Barua ya wazi kwa IGP: Kuna uwezekano mkubwa hawa watuhumiwa wakafia kituo cha polisi kwa uzembe wa wafanya kazi wako

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Hii ni barua ya wazi Kwa IGP wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, ninaekuandikia barua ni raia mwema nisiye na masilahi yoyote na watumishi wako, ila ni Mtanzania ambaye ningependa watendaji walioko chini yako wazingatie weledi wanapokuwa wanatimiza wajibu wao wa kazi pasi uonevu wowote.

IGP, barua hii itakufikia kupitia pahala hapa lakini baada ya hapa nitumia email moja kwa moja na nakala ya barua hii nitaifikisha kwa Mteule wako Ili nae aweze kupata picha dhidi ya matendo machafu na ya ovyo yanayofanywa na watendaji walio chini Yako.

IGP, mimi ni mwananchi nilie karibu sana na Kituo Kikuuu cha Polisi kilichopo wilaya ya Moshi vijijini yaani Himo Police Station. Tarehe 12/12/2022 nikiwa nyumbani kwangu nilivamiwa na mtu mmoja ambaye siwezi mtaja hapa, na kufanikiwa kuniibia baadhi ya vitendea kazi vyangu.

Katika harakati za kutafuta msaada, nilikwenda kituo cha polisi Himo na kupokelewa na Maafisa wa Jeshi la polisi ambao ninaomba nikiri yakuwa si weledi kabisa sio waaminifu ni wanuka rushwa. Hapa naomba unielewe vyema ukimtoa Mkuu wa Kituo, askari wote waliokuwa zamu siku ya tarehe 12/12/2022, na tarehe 13/12/2022 wakiongozwa na Mkuu wa Upepelezi ni genge la wara rushwa.

Nilifika kituoni kwa lengo la kutoa taarifa na kuomba msaada wa kukamatiwa mtu niliyekuwa na uhakika ya kuwa ndiye mwizi wa mali zangu, cha kushangaza IGP, nilibadilishiwa kibao mimi na kuwa niliyejiibia na mwisho wa yote pasipo hata kunifungulia file na kuniabia kosa langu ilitolewa order ya mimi kuwekwa chini ya ulinzi haraka

IGP, kiunyonge niliwekwa ndani, sikukubali kulala ndani ya kituo. Nilipiga kelele za kuwataka waniambie kosa langu na wanifikishe mahakamani haraka, sasa kilichojili ni aibu nitakueleza private.

IGP, naomba nikuelezee hatari iliyopo Mahabusu ya Kituo cha Polisi Himo;

~ Kwanza nilikuta mzee mwenye miaka si chini ya 55yrs akiwa mahabusu ya kituo cha polisi kwa kosa la kukutwa na nyama pori ya nguruwe na alikamatwa na Askari wa hifadhi, mzee huyu ndani ya siku kumi, hajawai kula chakula kutoka kituo cha polisi.

Sababu ya kukuandikia barua hii nataka kujua hivi ni halali polisi wasio na uwezo wa kumpa chakula mtuhumiwa kukaa nae kituo cha polisi zaidi ya siku kumi? Ikitokea mzee hana pesa au pesa alitokamatwa nayo ambayo kila siku anampa Askari amnunulie chakula maana hana mtu wa kumletea chakula ikaisha atakula nini?

Askari wa wanyamapori walikuja wakambwaga wakaondoka, hakuna lolote wanafanya. Je, ni haki mtu huyu kukaa kituoni zaidi ya siku 10 pasipo kufikishwa mahakamani? Je, hatuoni hatari ya mzee huyu kufa kisa njaa?

Nikiwa ndani nikakutana bwana mmoja aliyejitambulisha kwangu kwa jina la Omari, yeye ana siku 5 polisi. Mkewe ameleta chakula mara mbili baada ya hapo pesa imekata, mke haleti chakula polisi tena. Omar amekaaa kituo cha polisi siku 3 pasipo chakula, huyu anatuhumiwa kuiba, aliye mfikisha kituoni hajawai rudi kituoni, mshitakiwa bado yupo mahabusu.

~ Msuguano: Mkuu wa Kituo anatoa order mtuhumiwa ajidhamini awe anaripoti kituoni, Mkuu wa Ppelelezi anagoma kwa sababu anazozijua yeye huki akijitamba mbele ya kikosi kazi chake kinachomzunguka kilichojaa vijana wa ovyo ilihali ni vijana wadogo sana.

Omari akizidi leo lazima kuna uwezekano wa kufa kwa njaa akiwa kituo cha polisi kisa ukiritimba wa mtu mmoja tu Bwana Machibya!

Nikiwa ndani nikakutana na kijana mmoja ambaye simkumbuki jina lake, yeye amekaaa siku sita, kosa lake ni kukutwa amelewa akiwa lindoni na akiwa na silaa. Ili kosa kubwa sana, ila aliyemkamata na kumfikisha hapo hajawai fika kituoni. Yule kijana tangu amekaa ndani, siku zote hakuna Askari anaejua anakulaga nini, no body cares. Hajafikishwa mahakamani anahojiwa kama mtuhumiwa wa mauaji.

IGP, nikiwa ndani nilisikitika sana, kuna jamaa ambao sitaweza waelezea kwa kweli jinsi walivyopokelewa na Mkuu wa Upelelezi mpaka wanawekwa mahabusu Mungu awasimamie. Maana jinsi walivyowashiwa moto na Askari yule, pamoja na kijana mmoja ambae aliwekwa na mimi ndani pia, hakika Mungu ni mwema.

IGP, kuna askari wako mkoja siwezi mtambua kwa no za ajira, kwa tarehe 13/12/2022, alikuwa mapokezi, binafisi nimekuwa na bahati nzuri nae. Tarehe za nyuma niliwai kukutana nae maeneo ya mwanzo wa Katani nikiwa naendesha gari, alinipiga mkono nikasimama, aliponifata kwenye gari aliingia na kuomba nimpe pesa kiutu.

Kwa kuwa sikuwa na kosa nilimgomea, yaliyojiri mimi nilimwonea tu huruma, maana kila kitu nina video yake mpaka anapokea rushwa ya elfu kumi. Nilichokifanya nilipeleka clip ile niliyoirekodi kwa saa yangu ya mkononi kwa TAKUKURU mpaka leo namwonaga tu. Nilitamani nimwoneshe hiyo clip ila kwa sbaabu za usalama wangu niliacha kwako nipo tayari kukufikishia.

IGP, epusha mateso wanayo yapata mahabusu wanaorundikwa kituo cha Himo, ni janga kwa taifa letu. Nina kuandikia barua hii nikiwa nje kwa dhamana, itoshe kukwambia nina mengi moyoni dhidi ya watendaji wako walioko kituo cha polisi Himo. Wapo watendaji walio na wanaozingatia wwledi, changamoto nahisi ni upya wao katika vituo vyetu kwa kuanzia na hapo utapata mengi.

Barua isiyo na ushauri si barua!

~ Kwanza nikushauri nilichokuandikia utume timu ya kukichunguza.

~ Pili Ili upate ukweli wa mambo haya, Mkuu wa Upelelezi wa kituo cha Himo na team ya vijana wake alionao hapo ofisini kwake iwekwe pembeni au ikiwezekana isambaratishwe kabisa, inafanya kazi kwa mazoea na viburi vya hali ya juu sana, wanajiona wao ndo kila kitu.

~ Mkuu wa kituo cha polisi Himo apewe team iliyosafi ambayo anaweza ikomandi kijeshi na ielewe.

Mwisho nakutakia kila la kheri katika ujenzi wa Taifa.

Ni mimi mtuhumiwa nisiyejua file no ngapi nimefunguliwa hapo na pia ni jirani niliyekaribu na kituo kwa shughuli ya genge. Nawakaribisha polisi wote wa Himo hapa kwenye genge langu maana nyinyi ndo wateja wangu wazuri sanaa wa ndizi.
 
Mkuu asante kwa taarifa. Huyu ni wewe pia?

Ila inaonekana unamsagia sana kunguni Mkuu wa Upelelezi na umesimulia kitaalam sana kama na wewe upo chomboni
Yote kwa yote mamlaka zifanyie uchunguzi tu jameni
 
Ila barua yako imekuwa ndefu na yenye kutia uvivu kusoma.
Ungejikita zaid katika mambo yako ili ueleweke zaidi.

Nitamfikishia kilio chako
 
Mmoja amtag aijipiii kwa hendo yake hapa JamiiForums.

Ukweli ukiwa na tatizo ukaenda kituo cha polisi ndio utagundua kiasi gani jeshi limeoza. Limejaa vijana wabishi wabishi
Kuna jamaa yangu alinihadithia alichokutana nacho kituo kimoja alikwenda kumdhamini ndugu yake kwa minajili na yeye ni mwajiriwa wa moja ya vikosi vya usalama tena mwenye cheo kiasi labda kutakua na fair kidogo, rushwa aliyoombwa pa1 minyota nyota yake nikajiuliza imagine walamba chumvi wakiwa na shida kama ile inakuaje ikiwa mwenzao tu ndio wamemfanyia vile!
 
Mkuu asante kwa taarifa. Huyu ni wewe pia?

Watekelezaji wa sheria wanapoiteketeza sheria
 
Hii ni barua ya wazi Kwa IGP wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, ninaekuandikia barua ni raia mwema nisiye na masilahi yoyote na watumishi wako, ila ni Mtanzania ambaye ningependa watendaji walioko chini yako wazingatie weledi wanapokuwa wanatimiza wajibu wao wa kazi pasi uonevu wowote.

IGP, barua hii itakufikia kupitia pahala hapa lakini baada ya hapa nitumia email moja kwa moja na nakala ya barua hii nitaifikisha kwa Mteule wako Ili nae aweze kupata picha dhidi ya matendo machafu na ya ovyo yanayofanywa na watendaji walio chini Yako.

IGP, mimi ni mwananchi nilie karibu sana na Kituo Kikuuu cha Polisi kilichopo wilaya ya Moshi vijijini yaani Himo Police Station. Tarehe 12/12/2022 nikiwa nyumbani kwangu nilivamiwa na mtu mmoja ambaye siwezi mtaja hapa, na kufanikiwa kuniibia baadhi ya vitendea kazi vyangu.

Katika harakati za kutafuta msaada, nilikwenda kituo cha polisi Himo na kupokelewa na Maafisa wa Jeshi la polisi ambao ninaomba nikiri yakuwa si weledi kabisa sio waaminifu ni wanuka rushwa. Hapa naomba unielewe vyema ukimtoa Mkuu wa Kituo, askari wote waliokuwa zamu siku ya tarehe 12/12/2022, na tarehe 13/12/2022 wakiongozwa na Mkuu wa Upepelezi ni genge la wara rushwa.

Nilifika kituoni kwa lengo la kutoa taarifa na kuomba msaada wa kukamatiwa mtu niliyekuwa na uhakika ya kuwa ndiye mwizi wa mali zangu, cha kushangaza IGP, nilibadilishiwa kibao mimi na kuwa niliyejiibia na mwisho wa yote pasipo hata kunifungulia file na kuniabia kosa langu ilitolewa order ya mimi kuwekwa chini ya ulinzi haraka

IGP, kiunyonge niliwekwa ndani, sikukubali kulala ndani ya kituo. Nilipiga kelele za kuwataka waniambie kosa langu na wanifikishe mahakamani haraka, sasa kilichojili ni aibu nitakueleza private.

IGP, naomba nikuelezee hatari iliyopo Mahabusu ya Kituo cha Polisi Himo;

~ Kwanza nilikuta mzee mwenye miaka si chini ya 55yrs akiwa mahabusu ya kituo cha polisi kwa kosa la kukutwa na nyama pori ya nguruwe na alikamatwa na Askari wa hifadhi, mzee huyu ndani ya siku kumi, hajawai kula chakula kutoka kituo cha polisi.

Sababu ya kukuandikia barua hii nataka kujua hivi ni halali polisi wasio na uwezo wa kumpa chakula mtuhumiwa kukaa nae kituo cha polisi zaidi ya siku kumi? Ikitokea mzee hana pesa au pesa alitokamatwa nayo ambayo kila siku anampa Askari amnunulie chakula maana hana mtu wa kumletea chakula ikaisha atakula nini?

Askari wa wanyamapori walikuja wakambwaga wakaondoka, hakuna lolote wanafanya. Je, ni haki mtu huyu kukaa kituoni zaidi ya siku 10 pasipo kufikishwa mahakamani? Je, hatuoni hatari ya mzee huyu kufa kisa njaa?

Nikiwa ndani nikakutana bwana mmoja aliyejitambulisha kwangu kwa jina la Omari, yeye ana siku 5 polisi. Mkewe ameleta chakula mara mbili baada ya hapo pesa imekata, mke haleti chakula polisi tena. Omar amekaaa kituo cha polisi siku 3 pasipo chakula, huyu anatuhumiwa kuiba, aliye mfikisha kituoni hajawai rudi kituoni, mshitakiwa bado yupo mahabusu.

~ Msuguano: Mkuu wa Kituo anatoa order mtuhumiwa ajidhamini awe anaripoti kituoni, Mkuu wa Ppelelezi anagoma kwa sababu anazozijua yeye huki akijitamba mbele ya kikosi kazi chake kinachomzunguka kilichojaa vijana wa ovyo ilihali ni vijana wadogo sana.

Omari akizidi leo lazima kuna uwezekano wa kufa kwa njaa akiwa kituo cha polisi kisa ukiritimba wa mtu mmoja tu Bwana Machibya!

Nikiwa ndani nikakutana na kijana mmoja ambaye simkumbuki jina lake, yeye amekaaa siku sita, kosa lake ni kukutwa amelewa akiwa lindoni na akiwa na silaa. Ili kosa kubwa sana, ila aliyemkamata na kumfikisha hapo hajawai fika kituoni. Yule kijana tangu amekaa ndani, siku zote hakuna Askari anaejua anakulaga nini, no body cares. Hajafikishwa mahakamani anahojiwa kama mtuhumiwa wa mauaji.

IGP, nikiwa ndani nilisikitika sana, kuna jamaa ambao sitaweza waelezea kwa kweli jinsi walivyopokelewa na Mkuu wa Upelelezi mpaka wanawekwa mahabusu Mungu awasimamie. Maana jinsi walivyowashiwa moto na Askari yule, pamoja na kijana mmoja ambae aliwekwa na mimi ndani pia, hakika Mungu ni mwema.

IGP, kuna askari wako mkoja siwezi mtambua kwa no za ajira, kwa tarehe 13/12/2022, alikuwa mapokezi, binafisi nimekuwa na bahati nzuri nae. Tarehe za nyuma niliwai kukutana nae maeneo ya mwanzo wa Katani nikiwa naendesha gari, alinipiga mkono nikasimama, aliponifata kwenye gari aliingia na kuomba nimpe pesa kiutu.

Kwa kuwa sikuwa na kosa nilimgomea, yaliyojiri mimi nilimwonea tu huruma, maana kila kitu nina video yake mpaka anapokea rushwa ya elfu kumi. Nilichokifanya nilipeleka clip ile niliyoirekodi kwa saa yangu ya mkononi kwa TAKUKURU mpaka leo namwonaga tu. Nilitamani nimwoneshe hiyo clip ila kwa sbaabu za usalama wangu niliacha kwako nipo tayari kukufikishia.

IGP, epusha mateso wanayo yapata mahabusu wanaorundikwa kituo cha Himo, ni janga kwa taifa letu. Nina kuandikia barua hii nikiwa nje kwa dhamana, itoshe kukwambia nina mengi moyoni dhidi ya watendaji wako walioko kituo cha polisi Himo. Wapo watendaji walio na wanaozingatia wwledi, changamoto nahisi ni upya wao katika vituo vyetu kwa kuanzia na hapo utapata mengi.

Barua isiyo na ushauri si barua!

~ Kwanza nikushauri nilichokuandikia utume timu ya kukichunguza.

~ Pili Ili upate ukweli wa mambo haya, Mkuu wa Upelelezi wa kituo cha Himo na team ya vijana wake alionao hapo ofisini kwake iwekwe pembeni au ikiwezekana isambaratishwe kabisa, inafanya kazi kwa mazoea na viburi vya hali ya juu sana, wanajiona wao ndo kila kitu.

~ Mkuu wa kituo cha polisi Himo apewe team iliyosafi ambayo anaweza ikomandi kijeshi na ielewe.

Mwisho nakutakia kila la kheri katika ujenzi wa Taifa.

Ni mimi mtuhumiwa nisiyejua file no ngapi nimefunguliwa hapo na pia ni jirani niliyekaribu na kituo kwa shughuli ya genge. Nawakaribisha polisi wote wa Himo hapa kwenye genge langu maana nyinyi ndo wateja wangu wazuri sanaa wa ndizi.
Hii ungetuma kwa Waziri wa mambo ya ndani, TAKUKURU, haki za binadamu, Waziri Mkuu, RC, DC ungepata msaada mapema sn
 
Itoshe kusema kuwa, hali hii ipo kwenye vituo vyote vya police Tanzania.

Na mama Samia alionya sana haya mambo ya kuumiza watu na kuwaonea,ndo maana akabadili IGP.

Why Tanzania mambo hayabadiliki?
 
Hamna kitu tuna Rais ambae hakumbushii maagizo yake alotoa mbele ya hadhara Kwa hio anaongea furahisha Umma tu.
 
Back
Top Bottom