Kama Hayati Magufuli angeshirikiana na Tundu Lissu Mafisadi na wala rushwa wengeisha. Maendeleo fasta

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,905
44,017
Tukubaliane kwanza kuwa Utendaji wa Hayati Magufuli akiwa Waziri wa Miundo mbinu ambapo alitumikia Taifa kwa zaidi ya miongo mitatu ulitia fora. Angalau kwa hilo tulimpongeza sana.

Jambo la pili ambalo tunakubaliana sote kwa pamoja ni kuwa Mh Adv Tundu Lissu alitia fora ktk vipindi vyote vya utumishi wake kama Wakili Msomi na pia kama Mbunge.

Alitenda wajibu wake impasavyo ikiwemo kuibua nyufa za wezi, kupambania haki na kutetetea utawa wa Sheria. Ni mtu aliyekuwa akiamini kwa wakati wote ktk Utawala bora.

Haiba yake ya usomi usiotia shaka unaothibitika pasi na shaka ktk hoja zake ulimfanya mtu huyu kupendwa sana.

Hii combination ya Tundu Lissu na Hayati Magufuli ingekuwa ni mkombozi kwa Nchi yetu.

Sifa ya pekee ya Hayati ni kuwa ametumikia serikalini anajua mianya yote ya wezi. Ndio maana wakati mwingine alikuwa hamwamini mtu yeyote.

Sasa tumejifunza na tuendelee kujifunza. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
 
Kwani Magufuli kwenye kampeni 2020 si alitaka kufanya kazi na Tundu Lissu, Tundu Lissu akamibu yeye sio kama wale aliowaokota jalalani?
 
Kwani Magufuli kwenye kampeni 2020 si alitaka kufanya kazi na Tundu Lissu, Tundu Lissu akamibu yeye sio kama wale aliowaokota jalalani?

Magufuli alisema hivyo kama kejeli. Na alisema hivyo baada ya kuona watu wana hamasa sana na Tundu Lisu kuliko alivyotarajia, kwani serikali yake ilimchafua sana Lisu ili kufunika shambulio lake ambalo serekali yake ilihusishwa moja kwa moja.
 
Ni kweli ujio wa TL wakati wa kampeni ulimtoa kwenye Mood kabisa.
 
Back
Top Bottom