - Tarime Vijijini

2: Tulia Acskon Vs Sugu - Mbeya Mjini

3: Askofu Gwajima Vs Halima Mdee - Kawe

4: Mrisho Gambo Vs Godbless Lema - Arusha Mjini

Hizi ni mechi kali sana za kukata na shoka .

Nategemea wote wafanye kampeni za kistaarabu, wakinadi sera zao ili tuamue nani wawe wawakilishi.
 
1. Nabetia upande wa John Henche

2. Nabetia upande wa Sugu (Nguvu ya uma italazimisha matokeo halisi )

3. Nabetia upande wa Mdee ( Tofauti ndogo ya kura)

4. Nabetia upande wa Lema ( Ushindi kupewa baada ya vurugu kubwa na CCM kupata aibu ya Kimataifa)
 
1. Nabetia upande wa John Henche

2. Nabetia upande wa Sugu (Nguvu ya uma italazimisha matokeo halisi )

3. Nabetia upande wa Mdee ( Tofauti ndogo ya kura)

4. Nabetia upande wa Lema ( Ushindi kupewa baada ya vurugu kubwa na CCM kupata aibu ya Kimataifa)
Tusubiri tuone ,muda ni mwalimu
 
Hivi kweli unategemea Gwajima kumshinda Halima Mdee? Kwa wafuasi wapi alionao, hao wa jumapili tena wa kusombwa na mabasi toka Mkuranga, Kibaha, Gongo la Mboto, Chanika na hata Morogoro? Hao wala si wapiga kura wa jimbo la kawe.
Wewe kukalishwa ndio kushinda au haujasoma vizuri comnent yangu?
 
Mdee Lugha zake na matendo yake si aibu Kwa familia yake tu Ila Jimbo lote la kawe. Mda mwingi anatumia kwenye adhabu za ki bunge kuliko kuwatumikia wananchi. Ata familia yake ita pumzika kwa fedheha ambayo huwaletea pindi anapokua bungeni na nje ya bunge.
 
JE GWAJIMA ATATOBOA KWA HALIMA MDEE?

Na, Robert Heriel

Askofu Gwajima ni miongoni waliopeta kupeperusha Bendera ya CCM kwa nafasi ya Ubunge, Jimbo la kawe.
Nimpongeze kwa kupewa nafasi hiyo, lakini swali pekee analopaswa awe nalo muda huu; Je atatoboa mbele ya hasimu aliyejichimbia mizizi jimboni humo, Halima Mdee.

Bila shaka Gwajima amejipanga na mpaka anaamua kugombea tayari ameshaona kuna uwezekano wa kushinda katika jimbo hilo.

Halima Mdee naye najua kwa sasa yupo roho juu, kwani Gwajima sio mtu wa kubeza. Gwajima ni mtu mkubwa, anataasisi ya kidini iitwayo UFUFUO NA UZIMA, Gwajima ni msomi mzuri tuu hivyo elimu kwake sio tatizo, Gwajima anapesa, Gwajima pia anamdomo, anajua kuongea mno.

Hivyo ni kusema Gwajima anabebwa na mambo haya
1. Mmiliki wa taaasisi ya Kidini "KANISA LA UFUFUO NA UZIMA"
2. Msomi kWA ngazi ya PhD katika falsafa katika Teolojia
3. Mchungaji na Mhubiri wa kimataifa
4. Anajua kujenga hoja na kutetea hoja. Anamdomo.
5. Anapesa

Mpinzani wake ambaye ni Halima Mdee

1. Mwanasiasa wa kitaifa, sio kimataifa
2. Msomi wa ngazi ya shahada kama sijakosea LLB(Mwanasheria)
3. Mwanasheria kitaifa sio kimataifa
4. Anajua kujenga hoja na kutetea hoja, anamdomo.
5. Pesa za kawaida

Mambo ambayo Gwajima anamzidi Halima Mdee
1. Pesa. Hii nguzo kuu
Gwajima anautajiri wa kuonekana zaidi ya Halima mdee. Hivyo ni rahisi kuwashawishi watu kwa utajiri wake.
2. Umiliki wa taasisi kubwa
Gwajima anamiliki kanisa, kwani yeye ndiye aliyelianzisha, Kwa watu kama mimi tunajua kanisa ni kama kampuni tuu ya biashara. Hivyo muanzilishi ndiye anayepata faida zaidi. Gwajima kafanikiwa katika hili, Halima hamiliki taasisi yoyote inayofahamika.

3. Gwajima yupo kimataifa.
Gwajima kamzidi Halima katika kipengele hicho. Gwajima ana-connection kubwa kimataifa ukilinganisha na Halima Mdee. Hii ni kutokana na taasisi yake aliyoianzisha

4. Kamzidi Elimu
Gwajima anaelimu kubwa kuliko Halima mdee, nitaomba kusahihishwa ikiwa nitakuwa nimekosea. Halima Mdee anashahada moja akizidi sana basi ni mbili, wakati mwenzake anazozaidi ya tatu.

5. Umri
Gwajima kamzidi pakubwa Halima Mdee. Gwajima ni mtu mzima. Hii inaweza ikampa nafasi ya uzoefu katika maisha

6. Gwajima anafamilia
Gwajima anamke na watoto, wakati Halima Mdee hana Familia na sina uhakika kama anamtoto. Ni rahisi kumuamini mtu mwenye familia kuliko asiye na familia. Hii inamnyima nafasi kubwa Halima Mdee kwani wengi watamchukulia kama Mhuni.

Mambo ambayo Halima Mdee kamzidi Gwajima
1. Uzoefu katika Siasa
Halima Mdee kamzidi Gwajima uzoefu wa kisiasa. Halima Mdee anauzoefu mkubwa katika siasa kwani yeye katangulia kwenye mchezo wa siasa. Hii ni adavantage kwake, na inaweza kumsaidia kushinda

2. Taaluma ya Sheria inamahusiano makubwa na siasa.
Halima Mdee kutokana na kuwa yeye ni mwanasheria ambapo kwa sehemu kubwa siasa inaingiliana na sheria, na sheria ipo kwenye siasa, hii amemzidi Gwajima.
Gwajima mpaka aombe msaada wa kisheria kutoka kwa mwanasheria wake.

Kama utakuwa nami utaona jinsi Gwajima alivyomzidi mambo mengi Halima Mdee. Lakini hiyo itamfanya atoboe? Embu tuone.

Madhaifu ya Gwajima

1. Migogoro na jamii
Gwajima anamigogoro mingi na jamii. Nitatoa mifano

1.1 Mgogoro wa Gwajima na Waislamu
Gwajima alishawahi kuwa na Mgogoro na Waislam pale alipopinga hadharani kuhusu mahakama ya kadhi. Japo siku za baadaye alijidai kujisafisha mbele ya waislam kwa kusema kuwa ati walimlea sijui blah blah. Lakini baadhi ya waislam hawakupendezwa na matamshi yake. Na hata sidhani wamemsahau.

1.2 Mgogoro wa Gwajima na Kadinali Pengo
Ni katika tukio lile lile la kupinga mahakama ya kadhi hadharani ambapo Gwajima alimtolea maneno machafu Mzee Pengo. Hii ilifanya Gwajima apelekwe polisi. Mgogoro huu ulisababisha baadhi ya wafuasi wa Pengo na wafuasi wa Ukatoliki kutokumuelewa Gwajima, Sidhani kama Gwajima aliomba msamaha, na kama hakuomba msamaha sidhani kama wakatoliki walimsamehe.

1.3. Mgogoro wa Gwajima na Makonda
Moja ya migogoro iliyopandisha jina la Gwajima kitaifa ni pamoja na Mgogoro wa Makonda. Gwajima alishutumiwa kuhusika na Madawa ya Kulevya, sio yeye na wengine pia.
Gwajima aliibua swala la Mkuu wa Mkoa wa Dsm kuwa na vyeti feki, Mgogoro ule ulipelekea mambo mengi lakini aliyeshindwa alikuwa ni Gwajima. Huu mgogoro baadaye ulienda kuwa mgogoro binafsi baina ya Gwajima na Makonda

1.4. Mgogoro wa Gwajima na serikali.
Kupitia shutuma za madawa ya kulevya Gwajima alijikuta kaingia kwenye mikono ya dola. Hata hivyo alichomoa, na kusuluhisha.
Lakini juzi juzi Gwajima aliingia Mgogoro Mwingine na serikali ambapo Jeshi la Polisi lilimuita baada ya kuona kipeperushi na audio yenye sauti ya Gwajima ambayo ilikuwa inaelezea masuala ya ukabila. Hapa Gwajima alionywa.


2. UKABILA
Udhaifu mwingine aliouonyesha Gwajima ni suala la Ukabila. Kupitia vipeperushi na audio yenye sauti yake akihamasisha kabila la wasukuma kuunda vikundi vya watu 2000, kisha wasukuma matajiri wawasaidie masikini. Jambo hilo lilikemewa vikali na jeshi la polisi

3. SKENDO CHAFU
Gwajima anaskendo chafu, Skendo inaweza kuwa kweli au isiwe kweli.
Skendo ya umalaya, Gwajima anaskendo ya umalaya na hata baadhi ya video zilizoonyesha mtu afananaye naye kwa sura kwa asilimia mia moja zilivuja. Skendo hii aliikataa.
Skendo ya madawa ya Kulevya, hii pia alichomoa
Skendo ya kuwa na watoto wa nje, hii nayo anadai aliundiwa.

4. Lugha CHAFU
Gwajima kwa sehemu fulani analugha Chafu. Na hii inathibitishwa na alivyomtukana Mzee Pengo, Gwajima alitumia lugha chafu isiyoendana na taaluma yake. Pengine angekuwa mlevi ningemtetea

5. GWAJIMA NI KIGEUGEU
Gwajima ukimfuatilia vizuri utagundua ni mtu asiye na msimamo. Leo yupo hvii kesho yupo vile. Hii inadhihirishwa na kipindi alivyokuwa upande wa CHADEMA lakini tangu aingie Magufuli akabadili mfumo.
Pia Gwajima kwa nje anajionyesha kama mtu anayependa Waislam lakini msimamo wake wa kupinga mahakama ya kadhi kwa waislamu huku akitumia kigezo cha amani, kinadhihirisha hana msimamo.

Huenda madhaifu ni mengi lakini niishie hapa kwa Gwajima.

Madhaifu ya Halima Mdee

1. SKENDO
Halima Mdee anaskendo ya kuwa mfuasi wa mapenzi ya jinsia moja. Kumbuka Skendo inaweza kuwa kweli au isiwe kweli. Lakini wanaoisapuza Skendo hiyo wanatumia ushahidi wa baadhi ya picha ambazo zinamuonyesha Halima Mdee akimpelekea ulimi mwanamke mwenzake kama anataka kumnyonya ndimi. Hata hivyo Halima hajawahi kulikanusha jambo hili, na kama amekanusha basi mimi sikuwahi kumsikia.

2. Kutokuwa na Familia
Halima Mdee ni mwanamke mwenye umri mkubwa tuu wa kuweza kuwa na familia. Lakini mpaka hivi leo bado watu wengi hawajajua famiilia yake. Huenda anayo lakini kwa vile alifahamika hana, na hajawahi kuonekana nayo na wengi, basi watu wanajua Halima hana Mume.
Madhara ya udhaifu huu ni kuwa anaonekana kama mwanamke mhuni aliyeshindikana na wanaume, hata skendo ya usagaji inapata nguvu hapa.


Halima Mdee hana madhaifu mengi ukilinganisha na Askofu Gwajima. Halima Mdee hana Migogoro mingi na jamii ukilinganisha na Gwajima.

Mambo wanayolandana katika ya Gwajima na Halima Mdee.
1. Wote wanagombea Jimbo ambalo wao sio wazawa.
Halima Mdee asili yake ni huko Upareni, Kilimanjaro
Askofu Gwajima asili yake ni Msukuma, huko Mwanza
Wote wapo Ugenini.

Nani ananafasi ya Kushinda?

Gwajima
> Chama chake kinanguvu, kinanafasi ya kumpigania mpaka akashinda
> Taasisi yake ya dini.
Gwajima akiungana na Maaskofu wenzake mathalani, Kakobe, Mwamposa, Lusekelo na MWINGIRA Ambao kimsingi wapo maeneo ya karibu na jimbo la Kawe basi Gwajima anaweza akashinda.
Lakini kama hatakuwa na mahusiano mazuri na makanisa hayo nafasi yake ni ndogo
Sijajua Halima mdee anasali kanisa gani, lakini kama anasali makanisa makubwa najua watamsapoti. Ila hoja hii Gwajima itambeba zaidi kama atakuwa na mahusiano mazuri.

> Pesa, ingawaje eneo hili wakazi wake wengi wanajiweza lakini wanasema pesa haikinai. Gwajima ananafasi kubwa ya kushinda kwa kigezo cha pesa.

> Media na vyombo vya habari
Gwajima ni mpenda media, pia ana-connection na vyombo vya habari. Nafasi hii itambeba kujitangaza.
Pia Wanaofuatilia online Tv ya Gwajima ni watu karibia laki mbili hivyo hii pia inampana nafasi kujitangaza. Sisemi kuwa na wafuatiliaji wengi kwenye tv yako ndio kuchaguliwa, bali naeleza nafasi ya media kujitangaza.


HaLIMA MDEE
> Halima Mdee atahitaji kutumia udhaifu wa Gwajima kiasi kikubwa kumchafua ili watu wasimchague
> Wakazi wengi wa Kawe asili yao ni watu wa kaskazini hii itambeba Halima Mdee
> Kwa wale waliowaislamu wengi watabaki na chaguo moja tuu ambalo ni Halima Mdee
> Mazoea.
Wapo waliomzoea Halima Mdee, watamchagua kwa mazoea tuu.

Ukiangalia unaweza kuona jinsi ilivyongumu kwa Halima Mdee kushinda.

Lakini siku zote siasa ni mdomo,

Halima ajikite zaidi kushambulia madhaifu ya kimaadili aliyonayo Gwajima hiyo ndio pona pona yake.

Kwa bahati watu wa kawe ni watu wasioamini kuwa mbunge ndiye analeta maendeleo kwani wengi wao wameenda shule. Wakazi wa KAWE wanajua serikali ndio inaowajibu wa kuleta maendeleo. Bila kujali mbunge ni upinzania au chama tawala.
Watu wa Kawe wanajua Mbunge ni Mwakilishi wao.

Hivyo Gwajima asije akajikorga akasema kuwa atawaletea maendelep wakati wao wanajua kuwa maendeleo huletwa na serikali na yeye atakuwa mwakilishi wao tuu.

Watu wa Kawe ni wasomi hivyo wanajua Halima Mdee jukumu lake ni kuwasemea ndani ya bunge ili serikali itatue kero zao. Hivyo kama kero zao hazijatatuliwa wakati Mbunge wao Halima Mdee amepeleka Kero zao bungeni, wanajua kuwa serikali ndio imegoma kuwatatulia kero zao.

Baada ya kusema hayo kwa maoni yako, je GWAJIMA atatoboa mbele ya Halima Mdee?

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Back
Top Bottom