Kama Mwema unapita hapa nakupa taarifa hizi sasa uzijue

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Kwa mara ya 3 mfulizo kwa nyakati tofauti nimefika katika kituo cha Polisi cha Buguruni na Selandar Bridge. Ndugu IGP, napenda ujue kwamba baada ya Rais kuugawa Mkoa wa Dar na kuweka madoiko kibao kwa jina la usalama, nk, which I have no problem with, imepelekea maonevu na rushwa kushamiri. Ukiingia Buguruni unaomba rushwa wazi wazi hata kama hakuna jambo la kukufanya ufikie hatua hiyo. Ni vigumu kusema nani kaomba rushwa lakini ninaweza kutoa baadhi ya watu wanaohusika na vituko na huku uongozi unajua yanayojiri.

Ndugu IGP, nimeshuhudia mtu anahojiwa behind the Counter ya polisi akiwa chini ya Ulinzi lakini anapigwa na polisi zaidi ya mmoja openly kisa anakataa kutaja jina lake akidai awepo Hakimu kama mlinzi wa amani ama ndugu zake ama Mwansheria. I went far na kuhoji kwa nini alikuwa anapigwa akiwa hakati amri ya kuwekwa chini ya Ulinzi lakini majibu yalikuwa ni matusi kwangu hata bila ya kujua wanasema na nani.

Buguruni kuna uhuni mkubwa kiasi kwamba hata kumuona Mkuu wa Kituo ama OC CID na OCD ni big deals. Watu hukamatwa Buguruni na walio wakamata kwa kujenga mazingira ya rushwa huwaacha ndani na kuondoka kwa masaa mengi ndugu zao wakihaha kuwatafuta na wao wanasema wameenda lunch ama kunywa chai. Ukiwapigia simu wanakuita uende huko mkamalizane.

Je, Mwema, haya unayajua? Unajua walala hoi wanavyoteswa na kukamliwa senti zao na wao hutoa pesa kwa kuhofia na kuogopa kukaa ndani?
 
Kaka Hakuna Haki Duniani Popote Unapoenda Hayo Mambo Yapo Mndugu Yangu.kama Huyo Jamaa Alikuwa Hataki Kutaja Jina Lake Ulitaka Wambembeleze,kwa Kuwa Kuta Jina Lake Haikuwa Na Uhusiano Na Mlinzi Wa Amani Na Wala Mahakimu Hawalazimishwa Kuwepo Mtu Akiwa Anahojiwa Na Polisi.
 
Kaka Hakuna Haki Duniani Popote Unapoenda Hayo Mambo Yapo Mndugu Yangu.kama Huyo Jamaa Alikuwa Hataki Kutaja Jina Lake Ulitaka Wambembeleze,kwa Kuwa Kuta Jina Lake Haikuwa Na Uhusiano Na Mlinzi Wa Amani Na Wala Mahakimu Hawalazimishwa Kuwepo Mtu Akiwa Anahojiwa Na Polisi.

Mtoto wa Fisadi
Pole sana. Labda uuliza uambiwe kwamba jamaa was only a suspect na hakukataa kutiwa nguvuni. Alikuwa chini ya ulinzi sasa polisi kumhoji ana haki ya kujibu ama kukataa hadi hatua zingine zifanyike .Poisi hana haki ya kumpiga mtuhumiwa wala kumtukana wala kumdhalilisha ni kinyume kabisa na sheria na haki za mtu . Ninaweza kuamua kutaja jina langu polisi na kuandika statement kama nina dhani kwamba ni sahihi lakini naweza pia kukataa kuhojiwa na kutoa maelezo hadi awepo mwana sheria ama hakimu ama shahidi ninaye mwamini . Kwa watu kuwaza kama wewe kuwapiga na ku force maelezo kumepelekea watu kufungwa kwa kuonewa ama majambazi na wajanja kushinda kesi nyingi. Siongei tu kwa kuwa nataka kuongea wewe Fisadi fungua macho yako.

Polisi hana haki ya kukupiga kama wewe si threat .
 
Kupigwa kwa suspects ni kawaida katika hivyo vituo vya polisi. Vijana kukusanywa na kubambikiwa mashtaka hadi ndugu zao watakapotoa chochote na yenyewe sishangai kusikia. Kitu kingine kinachoniboa ni kuandikiwa statement na polisi. Staement kurasa tatu, mtuhumiwa ana sign ya mwisho! Kuna kazi kubwa ya kufanywa katika vyombo vyetu vya usalama.
 
lakini tanzania polisi wetu ni wastaarabu sana wengi wao hatuwezi kuwafananisha na polisi wa kenya,unapotaka kumuona ocd kama wewe ni mtuhumiwa nchini kenya,unavuaviatu na kuoitishwa ktk kapeti limejaa vipini vinachoma balaa,sasa hapo polisi wa tanzania ni wema sana wanakufinya tu kidogo kaka unalalamika hivyo
 
Huyu Fisadi mtoto vipi?
Omba siku moja ukamatwe na kuswekwa kituoni au ukamatwe tu na hawa Tigo(ant-robbery)wanaolanda landa barabarani kwa pikipiki,ndipo utaona ujinga wao?Utadhani wao hawakosei na si binadamu waishio chini ktk sayari hii.
Polisi wa Ki TZ wana njaa sana alafu si wastaarabu.Hapo msimbazi police nilishatolewa upepo na cid mmoja jina nalihifadhi kwa kuhusishwa na upotevu fulani ambao aliyehusika alikuwa rafiki yangu nami nikajumlishwa.
Siku moja nimekuta naye eti anataka tena lift kwangu,niliangalia upande wala hata sikujali
 
lakini tanzania polisi wetu ni wastaarabu sana wengi wao hatuwezi kuwafananisha na polisi wa kenya,unapotaka kumuona ocd kama wewe ni mtuhumiwa nchini kenya,unavuaviatu na kuoitishwa ktk kapeti limejaa vipini vinachoma balaa,sasa hapo polisi wa tanzania ni wema sana wanakufinya tu kidogo kaka unalalamika hivyo

Fisadi mtoto, uonevu wanaofanya polisi wa kenya dhidi ya wananchi wa kenya hauhalalishi polisi wa tanzania kufanya huo unyama. Yaani mifano unayotumia haina mantiki hata kidogo kwa sababu inakwenda kinyume na sheria za nchi. Hatuongozwi kwa kuangalia kenya wanafanya nini. Jenga hoja ueleweke. Si lazima uchangie. Ni mawazo yangu. Samahani kama nimekukera.
 
Huyo ni MTOTO tenaFISADI kwanini mupoteze wakati wenu na mtoto? au wengine ndio hivvyo tena?
 
Waungwana kuhusu huo uovu na uonevu wa Polisi, Vipi mkasa wa ZOMBE na wenzake umeishia wapi?
 
siku moja nilikuwa nnasikiliza kipindi cha saidia polisi ikusaidie

wanasema wananchi hawatoi mshirikiano mzuri na polisi ndio uhalifu unaongezeka.

nilicheka sana baada ya kukasirika maana hapo mtaani kwetu kule unguja nyumba ya jirani kunauzwa bumbwi basi kuna jirani mmoja ikawa ina mkera ile maana wale wateja wakisha bwia hutuibia na kufanya mengi maovu.

akatoka akaenda Madema kuwasaidia polisi kukomesha v itendo viovu kilichofuata jamaa wakapewa habari kuwa hapo mtaani kuna mzee kakuchomeeni kuweni makini nae.

vijana hawakuimficha wakampa shua na wakamuibia kila kitu.

na siku nyengine utawakuta polisi huja kwa siri kuchukua chao.

sasa kwa ukweli polisi bado hawajaiva.

wao ni majirimia wakubwa na washenzi ajabu na anae wasifu polisi hayajamkuta.

mie nna jamaaa zangu wengi polisi hubaki ni jamaa zangu lakini vitendo vya polisi wengi aaaah mwisho.

hayo mateso ndio usiseme.
 
Mimi napendekeza vituo vipunguzwe vibaki vichache. Mapolisi wawe wanapatrol. Hii biashara ya kuwajengea ki'police post' kila kona kimewafanya waone wajibu wa kumkamata mhalifu ni wa mwananchi. Vituo vikiwa vichache itakuwa ni rahisi kuvisimamia na kuhakikisha kuwa hakuna anayesoteshwa bila sababu. Angalia kwa wenzetu. Bobby wa uingereza kazi yake ni mtaani na sio kukaa polisi posti. Mapolisi wamarekani nao hivyo hivyo. Kutwa nzima wanazunguka na magari yao. Hivyo vi polisi posti na viselo vyao ndio vinawafanya wawe limbukeni na kujiona viungu mtu. Waende wakabanane mle mle na raia.
 
uswahilini kwetu enzi hizo nikiwa home, watu walikuwa wanavizia "afande mwita" akiwa mitungu na kuangusha "gari" wanakula "washeli" au kwa jina jengine "kisamvu cha kopo" mtungo!!! katabia hako kalisaidia kwani majority wao walitolewa bikra, wakaanza kuogopa na kufanya kazi yao kihalali.

Nadhani hiyo ni dhambi lakini desparate people use desparate means, kwahiyo kila kitu ni halali in the name of justice.
 
Lazima tukubali kuwa MNYONGE HANA HAKI, analosema Lunyungu ni hali halisi Tanzania. If you are someone, then haki inaweza kuonekana kama hukutendewa haki, ukiwa kama Dito au Zombe, ukifanya kosa lolote ndio hata ndani hukai, unatesha nje tu......kawaida kabisa hapa bongo!
 
RUSHWA KWA BONGO kazi TUNAYO si ndogo. Kila mtu kweli ana matatizo, lkn TAMAA baadhi yetu ndio inayofanya kila idara ya serikali INUKE RUSHWA.

Mwananchi wa Kawaidai RUSHWA Kubwa HAIJUI, yeye Rushwa kubwa ni ile anayompa POLISI. POLIS/TRAFFIC anajiwekea kila siku lazima akusanye 20,000. Wakati nimemaliza F6 na UDSM baadhi ya ma-uncle zangu wakaniambia Chuma somea Utraffic au kaomba kazi kule kuna pesa sana. Hawa maa uncle zangu wengi wao ni Madereva wa Daladala, so ile adha ya kukumbana na Traffic kila mara na kumpa chochote si ndogo, so una Uhakika, ukiwa Traffic DSM kwa mwaka 1 tu unaweza kuangusha Bangaloo lako si mchezo. Binafsi KULA PESA YA HARAMU Si wezi...labda niisijue....naua kweli masikini, lkn Kula Nyama ya mwezio alie HAI....mmhhh haifai..better niwe masikini nashindia EMBE DODO kula kila siku CITY GARDEN na PESA HARAMU.
 
Mwaka Jana 2007 septmber kuna Rafiki yangu alikuwa anarudi kutoka Ughaibuni, nikaenda kumpokea airport, cha Ajabu wale Jamaa sijui TRA au Polisi Uchwara wanavyodai kitu kidogo hata aibu Hawana. Wakati anatoka wale jamaa wa getini wanadai Passport onyesha..mie nikawaambia Passport Control kashaonesha...vp tena? Dada mmoja akadai hawa jamaa wapo ktk kazi zao...mwingine akasema hao jamaa wa madawa ya Kulevya nikawaambie tokeni zenu hapa. IMEWEKWA Passport control maalum kucheti situation zote, na kukiwa na suspicions basi watu wa passport control watakwambia kaa pembeni na si WAHUNI wanaokaa GETINI kuchukua chochote kitu.

back 2005/2006, nilifika kikazi Mambo ya NDANI. nikafika reception, nikamuuliza mkuu Fulan yupo, nikaambiwa yupo. baada ya kurudi na kumpa shukran, yule askari wa reception akaomba 500. Binafsi sikuwa nayo, ningekuwa nayo ningempa lkn nilimuonea Huruma sana, maana yeye anajua kila mkubwa akifuatwa huko Juu anakwenda kuachiwa mchuzi. So far ukiona anaomba 500 ujue Hali yake Mbaya sana au ndio kashazoea.

SERIKALI YETU UOZO KILA SEHEM....KILA MTU AANZE KUCHUKIA UOZO KTK NAFSI YAKE
 
Tuendelee na mada yetu, polisi katika Tanzania wana (-) nyingi kuliko (+). Naomba kueleweka kuwa lawama kwa polisi (na ndiyo ukweli) zinazidi hata faida ya kuwepo kwao. Ukiacha wachache kama Solomon (Ubungo Robbery Incidence), Kamanda Tossi ambao wanabeba maana halisi ya "polisi" ambao ukiwasikia mwili unasisimka kuwa Tanzania tuko salama! "Polisi" maana yake ni "dhuluma, chuki, uonevu, kusingizia, kubambikiwa, torture, rushwa, dharau, n.k! Hiyo ndiyo "polisi" tunayoifahamu sisi! Tofauti na jinsi ilivyo kwenye vitabu, mafaili, madarasani, na Armed Forces! Polisi kama polisi inahitajika sana kuliko isivyohitajika, "question" nani wa kuibadili polisi?
 
Kaka Hakuna Haki Duniani Popote Unapoenda Hayo Mambo Yapo Mndugu Yangu.kama Huyo Jamaa Alikuwa Hataki Kutaja Jina Lake Ulitaka Wambembeleze,kwa Kuwa Kuta Jina Lake Haikuwa Na Uhusiano Na Mlinzi Wa Amani Na Wala Mahakimu Hawalazimishwa Kuwepo Mtu Akiwa Anahojiwa Na Polisi.

...this guy is a crazy jackass!
 
Juzi nilifika pale Magu nikiwa kwenye gari namba fulani na wadanganyika wenzangu . Mambo haya ya kuchoka basi nikautimba kwenye ki Bus kile lakini nikiwa naogopa maana hapa Tanzania ajali ni kama mchezo .Siwezi kushindana na Mungu nikalala bwana .Mara ghafla naamshwa kwa kuvutwa shati kwa nyuma .Yaani wewe husikii amri ya polisi ? Nikashangaa gari ilikuwa mwendo polisi tena nini ? Kuangalia nje nikakuta wale jamaa wa vikofia vyekundu na wengine kiraia na wengine magawanda ya polisi ambao si FFU.

Wakasema wanafanya msako wa mirungi toka Kenya .watu wote wanshushwa namatusi juu .Mimi nikasema kuna nini akasema utauliza ukiwa chini .Nikasema no .Sishuki na sanduku langu haliendi chini . Nikasema naomba polisi mkuu wa OP aje hapa . Wakaanza kushangaa nikakaza uzi nikasema ni makosa kuvamia gari .

Wakasema huoni tumevaa uniform nikasema majambazi huwa wamevaa hata nguo za jeshi.Still unapoteza muda wangu naomba mkuu wa OP aje hapa .Usingizi ukanitoka . Wakasema Mzee afande yuko kizuvulini nikasema jaka kukaa kivulini ? Naomba aje hapa .

Wakaogopa sana wakaacha kushusha watu wakaomba msamaha gari likachiwa ikiwa mbele yangu gari dogo la wasomali lilikamatwa na mirungu wakatoa 2m hapo hapo na gari ikaachiwa namirungi kuingia Mwanza .Kila mmoja aliona mchezo ule lakini walalhoi wakawa wanasgambuliwa .Baada ya kuondoka Bus zima walikaa kimya kidogo wakiulizana huyu Mzee ni nani . Wakasema Mzee umetuokoa tunapata shida sana . Tunapigwa hata makofi na traffic njiani humu . Hatujawahi kuona polisi anaywea namna hii na silaha zao .

Mwema ukae ukijua kwamba kule kwa Zelote vijana wako wana wahangaisha wananchi . Rushwa mtindo mmoja . Polisi wanasumbua na hata kuchukua wake za watu . Polisi post ni kitega uchumi .

Sasa njoo kwa hawa wanao zunguka na pikipiki hahahah wana vituko hadi Bus .Ila hawajaingia anga zangu watashangaa siku moja . Kilio changu ni kwa wanyonge jamani .Airport nako rushwa nje nje .Mwema kama unapata habari hizi ujue kazi bado sana .Polisi wako haya common sense hawatumii achilia mbali kwamba hawana ama ni msamiati mkubwa .Ukifika kituo cha polisi hata kama wamtafuta jamaa yako wao wanakuhesabu ni mhalifu tu .
 
Lunyungu,why do you put this on the open news paper to be a public consumption? Hapo Buguruni sitaki hata kupasikia kwani nilishazusha kasheshe hapo,baada ya kuniomba rushwa, nikadai siwezi kuongea mpaka mwanasheria wangu aitwe hapo na hawana ruhusa ya kuniweka ndani, good lucky my young brother is a lawyer, alipotia timu sikuulizwa shwari bali niliachiwa kwa amani kabisa
 
Back
Top Bottom