Kama uliweza kumaliza mitihani yako, weka hapa stori yako, mbinu, changamoto kuwapa matumaini watahiniwa

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
Duh aisee ule mziki wa CPA sijawahi ona, ulinipeleka mchaka mchaka mno hata nikiunganisha msuli wa form 6 E.C.A na degree bado haifiki hata robo, hata wanaotoka cpa kwenda masters huwa ni kama wameenda likozo na wanapasua masters si mchezo, lakini utoke masters uje cpa ni shughuli pevu.

Nilijisajili january ili nifanye sitting ya kwanza mwezi May, nilikuwa mgeni sana hivyo nikalipia tuition centre / review classes, mda huo nilikuwa nmeajiriwa kampuni private, nikitoka kazini naunganisha naenda centre mida ya saa 11, kwa ugeni wangu nilidhani system ni ile ile tu kama ya chuo nikachukua masomo 6 kwa mpigo bila kukaa chini na kutafakari kitu kizito nilichojibebesha, aisee nlikula za ovyoo ovyo hicho kitu kizito nilichijubebesha kilinitwanga kichwani nikaambulia kufaulu somo moja tu la B6 ambalo ni jepesi kuzidi yote, ni kama civics, siku hio nilivurugwa sana !!

Kosa nlilofanya hapo ni kwamba nilivamia masomo sita huku nikitarajia kwamba mitihni itakua kama kipindi nipo chuoni, nikawa napiga msuli wa kawaida tu juu juu wala sina presha, Yani hapo ndipo nilipopigwa kofi zito sana la uhalisia wa mitihani ya CPA jinsi ilivyo haitaki lele mama, maswali yanayotoka ni very very technical and more detailed, yanahitaji uwe umeelewa zaidi , inahitaji uwe umefanya revision ya maswali iliyoshiba si mchezo, tiketi ya ku clear mtihani ni kupata maksi 40% pekee ambayo ni "C" lakini hadi mtu aipate hio maksi ni shughuli pevu aisee, watu kibao wanapigwa kamba mguuni, wanaopata B inayoanzia 60% ni nadra sana huwa ni wa kuhesabika kati ya watahiniwa kibao, mtu kupata "A" sijajua maana mimi sikuwahi kuona japo nilikuwa naskia tu kuna mtu aliwahi kuipata.

Sitting ya pili nikaona wacha nijisomee kivyangu tu nikaona centre inanibana hasa nikzingatia muda wangu wa kusoma ni umeminywa na kazi, nikawa private candidate bila kujisajili kituo chochote, nililipia tu ada ya kufanya masomo bila kujaza sehemu naposomea tuition, nikachagua masomo yangu manne tu ili kuongeza umakini.

Material zangu nilinununua vitabu vingi vya pastpapers kwa wahitimu na kutuma mtu aninunulie pale ofisi za bodi vikitoka, nlikuwa nashusha pastpapers nyingi sana za bodi nyingine kama acca, cima, cpa ireland, cpa ghana, icpan nigeria, ca india, n.k. bando la elf 70 nilitenga kila mwezi kwajili ya youtube videos, notes , n.k.

Sitting ya pili nilirudia masomo manne B1, B2, B3 na B5, nikawa naamka kusoma saa kumi hadi mida ya saa moja kasorobo, nikifika kazini mida flani nakula pindi kimya kimya kwenye computer, saa 11 na nusu jioni nafika home nakaa hadi saa 12 ivi, naamsha naenda chimbo flani kulikuwa na college karibu na sehem nayishi haikuwa busy, napiga msuli hadi saa 3 narudi home. Weekends nako ivyo hivyo, ila ile ratiba ya jioni hadi usiku ilihamia saa 7 mchana hadi saa 10 jioni, jamani hiki kipindi sitasahau, musli hevi!! msuli wa notes ulkuwa asilimia 30 na msuli wa kusolve maswali asilimia 70, nilichomoa pepa zote B5 baba lao, B1 mama mwenye nyumba, b3 na b2, kiukweli nilipata motivation kubwa na nilisema lazima nimalize.

Mitihani ya sitting ya pili ilifanyika November huku tukisubiri matokeo, nikiwa nasubiria matokeo sikubweteka kwamba nianze kusoma bada ya matokeo kutoka january, nilianza kusoma masomo mawili ya b4 na c4 yote yanahusu taxation, baada ya takribani miezi miwili matokeo yalipotoka tayari nilikuwa mbali sana kwenye haya masomo niliyoanza kusoma mapema, hii mbinu ilinisaidia mno kubalance ratiba yangu kwenye sitting ya tatu inayofata na kunipa ahueni ya kupunguza msuli.

Sitting ya tatu ya may mwaka ujao nikafanya masomo manne, tayari masomo mawili ya b4 na c4 nilikuwa nina faida ya kuwa mbele, nikaongezea masomo mawili ya c1 na c2. masomo yale ya b4 na c4 nilikuwa nasoma weekend , msuli mzima niliufungulia kwenye c1 na c2, asubuhi c2 usiku c1 j3 hadi ijumaa, haya masomo ya c1 na c2 hayakua mapya sana maana hilo c1 ni kaka mkubwa wa b2 ambalo nilishafanya, nalo c2 ni kaka mkubwa wa b3 ambalo nilishafanya, upande wa c4 na b4 yote ni ya tax na uzuri ni kwamba ni mepesi ukishajua sheria za kodi ambazo nilizisoma kipindi wakati nasubiri matokeo ya sitting ya pili, pia c4 ina vitu vichache sana hata kitabu chake ni kidogo kuzidi vitabu vyote vya cpa hivyo ilikuwa advantage. matokeo ya sitting ya tatu yalitoka na nilifaulu masomo yote.

Mbinu ile ile, nikiwa nasubiria matokeo ya sitting ya tatu, nilikuwa nasoma somo lililobaki la c3 kidogo kidogo 😂 matokeo ya sitting ya 3 yalipotoka nikajihakikishia kwamba sasa nimebaki ulingoni na somo moja tu, hakuna tena michezo ya masomo mengi kunichangia huku mimi nipo pekeyangu, ikawa ni mimi na somo moja tu ulingoni, furaha ilioje!! ila sasa huyu C3 ni mfalme wa wafalme, huyu mjinga ukienda kichwa kichwa anakupa kichapo heavy na hana undugu na masomo mengine kama wenzake kina c1, c2 na c4, kitabu chake pia ni kikubwa😂 hapa silaha yangu kubwa ilikuwa focus na concetration ya asilimia 100 kwa somo moja tu, kiukweli nilichimba sana hili somo na kufanya maswali kibao, msuli nilipunguza hapa hata siku za jumamosi nlikuwa nasoma mchana tu na jumapili nipo free, kuamka asubuhi ikawa ni saa 11 sio saa kumi
emoji1783.png
siku ya mtuhani ikafika nikafanya pepa na nikaimaliza nikiwa na mategemeo ya kugonga "B", nimetoka kwenye pepa nikagundua kuna swali flani nimekosea hesabu a fedha ya kigeni, basi hapo matumaini ya alama ya B yakaisha na kweli nikaambulia "C", ilinipain kidogo ila nilifurahi sana kutua mzigo wa CPA.

Graduation sikwenda, ratiba zilinibana

Niliacha kazi private baada ya jambo kutiki serikalini

Nilimaliza CPA ila moto ilionipelekea siji sahau

CONCLUSION:

-Wahi kuanza kusoma cpa kabla ya majukumu mengi, ukimaliza tu chuo kama inawezekana, unganisha fasta.

-Kama umeamua kusoma cpa uwe umemaanisha, Cpa haisomwi kilelemama, cpa inahitaji jitihada kubwa mno, watu wengi hukatisha safari zao za cpa kwa kukata tamaa baada ya kufeli mara kwa mara ama sheria za bodi kuwalazimu kuacha, hivyo usitegemee kusoma cpa kama unavyosoma chuoni, huku mtu kufaulu somo inabidi upate alama ya C inayoanzia maksi 40 na hapo bado ni shughuli pevu inakubidi utie bidii, kuhusu kupata B ni nadra sana maana wanaozipata ni takribani asilimia moja tu ya watahiniwa, kuhusu alama A ni kama muujiza maana binafsi nimewahi kuiona moja tu kati ya maelfu ya watu wanaofanya mitihani hii.

-Solve sana maswali kuliko kusoma notes, solve maswali ya pastpapers ya Tz, ireland, india, nigeria, cima, acca, n.k

-Fanya walau masomo manne manne au matatu ili kupata timetable nzuri na concetration kubwa. kupiga masomo sita kwa mpigo si shughuli ya kitoto ile.

-Usifatilie matokeo ya wenzako unaweza kukata tamaa na kuwa jealous, binafsi sitting yangu ya kwanza nlipofanya masomo 6 na kufaulu 1 tu kuna wenzangu walifaulu manne, ila hadi navyohitimu walikuwa hawajamaliza maana kuna masomo yalikuwa yamewabana wanarudia hadi mara 3 ngoma inadunda, kiufupi kuwahi kuanza ku clear masomo mengi usimcheke yule ambae kafaulu moja au kafeli yote


-Mitihani ya may inakazwa sana kuliko novemba, tumia nafasi za novemba vizuri
 
Hongera
Ila yule Mama Zurii(Mke wa nick wa pili) Alifauluje kwa daraja la juu kabsa na kuwapita wotee?? Mimi na wewe hatujui
alipata zawadi ya kuongozea somo moja linaloitwa perfomance management (B5), yapo masomo mengi na kila somo anaeongozea anapewa zawadi.

kuongozea somo la b5 zawadi huwa ni kama laki 2 ukijumlishia zawadi za ziada za wanawake.

Kuna zawadi ya mwanafunzi bora kiujumla hii ndiyo yenye uzito, taasisi na mashirika mengi sana huwa yanatoa zawadi hapa, kama angechukua hii zawadi ukijumlisha na zawadi za wanawake hapa ni takriban fedha taslim milioni 12 na ofa ya ajira unaajiriwa safi tu.
 
Back
Top Bottom