Taifa letu linahitaji viongozi wenye maono ya muda mrefu

Tizzo G

Member
Jun 9, 2012
24
14
Yanipasa kufikiria mara mbili tatu kwanini haya yanatokea.

Serikali yetu ya Tanzania ilishawahi kuingia mikataba mingi huko nyuma ambayo imeliingiza Taifa letu kwenye Hasara kubwa na wizi wa kutisha.

Najiuliza mara nyingi sana, kwanini Hawa viongozi wanaotumia Kodi zetu wanakua na kiburi kilichopitiliza kwenye Mali za Taifa? Kwani wao wana haki zaidi wengine?

Utawala waweza kua chanzo Cha vita kwenye nchi, viongozi wetu waelewe wananchi wana uchungu na Mali za Taifa lao.

Enyi watanzania Tujiulize kwanini Mkataba wa Bandari unapingwa na wataalamu wa Sheria? Mawakili wetu wazalendo? Hivi Hawa viongozi wa serikali ambao sio wanasheria wanataka kutuambia wao ni wataalamu kuliko hao mawakili?

Najiuliza ni Nini kipo nyuma ya pazia Kwa watu wasio wataalamu wa Sheria kulipigia debe suala la kisheria? Kulitetea kwake kunahitaji utaalamu wa Sheria na sio utaalamu tu Bali ubobezi kwenye Sheria.

Kwanini wanaCCM wanafanya hivyo? Ni Kwa sababu hakuna kiongozi yeyote wa serikali ambao wanaweza kupinga mawazo ya Rais Kwa kuogopa kupoteza ugali wao au Kwa sababu wanafaida katika jambo husika?

Kwanini Serikali Kwa ujumla isitafakari hili?

Na je ni nani wa kuwajibishwa endapo mkataba huu utaleta hasara Kwa Taifa letu?

Basi Mimi naunga mkono mkataba huu ufanye kazi TU pale tutakapokubali Kubadilisha kipengele cha Kinga ya Rais kutoka kwenye katiba na kumwondolea Kinga ya kutokushtakiwa baada ya Mda wake wa urais.

Kinga ikiondolewa maana yake ni kwamba mkataba huu ukiwa na hasara Kwa Taifa Rais na waziri mkuu wake waburuzwe mahakamani na kushtakiwa na ikibidi kufilisiwa Mali zao zote.

Kwanini kama Taifa tunaibiwa halafu hakuna tunaeweza kumwajibisha? Kinga ya kutokushtakiwa Kwa Rais ndio inayotoa kiburi Kwa Kiongozi mkuu wa serikali, akiamini hata kama akifanya kosa, kosa hilo halitakua na madhara yoyote kwake Bali ni Kwa Taifa.

Kilichotokea Ngorongoro na Kilichotokea Loliondo hatujawahi kuambiwa faida tunayopata kama Taifa, ila watanzania wenzetu walikufa bila sababu na mpaka Sasa hatujui tunapata faida Gani?

Kiburi na ulevi wa madaraka Kwa viongozi wa serikali vinaoneshwa na ripoti ya CAG ya Kila mwaka jinsi wasivyo tayari kubadilika, Kila mwaka mambo ya ubadirifu unaibuliwa Kwa viongozi waliopo madarakani lakini hamna hatua zinazochukuliwa.

Kama watanzania yatupasa tuchukue hatua itakaytoa onyo kwenye kuwawajibisha viongozi waliopo madarakani. Mimi mtanzania naenda hospitali nakosa dawa Ile Hali nasikia Kuna mtu amekwapua mabillion ya Kodi zetu? Kweli kwa Hali hii niendelee kuwaamini wasakatonge hawa?

Taifa letu linahitaji viongozi wenye maono ya muda mrefu. Mungu tupe nguvu tupate umoja wa kuokoa mali zetu kutoka kwa wasakatonge.
 
Yanipasa kufikiria mara mbili tatu kwanini haya yanatokea.
Serikali yetu ya Tanzania ilishawahi kuingia mikataba mingi huko nyuma ambayo imeliingiza Taifa letu kwenye Hasara kubwa na wizi wa kutisha.
Najiuliza mara nyingi sana, kwanini Hawa viongozi wanaotumia Kodi zetu wanakua na kiburi kilichopitiliza kwenye Mali za Taifa? Kwani wao wana haki zaidi wengine?
Utawala waweza kua chanzo Cha vita kwenye nchi, viongozi wetu waelewe wananchi wana uchungu na Mali za Taifa lao.
Enyi watanzania Tujiulize kwanini Mkataba wa Bandari unapingwa na wataalamu wa Sheria? Mawakili wetu wazalendo? Hivi Hawa viongozi wa serikali ambao sio wanasheria wanataka kutuambia wao ni wataalamu kuliko hao mawakili?
Najiuliza ni Nini kipo nyuma ya pazia Kwa watu wasio wataalamu wa Sheria kulipigia debe suala la kisheria? Kulitetea kwake kunahitaji utaalamu wa Sheria na sio utaalamu tu Bali ubobezi kwenye Sheria.
Kwanini wanaCCM wanafanya hivyo? Ni Kwa sababu hakuna kiongozi yeyote wa serikali ambao wanaweza kupinga mawazo ya Rais Kwa kuogopa kupoteza ugali wao au Kwa sababu wanafaida katika jambo husika? Kwanini @tz_serikali Kwa ujumla isitafakari hili?
Na je ni nani wa kuwajibishwa endapo mkataba huu utaleta hasara Kwa Taifa letu?
Basi Mimi naunga mkono mkataba huu ufanye kazi TU pale tutakapokubali Kubadilisha kipengele Cha Kinga ya Rais kutoka kwenye katiba na kumwondolea Kinga ya kutokushtakiwa baada ya Mda wake wa urais. Kinga ikiondolewa maana yake ni kwamba mkataba huu ukiwa na hasara Kwa Taifa Rais na waziri mkuu wake waburuzwe mahakamani na kushtakiwa na ikibidi kufilisiwa Mali zao zote.
Kwanini kama Taifa tunaibiwa halafu hakuna tunaeweza kumwajibisha?
Kinga ya kutokushtakiwa Kwa Rais ndio inayotoa kiburi Kwa Kiongozi mkuu wa serikali, akiamini hata kama akifanya kosa, kosa hilo halitakua na madhara yoyote kwake Bali ni Kwa Taifa.
Kilichotokea Ngorongoro na Kilichotokea Loliondo hatujawahi kuambiwa faida tunayopata kama Taifa, ila watanzania wenzetu walikufa bila sababu na mpaka Sasa hatujui tunapata faida Gani?
Kiburi na ulevi wa madaraka Kwa viongozi wa serikali vinaoneshwa na ripoti ya CAG ya Kila mwaka jinsi wasivyo tayari kubadilika, Kila mwaka mambo ya ubadirifu unaibuliwa Kwa viongozi waliopo madarakani lakini hamna hatua zinazochukuliwa.
Kama watanzania yatupasa tuchukue hatua Kali sana kwenye kuwawajibisha viongozi waliopo madarakani.
Mimi mtanzania naenda hospitali nakosa dawa Ile Hali nasikia Kuna mtu amekwapua mabillion ya Kodi zetu? Kweli Kwa Hali hii niendelee kuwaamini wasakatonge Hawa?
Taifa letu linahitaji viongozi wenye maono ya Mda mrefu. Mungu tupe Nguvu tupate umoja wa kuokoa Mali zetu kutoka Kwa wasakatonge.
Siku wanausalama wetu wamekuwa wazalendo ya Gabon tunaweza kuyaona Tanzania.

Shida kubwa ni kwamba hata wana usalama wa TZ wengi ni wachumia tumbo
 
Umeandika kama mtanzania halisi, mzalendo na mwelewa ila umesahau zaidi ya watanzania 70% hawana ufahamu huo ulionao, viongozi ni reflection ya watu wake walivyo na ndio maana wanaweza kufanya lolote bila aibu maana pia wananchi hamuwezi kuwafanya lolote na wanajua kubaki madarakani ni lazima kura zinaamuliwa na wanaohesabu sio wanaopiga
 
Back
Top Bottom