Masikini sio mtu wa kumuonea huruma leo ndio nimejifunza zaidi

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Oct 21, 2021
4,741
11,099
Kuna mdau humu aliwahi kuliongelea hili na leo ndio nimepata funzo zaidi.

Masikini ukiishi kwa unyenyekevu bila kumuonesha dharau ya aina yoyote kwa akili zake atamuhisi umemuogopa, masikini wengi wenye umasikini uliopitiliza (absolutely poverty) pia huwa na sifa ya kuwa wapumbavu, na ndio hawa wengi wao ni mtaji wa CCM.

Masikini hatakiwi kuonewa huruma, masikini hatakiwi kuthaminiwa kabisa na ukimthamini sana ujue unajitengea janga hapo baadae lakini pia niongezee kidogo kutoa ushauri kwa vijana hasa ambao mmemaliza elimu za vyuo na mmebahatika kupata ajira aidha kwenye sekta binafsi au za umma

Unapopata mshahara wako wa kwanza tafuta nyumba nzuri yenye hadhi, usitafute nyumba za hovyohovyo eti unabana mshahara ili ufanye maendeleo hapo baadae yatakukuta makubwa kabla hata hujafanya hayo maendeleo.

Umeajiriwa na level yako stashahada au shahada na mshahara wako labda ni kuanzia laki tano na kuendelea uwezo wa kula maini au nyama ya kuku unao lakini mazingira unayoishi wenyeji wako ni dagaa na mchicha kila siku aisee mkuu yatakukuta tafuta makazi yenye watu wa hadhi yako vinginevyo yatakukuta.......
 
... maskini, anayejiweza, tajiri hawa wote wanategemeana, wewe unaweza kusema hivyo ila bado utamuhitaji huyo unayetaka asionewe huruma.

Maishani kuna life division so huruma, ukatili vinatendeka kutokana na tukio na siyo kila wkt kuvaa huruma au ukatili.

'UMASIKINI NI DHAMBI'
 
watu wengine bhana, we mwenyewe hapo ulipo masikini na unaishi kwa huruma ya wengine na misaada halafu unadharau maskini, really????
Una uhakika na unachokiongea mkuu? Mimi sio tajiri na wala sio masikini na siishi kwa kutegemea msaada wa mtu, ni kweli kuna nyakati naweza kupitia kipindi kigumu mpaka kufikia kuhitaji msaada, lakini hayo sio maisha yangu, mimi ni miongoni mwa watu wenye roho ngumu mpaka kufikia kuomba msaada basi ujue nipo taabani yaani tia maji tia maji😊
 
Niliendekeza urafiki na maskini mmoja(alifikuzwa kazi ya ulinzi) akawa anashinda ghetto kwangu, namsaidia chakula na mahitaji mengine, hatimaye akaniibia TV, simu, pasi, hela laki moja na nusu,subwoofer na vitu vingine vidogo_vidogo. Baada Ya uchunguzi na mahojoano kwa kina akakiri kuwa aliviiba.

umaskini unaambatana na Laana
 
una uhakika na unachokiongea mkuu? mimi sio tajiri na wala sio masikini na siishi kwa kutegemea msaada wa mtu, ni kweli kuna nyakati naweza kupitia kipindi kigumu mpaka kufikia kuhitaji msaada, lakini hayo sio maisha yangu, mimi ni miongoni mwa watu wenye roho ngumu mpaka kufikia kuomba msaada basi ujue nipo taabani yaani tia maji tia maji😊

mimi mimi mimi hilo ndio tatizo lako labda , …
 
Back
Top Bottom