Kama mliaminishwa kufungua Chaneli ya WhatsApp ni Mafanikio, sasa watawaaminisha Viwanja vya Mikoani ndio chanzo cha Matokeo Mabovu

THE FIRST BORN

JF-Expert Member
Apr 24, 2019
1,729
3,288
Mkishaonwa HAMNAZO mtakuwa mnapewa kila sababu na mtakubali because nyie ni HAMNAZO.

Yaani jitu linavuta Oxygen hii ya buree saiv zaidi ya miaka 20 halijawahi ilipia linakuja danganywa kuwa tunapata matokeo mabovu viwanja vya mikoani kwa sababu wachezaji wetu hawako comfortable na viwanja hivi?

Unajiuliza je, hawa wachezaji asili yao ni wapi? Ulaya kwenye viwanja lukuki au?

Utajiuliza swali jingine.

Hivi kipindi wanabeba Ligi hawa walikuwa wanatumia Viwanja vya Dar es Salaam tu au walikuwa wanashinda match za mjini Dar pekee?

Mwisho, kama viongozi wenu waliweza kuwaaminisha kuwa kufungua Chanel ni mafanikio ya Team sasa hivi hawawezi acha kuwaaminisha kuwa viwanja vya mikoani ndio sababu ya matokeo mabovu ila ukweli ni kuwa team yenu haina huo uwezo kama wa zamani kwa sasa.

Hizo zingine ni ngonjera za hodi hodi twaingia.
 
Back
Top Bottom