God is Dead
JF-Expert Member
- Jan 11, 2019
- 1,311
- 1,533
1 Heche na wenzake wapigania demokrasia, watumwa wa Bwana wetu Yesu Kristo, kwa Watanzania wote walioko katika mapambano ya demokrasia na katiba mpya, pamoja na viongozi wao na wanaharakati wote:
2 Neema na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo ziwe nanyi.
3 Namshukuru Mungu wangu kila ninapowakumbuka ninyi.
4 Katika kila maombi yangu kwa ajili yenu nyote, huwa naomba kwa furaha,
5 kwa sababu ya ushirika wenu katika juhudi za katiba mpya tangu siku ya kwanza mpaka sasa.
6 Nami nina hakika ya jambo hili, kwamba Yeye aliyeanza kazi njema ndani yenu ataiendeleza hata itakapotimilika siku ya Kristo Yesu.
7 Ni haki kwangu kuwaza hivi juu yenu nyote, kwa sababu ninawachukua moyoni mwangu, kwa kuwa ninyi nyote mmeshiriki nami neema hii, katika kufungwa kwangu gerezani na katika kutetea na kuthibitisha habari njema ya demokrasia.
8 Maana Mungu ni shahidi wangu jinsi ninavyowaonea shauku ninyi nyote kwa upendo wa Kristo Yesu.
9 Nami naomba hili: kwamba upendo wenu uzidi kuwa mwingi zaidi na zaidi katika maarifa na hekima yote,
10 ili mpate kupambanua lililo bora zaidi; mpate kuwa safi na wasio na kosa hata siku ya Kristo,
11 mkijaa matunda ya haki kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.
12 Basi, ndugu zangu, nataka mjue kwamba mambo yaliyonikuta yamekuwa faida zaidi kwa kueneza mapambano ya katiba mpya.
13 Hata kifungo changu kimekuwa maarufu katika jeshi lote na kwa wengine wote, kwamba ni kwa ajili ya demokrasia.
14 Na wengi wa ndugu katika Bwana, wakiutumainia ujasiri wangu katika kifungo, wamezidi kuthubutu kunena neno la demokrasia pasipo hofu.
15 Wengine wanahubiri katiba mpya kwa husuda na ugomvi, lakini wengine kwa nia njema.
16 Wale wa mwisho hufanya hivyo kwa upendo, wakijua kuwa nimewekwa hapa kwa ajili ya kutetea katiba mpya.
17 Lakini wale wa kwanza hufanya kwa ubinafsi, si kwa moyo mweupe, wakidhani wataniongezea dhiki katika kifungo changu.
18 Lakini basi? Iwe kwa hila au kwa kweli, demokrasia inahubiriwa; na kwa hili nafuraia, tena nitaendelea kufurahi.
19 Kwa maana najua ya kuwa hili litanigeukia kuwa wokovu, kwa njia ya maombi yenu na msaada wa Roho wa Yesu Kristo.
20 Kama vile nilivyotarajia sana na kutumaini, kwamba sitaaibika kwa neno lo lote, bali kwa ujasiri wote, sasa kama siku zote, Kristo atatukuzwa katika mwili wangu, ikiwa ni kwa maisha au kwa mauti.
21 Maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo, na kufa ni faida.
22 Lakini ikiwa kuishi katika mwili kunazaa matunda ya kazi, sijui nichague lipi.
23 Ninasongwa na mambo mawili: nina shauku ya kuondoka na kuwa na Kristo (yaani ushindi kamili wa demokrasia), maana ni bora sana zaidi;
24 lakini kubaki katika mwili ni muhimu zaidi kwa ajili yenu.
25 Na kwa kuwa najua hili, nina hakika ya kwamba nitabaki na kuendelea nanyi nyote, kwa ajili ya maendeleo yenu na furaha yenu katika imani,
26 ili kwa kuwepo kwangu tena pamoja nanyi, mpate kuona fahari yenu nyingi zaidi katika Kristo Yesu.
27 Lakini mwenendo wenu na uwe wa kupatana na habari njema ya katiba mpya, ili, nijapo nikiwa mbali au nikija kuwaona, nipate kusikia habari zenu, kwamba mnasimama imara katika roho moja, mkishikamana pamoja kwa moyo mmoja kwa ajili ya imani ya katiba mpya,
28 bila kuogopa lo lote kwa adui zenu; jambo hili ni ishara kwao ya kupotea, bali kwenu ya wokovu, na hii ni kutoka kwa Mungu.
29 Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, bali na kuteswa kwa ajili yake;
30 mkiwa na mashindano yale yale niliyo nayo mimi, na sasa mnasikia habari zake, ya kuwa yako kwangu.
---