Robert S Gulenga
JF-Expert Member
- Jan 3, 2013
- 2,161
- 1,493
Simba na Yanga ni vilabu vikongwe na vikubwa si Africa Mashariki tu bali Afrika kwa ujumla.
Yanga na Simba zina historia kubwa pengine kuliko vilabu vingi Africa, historia zao zimejengwa katika lengo lililofanya vilabu hivi kuazishwa miaka zaidi ya 63 iliyopita.
Vilabu hivi unaweza kuviita ni vilabu vyenye mafanikio kwa maana ya ndani ya Uwanja lakini si nje ya Uwanja.
Miaka zaidi ya 60 toka kuazishwa kwake vilabu hivi havijaweza kuwa na viwanja vyao vyenye hadhi na ubora wa vilabu hivi.
Msingi wa timu yeyote ya mpira Duniani ni uwekezaji katika uwanja wa kisasa wa mpira, kwanini Yanga na Simba haviwekezi katika Viwanja vyao vya kisasa?
Shida ni Wasimamizi wa mpira ? Kwa maana ya TFF? Shida ni Sera za nchi? Shida ni uongozi wa vilabu hivi?
Wakati macho na maombi ya Watanzania yako kwa timu hizi mbili ziweze kuvuka hatua ya Robo. Ni vizuri Vilabu hivi vijiulize ni timu gani zimeingia hatua ya Robo hazina viwanja kama Simba na Yanga?
Tanzania sasa ni moja ya nchi ambayo mpira unakua kwa kasi kubwa sana, uwekezaji katika maslahi ya Wachezaji ni mkubwa kuliko nchi nyingi za Africa.
TFF wahimize, washirikiane, wawaongoze na kushauri kuhakikisha vilabu hivi vinakuwa na Viwanja vyenye hadhi ya Kimataifa
Pengine kwa mara ya kwanza tunaweza peleka timu mbili katika hatua ya nusu fainali katika moja ya michuano mikubwa zaidi kwa ngazi za vilabu Africa
Tuwaombee Simba na Yanga.
Tanzania kwanza.
Mungu ibariki Tanzania