Bujibuji, cha muhimu si watu watasema nini wakisikia umekufa, muhimu ni wewe unafanya nini kujitayarisha na kifo chako wakati upo hai.
Waislaam tuna amini kuwa tunatembea na umauti na unaweza kutufika wakati wowote, mahali popote. Umauti hauna taarifa wala udogo wala uzee, hauna mzima wala mgonjwa, hauna mzuri wala mbaya. Upo na tunatembea nao.
Tuwe wacha Mungu, watenda mema, tujitahidi katika sadaka zitakazotusaidia hata tukisha kufa (Swadakat'uljaria). Kama kutowa elimu, kuwalea watoto zetu wawe wema, kuchimbisha visima, kujenga mashule na misikiti.
Nadhani bujibuji una point nzuri sana lakini ungeielekeza kuwa una/tuna jitayarisha vipi na umauti ingeleta raha zaidi.
Ukifa, watu watasikitika dakika moja au siku moja au wiki moja au mwaka mmoja lakini watakusahau na kuendelea na mambo yao. Muhimu ni vipi tunajitayarisha kuukabili umauti wetu.