Kama ni kweli na ushahidi upo....

mbona una kiherehere ,bashite hachomoki ,subiri kesi ya kikatiba ikianza cross examination ndo atabanwa mbele ya hon judge and ruling itaweka precedent kwenye law report kuwa kuchakachua vyeti ni criminal offence,
Asilete kwa nani? Ni mamlaka gani iliyomuagiza awasilishe vyeti vyake na akakosa kutekeleza?
Tunaichelewesha Tz kufanyaje?
Kesi ya kikatiba inahusiana nini na kesi ya jinai?
Zamani nilitegemea kuwa watu wenye majina, ingawa wanatumia avatar ghushi humu jf ni GT sana na huwaza mambo kwa kuchambua kitulivu, lakini sasa inaonekana baada ya wauza ngada kushikwa pabaya, tayari wamemwaga'ela zao kutuchafulia hali ya hewa humu jamvini.
Ingekuwa kinyume na ninayoyasema, Paulo Makonda kashika nyadhifa nyingi sana kabla ya u-RC. Yote mabaya anayoelekezwa ambayo hayakusikika kabla ya kuanzisha vita vya mihadarati yangekuwa yalishasikika kitambo.
Je interview waliyofanyiwa wazazi wake na mwandishi Mketema kueleza historia yake nayo ni ghushi?
 
Aisee!

So that is the standard of proof now?

Kwamba ukiamua kukaa kimya juu ya mambo yanayozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii basi una hatia?

Scratching my head.....literally!
Kama kuna kesi yoyote kuhusu hayo mambo ya vyeti basi itakuwa ni criminal. Criminal cases zote katika nchi hii zinakuwa prosecuted na DPP ama mtu anapewa ruhusa na DPP kushitaki. DPP kwa maana nyingine ni Jamhuri ndio maana kwenye kesi za criminal parties huwa ni Republic v Accused. Tanzania hatuna Private Prosecutors labda upate ruhusa ya DPP.
Katika kesi za jinai huwa ushahidi unaotakiwa ni beyond reasonable doubts yaani bila kuacha mashaka yoyote. Hii iko hivyo kwa sababu katika kesi hizi ukipatikana na hatia hukumu zake huwa kubwa ndio maana hawataki ushahidi unaotolewa uache shaka. Kukiwa na shaka mtu anaweza kuhukumiwa kunyongwa kwa ushahidi wenye mashaka.

Kwa upande wa kesi za madai kwenye ushahidi huwa inatosha tu kuwa kuwa na balance of probability. Hizi kesi huwa kwa KAWAIDA huwa hakuna vifungo bali kumlipa mshitaki damages siyo faini.
 
Paulo Makonda kashika nyadhifa nyingi sana kabla ya u-RC.

Zipi?

Yote mabaya anayoelekezwa ambayo hayakusikika kabla ya kuanzisha vita vya mihadarati yangekuwa yalishasikika kitambo.

Jaribu kuwa mfuatiliaji ndugu. Lakini tuchukulie kuwa tuhuma hizo ni za kweli kuwa ametumia cheti kisicho chake, na ni kweli mchapa kazi kwa sheria na taratibu zetu za sasa anastahili kutoshitakiwa?

Kwa mtazamo wangu, kufeli si kosa na ndio maana zikawekwa nafasi mbalimbali za kusahihisha makosa na hatimaye kufika hatua fulani kielimu. Pia nilidhani jambo mojawapo la "kuinyoosha nchi" ni kututoa wananchi katika hali ya kupenda njia za mkato ili kupata mafanikio kwa kuvunja sheria lakini naona tofauti.

Tumekuwa tukisisitizwa kutii sheria bila shuruti. Mamlaka husika ziwe kielelezo katika hili ili wananchi tuwe hata na moyo wa kusaidia mamlaka hizo. Mfano, kwa hali iliyopo juu ya suala hilo, kama kuna mtu ana ushahidi mzito kuwa ni kweli unadhani atakuwa tayari kuzisaidia hizo mamalaka?

Ukimya wa mamlaka hizo ndio unapelekea wananchi waamini kuwa kuna watu wanabebwa na ukanda, udini, ukabila, ukada wa vyama n.k. Kama tunawajali wanyonge ni lazima turekebishe mambo kama haya ili wanyonge wasiendelee kuwa mtaji wa "wenye nguvu".
 
Ni hivi mkuu Ngabu, Wanasema aliwaaibisha Watu kwenye Media bila Ushahidi Watu wakakasirika
Naye wakamchimba wakapata hizi tuhuma zinazobebewa Bango. Wanataka naye ajisafishe kwenye Media ile njia aliyotumia!
Hataki sasa
 
Hao wote uliowataja hawajaona kasoro yoyote na kuna taratibu ya kuanzisha uchunguzi wa jambo ambalo sio hatari kwa taifa mtu au jamii. Taratibu haziruhusu kuanzisha uchunguzi wa cheti cha mtu kwa sab ya tuhuma za mtandaoni au mtu fulani kupitia mtandaoni. Kuna zoezi la kuhakiki vyeti likifika kwa wakuu wa mikoa naye atahakikiwa. Lkn kama kuna raia mwenye malalamiko kuhusu jinai ya mtu yoyote anaruhusiwa kwenda mahakamani kufungua shauri dhidi ya mhusika.
 
Unapenda police kutoa taarifa. Na serikali inaanzia hapo. Mahakamani wewe itakuwa shahidi namba moja na sio mshitaki. Mshitaki ni Jamhuri kwa kuvunjwa sheria zake.
Kwahiyo inawezekana raia kwenda polisi au mahakamani kufungua kesi dhidi ya makonda kwa kosa la kufoji vyeti?
 
Ushauri asipouchukua itakuwaje? Hivi kama ni kweli kafoji cheti mnatarajia atajishitaki mwenyewe? Kwani msimshtaki ili sheria ichukue mkondo wake?
 
Kwahiyo watapata haki kupitia presha atakayopata mheshimiwa?
 
Kwahiyo watapata haki kupitia presha atakayopata mheshimiwa?
 
Baada ya kueleweka nini kinafuata?
 
Yeye ndiye mwenye ushahidi na ithibati ya uhakika kwa kuwa vyeti hutolewa kwa mhiitimu na sio jurani au ndugu. Wanamjua majina yake na Shule alizosona O,level
Kuweka Mambo sawa yeye aweke vyeti vyake
Asipoweka
 
Kama kweli amepata zero na kufoji atatoa vyeti? Hata ingekuwa mimi sitoi hata mjaze posterz nchi nzima. Itafutwe njia mbadala ya kumlazimisha atoe vyeti kwa ukaguzi na ikithibitika hatua zichukuliwe. Je mmefikiria kuhusu njia hii? Hopefully ni mahakama.
 
Vizuri kwa kujua hivyo
 
Ushahidi anao Gwajima na ndio maana juzi alifuatwa nyumbani kwake na wale jamaa ambao wao wanapoamrishwa tu wanakurupuka na kutumia nishati yetu ya mafuta bure hata km wanaona kile wanachokifuata hakina mashiko
Gwajima nae alikaa nao ndani kama fenicha?
 
Kumbe ushahidi ni mpk autoe makonda mwenyewe kuwa kafoji vyeti? Nani anaweza kujichoma kisu mwenyewe badala ya kujiokoa? Kama ni hivyo hii vita imefeli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…