Kama tumefikia hatua ya kuachia watuhumiwa kwa sababu za kisiasa, Taifa letu linaelekea pabaya sana

Usiwe na wasiwasi kuhusu watuhumiwa wa ugaidi kuwa free, wamelegezwa hata ukiwauliza majina yao sasa hivi watakwambia mimi naitwa Mgonja au Mushi. Wamepata elimu ya Utanzania na hawana hamu na kuaribu sifa za dini tukufu tena. Kwa kifupi wamenyooka kama rula.
 
Nahisi nawe hoja unaiinua kisiasa.Ushindwe.Mpo wengi wenye mtizamo wa kipuuzi juu ya uongozi uliopo sasa.Udikiteta wenu umeisha nguvu.Tuinue taifa linalozingatia haki. Hamtaki ? Mungu keshaamua na iwe.Tumepitia mengi unanitia uchungu kwa bandiko lako hili.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Nitakijibu baade
 
" ni wazi kuwa ofisi ya Dpp inatumika kisiasa na haifanyi kazi zake kwa weledi "

..hili jambo ndio umeliona leo ?? Ina maana huko nyuma kipindi cha uncle JPM hukuliona hili au ulijigeuza mbuni kufutika kichwa ardhini?! Nadhani spana inayotumika kufunga nati ndio hiyo hiyo hutumika kufungua au??!
 
Watuhumiwa
Usiwe na wasiwasi kuhusu watuhumiwa wa ugaidi kuwa free,wamelegezwa hata ukiwauliza majina yao sasa hivi watakwambia mimi naitwa Mgonja au Mushi.Wamepata elimu ya Utanzania na hawana hamu na kuaribu sifa za dini tukufu tena.Kwa kifupi wamenyooka kama rula.
 
..walawiti watoto walipoachiwa kwa sababu za kisiasa.

1623958007698.png
 
Wewe mleta mada fikiria wangelikuwa ndio wazazi wako wamewekwa gerezani miaka 9 Bila ya kusomewa hukumu ya mashtaka yao ungeli furahi?

Binafsi yangu nampongeza DPP kwa kuwaachia huru raia wenzetu sababu ushahidi ulikosekana wa kuwatia hatiani

Hivyo basi nakushauri hii mada yako ungeli ifuta maana imejaa chuki
 
Ni wazi kuwa ofisi ya Dpp inatumika kisiasa na haifanyi kazi zake kwa weledi.

Kama watuhumiwa wa makosa ya kijinai wanaachiwa ili kufurahisha umma ni jambo baya sana kwa muktadha wa taifa letu.

Watuhumiwa wa ugaidi walikabiliwa na makosa mabaya sana. Mbaya zaidi waziri wa mambo ya ndani wakati huo Emmanuel Nchimbi alipointi wazi kuwa walihusika na umwagiaji watu tindikali huko Zanzibar.

Mimi binafsi nina hakika kuwa Emmanuel Nchimbi alikuwa na info za kutosha na za ukweli.

Ok achana na watuhumiwa wa ugaidi, kuna wapigaji na wabadhirifu nao wanaachiwa ili kufurahisha umma.

Hii ni hatua mbaya sana kwa taifa letu. Na haifai maana ni kama kukubaliana na kuunga mkono uhalifu

Zaidi, soma:

1).Uamsho wakana kuhusika na vurugu za Zanzibar

2). CCM yataka Uamsho Zanzibar ifutwe; Yataka Waziri wa Sheria ajiuzulu

3). Mahojiano Ya Mwandishi Jackton Manyerere Na Wana- Uamsho Zanzibar
Bora hata ingekuwa siasa. Hapo ni dini kwa kisingizio cha siasa.
 
Ni wazi kuwa ofisi ya Dpp inatumika kisiasa na haifanyi kazi zake kwa weledi.

Kama watuhumiwa wa makosa ya kijinai wanaachiwa ili kufurahisha umma ni jambo baya sana kwa muktadha wa taifa letu.

Watuhumiwa wa ugaidi walikabiliwa na makosa mabaya sana. Mbaya zaidi waziri wa mambo ya ndani wakati huo Emmanuel Nchimbi alipointi wazi kuwa walihusika na umwagiaji watu tindikali huko Zanzibar.

Mimi binafsi nina hakika kuwa Emmanuel Nchimbi alikuwa na info za kutosha na za ukweli.

Ok achana na watuhumiwa wa ugaidi, kuna wapigaji na wabadhirifu nao wanaachiwa ili kufurahisha umma.

Hii ni hatua mbaya sana kwa taifa letu. Na haifai maana ni kama kukubaliana na kuunga mkono uhalifu

Zaidi, soma:

1).Uamsho wakana kuhusika na vurugu za Zanzibar

2). CCM yataka Uamsho Zanzibar ifutwe; Yataka Waziri wa Sheria ajiuzulu

3). Mahojiano Ya Mwandishi Jackton Manyerere Na Wana- Uamsho Zanzibar

Idugunde tusikilize na sisi huenda ukajifunza jambo:

KISA CHA ''MAGAIDI'' WAWILI: SHEIKH RAMADHANI RAJAB CHAMBUSO NA SHEIKH AHMADA KIDEGE

''Akauliza muulizaji katika kuwahoji kwa shutuma za ugaidi ni nani anawalipa kwa kazi hiyo ya kusomesha Qur'an. Jibu likatoka kuwa hakuna anaewalipa ila wanaifanya kazi hiyo ili Allah awaridhie na kesho kiama awatie peponi.''

Charles Dickens ameandika kitabu maarufu, ''A Tale of Two Cities.''

Nimechukua jina la kitabu hiki kufanya ndiyo anuani ya hii makala ambayo kwa kweli nimeaindika mwaka wa 2016 lakini nimeona niiweke tena upya watu waisome kwa kuwa muda uliopita unaweza kutufunza mengi ya manufaa katika hili tatizo la Waislam wanaosomesha Qur'an kukamatwa na kufunguliwa kesi za ugaidi.

Kama ilivyokuwa kwa Masheikh wa Uamsho ushahidi haupatikani na baada ya watuhumiwa kuteseka gerezani huachiwa.

Vijana hawa wawili wote ni waalim wa Qur'an na vijana wazuri na wema wao unafahamika na kila mtu mjini Tanga wanapoishi na kufundisha Uislam.

Kwa sifa hizi zao walipokamatwa kwa vipindi tofauti kwa tuhuma za ugaidi watu walisema, ''Si bure kuna jambo Chambuso na Ahmada walezi na walimu wa wanetu hawawezi kuwa magaidi.''

Hili jambo ni lipi?

Mpenzi msomaji wangu makala hii inaweza kukutegulia kitendawili hiki.

Soma na tafakari na ukimaliza kutafakari waombee dua vijana wetu wanaoshughulika na kukisomesha kitabu cha Allah:

Sheikh Rajab Ramadhani Chambuso ni katika vijana wadogo wa Tanga niliopata kusubiana naye kwa kipindi cha miaka 15 niliyoishi Tanga.

Nilifahamiana pia na mwenzake Ahmada Kidege ambao wote wakishughulika na kusomesha Uislam.

Sheikh Chambuso yeye ndiye alikuwa karibu na mimi zaidi.

Nilimjua kama mwalimu wa Islamic Knowledge akipita shule za sekondari akisomesha wanafunzi wa Kiislam elimu ya dini yao.

Kabla hatujafahamiana vizuri tulikuwa tukipishana alfajr tukifanya mazoezi ya kukimbia Barabara ya Bombo.

Nakumbuka kumuona akitembea kwa miguu shule moja baada ya nyingine jasho likimtoka kwenda kuwahi kipindi mimi nikiwa katika gari yangu na kiyoyozi kinaunguruma.

Wakati ule sikuwa sana karibu na yeye lakini nilipokuja kumzoea nikajafahamu kuwa anasomesha kote mjini na nje ya mji kwa kujitolea.

Haukupita muda alinunuliwa baiskeli na muhisani aliyeguswa na juhudi ile ya kijana mdogo kujitolea kuwasomesha watoto dini ya Allah bila ya malipo yoyote yeye akitegemea radhi za Allah.

Huu ukawa pia ni mwanzo wa uhusiano wangu na Sheikh Chambuso ikawa na mimi kwa namna yangu nasoma kwake kila tunapokuwa pamoja katika mazungumzo ya kawaida tu.

Ukiwa karibu ya waridi hukosi kunukia.

Sheikh Chambuso akanisoemsha historia ya Tanga na taasisi zake kubwa za Uislam kama Shamsiyya, Zahrau na Maawal Islam na baadae Shamsi Maarif ilipokuja kuanzishwa wakati mimi bado nipo Tanga.

Sheikh Chambuso ni kijana maarufu mjini kwa ile heshima yake ya kumtumika Allah na waja wake.

Wanafunzi waliopita mikononi mwake kuwasomeshsa hawana idadi. Kupitia Sheikh Chambuso na mimi rafiki na nduguye nikawa nasafiria nyota yake nikifahamika kama ‘’rafiki yake Chambuso.’’

Sheikh Chambuso hakutosheka na kuwa anapita kwenye shule kusomesha akawa sasa anaingia hadi kufanya ushauri kwa wanafunzi wa Kiislam katika wale aliokuwa akiwasomesha dini masomo gani wachukue kwa ajili ya mstakbali wao wa baadae.

Hapa ikawa sasa Sheikh Chambuso anaingia katika anga ambayo kwa hakika ilikuja kuwanufaisha vijana wengi na wengi wao wakafanikiwa.

Lakini kubwa lililokuja kunifurahisha ni pale alipoamua yeye na wenzake kuanzisha shule ya chekechea ya Kiislam na kuanza shule ya msingi.

Sasa tena Sheikh Chambuso akawa anaongeza ulezi juu ya kusomesha.

Madrasa yake na shule ya chekechea ikawa imejaa pomoni.

Mimi binafsi furaha yangu ilikuwa haina kifani.

Sheikh Chambuso akaongeza na ‘’idara,’’ nyingine siyo rasmi akawa anapita kwa Waislam kuwaomba kuwasomesha katika shule yake watoto mayatima na wale ambao wazazi wao Allah amewapa mtihani wa kipato.

Haikuwa ajabu kumuona Sheikh Chambuso amafatana na daktari kumpeleka katika nyumba ili amtie suna mwanafunzi wake ambae kwa shida za umasikini kapita umri wa kutiwa suna.

Huwezi kummaliza Sheikh Chambuso.

Siku moja baada ya kutoka Tanga kwa kustaafu kazi nilirudi Tanga na nikenda kumtembelea Sheikh Chambuso shuleni kwake.

Ile kuniona tu na baada ya kusalimiana ghafla akasimamisha masomo katika madarasa akawatoa wanafunzi wote nje ya wakapanga mstari ili wanisalimie.

Sheikh Chambuso alikuwa anazugumza na ule mkusanyiko kwa Kiarabu.

Niliyoshuhudia pale niliinamisha kichwa changu chini sikuweza kujizuia.

Machozi yalinilengalenga.
Kumbe mambo haya yanawezekana…

Lakini kuutumikia Uislam una changamoto zake hasa nyakati hizi za ''siasa za ugaidi.''

Haukupita muda Sheikh Chambuso akakamatwa na kuwekwa rumande kwa kesi ya ‘’kushawishi mauaji,’’ akawekwa ndani rumande Handeni majuma mawili.

Sheikh Chambuso hana sifa ya uovu mimi binafsi na kila aliyesikia habari hizi alisikitika na kushangaa.

Hii ilikuwa kesi ya kubambikizwa kama ilivyokuja kudhihirika hapo baadae.

Siku ya pili yake zilipopatikana taarifa kuwa Sheikh Chambuso kakamatwa mji mzima wa Tanga ulizizima kwani ni nani asiyemjua Sheikh Chambuso mwalimu na mlezi wa watoto wao?

Ule msururu wa ingia toka nyumbani kwake kuanzia alfajir kuna baadhi ya watu walidhani nyumbani kwake kuna msiba kafa mtu.

Sheikh Chambuso alihangaishwa sana na kesi hii ambayo alinifahamisha kuwa polisi wanaiita, ''kumfunga mtu paka mweusi shingoni.''

Sheikh Chambuso mwenyewe alikuja kunambia kuwa ile kesi imemfunza mengi na imemuongezea elimu ambayo asingeweza kuipata popote.

Kwangu mimi ikawa sasa Sheikh Chambuso kawa shule na mwalimu pia na mimi nasoma kwake na kujifunza.

Hii ilipelekea mimi kuandika mengi kuhusu madhila mengi yanayowakabili Waislam kiasi nilimkaribisha msikiti kwetu aje kuzungumza na Waislam na nilimwekea ukurasa makhsusi kwa ajili yake katika kipindi chote alichokuwa mahakamani kujibu tuhuma za ''kushawishi mauaji:''

Ukurasa huu wa Sheikh Chambuso ulisomwa na watu wengi sana na ulikuwa na taarifa nyingi za uchunguzi kwa kuhusu ukweli wa tuhuma za ugaidi dhidi ya Waislam.

Huwa kila akija Dar es Salaam basi Sheikh Chambuso atanipitia kwangu kunijulia hali na kunieleza shule inavyokwenda na taarifa nyingine za vijana wa Kiislam Mkoani Tanga.

Mara ya mwisho nilipokutananae nilimuuliza kuhusu mwanafunzi wake mmoja bint nillitaka kujua maendeleo yake.

Sheikh Chambuso akaniambia, ‘’Yule bint anamaliza shahada yake ya Udaktari.’’

Kama nilivyotahadharisha hapo awali.

Kabla hatujaagana Sheikh Chambuso akanifahamisha kuwa wamefungua shule ya ushoni kwa wasichana inayoongozwa na Sheikh Khamisi Shemtoi ambae yeye mwenyewe licha ya kuwa sheikh ni fundi cherahani bingwa.

Huwezi kummaliza Sheikh Chambuso na wenzake kila unapokutananao basi watakuwa na jema la kukueleza kukufurahisha.

Kubwa ninalofaidi kwa Shekh Chambuso ni kule kunifunza misemo ya Kiarabu ambayo imekuwa silaha yangu kubwa katika mijadala.

Mathalan siku moja tunazungumza jambo akanipa jibu kwanza kwa Kiarabu kisha akanifanyia tafasiri akasema, ''Ukiijua sababu inaondoa ajabu.''

Kuna mfano mmoja alinipa kueleza jambo lililovurugika na watu kujaribu kulirejesha kama lilivyokuwa hapa mwanzo.

Akanambia, ''Sheikh Mohamed chukua mfano wa kioo kishavunjika na wewe ukajaribu kukiunga, hakiwezi kuwa kama kilivyokuwa hapo mwanzoni.

Ukijitazama na kioo hicho utaiona tofauti.''

Sheikh Chambuso anasema yeye misemo hii kafundishwa na Sheikh wake Marehemu Sheikh Mohamed Ayub.

Siku moja tulikuwa katika gari yangu nikaweka CD ya Sheikh Mohamed Ayub anadarsisha tafsir ya Qur'an darsa za L'Asr Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Msomaji kasoma aya mbili tatu kamaliza Sheikh Mohamed Ayub anaanza kusomesha.

Nikamuona Sheikh Chambuso ghafla uso umembadilika kajiinamia akanambia, ''Sheikh Mohamed mimi hapo nipo sisi wanafunzi wadogo tuko safa ya nyuma mbele pale namuona sheikh mwenyewe kazungukwa na wanafunzi wake wakubwa ambao ndiyo walikuwa walimu wetu sisi, Sheikh Mohamed Bakari, Sharif Sayydid Hussein, Sheikh Zuher bin Ali bin Hemed bin Al Buhry...''

Sheikh Chambuso hakika ni kijana hazina kwa watu wa Tanga na umma wa Waislam wa Tanzania kwa usomi wake makini na jinsi amavyojibiidisha kuitumikia jamii.

Sheikh Ahmada Kidege hivi sasa yuko Gerezani kwa tuhuma za ugaidi na wakati anakamatwa alikuwa anasimamia ujenzi wa hospitali kwa ajili ya wanawake.

Picha: Sheikh Ramadhani Rajab Chambuso akigawa mashafu tafasiri ya Sheikh Ali Muhsin Barwani kwa wanafunzi wake St. Christina Secondary School Tanga.

Picha ilipigwa 2006 wakati akiwa Sheikh na Mwalimu ''mtoto.''

Picha ya pili kulia ni Sheikh Chambuso na Sheikh Ahmada Kidege Tanga 2012.

Screenshot_20210617-225640_Gallery.jpg
 
Ni wazi kuwa ofisi ya Dpp inatumika kisiasa na haifanyi kazi zake kwa weledi.

Kama watuhumiwa wa makosa ya kijinai wanaachiwa ili kufurahisha umma ni jambo baya sana kwa muktadha wa taifa letu.

Watuhumiwa wa ugaidi walikabiliwa na makosa mabaya sana. Mbaya zaidi waziri wa mambo ya ndani wakati huo Emmanuel Nchimbi alipointi wazi kuwa walihusika na umwagiaji watu tindikali huko Zanzibar.

Mimi binafsi nina hakika kuwa Emmanuel Nchimbi alikuwa na info za kutosha na za ukweli.

Ok achana na watuhumiwa wa ugaidi, kuna wapigaji na wabadhirifu nao wanaachiwa ili kufurahisha umma.

Hii ni hatua mbaya sana kwa taifa letu. Na haifai maana ni kama kukubaliana na kuunga mkono uhalifu

Zaidi, soma:

1).Uamsho wakana kuhusika na vurugu za Zanzibar

2). CCM yataka Uamsho Zanzibar ifutwe; Yataka Waziri wa Sheria ajiuzulu

3). Mahojiano Ya Mwandishi Jackton Manyerere Na Wana- Uamsho Zanzibar
1. Nionavyo mimi, mtu akituhumiwa huwa kuna "ushahidi wa kuanzia" kwamba katenda kosa fulani na ushahidi huo wa kuanzia unaendelea kutafutwa na haiwezekani kuutafuta hadi siku ya mwisho wa dunia (indefinitely). Lazima kuwe na kikomo cha uchunguzi na uamuzi uweze kutolewa.
2. Lazima kuwe na "muda wa kutosha" (reasonable time), lakini siyo muda mrefu kupita kiasi (prolonged time).
3. Kesi ikichukua miaka 7, 8, 9 au 10 nk na ushahidi kama haujakamilika, inawezekana hautakamilika tena.
4. Kwa muda huo huenda baadhi ya mashahidi watakuwa wameshafariki, wamehamia mbali na wengine wamehama nchi au aina yao ya kazi au biashara imewafanya wasafiri mara kwa mara na hivyo si rahisi tena kupatikana kutoa ushahidi mahakamani.
5. Kesi inaweza kuchunguzwa kuanzia siku ya 1 mtu anapotuhumiwa na kwa upande wangu kama itapita miezi sita bila uchunguzi kukakimilika inawezekana kabisa mtuhumiwa alipokamatwa huenda hapakuwa na "ushahidi wa kuanzia" unaoonyesha matumaini ya kuuendeleza hadi kufikia mwisho wake.
6. Katika mazingira kama haya, ili kutenda haki/haki ionekane ikitendeka (bila kucheleweshwa) kama muda mrefu wa kutosha (reasonable time) umepita na uchunguzi wa kesi haujakamalika, heri mtuhumiwa aachiewe huru kuliko kuendelea kumshikilia gerezani kwa maana kwamba endapo ushahidi mpya utapatikana unaoonyesha mwendelezo wa "ushahidi wa kuanzia" basi mtuhumiwa anaweza kukamatwa tena ili afikishwe mahakamani na kesi yake iendelee pale ilipokuwa imefikia kutokana na kutokuwepo dalili za kupata ushahidi zaidi.
7. Tukifanya hivi, tutakuwa tukitenda haki na hakutakuwa na ulazima wa kuwashikilia watu kwa muda mrefu kupita kiasi, halafu baadaye serikali iseme haina interest na kesi na kuwaacha watuhumiwa katika hali ya umaskini/ugonjwa au uzee unaotokana na kukaa rumande muda mrefu na bila fidia.
 
Back
Top Bottom