Rais Samia, vita ya kiuchumi ni ngumu sana kaza buti na mkanda hasa

KOLOKOLONI

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
2,477
2,360
BANDARI YA DARESALAM IMEMUINGIZA RAIS SAMIA KWENYE VITA VYA KIUCHUMI

Chukua kalamu na karatasi kwenye andiko hili unaweza kuandika chochote…. Ipo hivi….

Bandari ya Daresalam inahusika kwa asilimia 95% kwenye biashara za Kimataifa Tanzania. Ni eneo Muhimu mno na fursa kubwa sana kwa nchi yetu. Ukiigusa Bandari yetu kwa jema au baya basi umegusa asilimia 95 za biashara kati ya Tanzania na maeneo Mengine.

Kupitia rank za World Bank’s Conteiner Port Performance index (CPPI) inaonyesha mwaka 2022 Bandari ya Daresalam ilishika nafasi ya 361 kati ya Bandari 386 kwenye utoaji wa huduma za kibandari Duniani. Mwaka wa 2023 tukashika nafasi ya 312 kati ya bandari 348. Tafsiri yake ni kwamba bado Bandari yetu haifanyi vizuri hata kidogo pamoja na kwamba inatajwa kuwa ipo eneo zuri kuliko bandari Nyingi Duniani.

Kwa mfano mwaka 2021 World bank walitoa ripoti ya CPPI (Global ranking of container Ports) ambapo Bandari ya Daresalam ilishika nafasi ya 361 kwa ubora kati ya bandari 379 zilizoorodheshwa, yaani tulikuwa ni wa 9 kutoka Chini. Kwenye kipengele cha administrative approach bandari yetu ilikuwa na points negative -248 na katika kipengele cha Statistical approach tulikuwa na points negative -105. Tafsiri ya hizi negative ni kwamba Bandari yetu uongozi ni Mbovu, kupita kiasi na utendaji wake kwa ujumla ni mbovu kupita kiasi hivyo Bandari yetu inafanya kazi Chini ya kiwango na katika udhaifu mkubwa. Nakuwekea link kabisa uweze kupitia ripoti hiyo ya worl Bank:- https://thedocs.worldbank.org/en/do...nal/Container-Port-Performance-Index-2021.pdf

Kutokana na Kufanya huko vibaya nchi ambazo tulikuwa tukizihudumia zimeshaanza kutuhama hivyo kunahitajika juhudi za makusudi na za haraka kabisa kuponyesha bandari yetu kutokana na umuhimu wake kwenye uchumi wetu.

Wataalamu wanasema kutokana na hali ya Utulivu ya Tanzania kisiasa,na kijamii Bandari ya Daresalam imeendelea kuwa Chaguo la kwanza kwa nchi zote ambazo hazina bandari na tumepakana nazo. Bandari ya Daresalam imeendelea kuwa chaguo la Kwanza kwa nchi za Zambia, DRC, Malawi, Burundi, Rwanda na Uganda. Kwa sasa nchi hizi zimeanza kufikiria kuchukua Risk za kibiashara kupitisha mizigo yao kwenye Bandari za Mombasa, na Durban Africa Kusini kutokana na Huduma mbovu kwenye Bandari yetu. Tukicheza washindani wetu wataua kabisa Uchumi wetu hivyo hili jambo lazima tulijadili tukiwa tumetanguliza Uzalendo mbele bila kuwa na interest zozote zile.

Kwenye Bandari kumi bora Dunian taifa la China linaingiza Bandari zake saba kwenye top ten. Lakini ukifuatilia kwa nini China wanafanya Vizuri sana kwenye mambo ya Bandari utagundua kwamba katika Bandari zake tano ambazo zipo kwenye top ten ya Dunia anayeziongoza ni Mwekezaji toka nje. Sio kwamba China imeshindwa kuongoza ila kampa mwenye uzoefu zaidi hizi rasilimali za Dunia huwezi kuzifaidi zote kwa kuzikalia mwenyewe…. Wewe una dhahabu lakini huna Technolojia lazima ukubali kubadilishana ili nyote mnufaike.

APM terminals kampuni ambalo ni subsidiary ya kampuni Maersk toka Denmark ndio waliowekeza kwenye hizo bandari za China. Zaidi ya asilimia 50 ya uendeshaji wa bandari za China zinaendeshwa na makampuni ya nje (Wawekezaji). Kuna haja ya kutafakari sana wakati tukiendelea na mjadala huu wa Bandari kuwa issue si mkataba tu kukosewa ila ndani yake pia kuna Vita kubwa ya Kiuchumi.

Kwenye hili la Bandari Rais Samia ni Dhahiri ameingia kwenye Viunga vya Uwanja wa Vita ya Kiuchumi hili linaonekana wazi wazi kwa sasa. Tulizoea kumsikia Rais Magufuli akisema vita ya Kiuchumi ni Ngumu hatukuwa tunamwelewa. Ndio maana alivyoanza ujenzi wa Miradi Miwili Mikuwa wa Umeme na SGR ndio kipindi alichopigwa vita kuliko kipindi kingine nje na ndani ya Nchi. Na katika kipindi alichokaa madarakani SSH kama Rais wa Nchi wakati huu wa uwekezaji wa Bandari ndio wakati ambao kelele na kurushiwa mawe kumeongezeka.

Ukiachana na Bandari SGR nayo ilikuwa ni vita.

Kenya ndio wa kwanza kabisa kujenga mradi wa SGR wakishirikiana na Ethiopia kwa kukopa China. Mkopo huo waliokopa China uliziingiza nchi hizi mbili Kenya na Ethiopia kushika number mbili na number tatu kwa nchi zilizokopa Sana China Kutoka Africa. Yaani tukipanga wanaodaiwa fedha nyingi na China Africa basi kenya na Ethiopia zinashika number mbili na number tatu. Ni Mkopo ambao ni mkubwa Sana na kuulipa si kazi ndogo.

Jarida la African Report liliwahi kunukuu mtafiti mmoja aliyeandika kwenye Gazeti la Kenya (Daily Nation) kuwa:-.

"Kenya’s and Ethiopia’s SGR projects impacted significantly the amount of their debt to China and generally their ratio of debt relative to GDP,” researchers wrote in the Daily Nation in December 2019, “As of 2017, Ethiopia and Kenya ranked the second and third highest Chinese debtors on the continent respectively. Their debt relative to GDP has also risen exponentially compared to Tanzania’s.”

Further complicating matters is the fact that, despite accumulating debt and government focus over the past decade, Kenya and Ethiopia’s SGR’s have not delivered what they promised.

Pamoja na kwamba Wana Mkopo mkubwa Sana lakini hawatarajii kuvuna matunda yoyote yale kwenye mradi huo. Hawatarajii kuvuna Kama walivyopanga hapo awali. Yaani mipango yao imevurugika....

Sababu za kutokupata faida

Kutokana na mradi huo kutumia fedha nyingi Sana za Mkopo na ugumu wa kulipa Mkopo wenyewe Bandari ya Mombasa imekuwa si rafiki tena kupitisha bidhaa kwa nchi za Africa mashariki kutokana na masharti na Kodi walizoweka ili wapate fedha za kulipa Mkopo.

Kutokana na hilo bandari Daresalam Tanzania imeendelea kuwa kivutio kwa nchi za Africa mashariki na Kati. Balaa kubwa zaidi kwa Kenya limekuja kujitokeza kwa Tanzania ilipoanza kujenga SGR yake.

Baada ya Mradi kuanza mataifa ya Burundi, Rwanda, na Congo waliingia mkataba wa Reli hii kufika kwenye nchi zao. Kwa maana hiyo Nchi hizi zitakuwa na access ya Moja kwa Moja kwa njia ya Reli na bandari ya Daresalam. Jiulize bandari ya Mombasa Kenya itabaki inahudumia nchi nchi gani? Bandari yao itamlisha Nani? Kwa hiyo SGR yetu imekuja kuwa ni maziko ya bandari ya Mombasa.

Justification

Baada ya Tanzania kutiliana saini na nchi za Burundi, Rwanda, na Congo kuhusu ujenzi wa SGR Gazeti la nchini Kenya linalojulikana Kama the East Africa liliandika kuwa Kenya imepata pigo kubwa kutokana na makubaliano hayo ya Tanzania na Rwanda, Burundi, na Congo. Fuata Link kusoma walichokiandika.

Blow to Northern Corridor as Tanzania signs deal to link SGR to Burundi, DRC - The East African - Blow to Northern Corridor as Tanzania signs deal to link SGR to Burundi, DRC

Habari hii ilichapishwa pia na jarida la The China Project in Africa. Unaweza pia kusoma kupitia link ifuatayo kujionea kinachoendelea.

- Kenya’s Embattled SGR Suffers Major Setback as Burundi, DRC Opt for Tanzania Route to Port of Dar es Salaam

Vita nyingine ya kiuchumi ilikuwa Stiglers…

Mradi huu Rais Magufuli alipoanza kuugusia kuwa ataujenga utoke kwenye ndoto za Mwalimu Nyerere na kuwa kweli hakuna Taifa ambalo halikupinga. Mataifa ya Ulaya na kwingineko wote waliionya Tanzania wasijaribu. Sababu kubwa wataharibu mazingira....

Mwandishi Kutoka Kenya anayeishi Lusaka Zambia anayeitwa Mike Mwenda aliandika kwenye jarida la Lifegate Mambo ya ajabu kabisa na hata kumtuhumu Rais Magufuli. Kisa ni sisi kutaka kutengeneza Mradi wa Stiglers. Fuata link ifuatayo kumsoma Mike Mwenda na shutuma zake.

- Tanzania to build Stiegler's Gorge dam in a wildlife reserve and Unesco site - LifeGate

Stiglers itatuondoa kabisa kwenye uhaba wa umeme na kutufikisha kwenye Uchumi wa viwanda. Kila Tanzania inapojenga Kiwanda Moja kwa Moja unagusa Uchumi wa jirani ambao hutegemea Sana soko hapa Tanzania kutokana na sisi kuwa hatuna viwanda..

Tujiulize Kama Stiglers inaharibu mazingira je viwanda vya mabeberu haviaharibu mazingira?.....

Mwaka 1992 Marekani ulikataa kusaini mkataba wa Kyoto Protocol ambao ulihusu kupunguza viwanda ambavyo vinachangia mabadiliko ya Hali ya hewa.

Unaambiwa mataifa haya ya Magharibi pekee huchangia joto Duniani kwa asilimia 45 ya joto lote. Utafiti uliwahi kufanyika na kuonyesha kuwa Kama mataifa haya ya kibepari yatakubali kupunguza Viwanda vyao Basi Dunia inaweza ku maintain joto la centigrade 18°C.

Kwa maana hiyo hili la bandari Vipengele vya Mkataba vinatumika tu kama Silaha ya kupigana vita hii…. Tuangalie panapofaa kurekebisha tukamilishe hili dili haraka sana tumechelewa. Tumuunge mkoni Rais katika nia yake njema hii.
 
Hapa hakuna cha vita. Ni ubovu wa mkataba ndiyo tatizo. Vipengere vyote kwenye mkataba viwekwe vizuri, halafu tuone kama kuna atakayelalamika au kupinga.

Kwenye mkataba wa bandari kuna mambo mengi ya hovyo kabisa. Bandari yetu tumewekeza zaidi ya sh trilioni 10, DP atawekeza sh trilioni 1. Halafu kwenye biashara atachukua 100%, sisi 0%, kuna mwenye akili anaweza kulikubali hilo? Kule UK ipo DP, haiendeshi bandari mama, wapo kwenye bandari ya pili kwa ukubwa. UK kwa sababu ya uwekezaji wake kabla ya ujio wa DP, wamekuwa wabia wakimiliki 45%. Sisi hawa watu wametuonaje mpaka kutuwekea mkataba wa kishenzi namna hii?

Kungine kote wana mikataba inayoonesha muda wa mkataba, kwetu hakuna. Eti muda wa mkataba ni pale HGA zitakapomaliza muda wake!! Kungine kote wanalipa kodi kwa kadiri ya sheria za nchi, huku kwetu hawataki, badala yake wanataka walipe kodi chache na za viwango pungufu, kinyume na sheria yetu ya kodi. Kama sheria yetu ya kodi ni mbaya, tuifanyie marekebisho, hizo nafuu za kodi wanufaike wawekezaji wote, kwa nini iwe DP pekee?

Kukimbilia kwenye hisia hasi na kuwanyoshea wengine, ni kushindwa kuwajibika. Yaani unataka kutuambia tuamini kuwa Watanzania wote wanaopinga huu mkataba wa hovyo ni maadui Watanzania? Siyo kweli. Kama kuna watu tunaweza kuwahisi ni maadui wa ustawi wa nchi yetu, basi watakuwa ni hawa waliosaini na kupitisha huu mkataba wa hovyo kabisa.

Tuwakaribishe na tuendelee kuwavutia wawekezaji lakini iwe ni wawekezaji wenye dhamira njema kupitia mikataba iliyo bora kwa pande zote mbili, siyo wuzi kama huu wa mkataba wa bandari.
 
BANDARI YA DARESALAM IMEMUINGIZA RAIS SAMIA KWENYE VITA VYA KIUCHUMI

Chukua kalamu na karatasi kwenye andiko hili unaweza kuandika chochote…. Ipo hivi….

Bandari ya Daresalam inahusika kwa asilimia 95% kwenye biashara za Kimataifa Tanzania. Ni eneo Muhimu mno na fursa kubwa sana kwa nchi yetu. Ukiigusa Bandari yetu kwa jema au baya basi umegusa asilimia 95 za biashara kati ya kataba vinatumika tu kama Silaha ya kupigana vita hii…. Tuangalie panapofaa kurekebisha tukamilishe hili dili haraka sana tumechelewa. Tumuunge mkoni Rais katika nia yake njema hii.
Kweli kabisa.

Vita kubwa sana hii, kila mwenye maslahi nayo lazima apiganie. Yeye atazame maslahi ya Taifa. Na uamuzi wa kuifanya bandari kuwa kitovu cha mapato Tanzania ni uamuzi mwema sana.

Hiyo mimi nnauhakika ndani ya miaka 5, inalisha bajeti ya Tanzania kwa 80% kama siyo 100% kwa bajeti kama hii ya sasa.
 
Hapa hakuna cha vita. Ni ubovu wa mkataba ndiyo tatizo. Vipengere vyote kwenye mkataba viwekwe vizuri, halafu tuone kama kuna atakayelalamika au kupinga.

Kwenye mkataba wa bandari kuna mambo mengi ya hovyo kabisa. Bandari yetu tumewekeza zaidi ya sh trilioni 10, DP

Tuwakaribishe na tuendelee kuwavutia wawekezaji lakini iwe ni wawekezaji wenye dhamira njema kupitia mikataba iliyo bora kwa pande zote mbili, siyo wuzi kama huu wa mkataba wa bandari.
Kwenye gari taa za mbele ndio huonekana kwanza lakini zipo za nyuma pia

Ukishakuwa mwanasheria ukaweka ukaribu na harakati na siasa ikawa matamanio yake kuna vitu vingi utavuruga.

Hao wanaokuchambulia Mkataba huo hawajauelezea chochote juu ya faida ya Uwekezaji huo ndiyo maana nikakuwekea chapisho hilo lakini kwakuwa upo upande wa kupinga unatafuta madhaifu kwa nguvu zote na hutaki kunena yaliyo mema na Mazuri.

Nakukumbusha tu kuwa hakuna mkataba utaitwa Mkataba kama vigezo havijatimia ndiyo maana mkataba mkubwa hivyo umejadiliwa bungeni.futilia assard za bunge vizuri kisha rudi Youtube angalia malumbano ya hoja kwa kina ndani ya bunge .Utabaini wengi wanautaka huu mkataba na kuna vifungu vya kisheria ndani ya Mkataba virekebishwe. Lakini kuna vitu vingine havihitaji Elimu kubwa kujua kwanini vipo mule .

Mfano usifanye maboresho ya bandari mengine bila kuwasiliana nao hii inaonesha wazi mwekezaji anajilinda asije akavamiwa na mwekezaji mwingine akaboresha bandari ya Tanga au Mtwara maana meli zitakimbilia huko yeye atapata hasara. Mfano .aboresho ya bandari ya ziwa Victoria ikiboreshwa Kenya kisha Mwanza Mzigo utatoka Mombasa utakuja Bandari ya ziwa Victoria kenya kisha utaingia Mwanza kitendo hicho kitamfanya Mwekezaji kufilisika kwa kuwekewa Mwekezaji mwenye nguvu pia.

Mfano bandari uboreshwe ziwa Tanganyika kwa viwango vya juu na Congo DR waboreshe mzigo toka Mwanza utaingia kigoma utavuka kwenda DR na yote yanaweza fanyika bila Dp World kuhusishwa hivyo atahasirika katika uwekezaji wake. Kitu kibaya zaidi Wanasheria wa Upande wa kupinga hawasemi kwanini DP WORLD hawataki maendelezo yoyote ya bandari nyingine bila kuwasiliana nao na kukimbilia kusema tumenyang'anywa uhuru wetu kama Nchi .kumbuka tu wanadhibiti uwekezaji mwingine mkubwa ambao itawaathiri wao ila majeshi ambayo mambo yao ni vita na Makambi yao siyo biashara wala hayana madhara kwa DP WORLD.
 
Nikiitazama vita inayopiganwa Bandarini naoyaona maadui hawa:

1) Wazee wa kusambaza bidhaa za 'polomosheni" (promotion) waliojazana kila pembe ya Tanzania. Mzigo wao unatoka wapi na unapita wapi na ni kina nani? Utajaza wewe.

2) Wazee wa makontena ya loose cargo wanaoitumia bandari ya Dar.

3) Wazee wa misamaha ya "storage", hawa ni ma spesholisti wa kuchelewesha mizigo bandarini.

4) wazee waliokuwa wanalishwa na TOCTS.

5) Wenye makreni na vifaa chakavu vya kubebea mizigo pale bandarini.

6) wazee wa bandika banduwa seal za makontena bandarini.

7) bndari zote za jirani.

8) mashirika makubwa ya usafirishaji duniani.

9) Wakurugenzi wote wa bandarini, TPSA na shirika la meli waliovunjiwaa bodi zao, wapo wanaohenya mahakamani sasa hivi. Na wapo amabo karibuni watafikishwa mahakamani.

10) Wafanyakazi wa TPA wasio waaminifu.

11) Wenye kupeleka bidhaa muhimu meli zinapokuwa nangani, pamoja na wenye matisjhali.

12) Vyama vya siasa visivyokwa na sera, wamepatia upenyo. (opportunists).

13) Waanasheria njaa wasiokuwa na kazi za kufanya, wanatumiwa na makundi yote hayo ya juu.

Wengine jazeni nyinyi, nami nikiwakumbuka wengine nawaleta kujazilia nyama.

Mama uzi huohuo, wenye "exposure" wameona.
 
Hivi Unaakili kweli?? Hi nchi mbona Ina Wajinga namna hii.

JPM alipowagomea Wachina, aliwagomea Kwa kua Ni vita ya uchumi??. Si akiona Mkataba ni mbovu??.

Ya DP world, watanganyika hatupingi Uwekezaji, Tunapinga Mkataba, Mkataba ambao ni Wa Lose-Win situation , Kwa kufupisha, Prof Shivj akasema "Tanzania tumepewa Wajibu, Wadubai wamepewa Haki zote" .

Sasa inamaana Hawa Akina Shivj , na Wazalendo wote Akina Mwabukusi ambao walikua hawajulikan, wote Hawa wanapigana vita na Tanzania Yao? Kwamba nawao ni mafisadi?? Analipwa na Kenya ??

Hivi Huwa mnaandika kutafuta Teuzi au nn??.

Kuna Hoja, hoja za kisheria, zijibiwe Kisheria, ili watanganyika wawe na Amani !!.

Kwa hizi akili zenu , Hata kichaa anaweza kuongoza Nchi!!.
 
Ndiyo maana ulikwenda kujadiliwa
"Ulikwenda kujadiliwa" wapi, na nani, na ikawaje baada ya kujadiliwa?

Pamoja na kwamba andiko lako sijalisoma, kwa kuangalia tu kichwa cha mada na majibu kama haya uliyoweka hapa, inaniwia vigumu sana kuamini kwamba umeitendea haki mada yenyewe.
Andiko lenyewe refu namna hiyo, halafu mtu upotze muda kwa kusoma kitu kilicho chini ya kiwango, inaondoa hamu kabisa ya kusoma andiko zima..

Nimeamua nisipoteze muda.
 
Hivi Unaakili kweli?? Hi nchi mbona Ina Wajinga namna hii.

JPM alipowagomea Wachina, aliwagomea Kwa kua Ni vita ya uchumi??. Si akiona Mkataba ni mbovu??.

Ya DP world, watanganyika hatupingi Uwekezaji, Tunapinga Mkataba, Mkataba ambao ni Wa Lose-Win situation , Kwa kufupisha, Prof Shivj akasema "Tanzania tumepewa Wajibu, Wadubai wamepewa Haki zote" .

Sasa inamaana Hawa Akina Shivj , na Wazalendo wote Akina Mwabukusi ambao walikua hawajulikan, wote Hawa wanapigana vita na Tanzania Yao? Kwamba nawao ni mafisadi?? Analipwa na Kenya ??

Hivi Huwa mnaandika kutafuta Teuzi au nn??.

Kuna Hoja, hoja za kisheria, zijibiwe Kisheria, ili watanganyika wawe na Amani !!.

Kwa hizi akili zenu , Hata kichaa anaweza kuongoza Nchi!!.
Hakuna hoja pale zaidi ya kupiga kelele.
Maana Hoja zote zimejibiwa .Kumbuka wapo Maprofesa wa Sheria Wanaotetea mashoga na kusema ni haki ya binadamu halafu wakasahau ushonga Unaharibu muendelezo wa uwepo wa binadamu duniani .Nakushauri fikiri bila box siyo nje ya box. Ndiyo maana Maprofesa wa Uchumi ni maskini kwa theory zao za kwenye box halafu darasa la saba anawatuma kazi.

Andika hoja zako zijibiwe
 
"Ukajadiliwa" wapi, na nani, na ikawaje baaala ya kujadiliwa?

Pamoja na kwamba andiko lako sijalisoma, kwa kuangalia tu kichwa cha mada na majibu kama haya uliyoweka hapa, inaniwia vigumu sana kuamini kwamba umeitendea haki mada yenyewe.
Andiko lenyewe refu namna hiyo, halafu mtu upotze muda kwa kusoma kitu kilicho chini ya kiwango, inaondoa hamu kabisa ya kusoma andiko zima..

Nimeamua nisipoteze muda.
Ndiyo maana mnakurupuka na kuishia jela maana mnashabikia vitu kisiasa wakati hapo ni mambo ya sheria na Uchumi yanayohitaji fikra pevu. Bila shaka kama chapisho hilo hujasoma utawezaje kusoma Mkataba ule uliotengenezwa kama kitabu. Nakushauri soma ujifunze ili uache kubishana
 
Hivi Unaakili kweli?? Hi nchi mbona Ina Wajinga namna hii.

JPM alipowagomea Wachina, aliwagomea Kwa kua Ni vita ya uchumi??. Si akiona Mkataba ni mbovu??.

Ya DP world, watanganyika hatupingi Uwekezaji, Tunapinga Mkataba, Mkataba ambao ni Wa Lose-Win situation , Kwa kufupisha, Prof Shivj akasema "Tanzania tumepewa Wajibu, Wadubai wamepewa Haki zote" .

Sasa inamaana Hawa Akina Shivj , na Wazalendo wote Akina Mwabukusi ambao walikua hawajulikan, wote Hawa wanapigana vita na Tanzania Yao? Kwamba nawao ni mafisadi?? Analipwa na Kenya ??

Hivi Huwa mnaandika kutafuta Teuzi au nn??.

Kuna Hoja, hoja za kisheria, zijibiwe Kisheria, ili watanganyika wawe na Amani !!.

Kwa hizi akili zenu , Hata kichaa anaweza kuongoza Nchi!!.
Unaongea nini wewe?

Unafahamu kuwa kampuni iliyositishiwa mkataba wao na Mama Samia pale bandarini inayoitwa TICTS ni Wachina?

Walikuwepo toka enzi ya Mkapa, Kikwete, Magufuli mpaka mama ndiyo kuwapiga full stop.

Na vibaraka wao kina Karamagi na anna Tibaijuka.

Vita ndogo hiyo?

cc Mama Amon
 
Hivi Unaakili kweli?? Hi nchi mbona Ina Wajinga namna hii.

JPM alipowagomea Wachina, aliwagomea Kwa kua Ni vita ya uchumi??. Si akiona Mkataba ni mbovu??.

Ya DP world, watanganyika hatupingi Uwekezaji, Tunapinga Mkataba, Mkataba ambao ni Wa Lose-Win situation , Kwa kufupisha, Prof Shivj akasema "Tanzania tumepewa Wajibu, Wadubai wamepewa Haki zote" .

Sasa inamaana Hawa Akina Shivj , na Wazalendo wote Akina Mwabukusi ambao walikua hawajulikan, wote Hawa wanapigana vita na Tanzania Yao? Kwamba nawao ni mafisadi?? Analipwa na Kenya ??

Hivi Huwa mnaandika kutafuta Teuzi au nn??.

Kuna Hoja, hoja za kisheria, zijibiwe Kisheria, ili watanganyika wawe na Amani !!.

Kwa hizi akili zenu , Hata kichaa anaweza kuongoza Nchi!!.
Ahsante sana.

Kumbe nimefanya uamzi mzuri kutosoma takataka hiyo ndefu.

Nakushukuru kwa kunipa mwanga kuhusu yaliyomo kwenye andiko hilo.

Hawa watu wanahangaika sana. Sijui wanaokotwa wapi, watu wasiokuwa na uelewa wa jambo wanaloliandika juu yake.
 
Ndiyo maana mnakurupuka na kuishia jela maana mnashabikia vitu kisiasa wakati hapo ni mambo ya sheria na Uchumi yanayohitaji fikra pevu. Bila shaka kama chapisho hilo hujasoma utawezaje kusoma Mkataba ule uliotengenezwa kama kitabu. Nakushauri soma ujifunze ili uache kubishana
EeenHeeeee!
Unaiita takataka hiyo "chapisho"?

Kwa hiyo kwa maoni yako tukubali tu upuuzi wenu kwa vile mtatupeleka "jela"?
Mbona akili yako iko chini sana mkuu?
Unakuja hapa kutishia watu "jela"?

Uchumi gani unaoujua wewe kwa maandishi 'substandard kama haya!
 
Ndiyo maana mnakurupuka na kuishia jela maana mnashabikia vitu kisiasa wakati hapo ni mambo ya sheria na Uchumi yanayohitaji fikra pevu. Bila shaka kama chapisho hilo hujasoma utawezaje kusoma Mkataba ule uliotengenezwa kama kitabu. Nakushauri soma ujifunze ili uache kubishana
Uandishi wako tu, unaonyesha kiwango chako cha utambuzi juu ya unacho andika ni finyu sana.

Hapo nimekuuliza swali, wewe ukaishia kunitishia "jela"!

Huoni upungufu wako ulivyo?

Utaelewa vipi maswala ya "Mapambano ya vita ya kiuchumi" nahali duni ya uelewa namna hii?
 
Uandishi wako tu, unaonyesha kiwango chako cha utambuzi juu ya unacho andika ni finyu sana.

Hapo nimekuuliza swali, wewe ukaishia kunitishia "jela"!

Huoni upungufu wako ulivyo?

Utaelewa vipi maswala ya "Mapambano ya vita ya kiuchumi" na duni ya uelewa namna hii?
Umeeleza hujasoma mada bila shaka maswali yako yapo nje ya mada hivyo hayajibiwi .acha kukurupuka soma mada uelewe
Ndiyo maana mnafungwa bure kwa kiherehere na ushabiki kumbe hujui kitu sasa hapo umetishwa nini
 
Hakuna hoja pale zaidi ya kupiga kelele.
Maana Hoja zote zimejibiwa .Kumbuka wapo Maprofesa wa Sheria Wanaotetea mashoga na kusema ni haki ya binadamu halafu wakasahau ushonga Unaharibu muendelezo wa uwepo wa binadamu duniani .Nakushauri fikiri bila box siyo nje ya box. Ndiyo maana Maprofesa wa Uchumi ni maskini kwa theory zao za kwenye box halafu darasa la saba anawatuma kazi.

Andika hoja zako zijibiwe
Unaona ulivyo Punguani .

Kolokoloni wee .

Darasa la Saba ulifauli Kwa ufauli gan?
 
Back
Top Bottom