Nyani Ngabu,
Bila kujijua unatumia the very same cheap defensive tactics used by all corrupt politicians in Africa!!
Wakati wa mchakato wa katiba mpya nilizungumza hapa kwamba miongoni mwa mifumo yoooooote ambayo tuliletewa na Western Countries, ni mfumo wa Utawala Bora pekee ndio haujapigiwa kelele na viongozi wa Afrika tofauti ni mifumo mingine ya kisiasa na kiuchumi ambayo ilikejeliwa na kuitwa majina mbalimbali yaliyolenga ku-discredit hiyo mifumo!!
Kwa mfano, Utandawazi ukaja kuitwa Utandawizi!! Soko Huria likaja kuitwa Soko Holela!!
But why Utawala Bora haukuwa discredited na watawala pamoja na mawakala wao?! The answer is very simple like ABC... YES, and I mean it!!!
Kwa nchi zilizojaa uovu na ukosefu wa maadili, utawala bora ni kichaka tosha cha kuficha uhalifu na uovu wa watawala na mawakala wao!
Moja ya nguzo kuu za Utawala Bora ni Utawala wa Sheria!! Kiongozi mwizi; ukimtuhumu kwamba ni mwizi atakuambia TOA USHAHIDI kwamba mimi ni mwizi!! Atazungumza hili with confidence kwa sababu anafahamu vema hutakuwa na uwezo wa kutoa ushahidi ingawaje hili halifuti ukweli kwamba yeye ni mwizi!!!
Watawala wetu na mawakala wao wakaupenda mfumo huu wa utawala bora kwa sababu walijua pale tutakapowatuhumu uovu na uhalifu wao watatupiga bakora ya kwamba tutoee ushahidi dhidi yao sawa na wewe NN unavyowataka watu watoe ushahidi hapa JF kwavile unafahamu majority hawatakuwa na access ya kutoa huo ushahidi!!
Unawataka watu watoe ushahidi against senior government official na wapate ushahidi huo kupitia government agencies!! Unless there's something behind your thread because both you and I know no one can give that, at least here!!
But how does these games played?!
Fine, kwamba wananchi huwa wanakosa tangible evidence kwahiyo huwa wanaamua kupeleka mashitaka yao mbele ya umma!! Akina Dr Slaa kwa kufahamu wasingekuwa na tangible evidence ya kuwa-implicate watu; wakaamua kuwashitaki wezi wa EPA kwenye mahakama ya umma kama inavyofanyika kwa Makonda!!
The idea behind, kiongozi wa umma hapaswi kuwa na makando makando!! Na kwavile hapaswi kuwa na makando makando pia hapaswi kutumia legal loopholes la kuwataka watu wathibitishe tuhuma dhidi yao kwavile system haiwezi kuwa rahisi kufanya hivyo!!
Kutokana na hilo, kiongozi mwadilifu ni yeye ndie anatakiwa kutoka clean dhidi ya tuhuma zozote dhidi yake!!! Hizi si tuhuma ndogo! Na pamoja na cheap arguments kwamba it's all about his drugs "fight" lakini ukweli ni kwamba tuhuma dhidi ya Makonda hazikuanza baada ya sakata la dawa za kulevya!!!
Sasa kama kila wakati unatuhumiwa; why don't you come clean to prove how wrong those haters are?!
NN unataka upewe ushahidi hapa... hivi ni ushahidi gani ambao utawekewa hapa na kuukubali kwamba ni tangible evidence?! Sitarajii kwamba unachotarajia ni kuwekewa vyeti hapa cuz' unless viwe certified bila kuacha shaka yoyote ile vinginevyo bado huo hauwezi kuwa ushahidi!!!
Na kuna kitu very interesting kuhusu hii issue!!!
Mwaka 2012 hapa hapa JF kuna watu walileta mada kuhusu Ali Hapi!! Makumi kwa makumi ya members wa JF walitoka mbele kutetea uwezo wa Hapi kielimu ingawaje kwa kuangalia comments zao wala sio wana CCM!! Juzi juzi tu hapa mada kuhusu Hapi ikaletwa tena!! Kama ilivyotokea 2012 dhidi ya Hapi, ndivyo ilivyotokea majuzi!!!
Kinyume chake, hakuna hata mmoja anayeelezea positive side ya mlolongo wa elimu wa Makonda!!! Makonda kasoma juzi juzi tu... mbona watu hawajitokezi kumtetea kama walivyomtetea Hapi zaidi ya kutoa hoja dhaifu kwamba "ni majungu tu hayo!!" WHY?! Makonda hajasoma miaka 50 iliyopita tudhani kwamba aliosoma nao wamekufa....!!!
Nimekupa mfano huo hapo juu kuonesha wakati mwingine sio lazima uletewe makaratasi as a source of evidence!!! Mazingira peke yake, ukichanganya na uwezo wa kufikiri aliokupa Mungu; kwa pamoja vinaweza kukusaidia kufikia conclusion!!!
Narudia, Makonda kama kiongozi hatakiwi kuishi na makando makando!! Pale tuhuma kali dhidi yake zinapotolewa anatakiwa kutoka mbele na sio kutumia legal loopholes kuwataka watu wathibitishe kwa sababu tu unajua hawataweza!! Na katu kuwataka watu wathibitishe si tu kwamba haitaondoa uwezekano wa yeye kuwa fraud bali pia itaendelea kuacha shaka nyingi dhidi yake!!!
Tuhuma za kuwa fraud ni tuhuma mzito kwa kiongozi mwandamizi wa serikali!! Mwanzoni angeweza kuzipuuza lakini inapotokea hadi viongozi wa kiroho nao wanatoa tuhuma hizo; nitakuwa mtu wa ajabu nikiungana na hoja kwamba "kwanini iwe yeye ndie wa ku-prove otherwise!"