Kalynda Wasishtakiwe, hii ndio maana halisi ya usimuonee Huruma masikini na mjinga

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,515
52,169
Kwema Wakuu!

Kuna watu hata uwape majibu ya mtihani bado Watafeli pakubwa, alafu watakuwa wakwanza kulalamika.
Taikon ni mtu wakuwapeni Magaka/majibu ya mitihani kabla ya kuingia Chumba cha mitihani. Ukiona Jambo nimeliandika ujue tayari nishalifanyia uchunguzi wa kina, na Kwa vile sio hulka yangu kuwa mchoyo au mbinafsi ndio maana nawapeni majibu.

Niliwahi andika hapa,👉👉Usisaidie masikini, acha wafe

Hapa nilieleza namna Bora ya kumsaidia masikini ni kumpiga mshindo mzito, kumdhulumu ili akili yake imkae Sawa. Umasikini WA Mtu unaanzia kwenye Akili yake. Hivyo namna Bora ya kumfanya mtu awe na Akili sio kumpeleka shule pekee Bali kumpiga na vitu vizito mpaka akili ifanye kazi.

Niliandika hapa pia kuhusu wawekezaji, nikasema Kama unataka kuwekeza basi wekeza Kwa watu wajinga na Masikini, utapiga pesa mpaka ulie. Alafu haohao masikini watakuabudu kama mungu wao. Niliandika hapa👉👉Tanzania ukitaka kutajirika wekeza kwa wajinga na masikini

Vijana wa sasa eleweni kuwa kwenye haya maisha hakuna mtu aliyekwaajili yako.

Eleweni kuwa Maisha ni Ligi kuu ya mabingwa hayana shortcut, na yanahitaji mtu jasiri, Mwerevu, na mtu wa timing

Eleweni kuwa hakuna atakayekusaidia kama huna utakachompatia. Na Kwa nature ya binadamu mtu hawezi kukusaidia ili umzidi Ila atakusaidia ili aendelee kukuzidi, yaani anakupa 10 alafu yeye anapata 1000. Hiyo ndio kanuni ya kupata, ambayo ili upate itakupasa utoe. Na ili ukose itakupasa upokee.

Hata katika uchumi, nchi ijayo export zaidi ndio hutajirika kuliko Ile inayo-import. Bado hujaelewa tuu!

Kijana elewa kuwa hakuna kitu cha Bure dunia ingalipo binadamu akiwepo.

Kuna watu wanawasema watu Fulani ni wakarimu na wanatoa misaada Sana. L😂😂 Hakuna mtu anayefanya hivyo pasipo Hesabu ndefu ambayo wajinga hawaioni.

Wanasiasa wao wanaelewa zaidi, ukitaka kujua Hilo, jaribu hapo kwenye jamii yako kujifanya unatoa misaada mikubwa mikubwa utaona Serikali na wakubwa wa hapo wakikuzuia kufanya hivyo hata kama utasema kuwa unatoa bure na hauna agenda yoyote. Watakuambia Kama hauna agenda yoyote basi wape wao hiyo misaada alafu wao ndio wakatoe😂😂.

Masikini na wajinga utamu wao ni kuwapa vitu rahisi ili uendelee kuwpiga Kwa vitu vizito ambavyo wao hawavioni.

Hivi Kwa mtu mwenye akili na mfanyabiashara utawezaje kumshawishi akupe milioni moja alafu ndani ya wiki moja umrejeshee milioni mbili. Kwa biashara ipi? Kwa namna ipi?

Yaani akupe milioni mbili naye hapohapo awe amepata faida😂😂 uliona wapi mambo ya hivyo ndugu yangu.

Serikali isiwafungulie watu wa namna hiyo mashtaka hasa kama wakiwa Watanzania, lakini kama sio Watanzania wafunguliwe mashtaka kwani watakuwa wametudhalilisha na kutuona taifa letu ni watu wajinga wasio na Akili.

Wasalamu
 
Walionywa lakini hawakuonyeka..

 
Walionywa lakini hawakuonyeka..


Michezo Kama hiii inatakiwa iwe mingi ili watu wachangamke, akili ikilala matokeo yake ndio hayo
 
Mathayo 19 : 23-24 "

Hapo Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kweli nawaambieni itakuwa vigumu sana kwa tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni. Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko kwa tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.”
.
 
Kila siku humu nasemaga hii nchi unaweza kusafiri Zaid ya kilomita 500 ukakutana tu na mapori yasiyoendelezwa lakini unakuta njemba zinataka "shotket" tu. Acha ya pigwe na vitu vizito vyenye ncha kali.

Hela ilivyo ngumu kutafuta na kuipata halafu unamkabidhi dume mwenzako kizembeeee na kirahis. Its not right, totally unacceptable and fundamentally wrong.
 
Yakobo 5 : 1-5"
Sikilizeni, ninyi matajiri! Ombolezeni na kulia kwa sauti kwa ajili ya dhiki inayowajia. 2 Utajiri wenu umeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo. 3 Dhahabu zenu na fedha vimeliwa na kutu! Hiyo kutu itakuwa ni ushuhuda dhidi yenu, na itaila miili yenu kama kwa moto. Mmejilimbikizia mali kwa ajili yenu katika kizazi hiki cha siku za mwisho! 4 Angalieni! Mmeyazuia malipo ya wafanyakazi waliopalilia mashamba yenu. Sasa wananililia! Na kilio cha hao wanaovuna pia kimeyafikia masikio ya Bwana Aliye na Nguvu.

5 Mmeishi maisha ya anasa duniani na kujifurahisha na kila kitu mlichotaka. Mmeinenepesha miili yenu, kama wanyama walio tayari kwa siku ya kuchinjwa. 6 Mmehukumu na kuua wale watu wasio na hatia, na ambao hawakupingana nanyi.
 
Kila siku humu nasemaga hii nchi unaweza kusafiri Zaid ya kilomita 500 ukakutana tu na mapori yasiyoendelezwa lakini unakuta njemba zinataka "shotket" tu. Acha ya pigwe na vitu vizito vyenye ncha kali.

Hela ilivyo ngumu kutafuta na kuipata halafu unamkabidhi dume mwenzako kizembeeee na kirahis. Its not right, totally unacceptable and fundamentally wrong.

Licha ya watu wema kujitolea kuwasanua kuwa hiyo michongo sio lakini watu wapi
 
Back
Top Bottom