SI KWELI Kakwenza Rukira aweka Makubaliano ya Siri na Umoja wa Ulaya kuhamasisha Ushoga Uganda

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Katika pitapita mitandaoni nimekutana na huyu chawa wa Mtoto wa Rais Museveni, Kainerugaba Muhoozi akimtuhumu Kakwenza Rukira kuingia makubaliano ya siri na umoja wa Ulaya nchini Uganda katika kuhamasisha ushoga nchini humo.

Nakumbuka Uganda imezuia mahusiano ya jinsia moja na Rais Museveni amebana kweli kweli wazungu hawana pa kupumulia, naona wameamua kupitia njia za panya kuleta ushenzi wao.

FAKE LGBT@+.jpg
 
Tunachokijua
Februari 8, 2024, taarifa za Kakwenza Rukia kuingia makubaliano ya Siri na Umoja wa Ulaya juu ya kueneza ushoga nchini Uganda kupitia mitandao ya kijamii zilianza kusambaa. Taarifa hiyo imehifadhiwa hapa.

Taarifa hii ilichapishwa na Mwesigye Frank, mzaliwa wa Kabula, Wilaya ya Lyantonde, Uganda, Mbunge wa Bunge la nchi hiyo na rafiki wa Karibu wa Kainerugaba Muhoozi, mtoto wa Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni.

Kwa mujibu wa Mwesigye, Kakwenza Rukia ambaye ni Mwanasheria na Mwandishi ameingia kwenye makubaliano ya Siri na Umoja wa ulaya kutumia mitandao yake ya Kijamii kueneza ushoga nchini Uganda.

Hata hivyo, tuhuma hii inatolewa wakati ambao Serikali ya Uganda tayari imeshasaini Sheria kali ya kupambana na Ushoga nchini humo.

Uhalali wa Barua hii
Je, barua hii ni halali na tuhuma zilizomo ndani yake zinamhusu mtajwa?

Pengine hili ndilo swali kubwa lililosalia. JamiiCheck imefuatilia mambo kadhaa kuhusu taarifa hii na kubaini kuwa siyo barua halisi.

Mosi, barua hii haina saini au muhuri wowote rasmi unaohusisha pande zote.

Pia, ina makosa mengi ya kiuandishi yanayoiondolea uhalali wake. Mathalani, neno LGBTQ limeandikwa LGBT2+. Aidha, mtu anayetajwa kuandika barua hii kajitumia pia nakala yeye mwenyewe.

Mapungufu mengine ambayo JamiiCheck imebaini ni mwandishi kuitaja Uingereza kama Sehemu ya nchi zinazounda Umoja wa Ulaya kitu ambacho siyo cha kweli. Februari 1, 2020, Uingereza iliondoka rasmi kwenye Umoja huo.

Katika kufuatilia zaidi nini kinaweza kuwa chanzo cha kuibuka kwa barua hii, JamiiCheck imebaini kuwa wawili hawa wamekuwa hawaelewani kwa muda mrefu, huku chanzo kikiwa ni Ukosoaji unaofanywa na Kakwenza kwa Serikali ya Uganda inayoongozwa na Museveni.

Aidha, Kakwenza alikanusha madai haya huku akituma ujumbe kuwa ni Kondoo pekee ndie anaweza kuandika barua ya aina ile na kisha kumsingizia yeye kuwa kaandika.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom