Kama Makamba atatenda anayoyazungumza kuhusu umeme ni jambo la muda, tutarajie umeme bora siku za mbeleni

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,283
3,274
Nianze kwakusema mimi ni muhanga wa huu umeme wa Tanzania kwani nilishawahi kupata hasara ya mamilioni mara kwa mara kwasababu ya low voltage.

Mimi ni mjasiliamali mwenye kiwanda kidogo hivyo kutokana na umeme kuwa mdogo ilikua inalazimu kuwasha machine mojamoja kwani mbili kwa wakati mmoja ilikua haiwezekani lakini pia hata kwakuwasha moja bado mota zilikua zinaungua hovyo.

Kuna mzee mmoja mstaafu Tanesco,mzee huyu baada ya kuona kadhia hii akaona anisaidie,mimi nilifikiri kwamba tatizo transformer ni ndogo kumbe sivyo ,ndipo kupitia huyu mzee nilipojua kumbe niliteswa na size ya waya zilizotumika na Tanesco kusambazia kutoka kwenye Transformer kuja kiwandani.

Mzee huyu akaniambia umeme kutoka kwenye transformer kuja kwa mteja unatakiwa usizidi 1km yaani zisizidi nguzo ishirini.Size ya waya akaniambia isipungue 50mm,wakati tanesco walikua wametumia 25mm tena zile zilizopo uchi.Ukifuatilia hata sasa utagundua miradi mingi ya REA wanatumia zaidi 25mm kwenye usambazaji mtaani jambo ambalo ni kosa.

Nilipoenda Tanesco miaka hio nilikosa ushirikiano wakawa wanasumbua na smtz wanataka rushwa,baadae huyu mzee akaona anisaidie Akaenda mwenyewe lakini ilichukia miaka ndipo wakaja kubadilisha kwenye 2015 nakumbuka.

Walipo badili waya tu tatizo likawa historia.

Hapa unajifunza kwamba tunaweza kuwa na umeme mwingi tu kutoka bwawa la mwl Nyerere lakini kama tanesco wasipozingatia standard kwenye kuusambaza umeme bado tutaendela kuteseka.Binafsi naona kitu fulani kwa Makamba.

Jana nimemsikia makamba kipindi cha dk 45 ITV anasema walifanya tafiti kujua matatizo ya umeme nchini.Inawezekana walitumia pesa nyingi sana kufanya hizi tafiti zao..Huyu mzee anasema matatizo ya umeme nchi hii hayahitaji tafiti kwani standard zipo tatizo Tanesco hawazifuatilii.

Ni kweli kupitia huyu mstaafu anayoyasema makamba mimi niliyafahamu toka 2012.

Hata hivyo mh Makamba anatakiwa ajue bado Tanesco wanaendelea kutumia waya nyembamba kwenye usambazaji.Mimi nimeshuhudia line ya usambazaji iliokuja kwangu imejengwa 2021 na waya uliotumika ni 25mm.

Wandengereko wanasema 'zilongwa mbali zitendwa mbali'..Makamba asipokua mkali ataishia maneno mazuri wakati watendaji wake huku chini wanaendelea kuboronga.

Ningeomba tumpe muda makamba anaweza akapunguza matatizo yanayoikumba nchi yetu kwenye umeme.

Asanteni.
 
Hata hivyo mh Makamba anatakiwa ajue bado Tanesco wanaendelea kutumia waya nyembamba kwenye usambazaji.Mimi nimeshuhudia line ya usambazaji iliokuja kwangu imejengwa 2021 na waya uliotumika ni 25mm.
Halafu quotation ni ya 50mm, sema wanatuweza kwakua hatupendi kusoma! Na tukisoma hatusomi Ili tuelewe.
 
Mkuu umetusanua sana.... Kumbe nyaya zinapaswa ziwe 50mm siyo chini ya hapo?

Basi siku navuta umeme nitakuwa macho sana...
 
Nazungumzia zile wanazotumia kwenye kusambazia yaani zile zinazowekwa kutoka kwenye transformer kuja mtaani mkuu.
 
50mm =5cm=2"!! Sijawahii kuona waya wenye diameter hiyo ukitumika kama power supply cable, labda mimi bado mshamba
 
Halafu quotation ni ya 50mm, sema wanatuweza kwakua hatupendi kusoma! Na tukisoma hatusomi Ili tuelewe.
Tumekua tukiunguza vitu vya umeme Sana kwasababu ya uzembe wa Tanesco.
Kuna kitu wanaita voltage drop.Hii hutegemea na umbali kutoka kwenye transforma kuja kwa mteja pamoja na size ya waya.

Kama transformer halijawa overloaded na size sahihi ya waya ikizingatiwa pamoja na umbali kutoka kwenye transformer,voltage drop huanza baada ya 1km.

Ukichunguza hili utagundua ndio tatizo sugu kwa Tanesco.Hata leo licha ya Makamba kulieleza kwa uzuri lakini Tanesco bado wanaendelea kuweka waya nyembamba.Madhara yake voltage drop ambayo ilitakiwa ianze nje ya 1km inaanza ndani ya 1km wanatuletea majanga kwenye vifaa vyetu.

Yule mzee huwa anaumia sana na huu uborongaji.

Alishawahi kuwafuata ofisini kwa kesi nyingine ambayo nayo nimemsikia makamba akiilalamikia;
Kuna hizi line za transmition yaani zinatoa umeme kutoka Kijiji kwenda Kijiji ama vijiji vingine.Sasa hizi line kwakawaida zinakua ni ndefu kutegemeana na umbali kutoka Kijiji kimoja kwenda kingine,sheria inawataka kwa umbali fulani waweke Isolator yaani ni kama swichi/vitenganishi,kazi ya hizi swichi husaidia kama Kijiji cha mbele kukiwa na hitilafu wanakata kwenye Kijiji hicho tu ili warekebishe lakini vijijini vingine waendelee kupata huduma.

Sasa hii tanesco ya sasa transmition line ya kuhudumia vijijini vinne unakuta Isolator moja ipo kwenye chanzo.Kijiji cha mwisho kikipata hitilafu inalazimu wakate umeme kwa vijiji vyote ili warekebishe tatizo lililopo kwenye Kijiji kimoja tu.Huyu mzee huwa anakerekaga Sana na Tanesco.
 
Nianze kwakusema mimi ni muhanga wa huu umeme wa Tanzania kwani nilishawahi kupata hasara ya mamilioni mara kwa mara kwasababu ya low voltage.

Mimi ni mjasiliamali mwenye kiwanda kidogo hivyo kutokana na umeme kuwa mdogo ilikua inalazimu kuwasha machine mojamoja kwani mbili kwa wakati mmoja ilikua haiwezekani lakini pia hata kwakuwasha moja bado mota zilikua zinaungua hivyo.

Kuna mzee mmoja mstaafu Tanesco,mzee huyu baada ya kuona kadhia hii akaona anisaidie,mimi nilifikiri kwamba tatizo transformer ni ndogo kumbe sivyo ,ndipo kupitia huyu mzee nilipojua kumbe niliteswa na size ya waya zilizotumika na Tanesco kusambazia kutoka kwenye Transformer kuja kiwandani.

Mzee huyu akaniambia umeme kutoka kwenye transformer kuja kwa mteja unatakiwa usizidi 1km yaani zisizidi nguzo ishirini.Size ya waya akaniambia isipungue 50mm,wakati tanesco walikua wametumia 25mm tena zile zilizopo uchi.Ukifuatilia hata sasa utagundua miradi mingi ya REA wanatumia zaidi 25mm kwenye usambazaji mtaani jambo ambalo ni kosai.

Nilipoenda Tanesco miaka hio nilikosa ushirikiano wakawa wanasumbua na smtz wanataka rushwa,baadae huyu mzee akaona anisaidie Akaenda mwenyewe lakini ilichukia miaka ndipo wakaja kubadilisha kwenye 2015 nakumbuka.

Walipo badili waya tu tatizo likawa historia.

Hapa unajifunza kwamba tunaweza kuwa na umeme mwingi tu kutoka bwawa la mwl Nyerere lakini kama tanesco wasipozingatia standard kwenye kuusambaza umeme bado tutaendela kuteseka.Binafsi naona kitu fulani kwa Makamba.

Jana nimemsikia makamba kipindi cha dk 45 ITV anasema walifanya tafiti kujua matatizo ya umeme nchini.Inawezekana walitumia pesa nyingi sana kufanya hizi tafiti zao.Huyu mzee anasema matatizo ya umeme nchi hii hayahitaji tafiti kwani standard zipo tatizo Tanesco hawazifuatilii.

Ni kweli kupitia huyu mstaafu anayoyasema makamba mimi niliyafahamu toka 2012.

Hata hivyo mh Makamba anatakiwa ajue bado Tanesco wanaendelea kutumia waya nyembamba kwenye usambazaji.Mimi nimeshuhudia line ya usambazaji iliokuja kwangu imejengwa 2021 na waya uliotumika ni 25mm.

Wandengereko wanasema 'zilongwa mbali zitendwa mbali'.Makamba asipokua mkali ataishia maneno mazuri wakati watendaji wake huku chini wanaendelea kuboronga.

Ningeomba tumpe muda makamba anaweza akapunguza matatizo yanayoikumba nchi yetu kwenye umeme.

Asanteni
makamba ni nani? Inamaana Tanzania ni mtu mmoja toka Bumbuli ndio mwenue mipango?? Tumpe Muda Makamba? Yaani tumeipa muda CCM tumpe muda Makamba. Hiyo ni akili ha wapi?
 
Kama ni hivyo Mbowe leo asingekua mwenyeketi kwa miaka yote hii,kwani mboe ni nani muda wote huu haachii wengine?
 
Tumekua tukiunguza vitu vya umeme Sana kwasababu ya uzembe wa Tanesco.
Kuna kitu wanaita voltage drop.Hii hutegemea na umbali kutoka kwenye transforma kuja kwa mteja pamoja na size ya waya.

Kama transformer halijawa overloaded na size sahihi ya waya ikizingatiwa pamoja na umbali kutoka kwenye transformer,voltage drop huanza baada ya 1km.

Ukichunguza hili utagundua ndio tatizo sugu kwa Tanesco.Hata leo licha ya Makamba kulieleza kwa uzuri lakini Tanesco bado wanaendelea kuweka waya nyembamba.Madhara yake voltage drop ambayo ilitakiwa ianze nje ya 1km inaanza ndani ya 1km wanatuletea majanga kwenye vifaa vyetu.

Yule mzee huwa anaumia sana na huu uborongaji.

Alishawahi kuwafuata ofisini kwa kesi nyingine ambayo nayo nimemsikia makamba akiilalamikia;
Kuna hizi line za transmition yaani zinatoa umeme kutoka Kijiji kwenda Kijiji ama vijiji vingine.Sasa hizi line kwakawaida zinakua ni ndefu kutegemeana na umbali kutoka Kijiji kimoja kwenda kingine,sheria inawataka kwa umbali fulani waweke Isolator yaani ni kama swichi/vitenganishi,kazi ya hizi swichi husaidia kama Kijiji cha mbele kukiwa na hitilafu wanakata kwenye Kijiji hicho tu ili warekebishe lakini vijijini vingine waendelee kupata huduma.

Sasa hii tanesco ya sasa transmition line ya kuhudumia vijijini vinne unakuta Isolator moja ipo kwenye chanzo.Kijiji cha mwisho kikipata hitilafu inalazimu wakate umeme kwa vijiji vyote ili warekebishe tatizo lililopo kwenye Kijiji kimoja tu.Huyu mzee huwa anakerekaga Sana na Tanesco.
Na Huyomzee Alikuwa mfanyakazi wa Tanesco leo ndio Anaona Tatizo sindio
 
Nazungumzia zile wanazotumia kwenye kusambazia yaani zile zinazowekwa kutoka kwenye transformer kuja mtaani mkuu.
toka kwenye transformer ni 95 sq. mm (nguzo to nguzo), baada ya mwendo 'flani' zinapungua tu 50 sq. mm (nguzo to nguzo) , then inashuka to 25 sq. mm ( nguzo to mteja )
 
makamba ni nani? Inamaana Tanzania ni mtu mmoja toka Bumbuli ndio mwenue mipango?? Tumpe Muda Makamba? Yaani tumeipa muda CCM tumpe muda Makamba. Hiyo ni akili ha wapi?
Ni mawazo yake na mtazamo wake, tuyaheshimu!
 
Binafsi naona kitu fulani kwa Makamba.....nimemsikia makamba kipindi cha dk 45 ITV anasema walifanya tafiti kujua matatizo ya umeme nchini.

wakati anazungumza hayo maneno, alikuwa kavaa ile style yake ya kujifananisha na uvaaji wa barack obama?....nazungumzia ile style ya kuvaa suruali ya kadeti na shati jeupe la mikono mirefu halafu mikono ya shati unaikunja.

kama ndio, basi fahamu hapo hakuna kitu, alikuwa anapiga siasa tu ili aendelee kujiamarisha ktk position ya kula mema ya nchi. wakati wao huu.
 
Back
Top Bottom