DOKEZO Waziri Makamba fuatilia kwa makini miradi mingi ya REA wakandarasi wanatumia waya za 25mm badala ya 50mm kwenye service line

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,283
3,274
Mh Makamba sijawahi kuona wafanyakazi wako wazembe mkiwawajibisha kwenye ziara zako zakusikiliza kero za wananchi nafikiri ndio sababu wakandarasi wakishirikiana na wakaguzi Kabla ya miradi ya REA kukabidhiwa kwa TANESCO wanaendelea kupiga pesa.

Mh makamba huwa nafuatilia sana makala zenu za kuelemisha kwenye TV,moja ya sababu ambazo umekua ukitolea ufafanuzi zinazopelekea umeme kuwa mdogo ni ukubwa wa waya unaotumika kwenye service line yaani kwenye zile nguzo za mitaani kutoka nguzo moja kwenda nyingine.

Mh Makamba pamoja na mtendaji mkuu wako wa TANESCO bw Maharage mlishawahi kuwawajibisha wakaguzi wangapi kwakuikubali na kuipitisha miradi ya REA kwakuwa chini ya kiwango?

Hili la usambazaji wa waya za 25mm hasa kwenye miradi ya REA ni tatizo kubwa sana ambapo wakandarasi wanazitumia ili kupiga pesa jambo ambalo linasababisha vyombo vyetu wananchi vinaungua kutokana na umeme kuwa mdogo.

Mh Makamba hakikisheni hili jambo linakomeshwa, hizi makala zenu zitakuwa hazina maana kama yale mnayoyasemea bado mnaendelea kuyafanya.

Nipo tayari kuwaonesha hizi waya zenu kama ninyi mtajifanya vipofu hamzioni huko mitaani.

Asante.

22/10/2022
Mpaka leo licha ya kuwatumia namba yangu ya simu pm TANESCO hawajanitafuta.

Binafsi nimejua ni kwanini wanakuwa wazito kunitafuta,

Katika tatizo sugu tanesco ni uzingatiaji wa matumizi sahihi ya size za waya,

Ukitembea humu mitaani naweza sema maeneo mengi wanatumia 25mm badala ya 50mm inayohitajika.

Niendelee kusisitiza kwa wizara waache ile kauli ya wazaramo,"zilongwa mbali zitendwa mbali".

Haya kama mnaona haina haja kunitafuta,zingatieni standard kwenye utekelezaji wa kazi zenu ili vifaa vyetu viwe salama.
 
Ndio raha ya Jf kufichua maovu na Mchwa wanaolitafuna Taifa letu.

200 (15).gif
 
Yaani kesi ya Tumbili unaipeleka kwa Nyani?

Wakati huyo Nyani ndio kinara wa wizi wenyewe!

Mwizi hawezi mkemea mwizi mwenzake,bali watakaa na kushauriana jinsi ya kuiba "vizuri".

Kwa mbinu mpya na nzuri kabisa.

Tanesco haiko kwenye mikono salama kwa sasa.

Tena waziri Makamba hajaridhika na uwaziri wa Nishati pekee,bali sasa hivi anafanya na uwaziri wa Afya,ana kampeni ya "Mama na Moshi"
 
Mh Makamba sijawahi kuona wafanyakazi wako wazembe mkiwawajibisha kwenye ziara zako zakusikiliza kero za wananchi nafikiri ndio sababu wakandarasi wakishirikiana na wakaguzi Kabla ya miradi ya REA kukabidhiwa kwa TANESCO wanaendelea kupiga pesa.

Mh makamba huwa nafuatilia sana makala zenu za kuelemisha kwenye TV,moja ya sababu ambazo umekua ukitolea ufafanuzi zinazopelekea umeme kuwa mdogo ni ukubwa wa waya unaotumika kwenye service line yaani kwenye zile nguzo za mitaani kutoka nguzo moja kwenda nyingine.

Mh Makamba pamoja na mtendaji mkuu wako wa TANESCO bw Maharage mlishawahi kuwawajibisha wakaguzi wangapi kwakuikubali na kuipitisha miradi ya REA kwakuwa chini ya kiwango?

Hili la usambazaji wa waya za 25mm hasa kwenye miradi ya REA ni tatizo kubwa sana ambapo wakandarasi wanazitumia ili kupiga pesa jambo ambalo linasababisha vyombo vyetu wananchi vinaungua kutokana na umeme kuwa mdogo.

Mh Makamba hakikisheni hili jambo linakomeshwa,hizi makala zenu zitakuwa hazina maana kama yale mnayoyasemea bado mnaendelea kuyafanya.

Nipo tayari kuwaonesha hizi waya zenu kama ninyi mtajifanya vipofu hamzioni huko mitaani.
Asante.
Ndugu Mteja,

Tunashukuru kwa taarifa na uzalendo mkubwa ulionesha, tafadhali onesha ni mradi wa eneo gani haswa na namba yako ya simu kwa ufatiliaji na hatua zaidi,

TANESCO tupo kukusikiliza

Asante
 
Hili la usambazaji wa waya za 25mm hasa kwenye miradi ya REA ni tatizo kubwa sana ambapo wakandarasi wanazitumia ili kupiga pesa jambo ambalo linasababisha vyombo vyetu wananchi vinaungua kutokana na umeme kuwa mdogo.
Duuh! Hii ni hatari kwa usalama wa nyumba na vyombo vingine vutumiavyo nishati ya umeme.
 
Bwana Maharage angekua na akili wakati mdogo asingekubali kuitwa hivyo,usikute walimpa hilo jina baada ya kuzaliwa msimu wa maharage na familia kupata maharage mengi. Lakini ni mmoja wa wafanyakazi hodari kabisa
 
Ndugu Mteja,

Tunashukuru kwa taarifa na uzalendo mkubwa ulionesha, tafadhali onesha ni mradi wa eneo gani haswa na namba yako ya simu kwa ufatiliaji na hatua zaidi,

TANESCO tupo kukusikiliza

Asante
Njooeni mcheki na huku Tunduma umeme kila ikifika jioni unakata na kuzima mpaka usiku saa tatu mpka saa nne ndo unakuwa stable wamefwata kufatilia kila siku majibu ni yaleyale as if sisi tumependa hizi kero hebu jiangalie bhana mtaa unaitwa kigamboni hili ni tatizo kubwa tena linakela yaani usiku nashindwa kutumia umeme na ikifika asubuhi tena mwendo ni uleule mpka saa tano au saa sita kwa kifupi mnakera tanesco
 
Ndugu Mteja,

Tunashukuru kwa taarifa na uzalendo mkubwa ulionesha, tafadhali onesha ni mradi wa eneo gani haswa na namba yako ya simu kwa ufatiliaji na hatua zaidi,

TANESCO tupo kukusikiliza

Asante
Niwashukuru kwa uungwana japo kuonesha kujali,
Nitakuja pm nitatoa no ya simu kwa mawasiliano,
Angalizo,
Akaunti zetu humu JF ni za siri hivyo natumai usiri huu utadumishwa mara baada yakutoa no zangu za simu kwa mawasiliano,
Mwishokabisa nawahakikishia wana JF nitawapa mrejesho wa nitakayoyapata kutoka TANESCO,
Asante!
 
Kwa Sasa,
Makamba kampita Hadi haji manara,
Anapiga mshahara wa uwaziri Kisha anapiga madili ya ubalozi na matangazo kibao pembeni ya gesi za ROSTAM
 
Asichokijua mtia mada ni kuwa , loadnstructure imebadikika sana kutokana na teknolojia , siku hiz watu wanatumia Led bulbs ambazo sio power hungry kama tungstens bulbs. , the era of big electrical cookers. Is almost over kila mtu kahamia kwenye gas !
Kwa mantiki hii kutumia waya mkubwa ni kama kupoteza reaources.

Kutoka kwenye nguzo kuja kwenye mita yako 25 sqmm ya aluminium haina tatizo, TANESCO wamekuwa wakiitumia siku nyingi tu.
 
Nilidhani REA ilisha simama kitambo kumbe bado ipo maana huu mwaka wa tano tunahaidiwa umeme lakini hamna kitu
 
Asichokijua mtia mada ni kuwa , loadnstructure imebadikika sana kutokana na teknolojia , siku hiz watu wanatumia Led bulbs ambazo sio power hungry kama tungstens bulbs. , the era of big electrical cookers. Is almost over kila mtu kahamia kwenye gas !
Kwa mantiki hii kutumia waya mkubwa ni kama kupoteza reaources.
Naongea ninalolijua vizuri,kwa watu wanaoutumia umeme kwakuwashia taa majumbani hawawezi kunielewa,ukitaka kufahamu ubora ama madhaifu ya umeme uwe unatumia three phase.
Makamba hua anazungumza mambo ambayo naamini kama kweli Tanesco wakiyafanyia kazi umeme wa nchi hii utakua na mabadiliko makubwa sana.
 
Mh Makamba sijawahi kuona wafanyakazi wako wazembe mkiwawajibisha kwenye ziara zako zakusikiliza kero za wananchi nafikiri ndio sababu wakandarasi wakishirikiana na wakaguzi Kabla ya miradi ya REA kukabidhiwa kwa TANESCO wanaendelea kupiga pesa.

Mh makamba huwa nafuatilia sana makala zenu za kuelemisha kwenye TV,moja ya sababu ambazo umekua ukitolea ufafanuzi zinazopelekea umeme kuwa mdogo ni ukubwa wa waya unaotumika kwenye service line yaani kwenye zile nguzo za mitaani kutoka nguzo moja kwenda nyingine.

Mh Makamba pamoja na mtendaji mkuu wako wa TANESCO bw Maharage mlishawahi kuwawajibisha wakaguzi wangapi kwakuikubali na kuipitisha miradi ya REA kwakuwa chini ya kiwango?

Hili la usambazaji wa waya za 25mm hasa kwenye miradi ya REA ni tatizo kubwa sana ambapo wakandarasi wanazitumia ili kupiga pesa jambo ambalo linasababisha vyombo vyetu wananchi vinaungua kutokana na umeme kuwa mdogo.

Mh Makamba hakikisheni hili jambo linakomeshwa, hizi makala zenu zitakuwa hazina maana kama yale mnayoyasemea bado mnaendelea kuyafanya.

Nipo tayari kuwaonesha hizi waya zenu kama ninyi mtajifanya vipofu hamzioni huko mitaani.

Asante.
Hapo si muangalie specifications na mripoti kwa wahusika hasa wakuu wa Mikoa maana mameneja wa Tanesco maeneo husika bila shaka wanashirikiana na hao makandarasi..

Hivi hapa Tanzania tuwe na mfumo gani mzuri wa uongozi Ili kudhibiti mambo kama haya?

Kwa sababu taasisi zilizopo hakuna kitu wanafanya,waulize hata hao Takukuru kama Wana kablasha hata moja la BoQ za mradi uwe Tanesco au TanRoads kwa ufuatiliji yet Wana wasimamizi wataalamu sasa wanashibiti vipi mambo haya na ilhali wanalipwa salary?
 
Naongea ninalolijua vizuri,kwa watu wanaoutumia umeme kwakuwashia taa majumbani hawawezi kunielewa,ukitaka kufahamu ubora ama madhaifu ya umeme uwe unatumia three phase.
Makamba hua anazungumza mambo ambayo naamini kama kweli Tanesco wakiyafanyia kazi umeme wa nchi hii utakua na mabadiliko makubwa sana.
Sikuwq nq lengo lq kupingana nawe bqli nilikuwa naongelea trend ya power consuption kutakana na tech, hata kwenye magari zile heavy specced wires hazipo tena ni mwendo wa led
Nakubaliana nawe pia kwa maeneo ya viwanda , three phase ,waya unatakiwa uwe mnene ulioshiba ,kama kweli wanaweka nyaya dhaifu maeneo kama hayo ni dhahiri watapata hasara maana zitaungua kila leo
 
Niliahidi kuleta mrejesho,
Nilituma namba zangu pm lakini mpaka sasa TANESCO hawanitafuta.
Nasubiri labda kesho watanitafuta nitawajulisha.Hata hivyo ukweli ni kwamba kwa ufuatiliaji wangu kwa maeneo mengi 25mm imekuwa kama ndio waya pendekezwa,kwajibu mapesi hili ni tatizo sugu.
Maharage kama mtakua hamuhusiki na huu upigaji tafadhali fuatilieni
 
Back
Top Bottom