Nilipotumia Mbinu ya wachina kufaulu mitihani

Beberu

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
3,945
7,945
.Happy Sunday to you all

Bas bwana, Enzi hizo nipo shule ya msingi walikuwa wanatoa zawadi kwa mtu wa kwanza hadi wa tatu, na mnasomwa kwa majina siku ya kufunga shule, so ni full maujiko kuitwa shule nzima inakuona, mpaka kufika darasa la nne mm nilikuwa sijawahi pata zawadi yeyote πŸ˜‚πŸ˜‚
Si kwamba nilikuwa natamani zawadi zile, la hasha! Moyo wangu ulikuwa unatamani zile sifa wanazopata watu, mana baada ya kuitwa yale majina story zote za wanafunzi kwa week inayofuata ni kuwadiscuss hao magenius ( tulikuwa bush so hata wakat wa likizo tulikuwa tunaonana kwa % kubwa)

Bas bana, BEBERU ikabidi niingie chimbo kubunu mbwinu ya mm pia kuingia pale top 3, kusoma ikawa hapana, sina hayo mazoea mimi, kuangalizia kwenye mtihani, nikikamatwa aibu itakuwa kubwa sanaaaa ( nilikuwa famous sana shule) hivo ikabidi nichekeche ubongo zaidi kupata mbinu bora na ndo nikaja na hii mbinu ya kichina

Pale darasani kuna jamaa alikuwa anaongoza (anakuwa wa kwanza ) toka tupo la pili hajawahi shuka kabisa, so mimi nikasema lazima nijue huyu jamaa anafanyaje, trick ya kwanza nikajiweka urafiki nae, (haikuwa kazi kubwa kwa sababu nilikuwa famous, na akili zipo top ten hunikosi shida top 3), step ya pili ndio uchina wenyewe sasa, nilikuwa namcopy yule jamaa kila kitu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ (sio kwenye mitihan, ulinzi ulikuwa mkali), ni kwenye maisha ya kawaida, yan natembea na jamaa muda wote, nakaa nae darasani kiti kimoja, akisema aanze kusoma nahakikisha nasoma anachosoma au tusome wote πŸ˜‚πŸ˜‚

In short nikawa kama yeye, nikajiunga uministrants (Wale wasaidizi wa padre pale kanisani kwa RC) Ili tu niwe karibu na jamaa nijue anafanyaje na anafaulu vipi, namba nawahi, yan tukawa marafiki sanaaa, ila ndo hivo mm namuiga tu jamaa sina mambo mengi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

#MATOKEO
Juhudi zangu zilizaa matunda kwan nikaanza kuwa wa pili darasani, toka darasa la tano mpaka la saba niliendelea kuwa wa pili darasani, sijawahi mshinda tule mwamba, jamaa hadi anamaliza alikuwa kajimilikisha namba moja nami kanipa mbili, ila ndo hivo, nadhani nilikosea kidogo, ningefanya kama wachina wa sasa (copy and improve) ningetoboa, mm nilifanya kama wachina wa zamani πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ just copy πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Nb.. sijawahi muangalizia kwenye mtihani mana tulikuwa tunapangwa upya, na kwa vile sisi huwa tunakaa class pamoja ko haikuwezekana kukaa pamoja kwa paper,
Ila ndo hivo, Nili improve ila sikumshinda master wangu
Vipi wew ulibunu mbwinu gani ili uweze kupanda kiufaulu au hata kimaisha ?

Karibuni snaa kwa mjadala,
Ni mimi yule yule Beberu J ila hapa nilitumia mbinu za kichina πŸ˜‚πŸ˜‚

Alamsiki πŸ‘‹
 
Binafsi sikuwa na mbinu zaidi ya kuongeza bidii kujisomea.
Wengi walikuwa wanajitahidi kushindana nami ila kwenye somo la hisabati ilikuwa utata wewe unishinde.

Kwa sasa maisha yamekuwa tofauti, nimewahi kuwa mwanafunzi wa kwanza kila ngazi ya kitaaluma darasani kwetu ila mfukoni huenda ninashika mkia😭😭😭
 
Mimi nilikuwa naiga hadi miandiko ya watu.

Naitoa vile vile wanavyoandika.

Naweza andika kwa hata mikono yote miwili alinivutia hivi jamaa yangu mmoja hivi anaandika mikono yote miwili.

Ukikaa na waridi lazima ununikie

Jamaa zangu wengi walikuwa wanaojiweza class ilinibusti na Mimi uzuri sikua vibaya sana.

Ndio kanuni ya maisha ilivyo ukikaa na vilaza na wazinguaji utafeli tu mishe zako
 
Hata mm bado napambana sana na uchumi mkuu, tulikuwa smart class ila mtaa unasumbua, ila kila jambo na wakati wake aisee
 
Basi Kuna wachina weusi wengi walikua wanapita na motion zangu kipindi hiko
Hahahaha mlitusaidia sana magenius, sisi tuliwacopy tu motion zenu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mimi nilikuwa naiga hadi miandiko ya watu.

Naitoa vile vile wanavyoandika.

Naweza andika kwa hata mikono yote miwili alinivutia hivi jamaa yangu mmoja hivi anaandika mikono yote miwili.

Ukikaa na waridi lazima ununikie

Jamaa zangu wengi walikuwa wanaojiweza class ilinibusti na Mimi uzuri sikua vibaya sana.

Ndio kanuni ya maisha ilivyo ukikaa na vilaza na wazinguaji utafeli tu mishe zako
Ahaaaaa wewe mwanangu ni nouma sana, sema kwenye maisha ya kawaida wenye pesa hawajiweki pamoja na mafukara, inabidi upambane kutoka kwanza chini ndo upate washindi
 
Mimi nilikuwa naiga hadi miandiko ya watu.

Naitoa vile vile wanavyoandika.

Naweza andika kwa hata mikono yote miwili alinivutia hivi jamaa yangu mmoja hivi anaandika mikono yote miwili.

Ukikaa na waridi lazima ununikie

Jamaa zangu wengi walikuwa wanaojiweza class ilinibusti na Mimi uzuri sikua vibaya sana.

Ndio kanuni ya maisha ilivyo ukikaa na vilaza na wazinguaji utafeli tu mishe zako
Ahaaaaa wewe mwanangu ni nouma sana, sema kwenye maisha ya kawaida wenye pesa hawajiweki pamoja na mafukara, inabidi upambane kutoka kwanza chini ndo upate
 
Kuna mwamba ilikua kila mwaka anakua wa mwisho na anaenda siku ya matokeo wanamtaja jina anasimama. Nlikua nashangaa sana yan unajua we unakuaga wa mwisho bado unaenda kuskiza matokeo. Uyo broo adi leo ni fala sana elimu muhim sana
Hahahaha huyo ana shida kwenye development yake, sio kawaida kabisa,
Pole yake sana
 
Kuna mwamba ilikua kila mwaka anakua wa mwisho na anaenda siku ya matokeo wanamtaja jina anasimama. Nlikua nashangaa sana yan unajua we unakuaga wa mwisho bado unaenda kuskiza matokeo. Uyo broo adi leo ni fala sana elimu muhim sana
Ufala wake Nini, kwenda kusikiliza matokeo au kuwa wamwisho kila Mara.
 
Ufala wake Nini, kwenda kusikiliza matokeo au kuwa wamwisho kila Mara.
Yani life inamsumbua sana sana juz apo nmeenda hom likizo nkamkuta amechoka sana anavaa danlop yale mabut ya shambn. Haelewi kesho yake ipoje ni huruma sana
 
Sasa primary unasoma nini??
Mi nilikuaga hata sisomi ila top 5 hunikosi.

Hiyo kitu imenisumbua sana nilipoanza form one, kule nilitakiwa kua nasoma mi nikadhani ni kama primary tu.
Mid term tests za mwezi wa tatu zilinitoa baru na nilikua kiongozi. Maticha walinipa mboko kichizi. Toka hapo nikabadilika na mimi nikaanza kusoma na kuwakimbiza...

Ila saivi ni mchimba chumvi mmoja huku kigoma, aloo elimu hizi.
 
Yani life inamsumbua sana sana juz apo nmeenda hom likizo nkamkuta amechoka sana anavaa danlop yale mabut ya shambn. Haelewi kesho yake ipoje ni huruma sana
Huyo jamaa pengine ana shida kwenye mfumo wa fahamu mkuu
 
Sasa primary unasoma nini??
Mi nilikuaga hata sisomi ila top 5 hunikosi.

Hiyo kitu imenisumbua sana nilipoanza form one, kule nilitakiwa kua nasoma mi nikadhani ni kama primary tu.
Mid term tests za mwezi wa tatu zilinitoa baru na nilikua kiongozi. Maticha walinipa mboko kichizi. Toka hapo nikabadilika na mimi nikaanza kusoma na kuwakimbiza...

Ila saivi ni mchimba chumvi mmoja huku kigoma, aloo elimu hizi.
Hahaha mkuu unadhani kwanin hukuwa wa kwanza ? Hicho ndo kitu mimi nilianza kukitafuta kwa mshikaji, mwenyewe nilikuwa sisomi na nilikuwa position nzuri tu
 
Back
Top Bottom