Vyeti Kumng`oa Rc Makonda? - Udaku Special Blog
Wakati Gwajima akidai kuwa na nakala za vyeti vyote viwili vya Paul Makonda, vikiwemo vile alivyotumia kuanzia kidato cha nne, upo mkanganyiko mkubwa kutokana na maelezo ya Paul Christian (mtu aliyedaiwa kumpa vyeti Makonda) aliyoyatoa kwa gazeti moja la kila siku la hapa nchini.
Paul Christian, anayedaiwa kuwa ndiye ambaye cheti chake kilitumiwa na Paul Makonda aliliambia gazeti hilo;
“Paul Makonda nimemfahamu kupitia habari na jina wanavyolitaja (waliotunga taarifa ya mtandaoni) wanakosea kwani mimi naitwa Paul Pierre Christian Kagezi, hatuna uhusiano, mimi Mhaya yeye Msukuma.”
“Taarifa hizo (za kumpa cheti Makonda) si za kweli kwa sababu huwezi kutoa cheti wakati umepata daraja la kwanza kidato cha sita, utakwenda vipi chuo kikuu? Sasa niliwezaje mimi kwenda chuo kikuu halafu kwa wakati huo nimpe naye aende chuo kikuu?”Alihoji.
Cristian aliendelea kudai kuwa katika kidato cha tano na sita, alichukua mchepuo wa sayansi masomo ya Fizikia, Kemia na Hesabu (PCM), hivyo si rahisi kutoa cheti hicho kwani angeshindwa kumudu huko alikokwenda.
Alihoji kama Makonda hakufanya vema kidato cha nne au hakusoma kidato cha sita, akatumia cheti cha mtu mwingine, angeweza vipi kufanya vema katika mitihani yake ya chuo kikuu?
Alifafanua kuwa watu wamekuwa wakipika na kuoanisha majina yao, huku akiendelea kukanusha kuhusu taarifa hizo.
“Kama wanataka kumpata huyo bwanamdogo (Makonda) kwa njia hiyo wamemkosa, kwani kwa mantiki nimekuuliza ukipata daraja la kwanza kidato cha sita lazima uende chuo kikuu?” alihoji.
“Huyo bwana anajitegemea yeye kama yeye na walichokifanya wao (waliosambaza taarifa mtandaoni) kwa makusudi yao bila shaka wana lengo lao, wao wametaka kuingiza hoja ambazo hazina mshiko