Kwa hili bora waniue tu. Sio Makamba wala Rais nina imani nao kuhusu mradi wa Rufiji. Tumepigwa

Makimuda255

Senior Member
Jul 31, 2020
165
286
Sina imani na Makamba na Rais Samia kuhusu mradi wa bwawa la Nyerere, huenda Makamba anatumiwa na nchi za kigeni.

Hivi huu mgao wa umeme mnaounaje? Kiukweli maswali ni mengi mno, wanasema wanarekebisha ili tuhamie kwenye umeme wa gesi, ukiwauliza kwa gesi ipi wakati gesi ina mwenyewe?

Utaratibu uliopo ni kuwa serikali kupitia Tanesco itanunua gesi kutoka kwa mwekezaji pale mtwara wakishanunua ndo nao wazalishie umeme na watuuzie.

Zamani nilifikirigi ni serikali inachukua tu gesi yake inazalisha umeme kumbe sio kweli kumbe tunaenda kununua gesi kutoka kwa hao wawekezaji wenye vitalu then wanatuuzia na sisi ndo tunaipeleka Tanesco wanazalisha umeme nao wanauuza kwa wananchi.

JPM baada ya kuingia madarakani na kugundua gesi ilishachukuliwa na mikataba ishasainiwa huwezi kuivunja, ilibidi kinyonge akubali tu kuwa tushapigiwa.

Unaambiwa hakuna mkataba ulimuumaga Magufuli kama mkataba wa gesi wa Mtwara, mzee wa watu akaona isiwe kesi akaona wacha apambane ajenge mradi wa Steglaz wa bwawa la Nyerere tupate megawatt 2200 kwa wakati mmoja.

Umeme ambao ni mwingi kwani hata mamitambo yote ya gesi yaliyoko nchi hii uyaunganishe yote hayawezi toa megawat 300 lakini maporomoko ya Rufiji Nyerere Dam pekee yatatoa megawatt 2200 kwa wakati mmoja huu ni umeme mwingi tutauza nchi zaidi ya 5 nje!

Lakini cha ajabu sasahivi wameachana na huu mradi ghafla wamerukia kwenye umeme wa gesi.

Wamerukia kwenye umeme wa gesi ambao ni ghali na gharama kubwa kwa faida ya nani? Ni nani anafaidika na hiyo mikataba ya gesi? Ninani yupo nyuma ya hili?

Kwanini wameacha umeme nafuu wa bwawa la Nyerere na umeme wa uhakika na bei rahisi na kurukia umeme wa gesi ambao ni ghali na ni gesi ya kununua kwa mwekezaji?

Nani atafaidika tukianza kununua gesi kwa mwekezaji halafu wanatupangia bei halafu na tanesco watuuzie hawaoni ni biashara kichaa ya hasara watakaofaidika ni wawekezaji wanaotuuzia gesi yetu wenyewe?

Muulizeni Makamba iko wapi output ya mradi wa gesi wa Kinyerezi? maana nasikia megawatts zilizotarajiwa zingepatkana hazijafikia hata nusu?

Hivi mnajua mradi wa bomba la gesi Mtwara inasemekana serikali ya Jk ilikopa? Mradi wa gesi wa Kinyerezi wa gesi pia walikopa sasa chukua hyo mikopo yote jumlisha na bado hiyo gesi watauziwa na mwekezaji maana gesi siyo yetu tena bado watapangiwa bei ya kutuuzia umeme hao tanesco sasa kwa haya yote mnadhani tutafaidika nini kama nchi?

Hivi wanadhani mwendazake alikua hana akili alivyoachana na haya mauzauza ya gesi? Hivi hawa jamaa wanatuonaje?

Makamba aliingia mkataba na kampuni ya kihindi kutoka India kwa ajili ya kukodi app (application software) ya kutumika Tanesco eti hiyo software alikodi kwa bilioni 70 jamani hii nchi daaah, bilioni 70 ukodi software? Uwiiii hivi kuhama bongo unabonyeza ngapi?

Ilitakiwa ikifika November 2021 bwawa la Nyerere liwe limeshajazwa maji tayari kwa kuanza kazi, lakini cha ajabu Mama akamtoa Waziri Kalemani mchapakazi na akamuweka Makamba!

Hadi leo Kalemani katolewa bila kufanya kosa lolote lile. Halafu Makamba anaulizwa bungeni kwanini maji hayajajazwa hadi leo anatoa sababu ambazo hazieleweki, mara ooh et winchi ya kuchimbia moja haipo eti hadi iagizwe nje! Mara shimo lilikosewa kuchimbwa! Huu mradi nahisi unacheleweshwa tu, na nchi za magharibi wanaupiga vita huu mradi kwasababu.

Wanaupigavita huu mradi maana wanajua mkishakua na huu mradi tatizo la umeme litabaki historia nchini, na watapoteza soko la kuuza solar, majenereta, mafuta na maumeme yao ya ghali nchini.

Huu mradi unapigwa vita balaa kila rais alotaka kujenga huu mradi alizuiwa na kupigwa biti na wazungu na mabepari wa dunia hii kuanzia Nyerere, Mwinyi, Mkapa, JK

Wote walitaka jenga ila mabeberu wakawapiga biti wasijaribu JPM ndio mwanaume pekee alosema liwalo na liwe na siogopi, Uwiii sina imani na Makamba juu ya huu mradi. Sidhani kama ana nia ya huu mradi uishe hata maza simuamini ktka hili.

Jamani leo kwa mara ya 1 nasema simwamini mtu yeyote juu ya huu mradi sina imani kabisa na yoyote yule.

Bimkubwa kwanini alimtoa Kalemani? Unajua nyie watu mimi sielewi mjue! simwamini Makamba toka aingie ni migao tu ya umeme na umeme kukatika ovyo.

Sasa nitaamini vipi kwamba ana nia ya dhati ktk kukamilisha miradi ya mwendazake ambayo alijitoa sadaka liwalo na liwe ili huo mradi ujengwe?

Kwa hili na waniue kabisa lakini hivi vitu vinakera kabisa!!!
 
Sio wewe tu..hata mimi naona hakuna la maana hapo tayari wahuni..mafisadi wazee wa mipango wapo kazini..sumeona mara mgao kila siku..hapo wazee wadili wamewekwaa kuwamisha hilo la Bwawa la Nyerere waendelee kuuza gesi.

Kiufupi tumeshapigwa tutarajie maumivu tu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ukisoma report ya ukaguzi ya Tanesco ya 2020, utaona kua walipata faida ya 45B baada ya miaka na miaka ya kupata hasara na kutegemea ruzuku.

JPM aliwanyima ruzuku na still wakaweza kutengeneza faida.
Ktk report yao wamesema kabisa umeme wa Gas ni Aghali, ila wahuni vichwa ngumu wanaupenda sana...
Kile kitu mzungu alikifanyia kichwa cha muafrica enzi za utumwa ni Mungu tu anajua.
 
Waliozoea kuishi kwa uongo na propaganda watateseka sana zinapokuja zama za ukweli.

Lile bwawa hakuna mhandisi wala mkandarasi duniani ambaye angeweza kulijenga kwa ubora na muda mfupi kama tulivyokuwa tunaimbiwa mapambio.

Hata ujenzi wa SGR ni hivyo hivyo.
 
Ukisoma report ya ukaguzi ya Tanesco ya 2020, utaona kua walipata faida ya 45B baada ya miaka na miaka ya kupata hasara na kutegemea ruzuku.
JPM aliwanyima ruzuku na still wakaweza kutengeneza ruzuku.
Ktk report yao wamesema kabisa umeme wa Gas ni Aghali, ila wahuni vichwa ngumu wanaupenda sana...
Kile kitu mzungu alikifanyia kichwa cha muafrica enzi za utumwa ni Mungu tu anajua.
Hata TTCL na ATCL zilitoa faida na gawio enzi za Jiwe. Upuuzi mtupu wa propaganda na kujilisha upepo wakati kiuhalisia tulikuwa hoi
 
Hata TTCL na ATCL zilitoa faida na gawio enzi za Jiwe. Upuuzi mtupu wa propaganda na kujilisha upepo wakati kiuhalisia tulikuwa hoi
Umesoma report ya ukaguzi ya CAG kuhusu Tanesco?

Kampuni inaweza kupata faida but ikawa na accumulative loss, board of directors inaamua kama itoe gawiwo or isitoe na kama inatoa itoe kwa kiwango gani.

anyway haya mambo yanaonekana ni makubwa kwako

Screenshot_20220206-204926_WhatsApp.jpg
 

Attachments

  • Screenshot_20220206-204926_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20220206-204926_WhatsApp.jpg
    17.1 KB · Views: 61
Ukweli uko hivi, wale waliotufisadi gesi yetu kwa mikataba ya kijinga ya enzi za fisadi Kikwete ndio wanafanya kila linalowezekana ili mradi usikamilike kwa kuwa hiyo ni heri kwao kwa kuendelea kutuuzia gesi yao ya bei ya juu tuzalishie umeme.

Mradi wa JNHPP ukikamilika maana yake ni kwamba tutajitosheleza kwa mahitaji ya umeme na kupata ziada ya kuuza nje, bila kuwategemea hao wanyonyaji wanaotuuzia gesi.

Kwa hiyo ni lazima wafanye juu chini ili mradi usikamilike ili waendelee kutupiga. Sina uhakika sana kama Kikwete hana share kwenye hayo makampuni ya gesi.

Inabidi tufike mahali tuchague aidha kuendelea kuwa na Kikwete/ makamba & co, au tuwafyeke watuachie mradi wetu!
 
Tumeshawahj kuwa na maraisi wawili tu.
Nyerere na magufuli.
Nadhani Kanda ya ziwa iko poa kutoa viongozi hata kada ya ulinzi nadhani wanaihimili.
Kuna siku tutapata raisi mkurya ndo mtajua hamjui
Hili swala la viongizi wa kanda ya ziwa kuonekana kuwa na "outstanding performance" nimewahi kulizungumza sehemu Ila watu hwakuniamini,but ukweli kwamba hii kanda inatoa Marais waziri Sana. Na hata utakuta mafisadi hawatoki huko Sana.
 
SINA IMANI NA MAKAMBA NA SAMIA KUHUSU MRADI WA BWAWA LA NYERERE HUENDA MAKAMBA ANATUMIWA NA NCHI ZA KIGENI
Hivi huu mgao wa umeme mnaounaje?Kiukweli maswali ni mengi mno, wanasema wanarekebisha ili tuhamie kwenye umeme wa gesi, ukiwauliza kwa gesi ipi wakati gesi ina mwenyewe?Utaratibu uliopo ni kuwa serikali kupitia Tanesco itanunua gesi kutoka kwa mwekezaji pale mtwara wakishanunua
Mimi simuamini kuanzia Makamba Senior mpaka huyu njaa nuari ma - kamba!

Kizazi cha nyoka.
 
Gas yetu afu bado tunanunua? Hii nchi JK angetawala kwa miaka 20 tungepigwa mnada aseee. Moja ya maraisi walokua wanasaini mikataba ya hovyo sana ambayo haina maslahi kwa watanzania.

Hawangalii future ya watanzania wanajali matumbo yao hii ndo Tanzania. Hizi dhuluma wanazotufanyia Mungu atadeal nao.

Gas yetu ila bado tunanua inshort tumeuza au mikataba mibovu.
 
Back
Top Bottom