Najishangaa kwanini ninakuwa na hii roho ya huruma kiasi hiki. Najiona mjinga asee

Macbook pro

JF-Expert Member
Jul 15, 2020
665
902
Habari za kwenu ndugu zangu! Niende kwenye mada moja kwa moja.

Siku za hivi karibuni nimenunua kausafiri ambako kananisaidia kwenye stunting zangu za hapa na pale hapa mjini. Lakini nimenunua huu usafiri baada ya kununua nimekuwa nikipata udhoefu tofauti tofauti ikiwemo kumwazimisha mtu ambapo baada ya kumwazimisha roho yangu inaanza kujutia kwanini nimemuazima na wakati anapokua anaomba naku nataka kukataa ila roho ya kukataa inashindwa na roho ya kumwazimisha. Ila baadae najutia kwanini nakua mrahisi hivi kumwazimisha mtu wakati sina imani naye.

Na hii hali imekua ikinisumbua sana na najiona kama mjinga na hapo unakuta unamuazimisha mtu akirudi hajaweka mafuta anakurudishia funguo ila akili hii haija aacha kubarimdlika nataka niwe nawanyima sijui inatokeaje daah!

Najua hii kitu mnaweza mkaniona kama natania ila deep down najiona fala kabisa. Na kuna wakati najua huyu mtu nimnyime tu maana hawekagi mafuta ila akiniomba muda mrefu nampa roho ya kukataa haipo.

Hii imekaaje au ndio roho wa umasikini ananiandama? Hapa kuna jamaa nimemuazima ameondoka tu nimeanza kujilaumu sasa hata sijui nikoje. Hii imekaaje aseee kudadeki, najichukia kijinga sasa hivi.
 
Kasome japo basics za Human pyschology, utaona hiyo tabia yako ni mojawapo ya personality traits zako, na ndio zinakufanya wewe uwe wewe na mimi niwe mimi. Wala usijilaumu hata kidogo ndivyo ulivyozaliwa, cha msingi jitahidi kuwaazima wale unaowaamini na wana leseni za udereva.

Mimi nina tatizo hilo hilo, yaani kumsaidia mtu huwa nashindwa kabisa kukataa, mpaka kamkweche kangu kakazungusha injini nikiwa nimewaazima jamaa waende msibani.
 
Habari za kwenu ndugu zangu! Niende kwenye maada moja kwa moja. Siku za hivi karibuni nimenunua kausafiri ambako ameondoka tu nimeanza kujilaumu sasa hata sijui nikoje. Hii imekaaje aseee kudadeki, najichukia kijinga sasa hivi.
Hii inaitwa roho ya kinafiki unatoa kitu ila moyoni hupendi.

Basi kuitoa kwako anza kuwa real acha mara moja unafiki haitakuwa shida kuwaeleza ndugu na marafiki kuwa hiki napenda au sipendi.

Pole sana ila uwa hii roho mara nyingi inapona maana kuna matukio yanakufikisha kwenye climax kumwambia muhusika yeyote kuwa sitaki haitakuwa shida tena.
 
Sawa Mkuu tushajua kuwa unamiliki Chombo cha Moto.

Huruma unaiendekeza wewe mwenyewe na sio vyenginevyo, ukiamua kuwa Mbandidu unaweza pia.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Habari za kwenu ndugu zangu! Niende kwenye maada moja kwa moja. Siku za hivi karibuni nimenunua kausafiri ambako kananisaidia kwenye shunting zangu za hapa na pale hapa mjini. Lakini nimenunua huu usafiri baadabya kununua
Ndo maisha ndugu kama umebahatika wasaidie na wenzio tu ila haya maumivu huwa hayatuishi na tunaendelea kuishi usijilaumu sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom