Kama ni kweli na ushahidi upo....

Kama ni kweli na ushahidi upo....

W
Nianze kwa kusema tu kuwa mimi ni mbeba maboksi nisiyejua mengi hususan kwenye hiyo fani ya 'wasomi' wabobezi [wanasheria] ambao ndiyo majiniasi wetu wenye kuongea Viingereza hatari lakini salama. Nimeishia kidato cha nne tu. Kwa hiyo msinihoji sana kuhusu elimu yangu. Ni ndogo sana.

Sasa hapa nilipo na ujinga wangu huu najiuliza maswali kadha wa kadha na sipati majibu.

Hivi kinachodaiwa dhidi ya Makonda ni kosa la jinai?

Kama ni kosa la jinai na kama kweli ushahidi upo, tena ambao ni wa kutosha na kuridhisha kabisa, kwa nini hao watu waolizitoa hizo tuhuma hawaendi kumfungulia kesi mahakamani?

Au haiwezekani kwa raia kwenda kufungua kesi mahakamani kwa manufaa ya umma dhidi ya kiongozi?

Manake mpaka sasa kilichopo au niseme ambacho nakijua mimi kupitia hii mitandao ya kijamii ni maneno tu kuwa Paul Makonda si jina lake halisi.

Jina lake halisi ni Daudi Bashite. Lakini sijaona ushahidi wowote ule uliotolewa na hao watuhumu unaothibitisha hizo tuhuma zao.

Sasa maneno tu peke yake si ushahidi wa lolote maana mtu yeyote yule anaweza kuzua lolote lile dhidi ya yeyote yule kwa sababu yoyote ile.

Nyie 'wasomi', hivi kweli haiwezekani kwenda kumfungulia mashitaka huyo Paul Makonda kama kweli ushahidi wa yanayosemwa dhidi yake upo?

Si mumburute tu mahakamani huko akaaibike rasmi. Au ni majungu tu?
We we piga box huko...ya huku tuachie. Kaungane na mm mwanakiji muendelee kumpigia debe Faru John
 
Licha ya kwamba Makonda mwenyewe alichemka vibaya kwenye hiyo vita, lakini hapa nilipo najiuliza kwa nini yote haya ya Daudi Bashite yameibuka sasa hivi na si awali hususan kama watu walikuwa wanajua kuwa hilo jina la Paul Makonda si jina lake kweli.
Hilo ni swali zuri sana.
 
Wewe unayemtetea unao ushaidi kwamba wanamsingizia?

Unaona sasa...mambo ya kusoma jambo na kushindwa kuelewa ulichokisoma.

Mimi sijamtetea mtu yeyote kwenye hili suala.

Nimehoji ushahidi wa madai au tuhuma zilizotolewa.

Je, ushahidi kwamba Paul Makonda si Paul Makonda bali anaitwa Daudi Bashite uko wapi?

Unaweza kunipa/ kunionyesha?
 
How can you trust, they are FAKE VYETI in the first place wakati hata vyeti vyenyewe hatujaviona - aliyeibiwa JINA na Vyeti hajazungumza chochote kama yupo - Tushaanza kuamini tu kwasababu Mange kasema
Kama mwenye vyeti kawekwa sehemu tulivu,hotelini,ale na kunywa kwa mfuko wa BASHITE tutajuaje?
 
Sasa mpenzi kama asipovitoa utafanyaje?

kwa nini tunawapa nguvu watuhumiwa eti , avitoe,ajitetee, aombe msamaha n.k

ni lini tutaamka kama wenye nguvu na kufanya anachoshauri ngabu??

wewe binafsi haupendi kuona kabisa huo ushahidi unawekwa hapa? usingependa?

suppose umedanganywa sasa!!!

au unapenda kuamini?
Kwani hapa pana hadhi gani ya kupokea huo ushahidi?
 
View attachment 475492 View attachment 475492

Cheki kwenye snapshot ya page ya mke wa Paulo, Mke wake Paulo yeye mwenyewe toka January mwaka 2016 kule Insta anajiita Mama Daudi, sasa jiulize Daudi huyo ni nani wakati hajajaaliwa mtoto?

Paul ndiyo Daudi mwenyewe hapo akili kumkichwa!!
Labda alishawahi kuzaa na mtoto huyo aliitwa Daudi au labda Makonda alimwoa akiwa tayari na mtoto - Maana mnasema Makonda hazalishi, Mange kawaambia ?
 
Nianze kwa kusema tu kuwa ...

Nyie 'wasomi', hivi kweli haiwezekani kwenda kumfungulia mashitaka huyo Paul Makonda kama kweli ushahidi wa yanayosemwa dhidi yake upo?

Si mumburute tu mahakamani huko akaaibike rasmi. Au ni majungu tu?

Nyani Ngabu: unaamini maneno ya mitandaoni yanayoandikwa na watu wenye kujificha kwenye ID ' fake' au ya Mchungaji Gwajima, madhabahuni, kuwa kuna ushahidi!

Nimeandika humu, hata kumshauri Pascal Mayala, kwenye bandiko lake, kwamba hakuna ushahidi ni majungu, atumie uandishi wake kupata ushahidi, badala naye kuhoji, kama wewe!

Mbona ushahidi uko wazi tu. Ni kwenda shule na vyuo zinazodaiwa amesoma akafeli na ikibidi kutumia vyeti vya watu wengine, kupata huo ushahidi. Kwa kuwa huko shuleni au vyuoni, kuna majina na picha za wanafunzi, na kwa ziada kuna taarifa kamili za mienendo na maendeleo ya kila mwanafunzi.

Kama ametumia majina ya watu wengine, je, hao wanatumia majina gani katika kujisajiri kwa mahitaji ya vitambulisho mbalimbali (km uraia, passport, benki, kupiga kura, bima ya taifa, na kadhalika), au ni marehemu!
 
Kama mwenye vyeti kawekwa sehemu tulivu,hotelini,ale na kunywa kwa mfuko wa BASHITE tutajuaje?

Kwa hiyo sasa hivi yamekuwa mambo ya 'kama', siyo?

Kama ni hivi, kama ni vile....lakini ushahidi wa kuwa yeye si Paul Makonda bali ni Daudi Bashite mpaka hivi sasa hakuna.

Kwa nini?
 
Unaona sasa...mambo ya kusoma jambo na kushindwa kuelewa ulichokisoma.

Mimi sijamtetea mtu yeyote kwenye hili suala.

Nimehoji ushahidi wa madai au tuhuma zilizotolewa.

Je, ushahidi kwamba Paul Makonda si Paul Makonda bali anaitwa Daudi Bashite uko wapi?

Unaweza kunipa/ kunionyesha?
Basi jilaumu wewe mwenyewe maana umehoji na kutetea hoja wakati huo huo. kama ni kuhoji ulitakiwa uhoji bila kuweka maneno ya kutetea.
Angalia maneno yako "Manake mpaka sasa kilichopo au niseme ambacho nakijua mimi kupitia hii mitandao ya kijamii ni maneno tu kuwa Paul Makonda si jina lake halisi. Jina lake halisi ni Daudi Bashite. Lakini sijaona ushahidi wowote ule uliotolewa na hao watuhumu unaothibitisha hizo tuhuma zao. Sasa maneno tu peke yake si ushahidi wa lolote maana mtu yeyote yule anaweza kuzua lolote lile dhidi ya yeyote yule kwa sababu yoyote ile."
Umeona utetezi wako
 
Hahaaa...nipo huku Ikungulyabashashi kaka.

Nasikia tu hadi wachungaji wanasema eti Paul Makonda si jina lake bali jina lake ni Daudi Bashite na ushahidi wanao lakini hawatuonyeshi huo ushahidi.

I wonder why!

Things that make you go hmm....

Ngosha wa Ikungulyabashashi,
Ulichosema ni sawa. Lakini wewe umemsikia Jaji wa Mhakama Kuu huko Arusha alichosema kuhsu DPP na kesi ya Lema?
Kwamba Mahakama imeshabakwa na Wanasheria uchwara wanaotekeleza MAELEKEZO KUTOKA JUU. Kwa maana hiyo hata kama kuna Wazalendo watakwenda Mahakamani dhidi ya Daudi Bashite hakuna kesi hapo. Itapigwa danadana na mambo yataishia hapohapo!!!!
 
Nianze kwa kusema tu kuwa mimi ni mbeba maboksi nisiyejua mengi hususan kwenye hiyo fani ya 'wasomi' wabobezi [wanasheria] ambao ndiyo majiniasi wetu wenye kuongea Viingereza hatari lakini salama. Nimeishia kidato cha nne tu. Kwa hiyo msinihoji sana kuhusu elimu yangu. Ni ndogo sana.

Sasa hapa nilipo na ujinga wangu huu najiuliza maswali kadha wa kadha na sipati majibu.

Hivi kinachodaiwa dhidi ya Makonda ni kosa la jinai?

Kama ni kosa la jinai na kama kweli ushahidi upo, tena ambao ni wa kutosha na kuridhisha kabisa, kwa nini hao watu waolizitoa hizo tuhuma hawaendi kumfungulia kesi mahakamani?

Au haiwezekani kwa raia kwenda kufungua kesi mahakamani kwa manufaa ya umma dhidi ya kiongozi?

Manake mpaka sasa kilichopo au niseme ambacho nakijua mimi kupitia hii mitandao ya kijamii ni maneno tu kuwa Paul Makonda si jina lake halisi.

Jina lake halisi ni Daudi Bashite. Lakini sijaona ushahidi wowote ule uliotolewa na hao watuhumu unaothibitisha hizo tuhuma zao.

Sasa maneno tu peke yake si ushahidi wa lolote maana mtu yeyote yule anaweza kuzua lolote lile dhidi ya yeyote yule kwa sababu yoyote ile.

Nyie 'wasomi', hivi kweli haiwezekani kwenda kumfungulia mashitaka huyo Paul Makonda kama kweli ushahidi wa yanayosemwa dhidi yake upo?

Si mumburute tu mahakamani huko akaaibike rasmi. Au ni majungu tu?

Cheki hiyo picha aliyopost MKE WAKE WA NDOA KATIKA AKAUNTI YAKE ya instagram with caption MAMA DAUDI. Huyo ni mke wa Mheshimiwa inamaanisha directly au indirectly ana mahusiano na hilo jina. Mpaka sasa inawezekana akawa kafoji cheti. Ila ukweli anaujua mwenyewe

. Na sisi kama watanzania na wana dar es salaam hatujui tumwamini nani kati ya hao maadui zake wanaopost facts au yeye mwenyewe aliyeamua kukaa kimya.
 
Unasubiri nini na wewe kufanya Research yako kupata majawabu ?

Viashiria vi dhahiri kuwa jamaa ni Daudi Bashite.
Kama kweli ana vyeti Original tofauti na Madai ya watu kitu gani kinamzuia kujitokeza na ku Clear atmosphere ?

Mbona yule DED mteule ambaye watu walimzushia kuwa ni Manager wa hotel na ana Certificate tu ya Hotel Management Mamlaka yake ya uteuzi ilikuja na kutoa Clarifications na yeye akatoa vyeti vyake hadharani

Why ya Bashite kunakuwa na kigugumizi sana ?

Wengi wanajenga hoja based on this,watu hawana haja ya kumpeleka Mahakamani,wanataka Mamlaka yake ya uteuzi either itoe clarification ama imchinjie baharini
Siyo lazima hiyo mamlaka ifate mawazo yako
 
Nianze kwa kusema tu kuwa mimi ni mbeba maboksi nisiyejua mengi hususan kwenye hiyo fani ya 'wasomi' wabobezi [wanasheria] ambao ndiyo majiniasi wetu wenye kuongea Viingereza hatari lakini salama. Nimeishia kidato cha nne tu. Kwa hiyo msinihoji sana kuhusu elimu yangu. Ni ndogo sana.

Sasa hapa nilipo na ujinga wangu huu najiuliza maswali kadha wa kadha na sipati majibu.

Hivi kinachodaiwa dhidi ya Makonda ni kosa la jinai?

Kama ni kosa la jinai na kama kweli ushahidi upo, tena ambao ni wa kutosha na kuridhisha kabisa, kwa nini hao watu waolizitoa hizo tuhuma hawaendi kumfungulia kesi mahakamani?

Au haiwezekani kwa raia kwenda kufungua kesi mahakamani kwa manufaa ya umma dhidi ya kiongozi?

Manake mpaka sasa kilichopo au niseme ambacho nakijua mimi kupitia hii mitandao ya kijamii ni maneno tu kuwa Paul Makonda si jina lake halisi.

Jina lake halisi ni Daudi Bashite. Lakini sijaona ushahidi wowote ule uliotolewa na hao watuhumu unaothibitisha hizo tuhuma zao.

Sasa maneno tu peke yake si ushahidi wa lolote maana mtu yeyote yule anaweza kuzua lolote lile dhidi ya yeyote yule kwa sababu yoyote ile.

Nyie 'wasomi', hivi kweli haiwezekani kwenda kumfungulia mashitaka huyo Paul Makonda kama kweli ushahidi wa yanayosemwa dhidi yake upo?

Si mumburute tu mahakamani huko akaaibike rasmi. Au ni majungu tu?
Mkuu, tuhuma dhidi ya Makonda Zipo wazi Sana, na mwenye jukumu la Kumshtaki Makonda si mtu aliyemtuhumu Bali ni mwajiri, aliyemtuhumu amedai anao ushahidi wa kutosha na yupo tayari kuisaidia mahakama.
Sasa hapo mwenye kuchukua hatua ni bosi wake tu na si vinginevyo.
kwani umesahau Makonda alivyowatuhumu watu kuuza wakati akijua kuwa, "A person cannot be made guilty if not proven by the court of law ",Sasa Makonda aliwataja publicly kitendo ambacho ni kuchafua image ya mtu, nadhani unajua kuwa, what goes around comes around ,alianzisha ugomvi wa mawe akasahau kuwa anaishi kwenye nyumba ya vioo, ugomvi umeanza akakimbilia kujificha humo humo.
Watu wenye akili Zetu tuliuona mwisho mbaya Makonda, if his boss won't fire him, his personality and political charisma in the state house will totally get faded.
 
Nianze kwa kusema tu kuwa mimi ni mbeba maboksi nisiyejua mengi hususan kwenye hiyo fani ya 'wasomi' wabobezi [wanasheria] ambao ndiyo majiniasi wetu wenye kuongea Viingereza hatari lakini salama. Nimeishia kidato cha nne tu. Kwa hiyo msinihoji sana kuhusu elimu yangu. Ni ndogo sana.

Sasa hapa nilipo na ujinga wangu huu najiuliza maswali kadha wa kadha na sipati majibu.

Hivi kinachodaiwa dhidi ya Makonda ni kosa la jinai?

Kama ni kosa la jinai na kama kweli ushahidi upo, tena ambao ni wa kutosha na kuridhisha kabisa, kwa nini hao watu waolizitoa hizo tuhuma hawaendi kumfungulia kesi mahakamani?

Au haiwezekani kwa raia kwenda kufungua kesi mahakamani kwa manufaa ya umma dhidi ya kiongozi?

Manake mpaka sasa kilichopo au niseme ambacho nakijua mimi kupitia hii mitandao ya kijamii ni maneno tu kuwa Paul Makonda si jina lake halisi.

Jina lake halisi ni Daudi Bashite. Lakini sijaona ushahidi wowote ule uliotolewa na hao watuhumu unaothibitisha hizo tuhuma zao.

Sasa maneno tu peke yake si ushahidi wa lolote maana mtu yeyote yule anaweza kuzua lolote lile dhidi ya yeyote yule kwa sababu yoyote ile.

Nyie 'wasomi', hivi kweli haiwezekani kwenda kumfungulia mashitaka huyo Paul Makonda kama kweli ushahidi wa yanayosemwa dhidi yake upo?

Si mumburute tu mahakamani huko akaaibike rasmi. Au ni majungu tu?
Ushahidi ni kwamba hajakanusha has a kwa kuzingatia yeye ni msemaji mahiri na chombo chake cha kusemea clouds kipo angeshasema neno tu tena kwa tambo za kufa mtu.

Suala LA pili ni kwa bahati mbaya Tanzania jinai inapelekwa mahakamani kupitia polisi, japokuwa kwenye penal code kuna kifungu cha 87 kama sijasahau kinamruhusu raia kwenda moja kwa moja Ku lodge shauri LA jinai mahakamani ila kwa sasa sio effective kutokana na mazoea ya kupitia polisi.

Polisi wenyewe ndio hawa hawa tulio nao unadhani ukatia pua kufungua ya bashite utasalimika?!
 
Nyani Ngabu: unaamini maneno ya mitandaoni yanayoandikwa na watu wenye kujificha kwenye ID ' fake' au ya Mchungaji Gwajima, madhabahuni, kuwa kuna ushahidi!

Nimeandika humu, hata kumshauri Pascal Mayala, kwenye bandiko lake, kwamba hakuna ushahidi ni majungu, atumie uandishi wake kupata ushahidi, badala naye kuhoji, kama wewe!

Mbona ushahidi uko wazi tu. Ni kwenda shule na vyuo zinazodaiwa amesoma akafeli na ikibidi kutumia vyeti vya watu wengine, kupata huo ushahidi. Kwa kuwa huko shuleni au vyuoni, kuna majina na picha za wanafunzi, na kwa ziada kuna taarifa kamili za mienendo na maendeleo ya kila mwanafunzi.

Kama ametumia majina ya watu wengine, je, hao wanatumia majina gani katika kujisajiri kwa mahitaji ya vitambulisho mbalimbali (km uraia, passport, benki, kupiga kura, bima ya taifa, na kadhalika), au ni marehemu!

Maswali kuntu kabisa hayo.

Tatizo, kwa mtazamo wangu, watu walio wengi wala hawana kabisa raghba ya kutaka kuujua ukweli.

Walicho na raghba nacho ni kumwona huyo Paul Makonda akiadhirika tu, basi. Iwe kwa sababu za ukweli au za kizushi.

Truth be damned but lies and rumors be advanced.
 
Wa Tanzania wengi ni bendera fuata upepo

Mangi kasema ,gwajima kasema ,nanihi kasema

Mtanzania unaweza kumchezea na kumshika akili ,mpe gossips tu utamhamisha kwenye agenda
Labda ukosefu wa ajira umegeuza mitandao ya kijamii kuwa vijiwe vya kusambaza udaku.

Au juhudi za Serikali kutumbua waovu, kubana matumizi, kurejesha uwajibikaji na uadilifu maofisini, vita dhidi ya biashara ya madawa ya kulevya, nk, inajenga chuki kati ya watawala na wahusika!

NI KELELE TU ZA CHURA AU MLANGONI
 
With all due respect, kuwa mbeba box siyo tatizo, tatizo ni wewe kujiingiza mzima zima na kung'ang'ania ndani ya box!.

Wanachofanya watu ni kufanya REFERENCE on related issues /decisions made wala siyo kwa sababu mange/gwajima kasema. Nikikuambia according to the late Nyerere, kuna waziri uingereza alituhumiwa kutembea na kimada na boss wake alivyokuwa infuriated (Kama ambavyo tulitegemea magu awe, kwa jinsi alivyojipambanua), akamteua mwingine bila kujibu resignation yake utasema tunafuata upepo?
 
Ushahidi ni kwamba hajakanusha has a kwa kuzingatia yeye ni msemaji mahiri na chombo chake cha kusemea clouds kipo angeshasema neno tu tena kwa tambo za kufa mtu.

Aisee!

So that is the standard of proof now?

Kwamba ukiamua kukaa kimya juu ya mambo yanayozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii basi una hatia?

Scratching my head.....literally!
 
Kwa hiyo sasa hivi yamekuwa mambo ya 'kama', siyo?

Kama ni hivi, kama ni vile....lakini ushahidi wa kuwa yeye si Paul Makonda bali ni Daudi Bashite mpaka hivi sasa hakuna.

Kwa nini?
Ngabu,,,we ni msomi na unamkingia kifua kisaikolojia zaidi tunafahamu.

Jamaa ajitokeze,ajibu tuhuma.Kukaa kimya hakutampa nafuu yeyote.

Akiponyoka kwenye hizi kelele,tutawatuma wabunge watupigie kelele bungeni.

Ikishindikana bungeni,wananchi watawawajibisha wanaccm wote katika masanduku ya kura,,amini hivo.

ACHA KUTETEA UOVU.
 
Back
Top Bottom