Kama mtu anakopa benki 5 tofauti za Tanzania na akaweza kukimbia nchi bila kugundulika ni ishara kwamba TISS na vyombo vingine vimelala

Mleta mada kama nawe unaweza kukopa na kusepa fanya tu.
Kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake.
Woga wako ndio umasikini wako.
Hapana tuache tamaa (greed) wizi na kupenda njia za mkato.

Tufanye kazi kwa bidii tulipe kodi na tujenge nchi kwa ajili ya vizazi vyetu vya baadae.

Mimi nimesoma, na hadi hapa nilipo nimefika kihalali kabisa na hata mkopo huwa napata kihalali kabisa kutoka katika benki zetu hakuna shida.

Nipo hapa Kibaigwa ndo makazi yangu na nafaidi matunda ya kazi zangu.
 
Hapa JF hayo mambo yako ya kuacha tamaa watu hawatakuelewa nenda kanisani/msikitini huko utapata kusikika na kueleweka.
Watu hapa wanatafuta pesa kwa namna yeyote hata iwe kwa uchawi nk.
Kila mtu ana akili na mawazo yake.
Kama wewe umeridhika na maisha yako hapo Kibaigwa hongera sana endelea hivyo hivyo.
 
Nimeshangaa zaidi Rais ameshindwa hata kumtaja huyo mwizi, tutajie mwizi wa pesa zetu tumjue, sioni sababu ya kumficha hata kama ni masuala ya kiusalama.

Siku hizi kuna interpol, wape information wafanye kazi yao, kuliko kutuambia tu kuna mtu amekopa benki tano akakimbia, naona ni bora angekaa kimya kabisa.
 
Hapana,mimi sijaridhika na maisha kwani bado natoa mchango wangu hapa JF na huko duniani ambako ndiko ujira wangu waingia kilaini kwa kazi zangu.

Kama serikali yajifungua nipo tayari kusaidia kimkakati na kitaalam kufanikisha uwezo wa idara zake kujiimarisha na kujiweka sawa kuendana na changamoto za kiteknolojia na kitaalam zaidi.

Wapo watu kama mzee Kipilimba ni wataalam wa "risk management" khasa kwenye vyombo vya fedha na masuala mazima ya usalama wa kisayansi lakini badala yake wamewekwa kando hivyo kukosa msaada wao wa kitaalam.

Natamani sana jamaa akamatwe na ajulikane na pia kuna mtu kasema kuna "Syndicate".

Hii Syndicate ni muhimu ikajulikana na waandishi wa habari za uchunguzi wapewe nafasi wafanye kazi zao.

Watu hawa (wezi) wakiwa wanafahamika inakuwa ni jambo la uzuri kwa nchi kwani kunaleta "awareness", if you know what I mean na yaleta chagizo kwa voymbo vya usalama, polisi na uhamjai kufanya kazi zao ipasavyo.

Lakini kusema ati mimi nimeridhika hapana, sijaridhika kabisa mkuu mpaka kieleweke.
 
Wapo watu kama mzee Kipilimba ni wataalam wa "risk management" khasa kwenye vyombo vya fedha na masuala mazima ya usalama wa kisayansi lakini badala yake wamewekwa kando hivyo kukosa msaada wao wa kitaalam.
Kwa maana hiyo hakuna watu wengine waliopikwa kwenye risk management wa kuziba nafasi ya kipilimba.
Angetangulia mbele za HAKI tusingesema kawekwa pembeni.
 
Haiwezekani mtu huyo kutokufahamika, abadani! H. A. I. W. E. Z. E. K. A. N. IIIII!!

Utaratibu wa kupata mikopo benki ipoje mpaka kutokumfahamu mtu huyo sshvi!!!?

Imefahamika vipi kua hayupo nchini!!!? ( Au ndio
)

Hili halikubaliki
 
Kwa maana hiyo hakuna watu wengine waliopikwa kwenye risk management wa kuziba nafasi ya kipilimba.
Angetangulia mbele za HAKI tusingesema kawekwa pembeni.
Huu ni utaalam maalum hivyo huitaji mkakati wa serikali kuhakikisha ina watu hawa.

Hivyo Kipilimba angeweza kupewa nafasi ya kufundisha vijana wapya na pale UDSM wakawa na Department ya masuala haya ya security and risk management.

Huko ughaibuni sasa hivi wana shahada za ujasusi yaani Security & Intelligence na zingine.

Yategemea na mtazamo wa serikali kuhusu masuala haya.

Wenzetu China wakituma vijana wake kwenda Ulaya kusoma wapo ndani yake wana shughuli zingine kusomea masuala kama haya.
 
Tafadhali Mods msifute uzi huu kwani wahusu zaidi usalama taifa kwa ujumla.

hirikiana na vyombo vingine kama Uhamaji na hata huko nje Interpol tayari mtu huyu angekuwa yupo kwenye "Wanted List".
Raisi aliyopo ndo tatizo wala sio bank unakuta ni jamaaa amekuja hapo na smart breefcase kutoka Nigeria akaondoka na 50b sio mchezo
 
Akili inaniambia huyo aliyefanya hivyo ni miongoni mwao
 
Raisi aliyopo ndo tatizo wala sio bank unakuta ni jamaaa amekuja hapo na smart breefcase kutoka Nigeria akaondoka na 50b sio mchezo
Na labda aingine nchi zingine kuhifadhi fedha hizo kwani huko Ulaya sasa hivi wamejipanga kukataa fedha chafu kuingizwa katika banking systems zao.

Sasa hivi wameweka masharti kadha wa kadha yanozuia kuweka fedha kama hizo kuzuia utakatishaji fedha na kuchukua fedha za wizi.

Labda kule visiwani Jersey na kwingine.
 
Wewe kama unafikiri kukopa benki ni rahisi neenda ukakope uone ugumu wake.
huyo mkopaji lazima alikuwa anashirikiana na wafanyakazi wa hizo benki. Benki ni taasisi binafsi kwa asilimia kubwa na wao ndiyo wanatakiwa kuwachunguza wateja wao. Hiyo mikopo haikuwa na securities zo zote au amepewa tu kienyeji (labda kwa kuwa mzungu au muhindi).
 
Hawajalala, ni mchongo,

Branch managers wote Wana mfumo uliounganishwa jikoni.

Haiwezekani ipite 5 banks wasijue.
 
Hiyo ni syndicate ya hali ya juu inajulikana vizuri na ma boss wa Bot......ila sisi raia wa kawaida tunaanza kujadili masuala tusio ya jua, kufanya justification ya wizi tu.
Nafkiri hii ndo ingekuwa comment ya mwisho na uzi ufungwe 👍🏾
 
Wewe kama unafikiri kukopa benki ni rahisi neenda ukakope uone ugumu wake.
Taasisi zetu za fedha bado ziko nyuma saana. Pia, nchi bado iko nyuma kuhusu individual financial records ikiwa ni pamoja fedha alinazo mtu, mali zisizohamishika alizonazo mtu, madeni aliyonayo, na credit rating ya mtu. Nchi zilizo na records nzuri ukiingiza namba ya uraia unaona haya yote. Mkopo unatolewa baada ya kuona uwezo wa kukopa na kurudisha upo. Kwa mfano hili la mikopo 5 au 6 lingeweza kuonekana na kutoa shaka haraka.

Naona TISS wanalaumiwa, lakini hapa TISS wangefanya nini? Hata huko Ulaya kosa kama FBI au NIS hawawezi kulizuia, ila likifanyika wanaweza kupeleleza na kuona jinsi ya kuwapata. Upelelezi kama huu hauychukui siku moja au mbili. Upelelezi hukukuwa muda kwa sababu tahadhari huchukuliwa na wahalifu na wakati mwingine husaidiwa na mitandao mikubwa ndani na nje ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…