Kama Iddi Amin angekuwa na full support ya jeshi then vita ya Kagera ingekuwa ndefu sana na ingetugharimu kiuchumi vibaya mno

Eli Cohen

JF-Expert Member
Jun 19, 2023
1,309
4,017
Uganda tayari ilikuwa fractured kuanzia serikalini hadi kwenye jamii. Watu wa Uganda waliishi kwa kumuogopa dadaa ila hawaku muheshimu.

Screenshot_20231117_081130_Firefox.jpg


So vita kutoka Tz ilikuwa ni fursa kwao kwa maana wanajeshi wa Tz walikuwa wanapata support kwa kila kituo walichokuwa wanafikia na naamini jeshi letu walisaidiwa intel na baadhi ya viongozi waliokuwa wanamchukia dadaa. So hii ilipelekea vita kutokuwa ndefu sana. amin alipoona mambo yanaanguka kwa kasi na kupoteza connection zote aliamua kukimbia mapema.

2094585b18f165ce35222d6ecea7d111.jpg



Kitabu cha "DELEVOPMENT CENTRE STUDIES: CONFLICT AND GROWTH IN AFRICA" kimeandika kuwa Tanazania ilitumia dola za kimarekani milioni 500 ambacho kiasi hicho kilikuwa ni asilimia 15 ya pato la mwaka 1978. Hii ilipelekea pia Tanzania kuingia katika madeni na kuwa tegemezi zaidi.

Ukweli ni kuwa baada ya vita dhidi ya Uganda uchumi wa Tanzania uliyumba. Sasa fikiria kama hii vita ingekuwa ndefu sijui tungeyumba kwa kiasi gani na matokeo ya umasikini yangekithiri.

All in All, kila ushindi unakuja cost yake. Mungu ni mwema kuwa vita haikuwa ndefu sana na pia pongezi kwa Nyerere na Ma-Veteran wa vita walioishinda hii vita.

Screenshot_20231117_083010_Firefox.jpg
 
Katiba muktadha wa hoja yako pia ukumbuke Uganda ingekuwa ni koloni la Tanzania kama ingeshindwa maana Tanzania ingepeleka azimio UN la kutaka kuikalia Uganda Kwa kipindi kirefu ili kufidia gharama za vita.
 
Back
Top Bottom