Decree Holder
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 2,559
- 3,747
Kwanza siyo kweli kwamba ukiwa na tetesi kuwa fulani ni mwizi unatakiwa kwenda mahakamani bali unatakiwa kwenda polisi kuripoti au kulalamika polisi ndiyo wataenda mahakamani maana hiyo ni kesi yao. Lengo la kwenda polisi ni kuripoti ili polisi wachukue hatua, swali je hapa kuna haja gani ya kwenda kuripoti wakati polisi wenyewe wamo humu mtandaoni na masmatifoni yao na wengine wameshasoma kwenye magazetini? Kwenda kuripoti kuna maana gani nyingine zaidi ya kuwataarifu kitu wasichokijua? Sasa tukawataarifu kitu wanachokijua? Watumie intelejensia yao ikibidi wamuhoji Makonda mwenyewe kwa tuhuma hizi za jinai.Hapana au ndiyo yote majibu. Lakini, kama una tetesi huyu mtu ni mwizi nadhani jukumu lako kubwa ni kwenda mahakamani kumshitaki ili haki itendeke. Kupiga makelele hovyo kama mbwa koko maana yake huna uhakika na ni majungu tuu. Na kusema ukweli ni majungu tuu au tuseme blaa blaa za wachungaji feki. Hivi Makonda kapata ukuu wa mkoa mwezi jana au lini? Kaanzia ukuu wa wilaya wakati wa JK na hawa watu wapo hapa hapa na makanisa yao yako hapa hapa. Magu kaja kampa ukuu wa mkoa wapo hapa hapa Dar es salaam hii. Walikuwa wapi? Huu ni upuuzi na inaonyesha kabisa ni kwa kiasi gani madawa ya kulevya ni tatizo kuuuubwa hapa nchini. Kwa taarifa yenu, Kitwanga mnaembez humu kila siku ni madawa haya haya ya kulevya baada ya kuwa anawakamata kwa hiyo kimya kimya yenu mnayosema au mnayotaka. Ni bira kuwataja hadharani kama makonda ili wapige makelele tuwafahamu hata sisi tusiokuwa na mitandao. Now we know them exactly. Makonda kwangu mimi hapaswi kutumbuliwa hata kama vyeti vyake vingekuwa na kutu ya aina gani. Ni kijana jasiri na tunamhitaji. Mabadiliko yatatokea CCM na si kwingineko. Hawa wapinzani tuliowashangilia sasa wameshalipwa na wauza unga na wanawatetea. Hakunaga sheria kwenye upuuzi. Sheria mtu akiua inaweza kumuachia huru kama ana wakili ajuae kupanga maneno. Na ndiyo chimbuko la neno sheria ni msumeno. Itumike kwa vitu vya kawaida si miraaaaa.
Mwisho hoja kwamba walikuwa wapi ni immaterial na haiwezi kusimama sehemu yeyote ile. Makosa ya jinai hayanaga time limit labda mtuhumiwa afe wanaweza wakamuacha sasa wakaja kumshitaki miaka 70 ijayo akiwa hai. Kusema walikuwa wapi walikuwepo ila walikuwa hawajui.