T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 10,650
- 34,938
Ni kazi kubwa sana kupima uwezo wa kijeshi wa nchi, kuna vigezo vingi hutumika na pengine kwa malengo tofauti. Kuna vyanzo ranking huzingatia namba kwamba idadi ya zana na wanajeshi, hii ni rahisi kufanya na hutumiwa pale mtu asipotaka mambo mengi ila sio sahihi. Hakuna ranking inayoweza kutoa majibu 100% kwa usahihi ila ranking nzuri inatoa makadirio yanayoendana na ukweli.
Kwanza kabisa ranking yangu haihusishi majeshi dhidi ya makundi ya waasi, magaidi au makundi ya kiitikadi yanayotaka kujitenga. Hii ni kulinganisha jeshi la nchi endapo lingepigana na jeshi la nchi nyingine.
Nimekwepa mtego huo sababu una mkanganyiko hata kwingineko duniani. Uturuki ina jeshi kubwa, ila ina waasi wa kundi la PKK wanaisumbua. Huwezi sema basi Uturuki haina nguvu sababu PKK hawaiwezi, ile ni ideology sio silaha. Au huwezi sema nchi ya Sao Tome and Principe yenye population ndogo kuliko idadi ya wanajeshi wa Misri, eti ina jeshi bora zaidi ya Misri sababu Sao Tome and Principe wenye wanajeshi less than 1,000 hakuna kundi la kigaidi na Misri kule Sinai kuna magaidi.
Imagine uiambie JWTZ ipigane na Wanyakyusa wakorofi iwaache watulivu. Sasa itajuaje kirahisi huyu Mwaikimba aliyepo Kigoma ni mkorofi, na huyu Mwamakula aliyepo Tanga ni msafi wakati wote wana act ni wasafi. Na Wanyakyusa wakorofi hawana kambi wala ofisi, wala hutakiwi kuua wote sheria za kimataifa zinakataa, na huwezi bomoa nyumba zote za Wanyakyusa utaathiri na wasio na hatia, na ukienda kuwatembelea hata ukihutubia wote wasafi na wakorofi wanakuona, wanajichanganya na wewe na wanakujua sababu umevaa sare unajulikana mwanajeshi wakati wao wamevaa fulana ya klabu au chama cha kisiasa wakati ni wakorofi.
Pia ukiachana na idadi ya silaha & zana na wanajeshi. Nimezingatia;
Ukubwa wa uchumi na rasilimali: Nchi yenye uchumi mkubwa inaweza piga nchi yenye uchumi mdogo. Inaweza kununua silaha bora na nyingi, inaweza chukua mkopo mkubwa wa silaha kama uchumi unaruhusu kulipa, ni suala la kutazama debt to GDP ratio na mambo mengine ya kiuchumi. Hapo usitarajie Rwanda kununua silaha sawa na DR Congo wakati wa shida.
Pia nchi yenye rasilimali nyingi kwa Afrika inaweza ziweka rehani ikakopa au ikaungwa mkono kwa misaada, silaha na kuungwa mkono kidiplomasia kama ambavyo Nigeria ilifanya kwenye vita ya Biafra. Waingereza wakapewa ahadi ya mafuta na USSR wakapewa ahadi ya iron ore, Wamarekani sijui walipewa nini. Kwa pamoja zikaiunga mkono Nigerian Federal government wakati kwa kawaida huwa hazikai pamoja kwenye migogoro na mwanzoni kila mmoja alikuwa upande wake (mojawapo ya sababu Kanali Ojukwu alikuwa na confidence, alijua anaungwa mkono).
Population: Nchi yenye watu wengi inaweza unda jeshi kwa muda wa dharula, ikapata reserves wa kutosha na kuendesha fronts nyingi. Inaweza sustain human loss kwenye vita, POWs, KIA, MIA, deserters.
Jiografia: 'Kiafrika' kuwa na bahari ni faida kijeshi, imports & exports sio rahisi kuzuiliwa na adui. Hapa Uganda ina disadvantage kubwa sababu iko landlocked inategemea Tanzania na Kenya. Ethiopia naona ina hasara kubwa ya kuwa landlocked kuliko nchi zote Afrika.
Pia nchi yenye majirani wengi kama Tanzania sio faida kiusalama kama nchi yenye jirani wachache.
Utawala wa nchi: Serikali za kidikteta hulizingatia sana jeshi hivyo zina majeshi makubwa, imara, yenye bajeti kubwa na utayari zaidi ya serikali za kiraia. Hata hivyo nchi za kiraia hupata support kubwa sana ya wananchi. Hapa Museveni au Kagame wako standby na majeshi ila kuna wananchi wengi sana wanaoamini jeshi ni la watawala wala haliwahusu raia. Kinachotokea mara nyingi kwenye vita na hizi nchi ni ushindi wa muda mfupi wa battles za mwanzoni, kisha nchi ya kiraia iki-gain momentum mobilization ya public inawapa nguvu kufanya counterattack. Yaleyale ya vita ya Kagera.
Pia nchi yenye rushwa, upendeleo wa matabaka, utawala mbovu, uongo na ufisadi iko more likely kuwa disorganized kwenye majeshi. Maofisa wa kamlete hawajawahi kuwa na uwezo mbele ya maofisa wanaojua waliopata kwa kustahili, wanajeshi walioingia ili waibe hela au wapate ajira ni hasara vita ikitokea. Iddi Amin alikuwa na Chief of Staff mpumbavu kwenye vita hadi maofisa waandamizi walipanga wamuue alikwamisha jeshi. Imagine Museveni ana mwanae Muhoozi ni Jenerali, hata akili zake na busara zake haziko sawasawa eti huyo aongoze jeshi.
Bajeti ya jeshi: Bajeti ina mchango wake ingawa exactly ni siri ila makadirio sahihi yapo na kwa sababu. Bajeti ya jeshi hupimwa kwa ratio ya GDP. Unakuta nchi inatumia 9% ya GDP yake kwenye ulinzi, wastani nchi nyingi duniani hazivuki 2%. Nchi Y inaweza kuwa ina $16 billion kama bajeti ya nchi nzima ila ikatumia 4% of GDP kwenye jeshi. Wakati X yenye uchumi mdogo wa $12 GDP inatumia 9% of GDP hivyo X ina bajeti kubwa ya jeshi.
Mazoea ya kuwa na bajeti ndogo kila mwaka husababisha kuwa na poor equipped military, unakuwa na zana za kizee na hazina maintenance nzuri (maintenance ya silaha ni gharama sana). Unakuwa na jeshi ilimradi, kupigia gwaride na kufanyia maonyesho. Hasara kubwa zaidi unakuwa huna uzoefu na silaha, mastering of arms ni suala la mazoea na makosa ya muda mrefu. Sio kama bodaboda unanunua tu kuendesha utajua mbele ya safari, silaha zina logistics zake, compatibility mfano umenunua fighter jets vipi kuhusu air to air missiles na spare parts, order yake ina muda wa kusubiri huendi yard China au Ufaransa ukafunga maboksi kama zana za kilimo, kuna geopolitics nyingi sana mara huyu anaona uko desperate na vita analazimisha ufanye kitu fulani ndio akuuzie silaha kwa bei ghali. Bado silaha zije uanze mafunzo na muda huo vita inaendelea, utapata matokeo mabovu sana ya matumizi. Silaha sio pikipiki kwamba kisa najua kuendesha Boxer basi hata TVS nitajua, yani rubani mzoefu wa Su-30 kwa miaka 7 ukimpa J-17 na mafunzo ya wiki ukamwambia kapigane unampa tiketi ya kifo.
Naishia hapa uzi usijefutika nikaanza upya...... Inaendelea